Moja ya masharti ya kujiunga na fani ya uanasheria ilikuwa ni kumaliza mafunzo ya internship kwa mwaka mmoja. Utaratibu huu umebadilishwa, hivyo kuanzia mwaka huu wahitimu wote wa Laws wanatakiwa kupitia kwenye Graduate School pale Mlimani (yalipo maskani ya muda)kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Tatizo lililopo ni masharti ya kujiunga. Kila mwombaji anatakiwa kulipa IN FULL kiasi cha Shs.1,570,000. Tangazo hili limetoka tarehe 10.03.2008 na tarehe ya mwisho ni 25.03.2008.
Hivi kweli pana mkulima au mlalahoi wa nchi hii anayeweza ku-raise kiasi hicho kwa muda mfupi kiasi hicho? Ikumbukwe kuwa wengi wa waombaji wamesoma kwa mikopo ya Bodi na wengi wanatoka mikoani na wanapaswa wajitegemee wakiwa hapa DSM.
a) Hii sio njia ya kuwaondoa walalahoi kwenye profession ya U-Lawyer?
b) Serikali - kupitia kwa Waziri Nagu aliyelianzisha hili - haikuweza kuandaa utaratibu mzuri tu wa kuwawezesha vijana hao ama kupata mikopo au kuwagharamia?
c)Kiasi cha hela hizo, hakiwezi kulipwa kwa awamu 3 au 4 kuwawezesha vijana hao kujiunga na masomo.
Kwa hili, naomba serikali - and especially Dr. NAGU, iwajibike kwa mipangilio hii mibovu.