Tuache siasa kwenye elimu ya Udaktari na Sheria. Jifunze kikwazo kilichopo Law School of Tanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Waliosoma Law school na kufaulu watanielewa vizuri kwenye uzi huu.

Tusirudie makosa ya kulazimisha watoto wote wa shule ya msingi hata wasiojua kusoma na kuandika wafaulu kilazima na kujiunga na sekondari.

Matokeo yake tumeshaanza kuyaona, Hawa watoto hawawezi kushindana na watoto wa wakubwa waliosoma shule bora, Watoto wa kufaulu bila kujua kusoma na kuandika wataishia kutawaliwa daima.

Kuna kazi kila mtu anaweza kufanya, Lakini kuna kazi zinahitaji specialization.

Taasisi zinazosimamia udaktari na sheria hazipaswi kwenda na mfumo wa kuwaridhisha wanasiasa eti kuongeza idadi ya madaktari na mawakili bila kuangalia uwezo na ubora wa taaluma.

Shule ya sheria Tanzania haina tatizo, Tatizo lililo mbele ni mfumo wa elimu ya sheria vyuo vikuu.

1. Wanafunzi vyuo vikuu Tanzania wanasoma nadharia tu na kukariri mambo, Wanapojiunga law school kuna mambo wanahitajika kuyaweka kwenye mfumo kazi, yaani Practical.

Batch ya pili Law School mwaka 2009± pale Law school nilishuhudia kwa baadhi ya wanafunzi waliofeli na kutaka kuanza kuwaaminisha watu kuwa law school ni ngumu.

Mfano: Vyuoni wanafunzi wanajifunza mambo ya charge sheet kwa kuelezea what is charge sheet? Hii ni hati ya mashtaka na swali hili liliulizwa kwenye ile batch ya 2009±

Law school, Mwanafunzi anaambiwa aandae charge sheet /Hati ya mashtaka kitu ambacho hajawahi kukifanya, Tena anaambiwa with practical example and evidence, ule mwaka wengi waliofeli walishindwa kuaandaa charge sheet lakini wanajua kudefine charge sheet.

2. Exposure ya wanafunzi na vitu vinavyoendelea mahakamani ni mdogo sana, Mambo ya Mahakama yamefanywa siri Tanzania. Kesi hazioneshwi kwenye Television hasa zile zinazovuta umma, Wanafunzi wengi inakuwa ngumu kuelewa uhalisia wa mambo yanavyokwenda kwa mfumo wa kazi, yaani Practical.

Suluhisho
Mfumo wa elimu ni mbovu na ufumuliwe hasa elimu ya nadharia inayowekewa mkazo kwa asilimia 100% vyuo vikuu inabidi igawanywe kwa mfumo wa prolata base yaani 50% iwe practical na watu waende maeneo ambayo kuna kesi nyingi mfano Mahakama ya Kisutu.

Mwanafunzi akitoka chuo practical vizuri ni ngumu kushindwa law school.

2. Muda ni mfupi sana pale law school na sio law school hata mfumo wetu kwenye Board za uhasibu ni vichekesho Sana. Baadhi ya nchi Mwanafunzi anaruhusiwa kusoma chuo kikuu huku akisoma kwenye hizi regulatory schools kama lawa schools na Bodi za uhasibu.

Mwanafunzi anapoanza chuo kikuu anajisajili pia law schools kwenye baadhi ya nchi ili kupata muda mrefu wa kuyafahamu mambo.

Hapa Tanzania Law school imekuwa kwa watu mpaka wanapohitimu sheria, Mfumo huu haufai kwani unampa mwanafunzi muda kidogo wa kujifunza.
 
Nimekusoma ulichoandika na kukielewa, lakini sioni kama umewatendea haki wanafunzi wa hapo Law School kwa haya maelezo yako.

Unazungumzia kufeli kwa wanafunzi wengi kunasababishwa na kutoandaliwa vizuri kule walipotoka, halafu ajabu, unatoa solution kuwa muda wa masomo ya hapo Law School uongezwe.

Sasa kama tatizo la kufeli wanafunzi wengi linasababishwa na ufinyu wa muda wa masomo, kwanini uwalaumu wanafunzi wanaofeli kwa ufinyu wa muda, na uache kuwalaumu wale walioweka huo muda mfupi wa masomo?

Ningeyaona madai yako yana maana, kama muda wa masomo ungekuwa wa kutosha, wanafunzi wapewe wanafunzi wapewe muda wa kutosha wa kujisomea, na mitihani, wapewe majibu ya mitihani yao kwa wakati ili wajue udhaifu wao uliopo waufanyie kazi mapema, ili wakishindwa kufaulu ndio walaumiwe.
 
Nawapongeza sana Law School kwa ku set standards, ukiona una kichwa cha kubebea mizigo , achana na mambo magumu kabebe mizigo kwa m'bichwa wako, mbona utapata tu pesa? Kuna msichana namfahamu ni graduate wa sheria Saut Mwanza, duh..... eti ana upper second kwenye cheti, kichwani hamna kitu kabisa. Nimefurahi sana Law School walivyosema arudie upya darasa la nne B
 
Hapo umesema watoto wa wakubwa, umedanganya. Ungeniambia wale wanaofaulu vizuri form six ndio wanaoperform law school hapo nitakuelewa vizuri.

Na wanaofaulu vizuri form six sio watoto wawakubwa tu, kundi kubwa ni watoto wa masikini pia ambao mara nyingi husoma shule za serikali.
 
Kupima uelewa kwa nchi zetu ni tatizo kubwa, wahadhiri wengi wa kiafrika wanafikiri kupima uelewa ni kutafuta namna ya kukomoa au kuwafelisha wanafunzi, wakati unahitaji kupima kama mtu ana basic understanding au right idea ya kile unachohitaji akifahamu. Huwezi kutegemea watu wabebe knowledge yote iliyo kwenye vitabu ndani ya fuvu la kichwa. Swala la muhimu ni kujua ni wapi unaweza kufanya reference kupata maarifa zaidi na siyo kukalili kila kitu.​
 
Kama ulivyosema tatizo ni mfumo wa elimu, mimi pia naunga mkono mfumo wa elimu ni shida na ni janga, na matokeo yake ndiyo haya. Baraza la mitihani kwa mtazamo wangu linaua sana viwango vya elimu ya nchi hii, ongea na walimu wanaoenda kusahihisha mitihani ya kidato Cha nne na sita wanafunzi wanalazimishwa kufaulu.

Miaka ya nyuma hakuna mtihani iliokuwa unatesa kama mtihani wa advance., kdato Cha sita, lakini kwa Sasa ndo mtihani ufaulu wake ni mkubwa kuliko mtihani wowote.

Kuna one nyingi na two nyingi ambazo hazikupaswa kuwepo na baadaye hawa ndo hudailiwa kujiunga na vyuo vikuu, nitoe mfano Mmoja halisi miaka ya nyuma nikiwa nasoma SAUT-Mwanza Kuna rafiki yangu tulikuwa tunasoma naye ,wakati huo alikuwa anamiliki tuition centre , Kuna dada Mmoja alikuwa anasoma Sheria, mdogo wake na dada huyo alikuwa anasoma kwenye tuition centre ya huyo rafiki yangu, siku Moja dada yule alimwandikia rafiki yangu barua ya kumjulisha kuwa amvumilie dogo asome pindi bodi wakiingiza Hela atamlipa, lakini hiyo barua dada aliandika kwa kiiengereza. Hicho kiingereza ndo kilimfanya rafiki yangu atutafute na kutuuliza kama huyu mtu ni mwanafunzi wa chuo kikuu, mbaya zaidi ni mwanafunzi wa LLB.

Shida ya elimu inaanza na elimu ya msingi Darasa la saba wengi wapo chini ya viwango, Sasa hivi Baraza wanawatumia walimu wa Sekondari kusimamia mitihani a Darasa la saba Ili kudhibiti mianya ya udanganyifu, walimu wamebana kweli, lakini inapokuja suala la kuchagua wanaotakiwa kujiunga na sekondari viwango vinashushwa sana kiasi kwamba ni sawa tu na kipindi udanganyifu ukiendelea.

Kuna mtihani wa kidato Cha pili ambao serikali inatumia pesa nyingi bila sababu, eti mtihani wote huo mtu anahitaji D mbili Ili afaulu. Sasa mtu aliyefaulu masomo mawili kwa kiwango Cha D tu anawezaje kusoma masomo yote ya kidato Cha tatu?

Law school isipewe lawama viwango vya ubora wa wahitimu kuanzia shule za msingi sekondari Hadi vyuo vimekuwa duni sana, na fani zote zingeweka mkazo kama law school matokeo yangekuwa haya haya.
 
Acha kufananisha udaktari na upuuzi mwingine, Udaktari ni taaluma hasa Sheria ni kama siasa tu!
Ujinga huu huu ulimponza Magufuri,Magufuri aliwapuuza na kuwadharau Wanasheria,Magufuri aliwapuuza na kuwadharau Madaktari,Magufuri aliwapuuza na kuwadharau Maaskofu,Magufuri aliuupuza Mfumo wa nchi ulioasisiwa tangu akiwa shuleni na kuudharau kabisa.matokeo yake ndiyo haya ameachia baadhi ya familia majonzi yasiyoisha.
 
Waliosoma Law school na kufaulu watanielewa vizuri kwenye uzi huu.

Tusirudie makosa ya kulazimisha watoto wote wa shule ya msingi hata wasiojua kusoma na kuandika wafaulu kilazima na kujiunga na sekondari.

Matokeo yake tumeshaanza kuyaona, Hawa watoto hawawezi kushindana na watoto wa wakubwa waliosoma shule bora, Watoto wa kufaulu bila kujua kusoma na kuandika wataishia kutawaliwa daima.

Kuna kazi kila mtu anaweza kufanya, Lakini kuna kazi zinahitaji specialization.

Taasisi zinazosimamia udaktari na sheria hazipaswi kwenda na mfumo wa kuwaridhisha wanasiasa eti kuongeza idadi ya madaktari na mawakili bila kuangalia uwezo na ubora wa taaluma.

Shule ya sheria Tanzania haina tatizo, Tatizo lililo mbele ni mfumo wa elimu ya sheria vyuo vikuu.

1. Wanafunzi vyuo vikuu Tanzania wanasoma nadharia tu na kukariri mambo, Wanapojiunga law school kuna mambo wanahitajika kuyaweka kwenye mfumo kazi, yaani Practical.

Batch ya pili Law School mwaka 2009± pale Law school nilishuhudia kwa baadhi ya wanafunzi waliofeli na kutaka kuanza kuwaaminisha watu kuwa law school ni ngumu.

Mfano: Vyuoni wanafunzi wanajifunza mambo ya charge sheet kwa kuelezea what is charge sheet? Hii ni hati ya mashtaka na swali hili liliulizwa kwenye ile batch ya 2009±

Law school, Mwanafunzi anaambiwa aandae charge sheet /Hati ya mashtaka kitu ambacho hajawahi kukifanya, Tena anaambiwa with practical example and evidence, ule mwaka wengi waliofeli walishindwa kuaandaa charge sheet lakini wanajua kudefine charge sheet.

2. Exposure ya wanafunzi na vitu vinavyoendelea mahakamani ni mdogo sana, Mambo ya Mahakama yamefanywa siri Tanzania. Kesi hazioneshwi kwenye Television hasa zile zinazovuta umma, Wanafunzi wengi inakuwa ngumu kuelewa uhalisia wa mambo yanavyokwenda kwa mfumo wa kazi, yaani Practical.

Suluhisho
Mfumo wa elimu ni mbovu na ufumuliwe hasa elimu ya nadharia inayowekewa mkazo kwa asilimia 100% vyuo vikuu inabidi igawanywe kwa mfumo wa prolata base yaani 50% iwe practical na watu waende maeneo ambayo kuna kesi nyingi mfano Mahakama ya Kisutu.

Mwanafunzi akitoka chuo practical vizuri ni ngumu kushindwa law school.

2. Muda ni mfupi sana pale law school na sio law school hata mfumo wetu kwenye Board za uhasibu ni vichekesho Sana. Baadhi ya nchi Mwanafunzi anaruhusiwa kusoma chuo kikuu huku akisoma kwenye hizi regulatory schools kama lawa schools na Bodi za uhasibu.

Mwanafunzi anapoanza chuo kikuu anajisajili pia law schools kwenye baadhi ya nchi ili kupata muda mrefu wa kuyafahamu mambo.

Hapa Tanzania Law school imekuwa kwa watu mpaka wanapohitimu sheria, Mfumo huu haufai kwani unampa mwanafunzi muda kidogo wa kujifunza.
Hoja nyingne?
Kwanini Sheria vyuo vingne Miaka mitatu, vingne minne?? Kwanini hili ombwe halipo Kwenye Kozi zingne??
 
Huwezi kulinganisha udaktari na sheria at the same level bana!!
 
Nawapongeza sana Law School kwa ku set standards, ukiona una kichwa cha kubebea mizigo , achana na mambo magumu kabebe mizigo kwa m'bichwa wako, mbona utapata tu pesa? Kuna msichana namfahamu ni graduate wa sheria Saut Mwanza, duh..... eti ana upper second kwenye cheti, kichwani hamna kitu kabisa. Nimefurahi sana Law School walivyosema arudie upya darasa la nne B
Kwa mfumo wetu wa elimu kukuta mtu ana As zote na GPA kubwa na kichwani hakuna kitu ni kawaida sana maana ni mfumo wa kukariri mitihani na kufaulu, kuzima moto na kufaulu.

Unakuta vyuo vikuu watu wanasoma tuition, vyuo vikuu watu wanauziana past papers na maswali yanatoka kwenye past papers. Ni mfumo sawa na wa sekondari, kariri maswali na majibu ufaulu basi.

Tunapaswa kupitia mfumo wetu wa elimu upya. Mfumo ujenge watu kua na uwezo wa kufikiri na kutafakari na kuchambua, na kuhoji sio kukariri tu na kutaka ufaulu mkubwa huku vitu basic tu vya common sense huwezi kuvidadavua.
 
Hivi utaratibu wa kuchagua wanafunzi wenye ufaulu wa masomo ya kiingereza (English Litterature)form six kama priority ya kuingia masomo ya sheria iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom