Afisa Mfawidhi LATRA mkoa wa Arusha Michael John wananchi wa King'ori na Kikatiti wanateseka mabasi yanaishia Maji ya Chai

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,157
Tumesema mara nyingi kuwa kuna haya mabasi yanaitwa Covid-19 yamesajiliwa na serikali kupitia LATRA kufanya safari zake kutokea maeneo ya Oldonyosambu, Ngaramtoni, Monduli, Kisongo, Morombo, Intel, Mapambazuko kupitia Stand ndogo Arusha mjini kwenda Kikatiti na King'ori. Ukweli ni kwamba hakuna basi linaloanzia mwanzo wa safari yake km nilivyotaja hapo juu, pili mabasi tajwa 90% yanaishia Maji ya Chai hayafiki mwisho wa safari kwa mujibu wa leseni zao. Kwa maana nyingine hizi Covid-19 hayaanzii mwanzo wa safari wala hayafiki mwisho wa safari, badala yake wananchi wanateseka wakati kanzi data ya serikali inaonesha yako mengi yamepewa leseni kusafirisha wananchi ktk maeneo hayo.

Wewe bwana Michael unayajua yote haya ila mmejifungia na maafisa wako ofisini kwani mna maslahi na mnapewa rushwa na wenye magari wafanye wanavyotaka, na wana kiburi isiyo kifani. Mbaya zaidi ukiwa bado uko mjini mpaka saa 1 jioni hutapata hata basi moja la kwenda maeneo hayo ya Kikatiti King'ori ndiyo usiseme yote huishia Maji ya Chai.

Haya mabasi vibao vyao mbele vinaonesha wanatakiwa waishie wapi. Kazi ni rahisi ni maafisa wako wa LATRA kukaa pale Maji ya Chai tena kwa kificho kila basi litakalogeuza lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria ikiwa pamoja na kunyanganywa leseni ya usafirishaji ktk hiyo njia maana mwenye gari aliomba hiyo ruti mwenyewe bila kushurutishwa na serikali.

Kama huwezi au una maslahi binafsi basi tunamwomba mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo atusaidie ikiwa ni pamoja na kutuletea Afisa Mfawidhi mwingine we una kibri, dharau na unakula rushwa za wenye magari. Kwanini mpaka dunia ya leo tusiishi kistaarabu, tunaishi kihuni, kwa wasiwasi kisa watu wachache wasiotaka kustaarabika. Arusha ni sehemu ya hovyo sana tofauti na watu wengi wanavyofahamu. Utafikiri tunaishi miaka ya 80. Mkurugenzi mkuu Habibu Suluo tunaomba wasaidie wananchi hawa wanateseka na suala la usafiri ktk maeneo yao.
 
Back
Top Bottom