Kaizer
Platinum Member
- Sep 16, 2008
- 25,320
- 17,823
Ruta
Aksante kwa mada hii hivi ni kweli mla nje hujisahau na kuja na shombo kweli??Haogopi kubambwa?
atakuwa hajui katiba yetu
Ruta
Aksante kwa mada hii hivi ni kweli mla nje hujisahau na kuja na shombo kweli??Haogopi kubambwa?
Rutashubanyuma
umenikumbusha zamani kidogo (1989) Mara tu baada ya shairi langu kutoka kwenye gazeti la "Uhuru" nilipata barua nyingi sana nyingine za kutaka... Ushairi ni jambo jema sana na watu wengi ambao ni wajuvi wa kutumia Lugha wao pia huwa ni werevu na weledi kwenye mambo mengi sana. Aakh! Bahati mbaya sana siku hizi matumizi ya lugha si jambo la kutiliwa maanani sana!!
atakuwa hajui katiba yetu
hisia zangu a kiuandishi hazina uhusiano na maisha yangu............hicho ni kipaji cha kufikisha ujumbe mahali pake..............na ni mbinu ya usanifu nguli tu.............usisome zaidi ya hapo.......ruta vipi mwezetu leo umetedwa nini? pole kwa yaliyokusibu umeandika uzi kwa hisia kali sana.penye penzi hapakosi udhia, na penye udhia penyeza rupia.
hi hi hi hi! shombo hiyo itakuja kugeuka uvundo mda si mrefu,
ni kiitafsiri kwa kimombo cha level yangu.............hapakaliki hata chembe......pambana na hiki kiswahili.......
mkuu ruta, ukiwa mwaminifu kwenye ndoa yako wala hutapata kichefuchefu, mafisadi wa ngono ndo yata/yana watokea puani mapilau wanayofakamia kwa wizi, teh teh teh!Zumbemkuu mbona wanitia kichefuchefu mie?
Pilau ale yeye tena kwa kificho huku akjijua ni mwizi tu.............akiwa kwenye chumba alichokishindilia komeo tena la viro ili asije kubambwa na mwenye mlo wake.............baada ya uporaji wa pilau ya watu aja mtaani na huanza kutubehulia.........na kuacha mafuta ya pilau na vipunjepunje vyake mdomoni.......
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Mwingine ametoka kumtafuna kuku wa watu khalafu kwa kasi ya ajabu hurukia kitandani kwa mkewe na kumshulizia manukato yatokanayo na siagi ya samli aliyopikiwa kuku wa watu aliyemtafuna ............kwa kufanya hivyo ni mithali ya kumtambia mkewe ya kuwa amejinoma kuku wa watu..........lakini swali ni
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Kwa nini asiende bafuni akaoga na kutakata na abakie akichekwa na dhamira yake badala ya kuwaadhibu waliokuwamo na wasio kuwamo..........kama ile hadithi ya panya aliyekusudiwa kuuawa na mtego lakini mtego ukamnasa nyoka ambaye mwenye nyumba aliposikia umenasa akawahi kummalizia panya gizani na matokeo yake akaumwa na nyoka mwenye hasira na kufa hapohapo.........matangani ng'ombe na kuku walichinjwa kumsindikiza mwendazake............na hivyo kukamilisha maono ya panya ya kuwa mtego ulomlenga yeye wataingia waliomo na wasiokuwamo........
Hivi walakini...........hiyo shombo amletea nani?
Eti mwingine kalishwa mijichips kuku huko na kidume cha jirani...anakuja kitandani na kuanza kuachia hewa zisizovutika sawia puani kwa mwenzie..hilo shombo amleteee nani??
Ana lambwa lambwa mdomo kama paka akiwa na kijike au kidume pori, anarudi nyumbani hataki hata kunawa mdomo anataka akugushishe mdomo wake..hilo shombo amletee nani??
Kaachia, kanyonywa nyonyo weeeee hata kuliko anavyoweza kuwamchia mwanae, eti baadae anarejea nyumbani anataka kumnyonyesha mtoto wake mchanga pasipo hata kujishwafi uzuri....eti hilo shombo anamletea nani??
Karuhusu kidume shume kimguse sehemu ambazo hata wewe mumewe/boy friend hujawahi kugusa, kanogewa huko, anarejea nyumbani, anakugezia nawe uguse huko asijue wewe sie yule aliyezoea mambo hayo..sasa hilo shombo la mtandao huo wenye wateja kidogo amleteee nani??