Kwenye hili la Jeshi la Polisi lawama ziende kwa Serikali ya CCM

Road Traffic Signal

JF-Expert Member
Mar 17, 2022
627
1,937
Kwenye hili la Jeshi la Polisi wa kulaumiwa 90% ni Serikali ya CCM na 10% ni lawama kwa jeshi lenyewe.

Ni ukweli usiopingika jeshi letu la polisi lina changamoto nyingi kuliko madhaifu yake, na hata hayo madhaifu yake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na changamoto linazopitia.

Tiririka nami.
Serikali ya CCM ilaumiwe kwa kuliingiza Jeshi la Polisi kwenye siasa. Katika kipindi cha miaka kadhaa nyuma tumeshuhudia mambo ya ajabu na ya hovyo kabisa kuwahi kufanya ama kutekelezwa na jeshi letu hili. Tumeshuhudia viongozi wa chama tawala wakitoa maelekezo kwa jeshi kana kwamba polisi imekuwa ni tawi kama UVCCM!

Tumeshuhudia viongozi wakubwa kabisa wa chama wakijitapa kuwa wao wanatumia dola (jeshi) kubaki madarakani. Na hii ni kweli kabisa wametuonyesha vile walivyokuwa wakiwatumia polisi kuiba masanduku ya kura, kuzuia mikutano ya ndani ya chama, kubambikizia wapinzani kesi, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama pinzani na mambo mengine ya hovyohovyo kabisa!

Kama hiyo haitoshi tulishuhudia vihoja na vitimbwi vingine, viongozi waandamizi wa jeshi walitembea na ilani ya chama, walihudhuria vikao vya chama, wengine walidiriki kusema kuwa CCM=Polisi na Polisi=CCM, na kutudhihirishia hilo hata wanachama wafuasi wa CCM walishona na kuvaa sare za Polisi (Jungle green)!

Viongozi wa Polisi ambao walionekana kukaidi maelekezo ya chama na kuamua kusimamia sheria na kanuni ama walitolewa kwenye nafasi zao (Aliyekuwa RPC Geita) na kurejeshwa kusoma magazeti makao makuu ya jeshi ama kuhamishwa pahala walipo na kupelekwa mahala ambapo hawatakuwa na madhara.

Katika hili la siasa tumeshuhudia mengi sana kwa kweli. Salamu ya chama ilikuwa salamu rasmi ya jeshi, (Kuna video huko youtube inamuonesha kiongozi wa CCM ngazi ya kata akimkoromea na kumfedhehesha koplo wa polisi huko mikoa ya pwani kwa vile tu aligoma kutamka 'Kidumu Chama Cha Mapinduzi').

Kwa makusudi kabisa Chama Cha Mapinduzi kiliamua kulitumia Jeshi la Polisi kufanikisha maslahi yake ya kisiasa na hivi sasa leo hii kimeshafanikiwa basi polisi wamekuwa ni takataka hawana maana. Polisi mjifunze kitu hapa, muache kutumika!

Watanzania wenye mawazo mbadala wameishi kwa tabu sana. Ilifika mahali hata kuvaa sare za ACT, CHADEMA, CUF nk ikawa jinai! Mlifika mbali polisi jamani! Waliokuwa wanawatumikisha kufanya haya leo hii wamewageuka!

Ni dhahiri chaguzi za 2015, 2019, 2020 kama kama sio mambo ya hovyo hovyo mliyoagizwa kuyafanya basi leo hii hao waliowaagiza kufanya hayo mambo ya hovyohovyo wasingekuwa madarakani. Ni nani asiyejua kilichofanyika 2015? Uchafuzi wa 2019? Uchafuzi mwingine wa 2020?

Haya leo hii wamewalipa nini hao CCM? Wamewanunulia magari? Wamewajengea nyumba? Wamewapandisha mishahara? Vielfu kadhaa mlivyolipwa kufanya mahovyo hovyo mnavyo leo hii? Au ndio wote tunaugulia ugumu wa maisha?

Chuki mlioijenga mioyoni mwetu Watanzania ni kubwa! Wengi wameumia kwa kutumika kwenu kisiasa.

Ili wananchi tuwe tena na imani na jeshi letu la polisi nashauri lifumuliwe upya!

Tunataka jeshi huru la polisi! Tunataka Jeshi la Polisi litakalokuwa halifungamani wala kupokea maelekezo kutoka kwa kiongozi yeyote wa kisiasa! Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake ibadilishwe, masuala ya waziri anayepatikana kisiasa kutoa maelekezo kwa jeshi hatuyataki, katiba ibadilishwe, masuala ya mkuu wa jeshi kuteuliwa na mwanasiasa hatuyataki!

Hii itatuepushia viongozi wa jeshi kujipendekeza kwa wanasiasa ili wapate promotion na vitengo vyenye maslahi.

Tuje kwenye changamoto nyingine inayolikabili Jeshi la Polisi ya uhaba wa vitendea kazi. Jeshi la Polisi ni taasisi ya Serikali, inaitegemea Serikali kwa kila kitu ili iweze kutekeleza majukumu yake. Tutegemee nini ikiwa Serikali haitimizi wajibu wake kwa taasisi hii nyeti?

Tunaambiwa ni mwaka wa 6 huu siyo tu mavazi, au buti bali hata soksi hawajawahi kupewa hawa askari! Askari anajinunulia mwenyewe kitambaa anashona mavazi, anatoa hela mfukoni anajinunulia buti! Kwanini asiombe elfu 5 pale barabarani? Kwa nini asitusingizie kesi ili apate elfu 20 ya kununua kitambaa?

Tunaambiwa magari wanayotumia polisi walipewa mgao 2005 na 2015 ili wawawezeshe kubaki madarakani! Baada ya kufanikiwa hitaji lenu siyo tu magari mapya bali hata hayo mliowapa sio mafuta wala vipuri mnavyowapatia!

OCD ajiongeze gari lake linapoharibika, ajiongeze kuweka mafuta kwenye cruiser yake afanye doria mji mzima, afuate watuhumiwa Nanjilinji, akimbize majambazi Kasulu. Huyu OCD ana mgodi wa dhahabu kuhudumia vipuri magari yaliyooza? Ana mgodi wa dhahabu kuweza lita 50 za mafuta kwenye gari kila siku?

Hapa mna tabu wananchi, maOCD wanatukamatakamata mtaani wapate hela ya kununua vipuri, RTO anatukamata apate hela ya kuweka mafuta, serikali ya CCM mmehalalisha haya!

Wapeni magari mapya hawa watu, wanunulieni vipuri, wapeni mafuta WATATUUA HAWA VIUMBE!

Tuje katika suala la maslahi. Hili ndio haswaa linapelekea tunaona watu wanadhulumiwa mali zao wanadhulumiwa hata na uhai wao! Hapa serikali inalaumiwa, polisi nao wanalaumiwa.

Hawa watu tumewapa mamlaka makubwa mno, sana lakini maslahi yao ni duni!

Nakumbuka kusoma mahala kuwa huko Kongo miaka fulani wakati wanajeshi wakimlalamikia kiongozi wa nchi kuhusu maslahi yao kuwa duni walijibiwa, 'Askari unalalamika maslahi duni na unamiliki bunduki'.

Hiki ndicho ninachokiona kinafanywa na Serikali ya CCM kwa polisi leo hii! Mamlaka tuliyowapa hawa watu na ujira tunaowalipa haviendani! Hapa ni sawa na kuwapa go ahead wajiongeze kama ilivyokuwa huko Kongo kwa askari jeshi.

Huyu askari amepewa bunduki, amepewa mamlaka ya kukamata, kuweka kizuizini na kushtaki, lakini ana ujira haba kwanini asi'abuse mamlaka yake kwa maslahi yake binafsi?

Turejee kwenye madhaifu ya polisi. Ni kweli serikali ya CCM imewatelekeza sio tu ninyi bali wafanyakazi wake wa kada mbalimbali kwa takribani miaka sita sasa hakuna ongezeko lolote la mshahara. Hii isiwafanye kuwa makatili kiasi hicho. Tunafahamu wapo askari wachache wenye tamaa wanaochafua taswira ya jeshi la polisi kwa kudhulumu mali za watu kufikia hata kutwaa uhai ili tu kupora mali.

Nini kifanyike?
1. Kufumuliwa na kuundwa kwa jeshi huru, jeshi ambalo halitapokea maelekezo kutoka kwa mwanasiasa.

2. Serikali kutimiza wajibu wake kwa taasisi hii. Wapewe vitendea kazi; magari, pikipiki, vipuri na mafuta kila wakati kama ninyi mnavyojinunulia mavieite yenye viyoyozi na kujiwekea mafuta kwenye kadi zenu za toto na pumha. Wapatiwe uniforms

3. Wawezeshwe kimakazi. (Makao makuu ya chama na serikali yanaongoza kwa kutia aibu makazi ya hawa watu, unaweza kujionea mwenyewe kambi iliyo pembeni ya central police ni aibu).

4. Maslahi yaboreshwe, wapatiwe ujira wao kama inavyostahili, mishahara na posho mbalimbali.

5. Kuundwa kwa chombo huru kitakachokuwa kinasimamia utendaji kazi haswa pale yanapotokea mauaji ya kutatanisha.
 
Hakika tusipobadili katiba, tukarekebisha sheria na kanuni za polisi hii taasisi itaendelea kuwa mwiba mchungu kwa watanzania!

Haya mambo ya kulifungamanisha jeshi na siasa ni uhuni. OCD anataka apande cheo, atapandaje? Kwa kuwapiga na kuwasweka mahabusu BAWACHA, RPC anataka apande cheo, atapandaje? Kwa kuwapa kipigo cha mbwa koko CHADEMA! RPC hataki kurudi makao makuu kusoma magazeti, atakataaje? Kwa kuhakikisha ma'OCD wote wanasimamia magari yawe na mafuta, vipuri vinunuliwe nk, OCD anayezingua anakula benchi.

Hivi ni kwamba viongozi wa serikali ya CCM hawayajui hayo au kwa vile tayari wamesharudi maofisini basi kiyoyozi kinawasahaulisha?

Hivi kwa mfano tuseme siku moja polisi waandamizi mkae kikao wote kwa pamoja kuanzia IGP mkubaliane hamfuati maelekezo ya CCM watam-demote na kum-promote nani?

Hebu tujaribu hiyo siku moja kipindi cha uchaguzi
 
Mleta mada umenena vyema hongera sana kwa mada nzuri.
Kila siku tumekalia kuwanyooshea kidole hawa wabeba bunduki bila kutazama mzizi wa haya yote ni nani!.

Leo hii eti Bwana Bashite naye analalamikia polisi! Loh! Wonders shall never end! Wakati anawatumia kisiasa hakujua what goes around comes around, leo na yeye ni mhanga
 
Utashangaa kwenye hii mada na hoja zake, atazuka mtu na kuanza kupinga kwa kutiririka na mapingamizi kibao, kisa tu imetajwa serikali ya CCM. Nchi hii tukitaka mambo yaende ni kutaja maovu bila kujali yanafanywa na nani.

Hongera sana mleta mada.
 
CCM ndio wamewafanya polisi wa Tanzania wawe na roho mbaya, wanapowatuma kulinda maslahi yao kwenye sanduku la kura huwaacha watumie kila njia kukamilisha lengo lao huku wakilindwa na viongozi wa CCM.

Lakini hata nje ya hapo, polisi bado wanaendeleza ukatili wao kwa raia wa Tanzania wenye uhusiano na wapinzani ili kulinda maslahi ya CCM, refer wakina Kingai na Goodluck walichofanya kwa kina Adamoo na wenzie halafu mwishowe DPP akakimbia kesi.

Haya malezi ya CCM kwa polisi wetu ndio yanawalemaza polisi waendeleze ukatili wao kwa raia wengine pale wanapokuwa kwenye mikono yao hata kama hawajihusishi na siasa.

Issue kama ile ya Mtwara ambapo kamati iliyoundwa kuchunguza tukio lile imegundua polisi walihusika kwenye uporaji wa fedha za marehemu na kipigo kilichopelekea kifo chake. Kwa kifupi CCM ni kama mzazi anayemlea vibaya mwanae halafu mwishowe anakuja kuleta matatizo kwenye jamii.
 
Kila siku tumekalia kuwanyooshea kidole hawa wabeba bunduki bila kutazama mzizi wa haya yote ni nani!.

Leo hii eti Bwana Bashite naye analalamikia polisi! Loh! Wonders shall never end! Wakati anawatumia kisiasa hakujua what goes around comes around, leo na yeye ni mhanga
Bila kusahau Sabaya aliwatumia polisi akina Kingai, Jumanne, na wengine katika mambo yake binafsi na hata katika kutengeneza kesi ya kubambika ya ugaidi dhidi ya Mbowe na walinzi wake. Mbaya zaidi hadi IGP inaonekana alidanganywa na yeye akadanganya mamlaka yake ya juu. Leo hii jeshi la polisi liko uchi baada ya kesi hii ya kihistoria kufika mahala ikafutwa na DPP na "mtuhumiwa" kuitwa Ikulu kuongea na Rais.
 
Inasikitisha sana vile hawa watu wamekuwa wakifanywa fanywa hovyo hovyo lakini kukataa wanashindwa kwasababu ya mfumo.

Leo hii ww RPC ukikataa kutii maelekezo ya CCM ukaruhusu maandamano na mikutano ya Upinzani kwenye mkoa wako basi ujue unarudi makao makuu kusoma gazeti na utabaki na cheo hicho hicho mpaka kustaafu kwako.

RPC huyo huyo hataki kuonekana ameshindwa kazi. RTO akimlalamikia gari za road patrol hazina mafuta au nozzel zimekufa anatolewa kitengo. Hii inahalalisha rushwa barabarani.

OCD anataka ugali dagaa wa mahabusu, anataka books&stationery, anataka mafuta ya doria, anataka tairi za land rover, hathubutu kumuomba RPC, maana atatolewa mjini apelekwe Rubondo, itapigwa doria moja kali watabambikiziwa watu kesi watawekwa mahabusu, kutoka ni hela zikafanye yanayohitajika.

Afande ana watoto 6 wanasoma shule za "Dadi aiyam goingi" wanahitaji ada, kula nk. Mkewe kafanyiwa operation, nyumba haijakamilika anaishi kwenye ya kupanga landlord anahitaji kodi, gari ya afande Tairod end na CV joint zimekufa, kijijini kuna mchango wa kuwajengea wazee kakibanda, mwezi ujao mwisho wa michango ya harusi, afande anafika kituoni anakoromewa na superior officer waelekee Kihonda kuna vijana wa CHADEMA wanaandamana.

Hebu tubadili mfumo (Katiba, Sheria na kanuni.) Hawa watu wawe autonomous, wasipokee maelekezo yoyote kutoka kwa waziri, RC, DC wala mtu yeyote wa chama.

Promotion na demotion zao ziwe za haki zisiegemee upande wa siasa. Sio lazima RPC awape kipigo cha mbwakoko CHADEMA ili apande cheo, sio lazima OCD asimame kupanda cheo kwa sababu aliruhusu kikao cha ndani cha ACT WAZALENDO
 
Kwenye hili la jeshi la polisi wa kulaumiwa 90% ni serikali ya CCM na 10% ni lawama kwa jeshi lenyewe.

Ni ukweli usiopingika jeshi letu la polisi lina changamoto nyingi kuliko madhaifu yake, na hata hayo madhaifu yake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na changamoto linazopitia.

Tiririka nami.

Serikali ya CCM ilaumiwe kwa kuliingiza jeshi la polisi kwenye siasa. Katika kipindi cha miaka kadhaa nyuma tumeshuhudia mambo ya ajabu na ya hovyo kabisa kuwahi kufanya ama kutekelezwa na jeshi letu hili. Tumeshuhudia viongozi wa chama tawala wakitoa maelekezo kwa jeshi kana kwamba polisi imekuwa ni tawi kama UVCCM!

Tumeshuhudia viongozi wakubwa kabisa wa chama wakijitapa kuwa wao wanatumia dola (jeshi) kubaki madarakani. Na hii ni kweli kabisa wametuonyesha vile walivyokuwa wakiwatumia polisi kuiba masanduku ya kura, kuzuia mikutano ya ndani ya chama, kubambikizia wapinzani kesi, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama pinzani na mambo mengine ya hovyo hovyo kabisa!

Kama hiyo haitoshi tulishuhudia vihoja na vitimbwi vingine, viongozi waandamizi wa jeshi walitembea na ilani ya chama, walihudhuria vikao vya chama, wengine walidiriki kusema kuwa CCM=Polisi na Polisi=CCM, na kutudhihirishia hilo hata wanachama wafuasi wa CCM walishona na kuvaa sare za Polisi (Jungle green)!

Viongozi wa Polisi ambao walionekana kukaidi maelekezo ya chama na kuamua kusimamia sheria na kanuni ama walitolewa kwenye nafasi zao (Aliyekuwa RPC Geita) na kurejeshwa kusoma magazeti makao makuu ya jeshi ama kuhamishwa pahala walipo na kupelekwa mahala ambapo hawatakuwa na madhara.

Katika hili la siasa tumeshuhudia mengi sana kwa kweli. Salamu ya chama ilikuwa salamu rasmi ya jeshi, (Kuna video huko youtube inamuonesha kiongozi wa CCM ngazi ya kata akimkoromea na kumfedhehesha koplo wa polisi huko mikoa ya pwani kwa vile tu aligoma kutamka 'Kidumu Chama Cha Mapinduzi').

Kwa makusudi kabisa Chama cha Mapinduzi kiliamua kulitumia jeshi la polisi kufanikisha maslahi yake ya kisiasa na hivi sasa leo hii kimeshafanikiwa basi polisi wamekuwa ni takataka hawana maana. Polisi mjifunze kitu hapa, muache kutumika!

Watanzania wenye mawazo mbadala wameishi kwa tabu sana. Ilifika mahali hata kuvaa sare za ACT, CHADEMA, CUF nk ikawa jinai! Mlifika mbali polisi jamani! Waliokuwa wanawatumikisha kufanya haya leo hii wamewageuka!

Ni dhahiri chaguzi za 2015, 2019, 2020 kama kama sio mambo ya hovyo hovyo mliyoagizwa kuyafanya basi leo hii hao waliowaagiza kufanya hayo mambo ya hovyo hovyo wasingekuwa madarakani. Ni nani asiyejua kilichofanyika 2015? Uchafuzi wa 2019? Uchafuzi mwingine wa 2020?
Haya leo hii wamewalipa nini hao CCM? Wamewanunulia magari? Wamewajengea nyumba? Wamewapandisha mishahara? Vielfu kadhaa mlivyolipwa kufanya mahovyo hovyo mnavyo leo hii? Au ndio wote tunaugulia ugumu wa maisha?

Chuki mlioijenga mioyoni mwetu Watanzania ni kubwa! Wengi wameumia kwa kutumika kwenu kisiasa.

Ili wananchi tuwe tena na imani na jeshi letu la polisi nashauri lifumuliwe upya!

Tunataka jeshi huru la polisi! Tunataka jeshi la polisi litakalokuwa halifungamani wala kupokea maelekezo kutoka kwa kiongozi yeyote wa kisiasa! Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake ibadilishwe, masuala ya waziri anayepatikana kisiasa kutoa maelekezo kwa jeshi hatuyataki, katiba ibadilishwe, masuala ya mkuu wa jeshi kuteuliwa na mwanasiasa hatuyataki!

Hii itatuepushia viongozi wa jeshi kujipendekeza kwa wanasiasa ili wapate promotion na vitengo vyenye maslahi.

Tuje kwenye changamoto nyingine inayolikabili jeshi la polisi ya uhaba wa vitendea kazi. Jeshi la polisi ni taasisi ya serikali, inaitegemea serikali kwa kila kitu ili iweze kutekeleza majukumu yake. Tutegemee nini ikiwa serikali haitimizi wajibu wake kwa taasisi hii nyeti?

Tunaambiwa ni mwaka wa6 huu siyo tu mavazi, au buti bali hata soksi hawajawahi kupewa hawa askari! Askari anajinunulia mwenyewe kitambaa anashona mavazi, anatoa hela mfukoni anajinunulia buti! Kwanini asiombe elfu5 pale barabarani? Kwanini asitusingizie kesi ili apate elfu 20 ya kununua kitambaa?

Tunaambiwa magari wanayotumia polisi walipewa mgao 2005 na 2015 ili wawawezeshe kubaki madarakani! Baada ya kufanikiwa hitaji lenu siyo tu magari mapya bali hata hayo mliowapa sio mafuta wala vipuri mnavyowapatia!

OCD ajiongeze gari lake linapoharibika, ajiongeze kuweka mafuta kwenye cruiser yake afanye doria mji mzima, afuate watuhumiwa Nanjilinji, akimbize majambazi Kasulu. Huyu OCD ana mgodi wa dhahabu kuhudumia vipuri magari yaliyooza?? Ana mgodi wa dhahabu kuweza lita 50 za mafuta kwenye gari kila siku?

Hapa mna tabu wananchi, maOCD wanatukamatakamata mtaani wapate hela ya kununua vipuri, RTO anatukamata apate hela ya kuweka mafuta, serikali ya CCM mmehalalisha haya!

Wapeni magari mapya hawa watu, wanunulieni vipuri, wapeni mafuta WATATUUA HAWA VIUMBE!

Tuje katika suala la maslahi. Hili ndio haswaa linapelekea tunaona watu wanadhulumiwa mali zao wanadhulumiwa hata na uhai wao! Hapa serikali inalaumiwa, polisi nao wanalaumiwa.

Hawa watu tumewapa mamlaka makubwa mno, sana lakini maslahi yao ni duni!

Nakumbuka kusoma mahala kuwa huko Kongo miaka fulani wakati wanajeshi wakimlalamikia kiongozi wa nchi kuhusu maslahi yao kuwa duni walijibiwa, 'Askari unalalamika maslahi duni na unamiliki bunduki'.

Hiki ndicho ninachokiona kinafanywa na serikali ya CCM kwa polisi leo hii! Mamlaka tuliyowapa hawa watu na ujira tunaowalipa haviendani! Hapa ni sawa na kuwapa go ahead wajiongeze kama ilivyokuwa huko Kongo kwa askari jeshi.

Huyu askari amepewa bunduki, amepewa mamlaka ya kukamata, kuweka kizuizini na kushtaki, lakini ana ujira haba kwanini asi'abuse mamlaka yake kwa maslahi yake binafsi?

Turejee kwenye madhaifu ya polisi. Ni kweli serikali ya CCM imewatelekeza sio tu ninyi bali wafanyakazi wake wa kada mbalimbali kwa takribani miaka sita sasa hakuna ongezeko lolote la mshahara. Hii isiwafanye kuwa makatili kiasi hicho. Tunafahamu wapo askari wachache wenye tamaa wanaochafua taswira ya jeshi la polisi kwa kudhulumu mali za watu kufikia hata kutwaa uhai ili tu kupora mali.

Nini kifanyike?

1. Kufumuliwa na kuundwa kwa jeshi huru, jeshi ambalo halitapokea maelekezo kutoka kwa mwanasiasa.

2. Serikali kutimiza wajibu wake kwa taasisi hii. Wapewe vitendea kazi; magari, pikipiki, vipuri na mafuta kila wakati kama ninyi mnavyojinunulia mavieite yenye viyoyozi na kujiwekea mafuta kwenye kadi zenu za toto na pumha. Wapatiwe uniforms

3. Wawezeshwe kimakazi. (Makao makuu ya chama na serikali yanaongoza kwa kutia aibu makazi ya hawa watu, unaweza kujionea mwenyewe kambi iliyo pembeni ya central police ni aibu).

4. Maslahi yaboreshwe, wapatiwe ujira wao kama inavyostahili, mishahara na posho mbalimbali.

5. Kuundwa kwa chombo huru kitakachokuwa kinasimamia utendaji kazi haswa pale yanapotokea mauaji ya kutatanisha.
Ulio ongea ni ukweli, lakini kumbuka ukweli unauma. Serikali ya CCM inayafanya yote hayo kimkakati, iendelee kutawala. Jiulize kazi za kamati za ulinzi na usalama na uozo wote unao fanywa kwa wananchi. Usalama wa taifa wapo kwa maslahi ya wananchi?
 
Walishakuambia 'wanatumia dola kubaki madarakani'
Hiyo ni kauli tosha kuonesha vile wana'abuse dola!

Kwahivyo haya yanayoendelea jeshi la polisi yana mkono na baraka za chama dola maana hata hao katika kubaki madarakani waliitumia hiyo dola wakafanya kila aina ya uhuni kwa maslahi yao
 
Siku CCM ikitoka madarakani, itakufa , maana haina ushawishi katika jamii
Ikitoka madarakani haitakuwa rahisi kurudi sababu inaishi kwa kuitegemea dola na viongozi wa serikali ngazi zote. Kama wa kuibeba hawatakuwepo itapotea mazima.
 
CCM ndio wamewafanya polisi wa Tanzania wawe na roho mbaya, wanapowatuma kulinda maslahi yao kwenye sanduku la kura huwaacha watumie kila njia kukamilisha lengo lao huku wakilindwa na viongozi wa CCM.

Lakini hata nje ya hapo, polisi bado wanaendeleza ukatili wao kwa raia wa Tanzania wenye uhusiano na wapinzani ili kulinda maslahi ya CCM, refer wakina Kingai na Goodluck walichofanya kwa kina Adamoo na wenzie halafu mwishowe DPP akakimbia kesi.

Haya malezi ya CCM kwa polisi wetu ndio yanawalemaza polisi waendeleze ukatili wao kwa raia wengine pale wanapokuwa kwenye mikono yao hata kama hawajihusishi na siasa.

Issue kama ile ya Mtwara ambapo kamati iliyoundwa kuchunguza tukio lile imegundua polisi walihusika kwenye uporaji wa fedha za marehemu na kipigo kilichopelekea kifo chake. Kwa kifupi CCM ni kama mzazi anayemlea vibaya mwanae halafu mwishowe anakuja kuleta matatizo kwenye jamii.
Jeshi la polisi maovu yake yanaoneka kwa kuwa kazi zao zipo kila siku karibu na wananchi. Ukweli ni kuwa hakuna idara ya serikali inayo sifiwa kwa utendaji mzuri. Hospitali, tra, mahakama, Magereza, shule ngazi zote, nk ni shida kupata huduma. Ama ucheleweshwe, au uliwe.
 
Inasikitisha sana vile hawa watu wamekuwa wakifanywa fanywa hovyo hovyo lakini kukataa wanashindwa kwasababu ya mfumo.

Leo hii ww RPC ukikataa kutii maelekezo ya CCM ukaruhusu maandamano na mikutano ya Upinzani kwenye mkoa wako basi ujue unarudi makao makuu kusoma gazeti na utabaki na cheo hicho hicho mpaka kustaafu kwako.

RPC huyo huyo hataki kuonekana ameshindwa kazi. RTO akimlalamikia gari za road patrol hazina mafuta au nozzel zimekufa anatolewa kitengo. Hii inahalalisha rushwa barabarani.

OCD anataka ugali dagaa wa mahabusu, anataka books&stationery, anataka mafuta ya doria, anataka tairi za land rover, hathubutu kumuomba RPC, maana atatolewa mjini apelekwe Rubondo, itapigwa doria moja kali watabambikiziwa watu kesi watawekwa mahabusu, kutoka ni hela zikafanye yanayohitajika.

Afande ana watoto 6 wanasoma shule za "Dadi aiyam goingi" wanahitaji ada, kula nk. Mkewe kafanyiwa operation, nyumba haijakamilika anaishi kwenye ya kupanga landlord anahitaji kodi, gari ya afande Tairod end na CV joint zimekufa, kijijini kuna mchango wa kuwajengea wazee kakibanda, mwezi ujao mwisho wa michango ya harusi, afande anafika kituoni anakoromewa na superior officer waelekee Kihonda kuna vijana wa CHADEMA wanaandamana.

Hebu tubadili mfumo (Katiba, Sheria na kanuni.) Hawa watu wawe autonomous, wasipokee maelekezo yoyote kutoka kwa waziri, RC, DC wala mtu yeyote wa chama.

Promotion na demotion zao ziwe za haki zisiegemee upande wa siasa. Sio lazima RPC awape kipigo cha mbwakoko CHADEMA ili apande cheo, sio lazima OCD asimame kupanda cheo kwa sababu aliruhusu kikao cha ndani cha ACT WAZALENDO
RPC Mwanza aligomea kuibeba CCM Nyamagana enzi za Masha. Matokeo alirudishwa Dar kusimamia magwaride ya ffu.
 
Back
Top Bottom