Kweli waTanzania wamechoka. Nchi imemwagiwa petroli. (MWANZA)

Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.
Wafanye kazi kwa bidii kisha kile kipatikanacho kinachukuliwa na wachache? kwanza kazi gani wewe unataka wafanye? walime kama kule Rukwa halafu hakuna mipango ya masoko kisha vyakula vinaozea ghalani? au wachimbe dhahabu kisha mazungu yakigundua kuwa hapo ipo dhahabu nyingi wanaiambia serikali toa hao tuwekeze wakibisha fukia? Kama hujui faida ya maandamano nenda Misri kaulize wanategemea nini baada ya hapo?
 
Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.

nawazo ya kina tambwe hizza haya...ufanye kazi kwa bidii wapi wakati kazi zenyewe hakuna...we vipi bana
 
Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.

kama akiwa m2 mwenye kipato cha chini anaishi kwa dola 1 USA vi2 ni gharama unategemea aendelea kufanya kazi uku ananyonywa kwani haina tofauti na kipindi cha wakoloni yaani head tax kipato chote cha cku kinaishia kulipia kodi ndio maana waliacha kazi wakaanzisha movement.
So kama wewe umetosheka acha mwenye shida naye anataka kufurahia maisha pia.
 
Najibu hiyo red hapo juu, Siku watakapotambua dhamani ya kura zao na watakapoacha kuwasifia wezi. Mtu kaanza kazi tu, mara ana ghorofa, na mali kibao, mtaani anasifiwa na kuheshimiwa, jamaa huyu kiboko kaingia tu kafanya vitu fasta.
 
Nini faida ya MAANDAMANO haya, nchi hii ni maskini watanzania wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na si maandamano.
Lowasa, Jk, Makamba, Rostam na Riz ni kazi ipi wanayofanya kwa bidii kuliko ndugu zetu wanaoteseka mashambani, baharini, barabarani na madarasani wakisubiri kujifia wakiwa bado maskini!!??
 
Uwafanyie Kazi halafu wao wale kiulaini. Wacha watu watoke barabarani waseme ufisadi = baasi !
 
wakuu... naamini huu ni mwendelezo wa operesheni sangara ..... within four years ... ccm kaput
 
Back
Top Bottom