Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,651
- 5,126
January Makamba, Mwigulu Nchemba,Nape Nnauye, Ridhiwani Kikwete na Hamis Kigwangala ukitazama vizuri ni baadhi ya vijana wa CCM ambao ama walikuwa "wanaandaliwa" au "kujiandaa" kutoa uongozi mkubwa kwa Taifa letu katika siku zijazo .
Nasema hivi nikizingatia " generational succession plan" ya Nchi yetu.
Viongozi Wakuu wa Nchi yetu kuanzia 2025 - 2035 watakuwa ni watu ambao wamezaliwa kati ya mwaka 1961 hadi 1985.
Sasa nini kimetokea au wamekosea wapi hawa vijana maana sioni katika " rada" yangu "nafasi zao " katika uongozi mkuu wa Nchi yetu katika nyakati zijazo nilizozitaja.
Muda huu ndo walipaswa kuwa na majukumu makubwa ya kuwawezesha kuijua Nchi yetu vizuri, misingi ya uchumi wetu, kujua vizuri ndoto na matarajio ya watanzania, kuijua dunia vizuri na jinsi inavyo- operate !
Mwigulu Nchemba yeye naona yuko kwenye sheria na katiba sehemu ambako nadhani hajifunzi chochote kwa siku zijazo kwa manufaa ya Taifa zaidi ya kupata " ugali" wake wa kila siku tu!
Yeye ni mchumi na sidhani kama anajua hata a,b,c za sheria.Hajui hata "mens rea na actus reus" na huu kwa mtazamo wangu ni mzigo sana kwa watu kama Prof.Ibrahimu Juma (CJ), Aderladius Kilangi (AG) na Biswalo Mganga (DPP) ambao wote ni wanasheria.
Ugumu wa ufanyaji kazi wa Mwigulu Nchemba katika sheria ni sawa tu na kuendesha kesi na mtu anayejua lugha moja tu, mfano lugha ya kisukuma au kijaluo basi!
Watanzania lazima tufike mahali tukubali kuwa huu upatikanaji wa viongozi wakuu wa Taifa letu kwa "kushitukizana" una faida zake na hasara zake na unaweza kutugharimu sana kwa miaka dahari.
Athari mojawapo kubwa ya kupata viongozi wakuu wa Nchi ambao mawazo yao,ideology beliefs zao hazikujulikana mapema ni kubwa sana kwani viongozi wa namna hiyo akipata madaraka ni kama vile Nchi imepata Uhuru siku alipoingia yeye madarakani,hakuna continuity katika progress ya Nchi.
Hivyobasi mimi kama mwananchi naona tunapaswa kuyaangalia na kuyajadili haya mambo kwa Uhuru, staha na ueledi kwa mstakabali mwema wa Nchi yetu.