Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

popo

Member
Aug 30, 2008
60
1
KWANINI WATANZANIA WANAMLAUMU MWALIMU NYERERE KWA KUKOSA ELIMU?

Sababu mbalimbali ambazo wametoa wadau ughaibuni

Hivi karibuni nilikuwa nje ya nchi nikakutana na watanzania waishio nje ya Tanzania na nikajaribu kuwauliza ni matatizo gani wanayoyapata au wanayokumbana nayo kwenye maisha yao ya kila siku nje ya Tanzania.

Wengi wao niliwasikia wakisema kwamba Elimu ndio kitu kikubwa kinachowafanya washindwe kuendelea mbele na kufikia kumlaumu Mwalimu Nyerere moja kwa moja.
Lakini nilipowauliza ni vipi Nyerere amewafanya wao wasisome hakuna hata mmoja ambaye alinipa sababu ya maana, Wengi waliniambia kulikuwa hakuna shule na University za kutosha na ndio maana wengi wao hawakufika mbali kielimu.

Nilipotaka kufahamu kwa undani wao elimu zao wakati wanakuja ughaibuni hakuna hata mmoja ambaye alitaka kuelezea au kutoa maelezo kuhusu hilo.

Kitu ambacho nilikiona toka kwao ni kuwa mbele sana kulaumu na sio kufanya jitihada zozote za kujikomboa kielimu.
kwanini nasema hivyo, nilipowauliza kwamba kama wameweza kugundua udhaifu wao ni Elimu kwanini wameshindwa kujiendeleza huko ughaibuni kwenye elimu bora na ni bure kwa wao ambao wamepata uraia wa huko? Sikupata jibu kuhusu swali langu hilo na nikazidi kubishiwa pasipo kuwa na sababu yoyote ya maana.

Niliendelea kuwauliza swali jingine kwamba Nyerere huku ughaibuni hayupo je nini kinawafanya wasisome? Pia sikupata jibu lolote na nikaona mmoja baada ya mwingine akiondoka hata bila ya kuaga.

Mdau mwingine akaniambia kwamba kwanini Nyerere alaumiwe ni kwa sababu wazazi wao hawakusoma kwahiyo kulikuwa hakuna changamoto ndani ya nyumba na pia kulikuwa hakuna role model wa kuwafanya wao waone umuhimu wa elimu.
Nikafikiria kuhusu hilo pia sikuona kama ni sababu ya maana kwa sababu Mwalimu Nyerere amekuwa madarakani miaka 23 tu, kipindi hicho wazazi wetu wengi walishapitia shule ya Mkoloni na sio kipindi cha Nyerere. Pili Nyerere mwenyewe amesoma bila ya kuwa na role model ndani ya Familia yake na nafahamu wengi wa Wazazi wetu wamesoma bila hata ya wazazi wao kwenda shule, kwahiyo sikuona sababu hiyo kama ndio imewafanya wao wasisome.
Na nilipojaribu kuangalia wengi wa wazee wetu ambao wamesoma, baba zao walikuwa kama sio wakulima basi ni wavuvi au wafanya biashara ndogo ndogo.

Kingine ambacho bado kinanitia shaka kuhusu watu kumlaumu Nyerere ni Je inakuwaje mtu ambaye hakupenda watu wasome ataifishe mashule yote ambayo yalikuwa yanamilikiwa na wamisionari pamoja na magabacholi na kuzifanya za Umma na kuhakikisha kila mtoto ambaye anatamiza umri wa kwenda shule anakwenda shule tena bure bila hata kulipa ada au kujinunulia daftari.

Nyerere huyo huyo tena akapitisha sheria ya kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anakwenda shule pale anapotimiza umri wa kwenda shule la sivyo mzazi ambaye hatampeleka mtoto wake shule atachukuliwa hatua.
kiongozi huyo huyo (Marehemu Nyerere) alifungua Taasisi ya Elimu ya watu wazima ambayo iliwapa nafasi watu wote ambao walishindwa kujiendeleza kielimu wakati wa ujana wao wajiendeleze.

Na ukiangalia takwimu za dunia wakati huu utakuta wengi wa watanzania walikuwa wanajua kusoma na kuandika kitu ambacho ni msingi mzuri wa kujiendeleza kielimu.Wako wazazi ambao walichapwa viboko kwa kutowapeleka watoto wao shule.Na vyuo vingi tu vilikuwepo kama vile

1. Business college (CBE) Dar-es salaam

2 .Business College(CBE) Dodoma;

3. DSA Dar-es-Salaam

4. DSA Mbeya wings,

5 .DSA Singida Wings

6. DSA Mtwara Wings

7. Arusha School of Accountancy

8. Institute of Finance and Management (IFM)

9. Mzumbe Management College

10. Sokoine University of Agriculture (SUA)

11.Chuo cha Uandishi wa Habari.

12.Chuo cha Masekretari Tabora

13.Chuo cha Usafirishaji

14.Chuo cha Utalii (Magogoni)

na Vyuo vingine vingi vya Mifugo, Kilimo, Uandisi na Ubaharia

Swali nikawauliza wadau je kama wao walikuwa kweli ni wasomaji basi hata kidiploma wangepata kwenye moja ya vyuo hivyo lakini kati yahao niliokuwa nao hakukuwa na hata mmoja ambaye anadiploma kutoka vyuo hivyo.

Swali la mwisho ambalo niliwauliza ni je iweje sasa hivi wao wapo nje ya nchi washindwe kusoma?
Kwani walipokuwa Tanzania walisema ni Nyerere ndio kasababisha wao wasisome; Je huku ughaibuni Nyerere hayupo na nani huku anawafanya wasisome?
Hapo sikupata jibu na nakaendelea na safari yangu kutafuta wadau wengine wanipe maelezo kuhusu hilo.

Ukiangalia Historia ya nchi yetu utagundua watoto wengi waliosoma Baba zao ni wakulima na wala sio wasomi kama wadau walivyotoa sababu zao. Kwani hata Nyerere mwenyewe ni watoto wake wachache tu ndio wamesoma. Wazazi wengine walitembea mpaka maili 15 kufuata shule kipindi cha mkoloni na kulikuwa hakuna role model yoyote wala changamoto yoyote iliyowafanya wasome.

Iweje mtu ambaye alikuwa anasisitiza kwamba maendeleo ya Tanzania hayatapatikana kwa kujenga majengo mazuri au mabarabara mazuri bali ni kuwapatia elimu nzuri na bora watu wake ili hata hayo mabarabara yakijengwa wasije wakayaharibu na hilo tumeliona sana kwenye karne ya 20 watu kuiba nyaya za umeme, Madini kwenye Transformer na kuiba vyuma na mabomba kwenye madaraja.

Je kuna haki kweli ya kumlaumu yeye kuhusu Elimu? Labda wadau wengine wanaweza kunisaidia kuhusu hilo.

Mdau mwingine akaniambia hakujenga University nyingi kwahiyo kulikuwa hakuna nafasi kwa wasomi wengine?

Hapa nikaona labda huyu anapoint za kujieleza nikamuuliza wewe umemaliza kidato cha ngapi? Au kuna watu wangapi unawajua wamemaliza kidato cha sita na wanamadaraja ya juu, bila kusita akaniambia yeye amemaliza form 4 na amepata division 4. Nikamwambia division 4 yako haitoshi wewe kuendelea na Elimu ya juu kwani ni dhaifu kwenye mfumo wetu wa elimu na hapo Nyerere hastaili lawama yoyote kwa hilo.
Kama kuna vijana wengi ambao wamemaliza kidato cha sita na wana division 2 point 11 niambie ni wangapi unaowafahamu na hawakubahatika kuchaguliwa kwenye vyuo vya juu? Kwani hata wale ambao walimaliza kidato cha 4 na division four zao walikuwa wanateuliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu.
Na kama basi wangepata angalau division Three vyuo vyote ambavyo nimevitaja hapo juu wangepata nafasi za kujiunga

MAONI YANGU
Vijana wengi wa kitanzania wanapenda maisha mazuri lakini bado ni wavivu kujituma hasa kwenye Elimu hata wanapopata nafasi nzuri za kazi; kwani Inashangaza sana kukuta mtu au watu wamekaa ughaibuni kwa miaka 20 bila hata ya Degree ya kwanza au hata Diploma, achilia mbali diploma basi hata wajifunze lugha ya watu kwa ufasaha bado ni tatizo kwao na bado wanajaribu kutaka kumtumia Nyerere kama ‘Scapegoat’. Huu ni ujinga wa hali ya juu kwani unapoingia darasani ni Akili yako na wala sio akili ya baba yako au Nyerere inayokufanya ufanikiwe kwenye masomo yako, bali ni akili yako.

Kama wameweza kusoma watoto wa jamii za wachungaji na wavuvi (mfano wamasai,watindiga) na makabila mengine mengi ambayo bado yanatunza utamaduni wao wa kurisishana elimu inakuwaje wengine washindwe kusoma na kufikia malengo yao.

Cha kushangaza zaidi watoto wengi baba zao ambao wamesoma na wanaelimu nzuri pamoja na Matajiri wengi wa Tanzania watoto wao hawana Elimu ya kutosha na wengi wao wanaishia form 4 au form 6.

Mimi nimesoma kwenye shule mbalimbali Tanzania kuanzia Dar-es-Salaam, Arusha, Moshi , Mbeya na Songea na nasema kwa experience yangu kwamba wengi wa watoto wa vigogo ambao nilikuwa nasoma nao walikuwa muda mwingi wanafanya ubishow shuleni na walikuwa hawajihusishi kabisa na kusoma na sio kwamba vichwa vyao ni maji lahasha ni kwa sababu zao binafsi,wengine utawasikia mimi Baba yangu anafedha nimekuja kumaliza miaka tu au nimekuja kukua, hayo ndio maneno ambayo walikuwa wanawaambia wanafunzi wengine na kudiriki pia kuwasumbua madarasani. Je na hawa pia watamlaumu Nyerere?

Vijana wa kitanzania hasa ambao wana nafasi za wazi kujiendeleza nawasa mchukue nafasi hizo kwa kujielimisha ili mkasaidie kuendesha gurudumu la maendeleo au basi hata maisha yenu tu na tuacheni lawama ambazo hazitatusaidia chochocte kwenye maisha yetu ya kila siku.

Ilifikia kipindi watu kuamini ni makabila fulani tu ndio wanauwezo kielimu na makabila mengine kuwa ni vichwa maji nabado zana hii ya kijinga inaendelea kwenye jamii yetu ya kitanzani. Kusoma hakuna udini wala ukabila wala rangi wala umri, ukiweka malengo utafanikiwa na ukisema ukae tu na mambo yatajiseti yenyewe hakuna kitu kama hicho hizo ni ndoto (Utopia) au “Unrealiable dream which will never come true”

Kitu kimoja nilichogundua kwa ndugu zangu wengi wa ughaibuni ni kutaka maisha ya harakaharaka na yamkato na sio kuchukua njia ndefu ambayo inabidi jasho likutoke kwa kusoma na kufanya kazi ya ziada kushindana na mitihani ya maisha.

Success in Education depends so much on Strength of Mind, Willpower, Purpose, Fortitude and Grit (No nonsense and No gimmick).

Note:Watanzania wengi walioulizwa maswali haya wametokea Reading, Milton Keynes, Slough, Manchester na East London

Mkereketwa ‘Kenge’

.

’
 
Mkuu

We unataka alaumiwe nani Kenyata ? Na sio elimu tu the only thing yule Mzee anadeserve credit ni AMANI and nothing else.Misingi ya hili jumba letu katuwekea yeye na tunaona nyufa kila kona sasa cha kusifia ni nini ?

SAHIBA
 
Yes, put everything on his head. Labda hata Rostam anatuibia kwakuwa Nyerere hakutusomesha!
 
Waache kuleta za kuleta, Nyerere kaichukua nchi haina kitu kielimu wala kiuchumi, alifanya kila linalowezekana watanzania waweze kusoma bure toka chekechea mpaka chuo kikuu, tulikuwa hatuna hata chuo kikuu hata kimoja, lakini kwa kuanzia akatupatia vyuo vikuu viwili, na vyuo vingine kemkem kama ulivyo vitaja hapo juu. Hatuna shukran kwa kweli. Tulitaka vyuo vikuu viote kama uyoga kwenye nchi ambayo wakati huo haikuwa hata na viwanda, hata uzalishaji wa kueleweka mashambani haukuwepo, na biashara zilikuwa za kubangaiza. Alitutoa katika hali ya chini kabisa, lakini tumeishia kumlaumu. Alitujengea viwanda tumeua, mashirika ya umma yote tumetoa bure, alituhifadhia madini tumegawaa bure kama njugu, alituhimarishia bandari tumewapatia washkaji, alitujengea reli ya TAZARA tumeua, Mabenki tumeyatoa kama njugu hata kubaki na hisa ailimia 49 kwa ajili ya watanzania hatutaki. Kila kitu ambacho kingeimarisha uchumi wa mtanzania kiko mikononi mwa wanyonyaji. Jamani Nyerere alifanya mengi sana lakini kwa vile tulivyokuwa na shingo ngumu hatukuliona na badala ya kuungana nae kufanikisha hayo malengo tuliishia kuwa sehemu ya wahujumu. Kumbukeni nchi hii wakati anaichukua haikua na kitu cha kujivunia. Leo kuna vijiji ukienda kuna zahanati na mateki ya maji ambayo hayafanyi kazi lakini yalijengwa wakati wa Mwalimu. Eti tunasubiri tukaombe hela kwa wahisani ili tuiboreshe wakati pesa tuliyonayo tumewaachia mafisadi wakitanulia.

Mtoto wa mkulima alipelekwa chuo kukuu akilipiwa kila kitu. Mzazi alikua hajui cha nauli wala gharama za kumsomesha mtoto chuo kikuu zilikuwaje. Achilia mbali shele ya msingi na sekondari. Tulitegemea waliofaidi elimu nzuri ya wakati huo wangeiboresha zaidi kwa ajili ya kuimarisha utaifa na moyo wa uzalendo kwa watanzania lakini wapi wamekengekeuka na ndio sumu kali ambayo haitaki mtoto wa maskini apate elimu waliyoipata.

Tuache kulaumu adui yetu yupo madarakani. Tuna mwaka mmoja wa kufanya maamuzi mazito lakini yenye uchungu na matumaini kwa aajili ya nchi yetu

Nasema Nyerere apewe sifa kwa hilo na tumwache apmzike kwa amani huko aliko
 
Andikile you real talked sense in which so many people they don't want to hear that.Congratulation kama kuna watu wenye akili kama wewe basi taifa letu lingekuwa mbali
 
KWANINI WATANZANIA WANAMLAUMU MWALIMU NYERERE KWA KUKOSA ELIMU?

Kwa sababu hawakuwa na Elimu na leo hii hawana elimu...Ni kazi mgumu sana kwa mjinga kufahamu kwamba yeye ni mjinga na akataka kujielimisha, lakini ni rahisi sana kwa mjinga kumnyooshea mtu kidole kuwa yeye ndiye sababu ya ujinga wake..
Kamwe hata elimika!
 
Sasa kama nyerere alisababisha wakose elimu, hata huko ughaibuni nako mzimu wa nyerere unawaandama au?
 
Waache kuleta za kuleta, Nyerere kaichukua nchi haina kitu kielimu wala kiuchumi, alifanya kila linalowezekana watanzania waweze kusoma bure toka chekechea mpaka chuo kikuu, tulikuwa hatuna hata chuo kikuu hata kimoja, lakini kwa kuanzia akatupatia vyuo vikuu viwili, na vyuo vingine kemkem kama ulivyo vitaja hapo juu. Hatuna shukran kwa kweli. Tulitaka vyuo vikuu viote kama uyoga kwenye nchi ambayo wakati huo haikuwa hata na viwanda, hata uzalishaji wa kueleweka mashambani haukuwepo, na biashara zilikuwa za kubangaiza. Alitutoa katika hali ya chini kabisa, lakini tumeishia kumlaumu. Alitujengea viwanda tumeua, mashirika ya umma yote tumetoa bure, alituhifadhia madini tumegawaa bure kama njugu, alituhimarishia bandari tumewapatia washkaji, alitujengea reli ya TAZARA tumeua, Mabenki tumeyatoa kama njugu hata kubaki na hisa ailimia 49 kwa ajili ya watanzania hatutaki. Kila kitu ambacho kingeimarisha uchumi wa mtanzania kiko mikononi mwa wanyonyaji. Jamani Nyerere alifanya mengi sana lakini kwa vile tulivyokuwa na shingo ngumu hatukuliona na badala ya kuungana nae kufanikisha hayo malengo tuliishia kuwa sehemu ya wahujumu. Kumbukeni nchi hii wakati anaichukua haikua na kitu cha kujivunia. Leo kuna vijiji ukienda kuna zahanati na mateki ya maji ambayo hayafanyi kazi lakini yalijengwa wakati wa Mwalimu. Eti tunasubiri tukaombe hela kwa wahisani ili tuiboreshe wakati pesa tuliyonayo tumewaachia mafisadi wakitanulia.

Mtoto wa mkulima alipelekwa chuo kukuu akilipiwa kila kitu. Mzazi alikua hajui cha nauli wala gharama za kumsomesha mtoto chuo kikuu zilikuwaje. Achilia mbali shele ya msingi na sekondari. Tulitegemea waliofaidi elimu nzuri ya wakati huo wangeiboresha zaidi kwa ajili ya kuimarisha utaifa na moyo wa uzalendo kwa watanzania lakini wapi wamekengekeuka na ndio sumu kali ambayo haitaki mtoto wa maskini apate elimu waliyoipata.

Tuache kulaumu adui yetu yupo madarakani. Tuna mwaka mmoja wa kufanya maamuzi mazito lakini yenye uchungu na matumaini kwa aajili ya nchi yetu

Nasema Nyerere apewe sifa kwa hilo na tumwache apmzike kwa amani huko aliko

Nyinyi kweli mna kasoro hapa mnamsifia mtu ambaye hata watoto wake wa kuwazaa wanajuta kuzaliwa nae.Hawana uwezo hata wa kuwa makatibu kata kwa maana alishindwa hata kuitake care familia yake.Tumegubikwa Watanzania tuna maradhi yasiyo na tiba may hapo alipodai uhuru kwa manufaa yake leo hii bila fikra za Nyerere za kibinafsi usingelisema nchi haikuwa na kitu alipoichukua.Shame on him. Think Twice.

SAHIBA.
 
Si kweli kwamba Mwalimu hakutaka tusome. Alitaka sana, but he went about it the wrong way. Alikamata, kwa nguvu, shule za Makanisa na shule nyingine za watu binafsi. That was a colossal mistake.

Leo hii, tungekataza shule za Makanisa na shule za watu binafsi kama alivyofanya Mwalimu si tungekwisha!

Mwalimu won some and lost some. Let us learn not only from his successes but also from his mistakes.
 
Mwl Moshi,

Hivi ni kweli Mwl JKN alikataza shule za makanisa na shule za watu binafsi?.........im lost.....please enlighten me............
 
Nyinyi kweli mna kasoro hapa mnamsifia mtu ambaye hata watoto wake wa kuwazaa wanajuta kuzaliwa nae.Hawana uwezo hata wa kuwa makatibu kata kwa maana alishindwa hata kuitake care familia yake.Tumegubikwa Watanzania tuna maradhi yasiyo na tiba may hapo alipodai uhuru kwa manufaa yake leo hii bila fikra za Nyerere za kibinafsi usingelisema nchi haikuwa na kitu alipoichukua.Shame on him. Think Twice.

SAHIBA.
Pole sana ndugu yangu, Sidhani kama mwalimu alikataa watoto wake wasisome, baadhi ya watoto wake wanaelimu nzuri tu wala usitudanganye hapa. Tulikuwa na mtoto wa mwalimu ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha (Makongoro Nyerere) kupitia NCCR Mageuzi na kwasasa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kama kumbukumbu zangu ziko sahihi. Hivyo kusema hawana hata uwezo wa kuwa wakatibu kata hapo unatudanganya.

Nakuomba urejee historia ya Tanzania na uangalie hali ya kiuchumi, kielimu na hata huduma nyingine za kijamii ilikuwaje. Utakapopata picha halisi ilivyokuwa ndipo uendelee kunijibu hoja zangu

Asante
 
Waache kuleta za kuleta, Nyerere kaichukua nchi haina kitu kielimu wala kiuchumi, alifanya kila linalowezekana watanzania waweze kusoma bure toka chekechea mpaka chuo kikuu, tulikuwa hatuna hata chuo kikuu hata kimoja, lakini kwa kuanzia akatupatia vyuo vikuu viwili, na vyuo vingine kemkem kama ulivyo vitaja hapo juu. Hatuna shukran kwa kweli. Tulitaka vyuo vikuu viote kama uyoga kwenye nchi ambayo wakati huo haikuwa hata na viwanda, hata uzalishaji wa kueleweka mashambani haukuwepo, na biashara zilikuwa za kubangaiza. Alitutoa katika hali ya chini kabisa, lakini tumeishia kumlaumu. Alitujengea viwanda tumeua, mashirika ya umma yote tumetoa bure, alituhifadhia madini tumegawaa bure kama njugu, alituhimarishia bandari tumewapatia washkaji, alitujengea reli ya TAZARA tumeua, Mabenki tumeyatoa kama njugu hata kubaki na hisa ailimia 49 kwa ajili ya watanzania hatutaki. Kila kitu ambacho kingeimarisha uchumi wa mtanzania kiko mikononi mwa wanyonyaji. Jamani Nyerere alifanya mengi sana lakini kwa vile tulivyokuwa na shingo ngumu hatukuliona na badala ya kuungana nae kufanikisha hayo malengo tuliishia kuwa sehemu ya wahujumu. Kumbukeni nchi hii wakati anaichukua haikua na kitu cha kujivunia. Leo kuna vijiji ukienda kuna zahanati na mateki ya maji ambayo hayafanyi kazi lakini yalijengwa wakati wa Mwalimu. Eti tunasubiri tukaombe hela kwa wahisani ili tuiboreshe wakati pesa tuliyonayo tumewaachia mafisadi wakitanulia.

Mtoto wa mkulima alipelekwa chuo kukuu akilipiwa kila kitu. Mzazi alikua hajui cha nauli wala gharama za kumsomesha mtoto chuo kikuu zilikuwaje. Achilia mbali shele ya msingi na sekondari. Tulitegemea waliofaidi elimu nzuri ya wakati huo wangeiboresha zaidi kwa ajili ya kuimarisha utaifa na moyo wa uzalendo kwa watanzania lakini wapi wamekengekeuka na ndio sumu kali ambayo haitaki mtoto wa maskini apate elimu waliyoipata.

Tuache kulaumu adui yetu yupo madarakani. Tuna mwaka mmoja wa kufanya maamuzi mazito lakini yenye uchungu na matumaini kwa aajili ya nchi yetu

Nasema Nyerere apewe sifa kwa hilo na tumwache apmzike kwa amani huko aliko
Kwa kuongezea mnofu hapo.
SPM MGOLOLO,investment kubwa baada ya TAZARA, inchi hii kuwekeza.

Wasomi wetu wameiuza kwa dola moja( 1 USd).So as to facilitate the exchange 4 accounting purpose.Lakini kwa lugha rahisi ni kuwa mwekezaji kapewa BURE.

MLAANIWE WOTE MNAOMLAUMU HUYU MZEE, KWA MATATIZO TULIYONAYO KAMA TAIFA.

KWA MAKUSUDI MLIAMUA INITIALY KUJIFICHA NYUMA YA MADAI OH IMF, OH WOLRD BANK WANAMASHARTI MAGUMU.DAMN YOU.

SASA MNAHAMIA KWA MWALIMU...?????!!!!!

DAMN YOU.SAMAHANI MOD.NIMESHINDWA KUVUMILIA.
 
kwa kuongezea mnofu hapo.
Spm mgololo,investment kubwa baada ya tazara, inchi hii kuwekeza.

Wasomi wetu wameiuza kwa dola moja( 1 usd).so as to facilitate the exchange 4 accounting purpose.lakini kwa lugha rahisi ni kuwa mwekezaji kapewa bure.

Mlaaniwe wote mnaomlaumu huyu mzee, kwa matatizo tuliyonayo kama taifa.

Kwa makusudi mliamua initialy kujificha nyuma ya madai oh imf, oh wolrd bank wanamasharti magumu.damn you.

Sasa mnahamia kwa mwalimu...?????!!!!!

Damn you.samahani mod.nimeshindwa kuvumilia.

naunga mkono!
 
Nyinyi kweli mna kasoro hapa mnamsifia mtu ambaye hata watoto wake wa kuwazaa wanajuta kuzaliwa nae.Hawana uwezo hata wa kuwa makatibu kata kwa maana alishindwa hata kuitake care familia yake.Tumegubikwa Watanzania tuna maradhi yasiyo na tiba may hapo alipodai uhuru kwa manufaa yake leo hii bila fikra za Nyerere za kibinafsi usingelisema nchi haikuwa na kitu alipoichukua.Shame on him. Think Twice.

SAHIBA.

wewe sasa ndo mwenye kasoro.. eti hata watoto wake wa kuwazaa wanajuta? nani kakwambia wanajuta na hawakwenda shule? msipende kusema vitu msivyo na uhakika navyo, au mpaka wawe kama kina richardmonduli ndo mtasema " unaona hao ndo watoto wa mwalimu wanashika madaraka kama baba yao, NO, that's very wrong! MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO, mifano tunaiona wazi.. na UKATIBU KATA NI KITU GANI? umesoma ukawe katibu kata? hizo dharau sasa.. fikiri vizuri kabla hujaweka fikra zako kwenye maandishi watu wasome..
 
andindile,hivi unafahamu elimu ya makongoro na ana taaluma gani ? lakini hiyo mosi je uinafahamu katiba ya ccm ili kuwa kiongozi kinachohitajika ni kujua kusoma na kuandika tu ?
 
andindile,hivi unafahamu elimu ya makongoro na ana taaluma gani ? lakini hiyo mosi je uinafahamu katiba ya ccm ili kuwa kiongozi kinachohitajika ni kujua kusoma na kuandika tu ?
Nina taarifa kwamba alisoma Tabora Boyz baada ya hapo sina taarifa zaidi. Unaweza kunisaidia
 
Mkuu

We unataka alaumiwe nani Kenyata ? Na sio elimu tu the only thing yule Mzee anadeserve credit ni AMANI and nothing else.Misingi ya hili jumba letu katuwekea yeye na tunaona nyufa kila kona sasa cha kusifia ni nini ?

SAHIBA

Kama ulikuwa na umri wa kusoma wakati ule, wewe ulisoma wapi? Kama ulisoma Tanzania, ulishawahi kulipa ada, na unakumbuka ni kiasi gani? Ulikosa nafasi ya kwenda shule. Kama ni mtaala ulikuwa pungufu, ni masomo gani ambayo yalipungua wakati wa Nyerere mpaka kufanya elimu ikosekane?
 
Mkuu

We unataka alaumiwe nani Kenyata ? Na sio elimu tu the only thing yule Mzee anadeserve credit ni AMANI and nothing else.Misingi ya hili jumba letu katuwekea yeye na tunaona nyufa kila kona sasa cha kusifia ni nini ?

SAHIBA

Hata hiyo amani aliikuta, hakuna historia inayoonyesha kutokuwepo na Amani Tanganyika, kama ni vita zilikuwa na wageni.
 
Mwl Moshi,

Hivi ni kweli Mwl JKN alikataza shule za makanisa na shule za watu binafsi?.........im lost.....please enlighten me............

Alikamata, kwa nguvu, shule za Kanisa na shule za mashirika mengine. Ni pamoja na shule zifuatazo:

(1) St. Mary's College (ambayo baadaye iliitwa Tabora Girls)

(2) Assumpta College (ambayo aliamua kuiita Weru Weru)

(3) St. Francis College (ambayo aliamua kuiita Pugu)

(4) St. Andrew's College (ambayo aliamua kuiita Minaki)

(5) Mariam Collge (Shule ya Wasichana Morogoro)

(6) Umbwe Secondary School

Etc. Ni list ndefu sana.

Alikamata vile vile shule nyingine binafsi kama Lyamungo Secondary School na Alliance High School.

Mwalimu aliacha Seminari na shule chache za Kanisa (kama Kibosho na Kiraeni).

Mwalimu alikataza watu binafsi kuanzisha shule. Kwa kufanya hivyo, alidumaza sana Elimu ya Tanzania
 
Pole sana ndugu yangu, Sidhani kama mwalimu alikataa watoto wake wasisome, baadhi ya watoto wake wanaelimu nzuri tu wala usitudanganye hapa. Tulikuwa na mtoto wa mwalimu ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha (Makongoro Nyerere) kupitia NCCR Mageuzi na kwasasa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara kama kumbukumbu zangu ziko sahihi. Hivyo kusema hawana hata uwezo wa kuwa wakatibu kata hapo unatudanganya.

Nakuomba urejee historia ya Tanzania na uangalie hali ya kiuchumi, kielimu na hata huduma nyingine za kijamii ilikuwaje. Utakapopata picha halisi ilivyokuwa ndipo uendelee kunijibu hoja zangu

Asante

Kuhusu hii para ya mwisho:

Mimi nilikuwepo wakati wa Nyerere, mwanzo mpaka mwisho na nimeshuhudia kuharibika kwa kila kitu ukijuacho tulichokirithi kabla ya kukabidhiwa madaraka.

Hakuna ambacho hakijaharibika wakati wa nyerere ila kitu kimoja tu: Nalo ni Kanisa Katoliki.
 
Back
Top Bottom