Kwanini Watanzania mnapotoshwa kirahisi na Lowassa?

du EL kawajaza si mchezo. wakati wa kampeni 2015 maneno machache yatasemwa. NYERERE ALIMKATAA EL HAFAI KATU

khakha nyerere alimkataa lowasa kwa sababu ya mfumo wa ujamaa na utajiri wa lowasa,sasa hatupo tena kwenye ule mfumo tupo kwenye ubepari wa kimagharibi.
angalia marekani matajiri ndio wanaoongoza nchi,hata nyerere angefufuka leo akute ujinga unaoendelea leo angebadili mawazo.
 
Siamini masikio wala macho yangu. Watanzania tuna tatizo gani? Lowasa anawapotosha kirahisi namna hii?!? Jamani, mbona mnasahau kirahisi issue iliyomtoa Lowasa Uwaziri Mkuu ni mazingira ya rushwa kupitisha mradi wa Richmond? Hata kama ni kweli alimpigia simu JK kusema wavunje mkataba wa Richmond, haifuti ukweli kwama alipitisha Richmond kwa nguvu katika mazingira ya kifisadi. Hilo ndio hatia yake, na hilo ndilo kamati ya Mwakyembe ililiona na kulisema. Lowasa si mjinga, nahisi alipiga hiyo simu kumtega JK na kujilinda baadaye mambo yakigeuka, akijua wazi walifanya jambo la ufisadi Richmond! Yaani mnadhani Lowasa hakujua wahusika wa Richmond?

Lowasa kawatega, amechukua kakipengele kadogo katika suala la Richmond na wote mkakimbilia huko na kusahau lililo kubwa katika mkataba wa Richmond. Jamani, jamani, jamani, be smart!!!

Hivi kweli kwa kauli moja ya Lowasa basi leo mnaona yale yote yaliyo kwenye taarifa ya Kamati ya Mwakyembe hayafai tena?

Hivi mnamjua Lowassa nyie? Ulizeni watu waliofanya naye kazi akiwa Waziri Wizara ya Ardhi, hadi ikafikia Mtanzania mhindi kusema Lowasa ananuka rushwa! Mhindi kukutuhumu unanuka rushwa, yaani wewe ndio basi tena, maana ana taarifa zote za rushwa wanazotoa wahindi wenzake! Hivi mmesahau Lowasa alituhumiwa nini na Nyerere katika kugombea uraisi hata akafukuzwa toka ukumbini kama mtoto mdogo?

Jamani kweli nawasikitikia Watanzania. Wasahaulifu mno!
Hili la Lowasa halina mjadala ndiyo ni mla rushwa! nitakalokufa nalo miye JK ni powerhouse ya hiyo rushwa na mlarushwa mkubwa. Yle Mwakyembe aloficha yatabumburuka siku si nyingi akipona "polonium". Mtawafahamu wasanii wawili maarufu JK na EL. Hivi hamjiulizi hii network ya EL RA Jk ikweje? Hao ndio wadau wakuu wa Urais wa JK. Turnover ya Ritz1 alipomaliza university mwaka juzi na sasa imepata muujiza gani wa kutuna ghafla? Jiulize?? JK hajauacha mtandao wa majambazi yaliyomwingiza ikulu ili watukombe!!!
 
katika ccm mtu msafi ni mmoja tu nae ni edward ngoyai lowasa.kashfa ya richmond alitolewa kafara tu aliyeiingiza richmond nchini ni samweli sita wakati huo akiwa anaongoza kitengo cha uwekezaji alicho nacho emanuel naiko kwa sasa.
lowasa alijiuzulu akadai kisa ni uwaziri mkuu,wenye akili tunajua ishu ya makundi ndiyo iliyomhukumu lowasa.kamati yote ya bunge haina ujasiri tena kwa sababu wanajua walizungukwa wakaenda kichwakichwa na wakiambiwa warudie tena watakuja na majibu tofauti.
mwakyembe alisema kuna mabo waliacha kwa sababu serikali ingevunjika,sasa jiulize kama waziri mkuu ameshajiuzulu ni nani tena yuko juu yake ili serikali ivunjike?
wenye richmond wanajulikana na lowasa keshawataja.
ccm 2015 ikmsimamisha lowasa mimi na familia yangu tutakuwa wa kwanza kuipigia ccm kura.
naomba mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa auweke hapa tofauti na hapo ni majungu tu.
Naona wenye ccm yenu mmeanza kurudi kinyemela kwenye chama mnachokipenda!kumbe huku upinzani mlikuja kutuzuga na kutafuta hifadhi ya kisiasa tu na kumuandalia "mwanaume wenu wa shoka" makazi kama akivuliwa gamba ndio aje huku mlikokuwa mmejihifadhi sio?

Ndio mana hatufanikiwi-mamluki kibao haya bwana ngoja tuione ccm yenu na lowasa wenu itakavyokuwa,sisi wengine tutaendelea kuwa wapinzani daima,hatutajihusisha kushabikia siasa za ndani za ccm kwa kuwa zinawasidia ccm kuondoa attention ya wananchi kwenye opposition!

Wajanja tulishtuka zamani ndio mana hatuingii kichwa kichwa kushangilia upande wowote kwenye mambo yao,sisi tunataka wote wakae pembeni tuingie wapinzani na serikali ya mseto bila wao!
 
Unakosea sana kutujumuisha watanzania WOTE. Sema CCM nyie ndio watu wa ajabu sana, mtu mmoja tu aliye ndani ya chama chenu ndiyo anayumbisha chama kizima. Usiseme watanzania, sema wana-CCM.
Mkuu nakiri makosa....labda tuseme ujumbe huu ulilengwa kwa wale wanaoshabikia kile alichosema EL katika vikao vya CCM na kuona kauli aliyotoa ni ticket tosha ya kumsafisha madhambi yote yaliyofanya huko nyuma na kuyabatiza kuwa tuhuma za kusingiziwa.

Hapo ndipo nilipoona kweli kuna wengi kati yetu tuna matatizo ya kufikiri. Sikumfurahia sana Mkapa katika uongozi wake, ambao katika kufikiri kwake aliona ana haki ya kujichukulia chake kwa kuwa yapo mazuri aliyofanyia nchi yetu (na mabaya mengi tu aliyoifanyia nchi yetu), lakini mara nyingi kauli yake kwamba watanzania wengi (hasa walio CCM) ni wavivu wa kufikiri ni moja wapo ya chache alizozitoa ninazomuunga mkono.

Na wale wanaosema Nyerere alimwona Mkapa kuwa safi, nitarudia kauli yangu kwamba ni kweli Mkapa alikuwa safi hadi siku Nyerere alipokufa, ndio alipooanza kuonyesha rangi za ke za kweli (true colours). Kuna mengi sana ambayo Mkapa asingethubutu kufanya ikiwa Nyerere angeendela kuwa hai, huo ndio ukweli wa mambo.
 
katika ccm mtu msafi ni mmoja tu nae ni edward ngoyai lowasa.kashfa ya richmond alitolewa kafara tu aliyeiingiza richmond nchini ni samweli sita wakati huo akiwa anaongoza kitengo cha uwekezaji alicho nacho emanuel naiko kwa sasa.

lowasa alijiuzulu akadai kisa ni uwaziri mkuu,wenye akili tunajua ishu ya makundi ndiyo iliyomhukumu lowasa.kamati yote ya bunge haina ujasiri tena kwa sababu wanajua walizungukwa wakaenda kichwakichwa na wakiambiwa warudie tena watakuja na majibu tofauti.

mwakyembe alisema kuna mabo waliacha kwa sababu serikali ingevunjika,sasa jiulize kama waziri mkuu ameshajiuzulu ni nani tena yuko juu yake ili serikali ivunjike?

Wenye richmond wanajulikana na lowasa keshawataja, ccm 2015 ikmsimamisha lowasa mimi na familia yangu tutakuwa wa kwanza kuipigia ccm kura. Naomba mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa auweke hapa tofauti na hapo ni majungu tu.

Wachagga bwana...ile MOU ya Lowassa na Mbowe vipi?
 
"Alibi" ya Lowassa kuwa alimpigia simu Rais kutaka kusitishwa kwa Richmond baada ya yeye kugundua mapema kua ilikua na dosari haileti mantiki yeyote zaidi ya kumuonyesha lowassa kuwa ni mpiganaji tu wa kisiasa na wala siyo kiongozi mahiri wala safi.

kama Rostam ndiyo anatajwa kuwa msukaji mkubwa wa mpango wa Richmond (mpaka kusafiri Marekani kutafuta hawa "wawekezaji") na ni Rostam huyu huyu aliyemsukuma Kikwete amweke Lowassa Waziri Mkuu na ni Rostam huyu huyu swahiba mkubwa kisiasa na kibiashara na Lowassa itakuaje Lowassa anayeaamini siasa za kulindana amtose Rostam kwa kumshauri kwa uwazi mkubwa Kikwete kuwa Richmond ivunjwe?

hii inanipa jibu moja tu Lowassa na Rostam walijua lazima wawe na kinga kama hili suala feki ikijulikana na hapo ndipo walipopiga hii simu kwa JK( kama "alibi") akiwa anakula "raha nje ya nchi "anasherehekea" bado ushindi wa Urais uliosababishwa na hawa maswahiba wake huku wakiwa wanaonyesha wasiwasi Kidogo wa mkataba huu (huku wakijua Rais ana maslahi yake katika hili na atakua mzito kukubaliana moja kwa moja na hili la kusitishwa kwa mkataba huku na wenyewe wakiwashinikiza wahusika wengine hapa Tanzania kuupitisha mkataba ).

Unataka kuniambia katika suala zima hili Lowassa alimpigia simu boss wake simu moja tu tena akiwa nje ya nchi kuonyesha wasiwasi wa dili hili ambalo yeye alikua hapati "vijisenti" vyetu vyovyote na kuna hatari ya kutumiwa yeye na ofisi yake kumuaribia kisiasa kama ikija gundulika? Lowassa ana akili zaidi ya hizi na hii inaonyesha kuhusika kwake m1 kwa m1 na Richmond na kwamba hili aliloongea jana ni "alibi tu iliyopikwa kama tahadhari ikiwa Richmond ingekuja kunuka....

Na hata kama hii simu siyo alibi yake mh lowassa na Kikwete alihusika 100% lakini hii haimfanyi Lowassa kuwa msafi kwani kama alijua uozo kwa nini aliingiza ofisi yake katika mchakato wa Tender pale TANESCO kinyume na taratibu zilizopo, (hii inamfanya Lowassa kuwa mshiriki mkuu hata kama alikua anatumiwa na Kikwete).. hapa hawezi kuwa exonerated na uchafu wa Richmond kwenye macho na hukumu ya watanzania..​

khakha nyerere alimkataa lowasa kwa sababu ya mfumo wa ujamaa na utajiri wa lowasa,sasa hatupo tena kwenye ule mfumo tupo kwenye ubepari wa kimagharibi.
angalia marekani matajiri ndio wanaoongoza nchi,hata nyerere angefufuka leo akute ujinga unaoendelea leo angebadili mawazo.

picha yako inaonyesha ni mshamba na huna elimu...mfumo wa ujamaa 1995? ujamaa ulikwisha na mwinyi pale 1985 na siyo 1995 nafikiri hata sababu ya kung'atuka Nyerere hujui kabisa wapumbavu kama nyinyi ndiyo Lowassa anawapenda na kuwatumia ipasavyo kwa ujinga na ujira mdogo sana
 
Mwambie Lowasa ataje mali zake na aeleze alizipataje!

alizipata kama wewe ulivyozipata

kwanza jiulize EL kaanza lini siasa? unaelewa nafasi ya uwaziri wanalipwa sh ngapi kama mshahara na posho?

je ulitegemea pesa anayopata aitumie kwa lipi? akiwekeza tatizo,akinywea mtasema,akihong mtasema,akikaa bila kitu mtasema ,binadamu haishi kusema
 
katika ccm mtu msafi ni mmoja tu nae ni edward ngoyai lowasa.kashfa ya richmond alitolewa kafara tu aliyeiingiza richmond nchini ni samweli sita wakati huo akiwa anaongoza kitengo cha uwekezaji alicho nacho emanuel naiko kwa sasa.
lowasa alijiuzulu akadai kisa ni uwaziri mkuu,wenye akili tunajua ishu ya makundi ndiyo iliyomhukumu lowasa.kamati yote ya bunge haina ujasiri tena kwa sababu wanajua walizungukwa wakaenda kichwakichwa na wakiambiwa warudie tena watakuja na majibu tofauti.
mwakyembe alisema kuna mabo waliacha kwa sababu serikali ingevunjika,sasa jiulize kama waziri mkuu ameshajiuzulu ni nani tena yuko juu yake ili serikali ivunjike?
wenye richmond wanajulikana na lowasa keshawataja.
ccm 2015 ikmsimamisha lowasa mimi na familia yangu tutakuwa wa kwanza kuipigia ccm kura.
naomba mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa auweke hapa tofauti na hapo ni majungu tu.

Watanzania tuna hali ngumu sana kiuchumi. Mfumuko wa bei unakimbilia 20%. Kwa mazingira haya, na ukweli kwamba EL na washirika wake wana pesa nyingi sana za wizi, achilia mbali sehemu ya tozo la Dowans, ni hakika atapata wafuasi. Kwa kuwa umeamua kuwa miongoni mwao, nakupongeza kwa kuchumia tumbo lako na familia yako.

Lowasa hajawahi kuwa safi, hata kuwa msafi na nina uhakika ccm wakimpa bendera ya kugombea utakuwa ni ukombozi kwa taifa. Lowasa na JK watakuwa wamefanikisha zoezi la kuiua ccm, na hii ni habari njema kwa watanzania.
 
katika ccm mtu msafi ni mmoja tu nae ni edward ngoyai lowasa.kashfa ya richmond alitolewa kafara tu aliyeiingiza richmond nchini ni samweli sita wakati huo akiwa anaongoza kitengo cha uwekezaji alicho nacho emanuel naiko kwa sasa.
lowasa alijiuzulu akadai kisa ni uwaziri mkuu,wenye akili tunajua ishu ya makundi ndiyo iliyomhukumu lowasa.kamati yote ya bunge haina ujasiri tena kwa sababu wanajua walizungukwa wakaenda kichwakichwa na wakiambiwa warudie tena watakuja na majibu tofauti.
mwakyembe alisema kuna mabo waliacha kwa sababu serikali ingevunjika,sasa jiulize kama waziri mkuu ameshajiuzulu ni nani tena yuko juu yake ili serikali ivunjike?
wenye richmond wanajulikana na lowasa keshawataja.
ccm 2015 ikmsimamisha lowasa mimi na familia yangu tutakuwa wa kwanza kuipigia ccm kura.
naomba mwenye ushahidi wa ufisadi wa lowasa auweke hapa tofauti na hapo ni majungu tu.

Waraka wa Godbless Lema wakati anaenda jela ulisema ......Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa. NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi. Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopatataarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani
wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao,
nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya
biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu,
Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe
yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.
Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani
inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na
mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote,
mwenye cheo chochote........
Haisaidii kusema mimi sio fisadi wakati ufisadi umefanyika mbele ya macho yako na UKAKAA KIMYA.

1. Lowasa alijua ufisadi uliokuwa unaendelea Akakaa kimya (eti alimpigia simu Raisi lakini maelekezo ya kupitisha akayatoa yeye) Kama hakuwa sehemu ya huo ufisadi mbona PCCB walipomsafisha alihangaika sana kuuzima mjadala wa Richmond? unataka kutuaminisha kuwa alikuwa hajui alichotaka kuficha. Mtu wa aina hii ambaye yupo tayari kuficha ufisadi unaotutafuna watanzania kwa kiasi hiki hafai kuwa hata kiongozi wa familia yake. Leo hii watanzania tunadaiwa zaidi ya Bilioni 111 kwa sababu Lowasa aliamua kukaa kimya wakati wezi wanafanya mikakati ya kutuibia. halafu unadai mwenye ushahidi atoe. Pamoja na ushahidi walionao akina Mwakyembe lakini ushahidi wa yeye kukaa kimya katikati ya wizi mkuu namna hii unatosha khoji uzalendo na mapenzi yake kwa watanzania masikini na hoi.
2. Lakini kama hilo halitoshi ukimya wake umetufanya tumchague huyo anayemlaumu sasa hapo ametusaidiaje? Kama aliamua kukaa kimya tangu mwanzo, basi na aendelee kukaa kinya maana kwa sasa haitusaidii zaidi ya kutupandisha hasira tu.
 
Naam...Lowasa si mtu safi! ila km kipimo ni Kikwete nitakua wa kwanza kumpigia kura Lowasa!...kwanini watu wazima wanafanya mchezo wa kutukanganya? Kwanini wanachezea akili zetu...vyovyote iwavyo,ni dhahiri miaka miwili ya utendaji wa Lowasa akiwa waziri mkuu Tanzania ilikua nchi tofauti na miaka ya utumishi wa Kikwete ambayo ameshindwa hata kuonya vijana wadogo wadogo ndani ya chama ambao hawakufunzwa maadili!
 
Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa ndugu zangu wa Nchi hii pale unapokosa namna ya kujenga hoja halafu unaanza kuwalaumu Watanzania inashangaza sana pale unaposema eti Watanzania wanapotoshwa kirahisi halafu wewe unajitoa humo kwamba wewe ni zaidi ya hao Watanzania ni kwa nini nawe pia usifikiri kuwa kwa hilo unaloliamini nawe pia umepotoka ni kwa nini utake kuonekana kwamba wewe ndiye uliye sawa kuliko Mtanzania mwingine yeyote awaye!

Mi nadhani busara ni kutumia nafasi yako kujenga hoja yako ni si kuwashawishi Watanzania au kuwalazimisha kuwa hawaki sawa ila wewe ndiye uliye sawa hii ni dharau ya ajabu. Wapo wanao amino na watazidi kuamini kuwa Liwassa is of no problem na wengine hawataamini hivyo sasa usiwe kama Litmus paper acha fikra zitofautiane wewe huwezi kuwa bora mpaka kufikia hatua ya kudhani kuwa Watanzania wote wanapotoka eti kisa wanamtetea Lowassa nenda mbele zaidi wapo waliodhani yale ya Richmond yalikuwa ya kweli per se ila juzi wamethibitishiwa ukweli pasipo shaka sasa sababu ni ipi wao wasibadili mitizamo yao!!!!! Tujaribu kupunguza UDIKTETA wa fikra na mawazo tuishi tukijua hata wengine wana uhuru wa kufikiria kama watu wengine......
Hoja hazitatusaidia kitu ktk UKOMBOZI WA TAIFA LETU,tunachotaka ni MAFISADI WOTE waliotuletea UMASIKINI watanzania wakamatwe,na wafikishwe ktk vyombo vya sheria ili haki ITENDEKE,hayo mambo ya HOJA ZENYE MASHIKO hayatatusaidia,afterall kila mtu ana hoja.
 
hapo umenena mdau nawashangaa watz wanaofurah kugombea Urais kwa lowasa 2015. Chonde chonde hatufai
 
Mi na haya magamba yenu yaliyokauka mnataka kuyafanya yawe mabichi kwa kuyamwagia maji siwaelewi mnataka kusema nini hayawezi tena kuwa mabichi asilia yatajuwa mabichi kwa kuforge tu mwisho yataoza tu wazee haya jamani nyie endeleeni kuyamwagia maji lakini kumbukeni mkiendelea mnayaozesha kabisa
 
Sio wewe tu mkuu.
Wenye utimamu woote tutampigia kura na atakayesimamia zoezi la kuhesabu na kusimamia kura zetu atakuwa Allah...

Tuseme inshaalah

Hakuna aliyemsafi kati yao, kwn wote ni wachafu kwa sababu ya sela zao
 
Back
Top Bottom