Lowassa hakuwa malaika, alikuwa kiumbe kama wengine na alikuwa na dosari zake. Mungu amuweke pema peponi

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Wacheni ujinga na unafiki, Leo Lowassa katangulia WOTE tunampaka maradhi na kumfukiza Udi. Tuache unafiki. Lowassa alikuwa KIONGOZI mzuri lakini alikuwa na makandondo yake.

1. Lowassa Akipokuwa PM, alikuwa mla Rushwa Mkubwa Sana hata akapewa jina la MR 10%.
2. Aliua watu KISIASA haswa wake waliotaka kuingilia siasa zake za ufalme wake WA Monduli.
3. Amepora Ardhi nyingi Sana za watu, wanavijiji na hata Ardhi ya Serekali. MFANO: kapataje hiyo Ranch ya huko Tanga, Ardhi zote za Arusha Mini anazimiliki yeye na Familia Take. Yeye ndiye mmiliki mkubwa WA Ardhi Arusha na Manyara.
4. Ushirika WA yeye na Mheshimiwa Rostam Aziz unahitaji Magnifying Glass, haswa walivyoipata share za VODACOM.
5. Richmond Inamhusu Sana Lowassa, Rostam na grange Lao, ushahidi uko wazi na ulikuwepo Wizara ya Nishati.

Kuna mengi yake Marehemu Mazuri, lakini hakuwa msafi hata kidogo, na tuache huu ujinga WA kutaka kuifanya yeye alikuwa Malaika pekee. WENGI LEO WANAUTUMIA MSIBA WAKE KAMA KETE YA KISIASA, NA PIA KUTUMIA FURSA KUWADHALILISHA WENZAO KUWA WALIMTENDEA MABAYA LOWASA, ULA WAO NDIO WAZURI, SIASA ZA KUPAKANA MAVI
 
Back
Top Bottom