Kwanini wanawake wanapenda kupewa fedha na wanaume?

Nadhani pia hili ni swali la kujiuliza nyie wanaume maana kwa namna moja au nyingine mmeshakuwa na wapenzi maishani mwenu hadi sasahivi. Je wanawake wote ulitoka nao walipenda kupewa pesa? Kumbuka kuna wengine wanaomba kabisa,utasikia honey nina deni au nataka kununua simu na vitu kama hivyo.
Wewe mwanaume kama hupendi kuombwa pesa na mwanamke si unaweza kumwambia kuwa huna hiyo tabia halafu uone itakuwaje kama atakuacha humpi pesa au laa!
Kwenye ndoa ni zaidi ya kpenda kupewa pesa,mwanaume ni kichwa cha familia tena wengine hata kama wake zao wanawazidi kipato wanapenda kuonekana wapo fiti financial ili hata watoto na ndugu wengine wajue na kumheshimu baba kuwa ndo anagharamikia familia.
 
Mzalendo
Hapo itakuwa safi sana ujue kuwa wanawake nao ni watoaji wazuri wa pesa.

BelindaJacob,

Ha ha ha! Taabu ni jinsi ya kuwapata majimama! Ila ingekuwa poa sana na experience nzuri!

sasa je itabidi nimwombe au saa yoyote unakatiwa tu michuzi???

Ila ngumu kama haujazoea!
 
BelindaJacob,

Ha ha ha! Taabu ni jinsi ya kuwapata majimama! Ila ingekuwa poa sana na experience nzuri!

sasa je itabidi nimwombe au saa yoyote unakatiwa tu michuzi???

Ila ngumu kama haujazoea!

Ni kweli sijui wanapatikanaje,nadhani kama watu wengine wanavyokutana kimapenzi. Hawa wanatoa sana hela na mara nyingi wanakuwa na vijana wadogo kiumri japo wanafurahi vizuri tu!
Ila pia kuna wanawake wengine huwapa pesa wanaume wao,yani kuna bf's wengine ukiacha kuwa na kazi nzuri au la lakini wanaomba pesa kwa gf's zao.
kwahiyo suala la pesa kwenye mapenzi ni gumu sana japo sisi wanawake tunaonekana tunapenda sana kupewa pesa na wanaume..
 
Womenofsubstanc,

Naheshimu sana michango yako ila 90% ya madem Tz yaani wanatarajia bwana uwe na pesa..hamna cha gender hamna cha mfumo dume au jike!

Love Bongo iwe true love or otherwise = pesa!

Ipo mifano mingi madem baada ya kupata shule, kazi nzuri na pesa wakawatosa waume zao wasio na pesa!

Kwa Bongo.. wanawake husema Pesa ni sabuni ya Roho!

Pesa !!! Pesa!! Pesa!!
Tena unaweza kumsomesha mkeo akapata kazi baada ya hapo anakuacha kufuata wanaume wenye fedha.Halafu mbona wanaume wasijiuze kwa wanawake wenye fedha kama changudoa wanavyofanya kwa wanaume.Vilevile changudoa wengine wanauwezo mkubwa tu kifedha.Labda wanawake wanapenda sana kupewa kuliko kutoa,maana hata kwenye mapenzi wanadai anayefaidi ni mwanaume.
 
Unapozungumzia 'kupenda kupewa' si suala la wanawake tu, hata wanaume nao 'hupenda kupewa' vilevile... tofauti inakuja wanapenda kupewa nini
Wanaume hupenda kupewa na wanaotakiwa kutoa hawataki hadi utoe fedha/takrima,lakini wanaume wao wapo tayari kutoa bila malipo.Mbona hivyo vitu Mungu alivitoa bure kwa mwanaume na mwanamke kwanini mwingine atake kuuza?hata mahari ni ya nini wakati wawili huungana kuwa kitu kimoja?
 
Ndio atakuwa na kipato lakini usimlazimishe kumpa majukumu. Kama mwanamke yeye mwenyewe akiona inafaa kutoa pesa kwa familia basi ni uamuzi wake tena mzuri. Kwa hiyo ni hiyari yake sio lazima.

Honestly,something is wrong somewhere!
 
mie naona hili swala la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke ni wajibu wa mwanaume. Hata kama mkeo au gf ana kipato chake lkn ww mwanaume lazima utoe pesa kwa mkeo. Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote na pesa ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. Hivyo kama mwanamke akiwa na utu tu ule wa kumpenda mwenzio ndio anaweza kumpa pesa mwanaume wake, au kama mume hana kazi au mgonjwa hapo mwanamke pia anweza kumsaidia mwanaume hivyo ni hiyari ya huyo mwanamke. Lkn mwanaume lazima atoe pesa kwa mwanamke iwapo anazo, haijarishi kama mke ana kazi au lah!

Duh hapo Pretty kweli umeniacha cha Mwanaume lazima atoe pesa kwa mke awe na kazi au lah je kweli huu ndo usawa ambao tunauhitaji?Wewe subiri wakusikie wenzetu walioenda Beijing...Nadhani haki sawa kwa wote na si usawa cha mwanamke ni chake na cha mwanaume ni cha wote kazi kweli kweli hapo!
 
Suala la mwanaume kuota pesa kwa mwanamke ni utashi wa mtu mwenyewe! Wanaume wengi huona kuwa ili waweze kum-possess mwanamke ni kutoa pesa ili mwanamke asirubuniwe na m/mme mwingine.

Pili sikatai kuwa kuna wanawake ambao pia huenda/hukubali mwanamme mwenye pesa, nadhani hili pia ni jukumu la mwanaume kumchunguza mtu anayemtaka, kama yuko kwako kwa ajili ya pesa rtu why should u put up wiht such a woman?? After all wanaume wengi huona sifa kuwa na demu wa status ya juu .. mambo ya woolworth ... steers... Q Bar n.k So jinsi mwanaume anavyoji-present kwa mwanamke ndivyo naye atakavyomchukulia.

Jingine, kama wasomaji wa misaaafu na biblia, jukumu halisi/kubwa la mwanaume kwa mwanamke ni kumtunza au ku-provide. Na namna ya kumtunza ni kuhakikisha kuwa anapata mahitaji yakle yote kulinganan na uwezo wako.

Lakini hatukatai pia kuwa kuna wanao-exagerrate hii na kuharibu maana halisi ya mapenzi na matunzo..
 
Nakwanini mwanamke anapenda sana kupokea kuliko kutoa alicho nacho?

Ni mawili ........ama hao wanawake ambao wewe umekutana nao ni wale wasiopenda kutoa......au labda wewe ni mmoja wa wale wanaume msiopenda kupokea vya wanawake.Wanawake tunatoa sana tu!
 
mie naona hili swala la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke ni wajibu wa mwanaume. Hata kama mkeo au gf ana kipato chake lkn ww mwanaume lazima utoe pesa kwa mkeo. Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote na pesa ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. Hivyo kama mwanamke akiwa na utu tu ule wa kumpenda mwenzio ndio anaweza kumpa pesa mwanaume wake, au kama mume hana kazi au mgonjwa hapo mwanamke pia anweza kumsaidia mwanaume hivyo ni hiyari ya huyo mwanamke. Lkn mwanaume lazima atoe pesa kwa mwanamke iwapo anazo, haijarishi kama mke ana kazi au lah!

this type of thinking!!! I reserve my comments!! but we have a long way to go....
 
Ni mawili ........ama hao wanawake ambao wewe umekutana nao ni wale wasiopenda kutoa......au labda wewe ni mmoja wa wale wanaume msiopenda kupokea vya wanawake.Wanawake tunatoa sana tu!

Ni kweli WoS. Kuna suala la watu kupenda kuchukulia mambo kijumla jumla (generalise) kuliko kuangalia hali halisi. Pia kuna suala la kipato. Kama mwanamke hana kipato na mwanamume ana kipati basi hapa kutakuwa hakuna hoja. Hata hivyo kuna wanawake ambao wana tabia mbaya. Wao ni kudai pesa tu bila kuangalia kipato cha mume. Ndo maana maeneo mengine nyumba haikaliki kama baba hajanunua khanga za siku kuu. Hata hivyo bado lawama nawatwisha wanaume. Kuna wale ambao wanawaficha wake zao kipato chao. Na inapotokea kuna mgeni (hasa ndugu wa mke), basi baba atajitutumua hata ikibidi kukopa. Kwa hiyo mama anadhani jamaa anazo. Ndo maana hata nguo mpya za siku kuu lazima zinunuliwe tu. Pia kuna wanaume wanaondekeza mambo ya kizamani sana. Lazima amwooneshe mpenzi wake kwamba ana pesa wakati wote hata kama analazima kuwapiga mzinga (kuomba) washikaji zake. Hilo pia linasababisha mwanamume ajione anakuwa ATM wakati yeye ndiye anajifanya BoT!! Hata hivyo lazima tutambue kuwa "lazima uliwe ili na wewe upate kula au kula ili uliwe".
 
Back
Top Bottom