Kwanini wanawake wanapenda kupewa fedha na wanaume?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Imekuwa ni kawaida wanaume kuwapa wanawake fedha aidha kwa kuwa ni marafiki au wachumba au wanandoa.Mwanamke katika ndoa hupenda kutumia fedha zake kwa mambo binafsi na mambo kama hayo.Je kama wanawake hawatabadilika si ni ngumu katika harakati za mapinduzi ya mambo ya jinsia?
 
Kwanza lazima ukubali kuwa si wanawake wote wako hivyo.

Wanawake wengi hawana nguvu za kiuchumi kama wanaume.Mfumodume umewafanya wasiwe na uwezo wa kiuchumi ingawa shughuli wanazofanya zina uzalishaji mkubwa kiuchumi.Kwa kweli wanawake hata nchi zilizoendelea wameanza kufanya kazi katika mfumo rasmi (na kuacha kuwa mama wa nyumbani) kuanzia miaka ya 1950 tu, mara baada ya mfumuko wa uchumi Marekani na Ulaya baada ya vita vikuu vya pili kuhitaji wafanyakazi zaidi viwandani na kazi nyingi zimekuwa typical low wages kama u secretary, kazi za ufundi viwandani na ualimu wa sule za chini.

Ukija katika mazingira ya Tanzania, amabako hatukuwa na uchumi uliofungamana na ule wa dunia kwa sana mpaka miaka ya karibuni (wengine watasema hata sasa bado) wanawake wamekuwa kwa kiasi kikubwa mama wa nyumbani, wakulima na wafanyabiashara ndogondogo, na wafanyakazi wa ofisini wengi wapo katika ngazi za chini. Hili linabidi kubadilishwa.

Kwa hiyo kihistoria wanawake hawakuwa na nguvu ya kiuchumi, lakini wana "bargaining power" kubwa kwa kuwa ukiacha mambo ya pesa, alichonacho mwanamke mwanamme anaonekana kukitaka sana kuliko alichonacho mwanamme. Mwanamke anayetafuta mwanamme atampata in a heartbeat, mwanamme anayetafuta mwanamke itabidi ampiganie, kwa hiyo hapa kanuni za soko linaloendeshwa na demand and supply, utility of service, scarcity na psychology za machismo zina apply kuwafanya wanawake wengi waone ni haki yao kupewa pesa na wanaume.

Lakini katika uchumi wa sasa unaobadilika, ambapo unaweza kuwa na wanawake wengi wanaofanya kazi zenye malipo na heshima kubwa kuliko wanaume, hasa sehemu za mjini, kama mwanamke anaendekeza haya atakuwa anafanya kwa tamaa au mazoea tu.

Kuna wanaume ambao kutokana na machismo effect hii hawawezi kukaa na mwanamke mwenye kazi au hela zaidi yao, of course utakuwa na wale wanaopenda mteremko pia, lakini there is no free lunch in this world.
 
Sidhani kuna popote imewekwa kuwa mwanamke lazima apewe pesa na mwanaume.Nadhani ni kutokana na unequal power relations ambapo mwanaume anatarajiwa na jamii kuwa juu ya kila kitu na mwanamke kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume ndipo tunaona mwelekeo huu.

Na kama tutarudi nyuma katika historia ya maisha yetu miaka ya nyuma ilikuwa ni kama desturi kama si kawaida kwa mwanaume kumiliki mali na kila njia ya uchumi kiasi kuwa ilitarajiwa na kuaminika kuwa mwanamke hana kitu japo alikuwa na mahitaji.Hapo ndipo mwanaume alionyesha uanaume wake kwa kutoa si pesa tu bali hata vitu vingine ikiwa na pamoja na ofa za hapa na pale.

Maendeleo na mchanganyiko wa jamii umebadilisha mambo kwa kiasi japo si sana na ndiyo maana hata sasa kuna wanawake wanawapa wanaume ( waume au wapenzi au marafiki zao) pesa na vitu vingine.

Hii ni kwa kifupi sana ukitaka zaidi utapata kadiri mada itakavyochangiwa.
 
Womenofsubstanc,

Naheshimu sana michango yako ila 90% ya madem Tz yaani wanatarajia bwana uwe na pesa..hamna cha gender hamna cha mfumo dume au jike!

Love Bongo iwe true love or otherwise = pesa!

Ipo mifano mingi madem baada ya kupata shule, kazi nzuri na pesa wakawatosa waume zao wasio na pesa!

Kwa Bongo.. wanawake husema Pesa ni sabuni ya Roho!

Pesa !!! Pesa!! Pesa!!
 
tena wanaume wabinafisi sana ukiwa nacho unampa tena kwa moyo mmoja wewe ukiishiwa siku huna kazi au nini basi hela atakayolkupa atakusimanga nayo weee.wanawake huwa wana moyo wa upendo wa kweli wala hajuti kumpa mpenzi wake ampendaye kitu kwani amempa kwa moyo mweupe,mwanaume sasa kama gari atakunyanganya akikasirika.mh wanaume kwa roho ya kwa nini
 
Nafikiri kuna kila tabia katika kila jinsia.

Kinachozungumwa hapa ni tabia inayoonekana kuzidi sana katika jinsia fulani, kuna watu wanasema "wanawake ni wambeya", hiyo haina maana kuwa hamna wanaume wambea, na wala haimaanishi kwamba hakuna wanawake wasio wambea, lakini labda kwa mujibu wa maoni ya watu hawa, ukiweka kundi la wanaume na kundi la wanawake utakuta wambea wengi katika kundi la wanawake, sasa swali linakuja kwa nini kunakuwa na wamea wengi katika wanawake.

Vile vile katika swala hili lililoulizwa.
 
mie naona hili swala la mwanaume kutoa pesa kwa mwanamke ni wajibu wa mwanaume. Hata kama mkeo au gf ana kipato chake lkn ww mwanaume lazima utoe pesa kwa mkeo. Kumbuka pesa ya mwanaume ni kwa familia yote na pesa ya mwanamke ni ya kwake mwenyewe. Hivyo kama mwanamke akiwa na utu tu ule wa kumpenda mwenzio ndio anaweza kumpa pesa mwanaume wake, au kama mume hana kazi au mgonjwa hapo mwanamke pia anweza kumsaidia mwanaume hivyo ni hiyari ya huyo mwanamke. Lkn mwanaume lazima atoe pesa kwa mwanamke iwapo anazo, haijarishi kama mke ana kazi au lah!
 
Huo ni uroho! Naelewa enzi hizo labda ambapo mwanamke alikua hafanyi kazi ya kuingiza kipato, lakini kama anaingiza kipato kwanini tugawane changu tu?
 
Huo ni uroho! Naelewa enzi hizo labda ambapo mwanamke alikua hafanyi kazi ya kuingiza kipato, lakini kama anaingiza kipato kwanini tugawane changu tu?
wala sio uroho, nadhani mlishaambiwa na muumba, mwanaume atakula kwa jasho lake na mwanamke atazaa kwa uchungu. hivyo swala la mke kutumia pesa kwenye familia ni uamuzi wake sio lazima.
 
Womenofsubstanc,

Naheshimu sana michango yako ila 90% ya madem Tz yaani wanatarajia bwana uwe na pesa..hamna cha gender hamna cha mfumo dume au jike!

Love Bongo iwe true love or otherwise = pesa!

Ipo mifano mingi madem baada ya kupata shule, kazi nzuri na pesa wakawatosa waume zao wasio na pesa!

Kwa Bongo.. wanawake husema Pesa ni sabuni ya Roho!

Pesa !!! Pesa!! Pesa!!

Ni kweli mkuu wangu, hii ya kuombaomba pesa ni kawaida kwa wanawake wengi wa ki-TZ, Yaani kwa ujumla wanaona ni haki yao kupewa ela na usipotoa hehehe..utashikiwa kibwebwe na utaambiwa huna mapenzi weye..mwishowe kibuti!

Nakumbuka enzi zile za ujana, nilipata kuwa na mwanadada mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi. Pamoja na kujua status yangu kipindi hicho ilikuwa ni mwanafunzi (sina kipato cha uhakika), alipoona nipo kimya kuhusu 'chenji', akaamua kuniingia kwa gia ya kuniomba mikopo midogomidogo isiyo na riba. Alikuwa anafanya makusudi kabisa akijua nikimpa nitaona soo kukumbushia deni.
 
hebu badilisha sentensi yako iwe: kwanini wanaume wanapenda kuwapa wanawake hela? unajua wanaume wengi wa bongo wanadhani kwa kumpa mwanamke hela basi ndo uhakika wa pezi na wanapoonyesha hilo katika siku za mwanzo za mapenzi ndo wanawake wengine wanachukua nafasi ya kumtumia na kumuacha maana at the end of the day mwanaume atamtumia tu na kumuacha kwa pesa chache alizo muhonga mwanzo.. ila tusisahua kuwa pia WANAUME WANAPENDA KUPEWA HELA NA WANAWAKE!!
 
wala sio uroho, nadhani mlishaambiwa na muumba, mwanaume atakula kwa jasho lake na mwanamke atazaa kwa uchungu. hivyo swala la mke kutumia pesa kwenye familia ni uamuzi wake sio lazima.

Pretty, u r pretty right kama tutaangalia katika mtizamo wa kiimani -
Ni kweli mwanaume alipewa jukumu la kutafuta na mwanamke naye akapewa jukumu la kuijaza dunia tena kwa maumivu makali ambayo wanaume hata hawayajui na hawatakaa wayajue labda kuyahisi tu.Hivyo mtoa mada elewa tu kuwa haya mambo ya kupewa, kutoa na kupokea yana dimensions nyingi.
Kinachoshangaza ni kuwa wanaume haohao wengi wao huwa wa kwanza kujitutumua kuonyesha wanazo.. na wanawake nao hawachelewi kuzichangamkia.Kadhalika kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo awali, wanaume nao hupenda kupewa hata kama siyo pesa.Ni siku hizi ndiyo tunaona malalamiko sana kutoka kwa wanaume kudai ati wanawake wanapenda watu wenye pesa.Ukweli ndugu kuna wanawake wengi sana wameumizwa kwa kujifanya kupenda mtu hohehahe asiye na mbele wala nyuma na kuwekeza mali , akili na mapenzi.Mwanaume huyo apatapo vijisenti humdharau yule mwanamke aliyemtoa tongotongo na kusaka vimwana wengine ili aonekane kuwa amekuwa siku zote matawi ya juu! Ndiyo maana wanawake wengi sasa hawataki kurudia makosa... wanataka mtu mwenye nazo ili hata kama atabadilika basi angalau asiwe na majuto mengi sana.Ni hapahapa tu iliwahi kujadiliwa mada ikitakiwa ushauri kwa mwanamke aliyepoteza muda hadi kumsomesha mwanaume na mwanaume alipoona mwanga akatafuta mwanamke mwingine na kumtelekeza yule aliyemhifadhi wakati wa shida!

Nadhani cha msingi siyo kujiuliza kwanini wanawake wanapenda kupewa pesa bali tujiulize kwanini vigezo na vipaumbele katika mapenzi au mahusiano vimekuwa jinsi vilivyo sasa.( wanaume na hata wanawake wana vigezo vyao wanapoamua kuingia kwenye mahusiano na ni haki yao)
 
Ni kweli mkuu wangu, hii ya kuombaomba pesa ni kawaida kwa wanawake wengi wa ki-TZ, Yaani kwa ujumla wanaona ni haki yao kupewa ela na usipotoa hehehe..utashikiwa kibwebwe na utaambiwa huna mapenzi weye..mwishowe kibuti!

Nakumbuka enzi zile za ujana, nilipata kuwa na mwanadada mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi. Pamoja na kujua status yangu kipindi hicho ilikuwa ni mwanafunzi (sina kipato cha uhakika), alipoona nipo kimya kuhusu 'chenji', akaamua kuniingia kwa gia ya kuniomba mikopo midogomidogo isiyo na riba. Alikuwa anafanya makusudi kabisa akijua nikimpa nitaona soo kukumbushia deni.

Mtindio,
I respect your views..ila nadhani tusi-generalise wanawake wote kuwa wanapenda kuombaomba pesa.Kuna wanawake wenye pesa zao na hawababaiki kuombaomba chenji za wanaume wao hata.Nimeona pia kuwa mwanamke akiwa anajiamini kipesa, mwanaume wake hujisikia insecure na huanza yeye mwenyewe kumpa pesa na vitu vingine ili ajisikie hajapoteza nafasi yake kama mwanaume katika uhusiano.Kwa hiyo basi ni dhahiri pia kuwa siyo wanaume wote wanakereka kuwapa wanawake wao pesa.
 
My dear pretty God never said man should do everything, alisema Adam for this sin "the ground will be under your curse. You will have to work hard all your life to produce enough food for you.Na mungu alipoomuumba Eve aliosema nitampa msaidizi (si tegemezi wa kila kitu)
Na tunaona ktk maandiko hayo hayo kwenye proverbs kuna chapter nzima ya capable wife Prov 31:10-31 ntakunukulia few lines
How hard is it to find A capable wife, she is far worth than money.....she keeps herself busy making wool and linen cloth......she is a hardworker,strong and industrous....she is always busy and looks at her family's needs.

Tukirudi kwenye mada nakataa kabisa kuwa Mungu alimuumba mwanamke awe tegemezi, apewe kila kitu bila yeye kuchangia.
Ni jamii zetu na makuzi ndio yametulea kutazama kuwa mwanaume ataprovide kila kitu. Tumekuzwa kuona baba ananunua kila kitu.. kwa kuwa mama alikuwa housewife. Binti aliyeondoka nyumbani na mtazamo huu hata afanikiwe na maisha apate kipato kizuri na mpenzi/mume bado atakuwa na fikra " jamaa atanipa pesa kudhihirisha ananipenda" na hata wakioana ataendeleza fikra hizo, yeye chake ataficha cha mumewe cha wote.

Lakini tungejiuliza, mapenzi ni nini haswa? nafikiri ni kurudhiana kuwa pamoja, kusaidiana, kushirikiana na kutulizana. Sio one way trafik- bali wote msichana na mvulana kila mmoja aonyeshe mapenzi kama kusaidiana wewe ukipew zawadi na wewe toa. Kama unatolewa out na wewe at times umtoe mwenzio out. Nafikiri kwa mwanaume timamu akiona binti yuko responsible na independent atampenda zaidi na kumheshimu.
Kuna mazingira ndio tunakubali kuwa msichana hana labda jamaa anafanya kazi na binti ni mwanafunzi basi kwa kile kidogo cha jamaa anaweza kusaidia mpenzi wake, na binti hapa asiwe ng'ang'anizi ati kila wakati apewe tuuu pesa kisa shoga yake ana kibuzi kinampa laki kila wiki!!!!

Kina dada wana tabia ya kujicompare na wenzao sana , kama ni vyuoni basi watashindana boyfriend wa nani ni bingwa wa kutoa pesa, wakiwa vyumbani husimuliana ohh jana nimepewa Simu kali na pesa, basi wenzie watamwambia eeh anaonyesha anakupendaa ehhh, sasa wale wengine (bila kufikiria other factors za wapenzi wao) huanza kujenga hisia kuwa ahaaa kumbeee kupendwa ndio huku... ni kupewa pesa, zawadi n.k na yeye akikutana na BF wake ataanza kudadisi eti unanipenda, mbona hunipi pesa; Namwambia hisia na fikra hizi zikisha jengeka kwenye akili ya binti basi ndio mwanzo wa balaa. Hata akipata kazi bado atataka apewe kila kitu na hatachangia hata chembe kwenye familia.

Ni wakati muafaka kina dada wakatambua kuwa mapinduzi ya kweli wanayoyahitaji ni pamoja na kujiamini kuwa wanaweza na kwenye mahusiano pia wanachangia na kwenye familia vile vile wanachangia. Ila kutegema kupewa tuuuu mwishowe ni kunyanyaswa na kudhalilishwa.
 
mie bwana pesa yangu ni yangu tu! wanaume hawatabiriki kabisa, wakati fulani nilikuwa nasaidiana na mr bega kwa bega, kila mwisho wa mwezi 2takaa 2pange mambo ya kimaisha na matumizi ya kifedha, alipokuja kubadilika kidogo nikaona na matumizi ya nyumbani yamepungua sana, hapo ni mie sasa na kila kitu ndani, alipokuja kujirudi alishanipa lesson, nilisema sasa changu ni changu chake kitakuwa chetu kufidia huyo wa nje alivyokuwa anavinjari, na yeye hakudhubutu tena kuniambia mambo ya kukaa chini na kupanga kwa pesa yetu bali tutapanga kwa pesa yake, waiiiiii
 
Mtindio,
I respect your views..ila nadhani tusi-generalise wanawake wote kuwa wanapenda kuombaomba pesa.Kuna wanawake wenye pesa zao na hawababaiki kuombaomba chenji za wanaume wao hata.Nimeona pia kuwa mwanamke akiwa anajiamini kipesa, mwanaume wake hujisikia insecure na huanza yeye mwenyewe kumpa pesa na vitu vingine ili ajisikie hajapoteza nafasi yake kama mwanaume katika uhusiano.Kwa hiyo basi ni dhahiri pia kuwa siyo wanaume wote wanakereka kuwapa wanawake wao pesa.

well said mamii! na inategemeana pia mlivyo date kwa mara ya kwanza, wanaume hapo ndipo wanapoonyeshaga hayo mambo ya fedha ili ucmuone namna gani vipi, kama ulishanizosha fedha tangu mtongozo wa kwanza leo tuna muda fulani ucponipa nitahic kuna mambo mengine yanaendelea, kuna wale wanaume wanatoa pesa bila kuombwa kabisaaa akujua ni wajibu wake, nikiwa binti nilitongozwa na kaka mmoja, huyo kaka maongezi yake kuanzia 2lipokutana cku ya kwanza yalikuwa kuhusu pesa, "ucjali, ucwe na shida ndogo ndogo nipo kwa ajili yako, hapo sasa na mie ndipo nilipoanza kumpendea pesa, mana nilikuwa nikikohoa tu hakuna mjadala, maisha ndio haya haya sio wote tunalia lia shida kwa wanaume but tukipata mteremko tunateremka nao.
 
Mtindio,
I respect your views..ila nadhani tusi-generalise wanawake wote kuwa wanapenda kuombaomba pesa.Kuna wanawake wenye pesa zao na hawababaiki kuombaomba chenji za wanaume wao hata.Nimeona pia kuwa mwanamke akiwa anajiamini kipesa, mwanaume wake hujisikia insecure na huanza yeye mwenyewe kumpa pesa na vitu vingine ili ajisikie hajapoteza nafasi yake kama mwanaume katika uhusiano.Kwa hiyo basi ni dhahiri pia kuwa siyo wanaume wote wanakereka kuwapa wanawake wao pesa.

Nakubaliana na wewe, ya kuwa si wanawake wote wenye tabia hii.

Lakini ukienda uswazi jinsi maisha yanavyoendeshwa, kwa asilimia kubwa PESA ndo rule of thumb. Mizinga kwa kwenda mbele ndio dili.

Hii tabia kumfanya mweza wako ktk mahusiano kuwa ATM ni mojawapo ya tabia ambazo zinahitaji kukemewa. Kuombaomba ela ni kuleta picha kuwa mhusika 'anauza' kitu fulani, jambo ambalo ni la kufadhaisha.

Kama mtu 'anauza' basi aweke bayana biashara, kuliko 'I love u' nyiiingi za uwizi.
 
Hii mada ni nzuri ila kwa walioolewa au kuoa ndo wanajua vizuri hili suala,kwa upande wangu c oni sababu ya mtu kukataa hela yake isitumike kama mnafanya kazi wote na ni wana ndoa. Na ktk mapenzi, suala la mwanaume kutake care girlfriend wake ni la muhimu saana ktk mahusiano,tatizo linakuja kwa wale wanaolazimisha.Kwa hilo c waungi mkono kama wapo!! Unamuacha yeye akupatie kulingana na alichonacho.
 
Back
Top Bottom