Kwanini wadada wengi siku hizi wanazaa bila kujulikana baba wa mtoto?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,233
4,749
Imekuwa ni fasheni kwa wadada na mabinti wengi wanazaa bila mtoto kujulikana ni wa nani hii hatua waliofikia hawa dada zetu naona tunaelekea kupoteza maadili yetu kama watanzania.

Nina dada yangu pia nina shangazi yangu hawa wote wamezaa bila kuolewa kibaya zaidi watoto haijulikani baba zao ni nani mtoto ana miaka minne mwingeni miwili sijawahi kuwaona baba zao sijawahi kuona wakitambulishwa wala kujulikana naona ndugu zangu wakipambana wenyewe kwenye malezi

Pia naona wanawake wengi na wengine najuana nao mtaani na mazingira ya kazi naona wengi ni single maza lakini baba za watoto hawajulikana hali hii imenifanya nakaa nawaza inawezekana maisha ya mbeleni hawa dada zetu naona wanaelekea kule kwenye njia za upandikazaji wa mbegu bila kuhitaji mwanaume
 
Kuna wanaozaa maana muda umeenda , kuna ambao wanakutana na wanaume wanapata mimba inakuwa i don't care, wengine wanazaa wanaume wawatu pasipokujua na kujua pia kuna wengine wanang'ang'ania wanaume ambao hawawataki basi wanabakia na picha zao na siku hizi wengi wanaambiana zaa tu uitwe mama hujui utaolewa lini kabinti kadogo shida ameharibikiwa .
 
hiki kizazi ni shida, ujinga walio nao wakiwa bado warembo na hawana mtoto below 23 kuolewa hawataki, wakisha zagamuliwa na matoto juu ndo akili zinawajia
Wengi wao ndio hawa feminist tunaowaona humu JF, mada yoyote inayoanzishwa kuhusu single mother wasiolewe bila kuonyesha makabuli ya wenza wao unakuta wanaishambulia wakiwa very toxic and bitter...
 
Kuna wanaozaa maana muda umeenda ,
Sio kwamba single mother wengi kipindi cha usichana wao wanakataa wanaume wenye nia njema ya kuwaoa, halafu wanakubali wanaume wahuni..

Tena utakuta kipindi cha usichana mdada anajua kabisa kuwa mwanaume fulani ananipenda sana na ni husband material, akitaka kuolewa hata kesho ataolewa, ila anamkataa, anaishia kumkubali mvaa jinsi za kubana na cheni shingoni..

Sio kwamba wanaozalishwa nyumbani, kipindi cha usichana wao walikuwa na tabia mbovu ambazo ziliwafukuza wanaume wa maana wenye nia ya kuwaoa.

Though pia wadada wengi kuzalia nyumbani inatokana na sisi wanaume, wengi wetu sisi wanaume ni watu wa ovyo tusiofaa kwenye jamii, mwanaume anakula mirungi na kushinda vijiweni bila kazi, mlevi, malaya, mwizi aliekubuhu etc atakuwa vipi mwanaume responsible wa kuendesha familia
Unique Flower Zemanda
 
Imekuwa ni fasheni kwa wadada na mabinti wengi wanazaa bila mtoto kujulikana ni wa nani hii hatua waliofikia hawa dada zetu naona tunaelekea kupoteza maadili yetu kama watanzania
Nina dada yangu pia nina shangazi yangu hawa wote wamezaa bila kuolewa kibaya zaidi watoto haijulikani baba zao ni nani mtoto ana miaka minne mwingeni miwili sijawahi kuwaona baba zao sijawahi kuona wakitambulishwa wala kujulikana naona ndugu zangu wakipambana wenyewe kwenye malezi

Pia naona wanawake wengi na wengine najuana nao mtaani na mazingira ya kazi naona wengi ni single maza lakini baba za watoto hawajulikana hali hii imenifanya nakaa nawaza inawezekana maisha ya mbeleni hawa dada zetu naona wanaelekea kule kwenye njia za upandikazaji wa mbegu bila kuhitaji mwanaume
Hawa watoto ambao baba zao hawajulikani, baba zao wapo tatizo baba hao ni baba wa familia zingine.

Tatizo hili linazidi kuongezeka kwani wadada hasa wale wenye umri mkubwa na kazi zao na kipato wanahitaji mwanaume aliye na utulivu emotionally na stable katika maisha na mwanaume aidha Azar nae tu au afanye nae maisha kizani, mwanaume mwenye sifa hizi kwa hali za maisha yetu lazima awe ni mwanaume ambaye ana familia yake tayari hivyo hawezi kutajwa Moja kwa moja kama baba wa mtoto.
 
Back
Top Bottom