Kwanini vyombo vya habari vilimgeuka JK?

Acha uwongo. Conservatives wa Uingereza hawakutoa fedha yoyote kwenye uchaguzi wa CHADEMA 2010.
Jambo usilolijua usibishe, hizo ni habari za kiusalama zaidi. Ni kweli Conservative walitoa fedha nyingi tu kwa CDM baada ya kuona ni chama ambacho kina dhamira ya kweli kabisa ya kuingia Ikulu lakini juu ya matumizi sina ushahidi nalo zilitumikaje? Amini hii vita hii ya CDM na CCM ina mikono ya mataifa ya nje na ndiyo maana CCM inakihara sana chama hiki yaani CDM kwa kuwa jamaa hawa wapo makini na utekelezaji wa majukumu yao na CCM wenyewe wanalijua hilo pasipo mashaka kabisa kwa sababu TIS ipo kwa ajili ya kuhakikisha mambo yote yanafahamika kabla hayajatokea ili hatua zichuliwe mapema lakini hili serikali ya JK haielewi ifanye nini kwa uhakika.
 
Mimi nilitia hofu toka 2005, nakumbuka nilikuwa karibu na mnara wa saa(DSM) majira ya jioni siku amabayo mchakato wa mwisho ndani ya CCM ulikuwa unafanyika Dodoma. Nilikuwa kwenye matatizo yangu ya kimaisha hivyo sikuwa nafuatilia sana mambo ya siasa. Ghafla nilisikia mlipuko wa shangwe na watu kuanza kushangilia huku wakikimbia kwa makundi kuelekea ferry(baadaye nilikuja ambiwa walikuwa wanazunguka mjini mpaka karibu na Ikulu wakishangilia). Hicho kitendo ndicho kilileta shaka akilini mwangu kama kweli Kikwete atapendwa kwa muda mrefu, mazingira yalionyesha watu walimpokea kama Masihi ambaye ataifanya Tanzania kuwa kama Marekani kwa muda mfupi. Mimi huwa naamini mtu ukupokelewa kwa shangwe sana ni rahisi pia kuchokwa mapema. Lakini ukweli ni kuwa jamaa ameshindwa kazi, ameachia nyani shamba na mavuno ni mabua.
 
It is just the 'law of dealth and life'. Kamba aliyotumia kunyongea wenzie wasio na hatia kama akina Salim Ahmed Salim, ndiyo inayotumika hivi sasa kumnyonga yeye. Na kwa style yake ya uongozi, hakuna rais mstaafu atakayesahaulika kwenye historia ya nchi hii kama yeye.
 
Alikuwa amevaa NGOZI ya KONDOO na sisi kondoo wenzake hatukumjua, heeeeee kumbe NDANI Mbwa Mwitu, yy kama yy sidhani kama ana
kashfa inayomgusa 100% ila Marafiki zake anao wasupport ni Mafisadi na kashindwa kuji tenga nao, wananchi wakajua heeee mbona huyu si
mwenzetu, ndio kumgeuka
 
Sio kwamba wamengeuka bali ni nyakati zimebadilika.
1. Waandishi walitumiwa sana na wanamtandao kwa kununuliwa ili wampambe JK. Yakazuka magazeti kazi yao ilikuwa kuwamamliza wapinzani wake kisiasa ''Character assassination'', Salim A. ni muathirika namba moja.
2. Waandishi wetu wengi hawaandiki habari za uchunguzi ila wanaripoti nani kasema nini. Hii iliwanyima fursa ya kumjua JK mapema.Hali haionekani kubadilika. Waandishi wanaandika sensational news na sio investigative news.
3. Hata wale wachache wanaochambua habari, sasa wamechoka. JK anapowaambia watu Dowans haijulikani mmiliki, halafu PM anasema tutawalipa 'maruhani'', Werema anasema mjadala umefungwa, ni mwandishi gani atakayeweza kubeba mkanganyiko kama huu.
4. JK amewatumia waandishi kwa manufaa yake, linapokuja suala la Richmond mathalani, anaongea Katibu mkuu kiongozi au mwandishi wa rais. Hali hii inawaudhi sana waandishi wachache makini, na wamegundua wanatumiwa. Wamegundua pia usanii uliokithiri wa serikali kuwageuza watu wajinga ikiwa ni pamoja na kuunda tume zisizo na maana.(mfano, tume ya Luhanjo kuhusu Richmond)
5. Kama wanakijiji wanahoji utendaji dhaifu wa serikali hii , ni mwandishi gani atakayeandika habari ikanunuliwa kwa kupulizia perfume rundo la uozo!!
 
Waandishi wa habari walimpenda kwani walidhani ndiye atakayekuwa mkombozi wa matatizo ya msingi ya wananchi licha ya vyombo vingi vya habari kurubuniwa kuweka habari nzuri za kwake..

Lakini walipoona amekuwa na maneno mengi na matendo machache ndipo shida ilipoanzia..

Jk amejaa fitna na anaendesha nchi wa majungu na ni mlipa visasa ..

Angalia wale wote waliounga mkono upinzani wameondolewa.

Mfano:-
tido mhando - tbc
basilo matei - rpc arusha
mbunda rafael - mkurugenzi manispaa arusha
 
Alikuwa amevaa NGOZI ya KONDOO na sisi kondoo wenzake hatukumjua, heeeeee kumbe NDANI Mbwa Mwitu, yy kama yy sidhani kama ana
kashfa inayomgusa 100% ila Marafiki zake anao wasupport ni Mafisadi na kashindwa kuji tenga nao, wananchi wakajua heeee mbona huyu si
mwenzetu, ndio kumgeuka
Ngozi ya kondoo huyu mbwa mwitu bado kaivaa ndiyo sababu unasema mwenyewe kuwa hana kashfa inayomgusa wakati yeye ndiye mtuhumiwa namba moja.
 
Back
Top Bottom