Kwanini vyombo vya habari vilimgeuka JK?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mwanzoni mwa utawala wa JK baadhi ya vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?
 
Awamu ya kwanza hawakumjua Kikwete, sasa wamemjua ni nani na anafanya nini, lingine wameibuka watu ambao ni zaidi yake (JK) na huwezi kuwalinganisha naye kiasi kwamba baadhi ya vyombo vya habari imebidi viseme kweli na hiyo kweli ndio iliyomgeuka JK.

Habari za huko ulikokuwa Mzee Mwanakijiji? Yalisemwa mengi hapa na kuulizwa pia.
 
i missed you mzee, nimefurahi sana kukusoma tena. Aligeukwa na vyombo vya habari baada ya kujulikana vizuri na matendo yake ya kifisadi kuonekana. Naishia hapo wengine waendelee.
 
mkuu hata wakati wanahabari wanamlamba miguu walijua fika walikuwa wakimpa sifa asizostahili,hata hivyo walikuwepo wachache waliothubutu kuanika mapungufu ya jk hata kabla hajaingia madarakani. Hali'ya maisha ilivyo sasa,hali ya kisiasa,udini na hali za kijamii, kumsifia jk kwa style ile ya kulamba miguu ni kusababisha chombo chako cha habari kipuuzwe na wadau
 
Wengi walizugika na sura yake kuwa na mvuto ukilinganisha na mtangulizi wake ambaye alikuwa mbabe kwa waandishi wa habari, wakadhani hata matendo yake nayo yatakuwa mazuri vivyo hivyo. Alikuwa akizungumza na vyombo vya habari alijitahidi kuwataja waandishi mmoja mmoja kwa majina kuwaonyesha alivyo karibu nao na ni rafiki yao wa karibu jambo ambalo liliwavutia wanahabari wengi na wakampanba sana.
Ndani ya kipindi cha miaka miwili ya awali ya utawala wake wagundua yeye sio na ngoma ikageuka toka Mdumange kuwa Gombesugu.
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

Ahadi za kupewa vyeo hazikutimia
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ni kama malaya wa baa. Ukiwanunulia bia moja unakuwa "kaka" yake. Ukimuongezea nyingine moja unakuwa "shemeji" na ukiongeza ya tatu unakuwa "shemeji" within a span of 2 hours. Hawa nao walivuta fedha nyingi kutoka "mtandao" na huo "mtandao" ulikuwa unasifika kama ni "mtandao wa vijana" na damu mpya! Sasa mwaka huu CHADEMA wamevuta fedha nyingi kutoka Conservatives wa Uingereza na fedha hizi zimemwagwa kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari.

Kama vyombo vya habari "vilimramba miguu" Kikwete mwanzoni mwa muhula wake wa kwanza na tunakubali kuwa wamemgeuka mwaka huu, basi it is equally true walikuwa wanamramba miguu mgombea mwengine. Sasa jiulize kwanini hao waandishi wa habari wawe "wanaramba miguu" ya mgombea mmoja tu na kwanini wasiwe wanaripoti bila ya upendeleo wowote?

Kama unafikiri kuwa tuna waandishi na wahariri HONEST kwenye nchi basi hii Tanzania haujui kabisa!
 
heshima kwako MM.

karibu jamvini.

siku za karibuni tulikuwa tunapanikishwa mpaka basi. kumbe upo?

safi.
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ni kama malaya wa baa. Ukiwanunulia bia moja unakuwa "kaka" yake. Ukimuongezea nyingine moja unakuwa "shemeji" na ukiongeza ya tatu unakuwa "shemeji" within a span of 2 hours. Hawa nao walivuta fedha nyingi kutoka "mtandao" na huo "mtandao" ulikuwa unasifika kama ni "mtandao wa vijana" na damu mpya! Sasa mwaka huu CHADEMA wamevuta fedha nyingi kutoka Conservatives wa Uingereza na fedha hizi zimemwagwa kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari.

Kama vyombo vya habari "vilimramba miguu" Kikwete mwanzoni mwa muhula wake wa kwanza na tunakubali kuwa wamemgeuka mwaka huu, basi it is equally true walikuwa wanamramba miguu mgombea mwengine. Sasa jiulize kwanini hao waandishi wa habari wawe "wanaramba miguu" ya mgombea mmoja tu na kwanini wasiwe wanaripoti bila ya upendeleo wowote?

Kama unafikiri kuwa tuna waandishi na wahariri HONEST kwenye nchi basi hii Tanzania haujui kabisa!

no evidence, shut-up.
 
Tanzania kwa ujumla tuna wandishi wa habari wachache sana, wengine ambao ndiyo wengi ni watunga habari i.e. Shikongo. #Watunga habari TZ ni kundi muhimu sana kwa wamiliki wa vyombo vya habari kwa vile ndio wanaouza magazeti. Siamini inakuwaje gazeti kama Kasheshe na thelikes yanakuwa magazeti maarufu kuliko Mwananchi au Raia Mwema. Mimi naona hii design ya magazeti iko TZ sijawahi kuona nchi nyingine watu wanapapatikia magazeti ya udaku kama kwetu.

Kwa hiyo hao watunga habari kama akina Shikongo ndiyo uliwaona kwenye ile katuni ya GADO wakilamba viatu vya JK 2006/07.
 
Vyombo ya habari vimegawanyika sehemu 2.
Wapo wanaoiunga mkono serikali ya ccm hata kama inafanya madudu, na kuna vyombo vingine vimesimama kidete kutangaza ukweli, haijalishi serikali imefanya madudu ama mazuri.

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema Two important things with different qualities.
 
Mwanzoni vyombo vya habari vilimpamba sana hadi kuonekana kuramba miguu yake; lakini, ilipofika mwisho wa muhula wake wa kwanza inaonekana ni kama vyombo vya habari vimeonekana kugeuka kabisa.

Ni tatizo la vyombo vya habari, au ni tatizo la yeye mwenyewe au ni kitu gani kimefanya vyombo vya habari vigeuke namna hiyo? What went wrong?

Karibu tena jamvini mzee mwenzangu,
... tulikukosa hapa na kila aliyekuulizia trherad inapotea!
 
amebaki Kibonde na rafiki zake radio uhuru, gazeti mzalendo, daily news, habari leo, rai n.k kuendeleza propaganda za kumpamba mkwere kinafiki!
 
Labda vyombo hivyo vimeamka na kugundua vinatumiwa kumpa umaarufu usio wa kweli? Yawezekana wameamua kukomaa na kugoma kukanyagwa migongoni nmwao ili JK aendelee kuangua maembe ya watu kisanii pasipo yeye mwenyewe kuonekana wazi bali akiwa mgongoni kwa wanahabari akiwaahidi pipi ambazo hatimaye hawazioni.

Kipindi hiki ni cha mwisho kwa JK uongozini kwa mujibu wa katiba ya JMT, ukijikokikoki kwa msanii huyo utaumia wewe maana anajua kwamba hataathiriwa na jambo lolote atakalolifanya, na lazima kipindi hiki ajilimbikizie utajiri wa kumtosha kutanulia baada ya 2015 yeye na wale wote wamtegemeao.
 
watampambaje mtu hapambiki?waandishi wa habari wamejaribu kadri ya uwezo wao kumpamba lakini wapi.tena raia wanapinga kwa mifano hai.hapa ni sawa na kuuza bidhaa mbovu sokoni.utapata wateja mwanzoni tu kabla hawajaistukia kua ni mbovu lakini wakishaistukia tu imekula kwako.ndio sawa na jk.uozo wote nje nje,hakuna anaekubali sifa zake tena.
 
Payuka umeiweka vizurikuliko mwanakijiji.
Yeye ameseme vyombo vya habari kana kwamba ni vyombo vyote vya habari wakati ni vichache tu. Ukiangalia kwa makini utagundua vyombo vinavyo muandika vibaya jk ni vile vipya ambavyo havikuwepo 2005,mfano Raia mwema haikuwepo.
Lakini vyombo vingi vya habari makini vilvyomsapoti 2005 bado vimeendelea kumsapoti hadi leo.Nitoe mfano tu,Rai,Daily News,Habari leo,Itv,Star tv,Channel 10,c2c,nipashe,the guardian,uhuru,to mention but few.
Ili thread yako mm iweze kueleweka utuoreshee vyombo vyote vya habari vilivyoko tz halafu ubainishe ni vipi kati ya hivyo vilivyogeuka halafu tuangalie ni asilimia ngapi ya hivyo vuilivyomgeuka then tutakuwa ktk position ya kukonclude kwamba kweli vyombo vya habari vimemgeuka.Vinginevyo thread yako itakuwa in uchokozi ndani yake.
 
Kusema ukweli MM siyo waandishi tu ila wananchi kwa ujumla wapo very disappointed.
Labda mimi mwenyewe nieleze nilivyokua namchukulia JK 2005 ndani ya akili yangu bila bias. Nilikua nikisikiliza hotuba zake kwa muda mrefu na kwa ahadi alizokua anatoa nikawa naona kama tz kweli tumepata rais sasa. Nilikua very confident hata nikikaa ofisin nilikua nina moyo wa kufanya kazi ili kujenga taifa langu.....Alikua mara kwa mara akifanya kazi kwa kasi mara utamwona kariakoo kaja gafla kukagua usafi mara bandarini mara tanesco ubungo na kwingineko na wakuu wa mikoa au viongozi wasiokua wanaenda sawa naye aliagiza wasimamishwe kazi mara moja.

Sasa balaa lilikuja pale kashfa ya Richmond ilipoibuka na mh. Lowasa kujiuzulu!!
Tangu hapo raisi amekua lege lege haeleweki hata TAKUKURU wakimkamata mtu na rushwa yeye anapiga simu aachiwe, matatizo mengi yamekua yakiandama nchi kama tatizo la umeme na malipo ya DOWANS rais kimya!!!
Nchi imekua haina msemaji kila mtu anaongea lake, mara PM kasema hili kuhusu katiba mara werema kasema lile mi nimechoka.
Nchi hii sasa ukishakua na hela wewe ndo kila kitu siku za karibuni mmeona wazungu na wahindi wanatunisha misuli kwa mawaziri wa ardhi na mambo ya ndani hii yote ni kwa sababu wana kiburi kutoka juu.
Sasa najiuliza huyu mh. kalewa madaraka au kuna mtu alikua akimshikia remote control? maana baada ya lowasa kujiuzulu basi!!
Mwisho nimekuja kugundua zile hotuba zake kumbe hua anaandikiwa na hua hafanyi editing ndo maana hua anatoa ahadi nyingi sana bila utekelezaji....Vijana wanamkaririsha hotuba usiku kucha mpaka akija kwenye jukwaa anakosa nguvu anaanguka.
Iam tied ....mwingine aendelee please!!
 
Back
Top Bottom