Vyombo vya habari mnatuangusha kwenye kusaidia nchi kuendelea

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Sijajua kwa hakika vyombo vya habari vya Tanzania hasa televisheni na magazeti mengi Yana ugonjwa gani..

Tabia ya kukwepa kujadili mambo muhimu kwa uwazi na kuwapa watu nafasi ya kuongea na kuchambua sera , Sheria na hata mambo ya jamii ( public participation) kutaifanya nchi hii kuwa nyuma kimaendeleo tofauti na ambavyo ingekuwa kama wananchi wangepewa nafasi ya kuchangia mawazo kwa uwazi na kusikika juu ya mambo yanayowahusu.

Kuna wakati nilihudhuria kongamano Fulani kwenye Moja ya nchi zetu za Africa mashariki .

Nakumbuka wakati wa mapumziko, tulikuwa na ndg kutoka Uganda na tulikuwa na mjadala kidogo.

Katika maongezi yote,.waganda walikuwa Kila mara wanasisitiza sifa ya watanzania kwamba ni kiswahili na kuimba.

Walikuwa wanatilia shaka sana uwezo wetu wa kujadili mambo. Nakumbuka mwenzangu tuliekuwa nae, alifikia mahali pa kuwa mkali na akikataa sifa yetu kwamba ilikuwa kujua kiswahili tu na kuimba.

Sababu ya kusema hivyo ilikuwa ni kwa kuwa, tulionekana walau tunaweza kujadili nao mambo mengi, hivyo usemi huo ilikuwa ni kama kushangaa kwamba kumbe watanzania nao wanaweza ku urge na kujadili mambo at length.

Nakumbuka baada ya kuachana nao, jinsi tulivyocheka kwa kuwatisha waganda huku upande mwingine tukikubaliana nao kwamba Kuna ka ukweli walikasema, ingawa tulisemea pembeni tukiwa wenyewe.

Nashangaa sana kuona mabadiliko makubwa haya ambayo serikali imependekeza juu ya demokrasia na mambo mengine, kuona vyombo vya habari havishirikishi jamii kuchangia mambo hayo.

Nenda kaone vipindi toka tbc, itv, mention any. Huoni mijadala ya watu mbalimbali kwa utofauti wa wasifu wao wakichangia .

Sana utawaona watu tu wa tabaka la utawala ambao kimsingi ni kulinda tu kile kinachoitwa status quo . Kusifu viongozi na kushabikia hata mambo ambayo mioyo yao haiyaamini, lakini Ili kulinda maslahi utasifia.

Kwani vyombo vya habari havijui dhana ya agenda setting? Hivi wakati huu ambao Kuna joto la mabadiliko yanapendekezwa kufanyika na Sasa yanapelekwa bungeni kwa Nini media wasingeichikua hii kama agenda?

Najua wanaweza wao kuanza agenda zao, kwenye suala muhimu kiasi hiki kwa Nini hiyo isiwe agenda?

Hivi vyombo vya habari hawajui kwamba Wana sehemu kubwa na jukwaa Pana kwenye kusaidia maendeleo ya nchi?

Wabunge Sasa wanaelekea bungeni, watajadilije at length masuala makubwa namna hii wakati public participation haijachukua mkondo wake?

Nchi zinazoendelea zimeruhusu watu kuonekana wakitoa mawazo yao bila uoga Ili katika mchanyiko wa fikra kupatikane majibu sahihi.

Swali langu, je vyombo vya habari havioni kwamba vina wajibu wa kuifanya nchi hii na wananchi wake kushiriki mambo kuyajadili na kuyaongelea mambo yanayowahusu?

Hiki kinachoitwa public participation hapa kwetu ni kiini macho tu. Watu kuitwa bungeni haiwezi kuwa public participation.

Public participation ni pale unapoiruhusu jamii Pana kushiriki mambo, kwa uwazi na kutoa mawazo yao bila masharti.

Kwa tabia hii ya vyombo vikubwa vya habari kutojua jukwaa lao katika kusaidia maendeleo ya nchi, mnatuangusha.
 
Mzee nakuunga mkono ila nikueleze kitu. Aisee Bongo yetu kuna maambo bado sana.

Exposing everything kwenye media miaka ya sasa unaweza kurise kitu mbaya sana kwa wenzetu wa nje, ndio maana i don't support kugandamiza uhuru wa vyombo vya habari ila noma kijana wangu. Wakiruhusiwa media inavusha vitu mbali sana. Acha tujitengeneze kwanza. Mambo yakiwa sawa isssue zitafanyika.

Ndio maana hata vyombo vya nje, huoni sana wanarusha revolution state zao zinazotokea kwenye nchi zao. Umeona juzi yule jamaa kule guinea muandishi wamemkamata anachunguza wale mafisadi. Ila huwezi kuta uingereza mtu anafanya vile. Soo sometimes tuhold mioyo yetu, si kila kitu cha kwenda mjini.

Tutakosa mialiko nchi za watu, tutakosa misaada, tutakosa wawekezaji. Tutakosa pesa ndugu zako tunaotoka sana huko nje.

Sijui kama umeelewa pointi yangu?
 
Sijajua kwa hakika vyombo vya habari vya Tanzania hasa televisheni na magazeti mengi Yana ugonjwa gani..
Sio ugonjwa,......Hawa jamaa zetu wa mbogamboga wanacontrol kila kitu. Utaona na utasikia kile wanachotaka wao.
 
Back
Top Bottom