Kwanini ukose uaminifu kwa mpenzi wako?

hii ya shetan kunipitia inanikumbusha miaka kama mi3 nyuma hv, nlikuwa saloon, mdada wa saloon akawa anamweleza shoga ake kuwa mme wake ame mmimba house girl wao,,,,baada ya kuulizwa akasema ni shetani tu mke wangu....

lililonifurahisha ni jibu la mdada alilodai kumpa mumewe, anasma alimwambia hivi,," pole sana mume wangu , kweli shetan huyu hata mie namshangaaa, yaan ameniacha mie ambaye natongozwa kila siku barabaran na wanaume wenzio, wenye hela sio ww mwenzangu na mie, akakufuata ww, na kukupa nguvu ya kumtongoza na kutembea na house girl mpaka amepata mimba..........."
Yaani mnamsingizia shetani kua anahusika kwa mwanadamu kua na vimeo vya pembeni...
 
kutokuwa mwaminifu ni kukosa kujiamini.... kama unajiamini kamwa huwezi kucheat and once a cheater, always a cheater... kumsamehe mpenzi asiye mwaminifu ni sawa na kujipalia makaa ya moto.
 
Punguza jaziba mwana JF mwenzetu, mm nadhani kaa chini na huyo umpendae na umuulize ni vitu gani vinafurahisha sana nafsi yake ukimfanyia, ujue mwingine unaweza kumletea mizawadi ya gharama ukiamini atafurahi sana kumbe yy anapendelea kutoka na ww kwenda mazingira tofauti. kk kuwa mwanaume sio kuvaa suruali bali ni kujiamini na kujua jinsi ya kukabiliana na matatizo.
 
Kama kuna kosa ambalo siwezi kumsamehe mpenzi wangu ni USALITI", yaani nikigundua hata kama nimechelewa kujua ila hukumu yangu ni hapohapo.

NI KITUGANI KIPELEKEACHO MTU KUVUNJA UAMINIFU KWA MWENZI WAKO?
ETI "oooh! shetani alinipitia" siipendi hiyo kauli kama nini, kwanini huyo shetani akikupitia usije kwangu mbiombio uchojoe haraka nikwangue mzigo huo? hakuna siku umenipa nikakata kula, badala yake mi ndo nataka kila siku mpaka unakimbia uwanja ila bado unaenda kumpa mwingine.
ETI " oooh! utakulaje kila siku mchicha, lazima ubadili mboga". au "mchele uleule mapishi tofauti".

MI NAONA KWA WANAUME NI KUTAFUTA SIFA ZA KIJINGA, KWAMBA YEYE NI DUME LA MBEGU AMETEMBEA NA MADEMU WENGI, HIVYO ANATEMBEA KIFUA MBELE KWA MARINGO.

JE KWA MADEMU NINI HASA MNATAFUTA UKIACHILIAMBALI SUALA LA PESA?

mapenzi hayana formula yanafuata upepo unavoenda, kama mko kwenye ndoa kusalitiana kunatokana na mazingira mnayoishi ya kuchokana, kuzoeana, maudhi yanapozidi n.k.
kama bado ni wapenzi tuu bado kuoana basi anayeanza kutoka nje anakuwa amepoteza mwelekeo kwa mwenzake na kuona hapa hamna future na mwisho uko karibu kwa hiyo bora aanzishe kwingine likivurugika anakuwa na pengine tayari anaendelea so haangaiki kutafuta akiwa single.
ingine inaweza kuwa basi tu kila kitu kiko sawa hamna shida wala ugomvi au wengine kesho ndo wanafunga ndoa na leo anaenda mmimbisha mtu mwingine hii ni kalaana kanakoendelea kutembea toka kizazi hata kizazi.
NB:- jiulize kwanini utakuta familia babu alizaa watoto wa nje ya ndoa lazima kuna mtoto wake nae atakuwa na watoto wa nje ya ndoa na wajukuu nao utakuta wanazaa nje ya ndoa na vitukuu hivohivo yaani hii kitu inaendelea na huoni kwamba itakuja tokea kizazi kitapita bila kuwa na mtoto wa nje ya ndoa. Ni vijana wachache sana wanaooa ambao hawana watoto wa nje au waschana wanaoolewa ambao hawana watoto wa nje. Yote hii hupeleka kusalitiana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom