Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.
Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).
Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.
Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?
Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?
Wanajamii kwani hamujui Tanzania ni nchi ambayo haina mfungamano na nchi yoyote. Kitu chetu cha maana ni amani na utu wa watu. Sasa sioni Marekani wamepeleka usuluhisho gani huko wao ndo kichwa kikubwa cha mwendawazimu. Raisi wao hasikilizi viongozi wa nchi yake na akaenda tuu kuanzisha vita huko. Kuhusu mzee Gaddafi nayeye anautata, kumpigia kifua utaambiwa kama unasaidia magaidi. Nchi nyingi sikuizi zinafuata mkumbo wa waamerika na waingereza nazani tanzania bado hatufuati mkumbo na hatujawahi kufuata mkumbo kwenye mambo ya ukombozi navyojua mimi. ndomaana msimamo wetu ni atufungamani na upande wowote. Tutamtetea mnyonge siku zote apate utu. Hatujali dini, kabila, wala rangi, kutoka huko seachels, afrika ya kusini, zimbabwe, mozambique na angola kote tumemsaidia mnyonge kumpa utu wake. Hatu ruki waamerica wakisema turuke. Kama wewe wafikiria waamerika wakisema turuke turuke fikiria tena utu wako.Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.
Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).
Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.
Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?
Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?
Nguruvi kinachonitisha mimi zaidi siyo tu ule ukimya ni hicho ulichokisema - hatujui tunasiimamia nini. Mtu mmoja amesema kuwa diplomasia yetu ya nje ni ya uchumi - hili lilikuwa tangu wakati wa Mkapa na Kikwete ameliendeleza. Yaani, hatujali tena suala la haki, utu, uhuru n.k
Unajua kutaka kila kiongozi afanye kila kitu kama alivyofanya Nyerere Miaka 40 iliyopita ni "insult" kwa akili za watu, Nyerere hajwahi kuwa mtu pekee anayejua solutions za matatizo yetu, wapo wengi lakini walikuwa kimya kwa kuogopa repercussions za kumuingage yule mzee katika fierce debates. Wewe Mwanakijiji unafahamu wazi kwamba kinachoendelea libya kuna ulterior motives za kuiba mafuta ya libya, halafu unakuja kuishauri serikali yetu iwe kibaraka wa wezi are you serious?. Hebu nikuulize Unataka serikali yetu iwatambue waasi, hebu niambie ni walibya wangapi wanawaunga mkono waasi?, ni asilimia ngapi ya walibya wanawunga mkono waasi?, ni kipi kinachowapa waasi legitimacy ya kuwa representatives wa libya?.atleast serikali ya sasa ya libya inayoongozwa na waziri mkuu imechaguliwa na watu kupitia councils zao, sasa wewe niambie ni system gani imewapa legitimacy waasi?. Mkjj fungua macho wewe, uone forces za neocolonialism zinavyofanya kazi, usiwe blinded na akina hillary clinton wanaokija africa na arrogance kuwaamrisha viongozi wetu "what to do with Africa". najua uko marekani na unaipenda sana, lakini hiki unachoadvocate ni hatari kwa uhuru wa Afrika!. Nyerere alimsapoti Savimbi at one time, Nyerere alifanya biashara na makuburu at some other time, Nyerere alikuwa independent minded, alifanya kile alichoamini ni sahihi, sasa waache viongozi wetu wafanye wanachoona ni sahihi at this time!. The other thing ni kwamba Nyerere alikuwa na jeuri ya kufanya vile kwa sababu ya cold war, pande mbili zenye nguvu za ussr na usa, kila mmoja akijaribu kuwin marafiki, kipindi hicho ungeweza kujialign na mmoja ukajihisi safe kiasi, sasa leo hii yupo mmarekani, utathubutu kumuwekea usiku katika maslahi yako atakuacha? Aisee siwezi kuamini nguvu za neocolonialism ni kali namna hii, zinatwist na kutongoza akili za watu wetu tunaoamini ni best. amka ndugu jikomboe kutoka katika utumwa mambo leo,maisha ya mtu, heshima na utu, vinasimama mbele kabla ya nadharia za kidemokrasi , capitalism, socialism na blah blah nyingine!
Sasa kwa nini Tanzania inashindwa kujitokeza wazi wazi na kusema inamuunga mkono Gadafi ?
Nguruvi kinachonitisha mimi zaidi siyo tu ule ukimya ni hicho ulichokisema - hatujui tunasiimamia nini. Mtu mmoja amesema kuwa diplomasia yetu ya nje ni ya uchumi - hili lilikuwa tangu wakati wa Mkapa na Kikwete ameliendeleza. Yaani, hatujali tena suala la haki, utu, uhuru n.k Kuna neno baya limenijia kulitumia naogopa lakini linaendana na wale mabinti wanaozunguka strips ya Las Vegas wakijipamba vizuri na kujitangaza kuwa ni maescorts. Sera zao ni za kiuchumi na haijalishi sana uchumi huo unatoka kwa nani na kwa nini. Tanzania imekuwa kama hao kwamba tuko tayari kulala na yeyote na hatuwezi kumkemea hata kama anafanya mambo ambayo hatuwezi kuyaandika hapa. Hii ndio Tanzania chini ya CCM hii.
Inashangaza kwenye kikao cha Bunge hadi hivi sasa hakuna hata mbunge mmoja (wa CCM au upinzani) ambaye amejaribu kupush serikali yetu kuchukua msimamo ambao unaendana na historia yetu (kama ulivyoidodosa kidogo hapo) na amali zetu kama taifa. Kwanini wabunge hawafikirii mambo hayo? Au wanafikiria Tanzania ni kama kakisiwa fulani tu.
Hamna taabu.Nimelipenda hili jibu kwa kweli; naomba niliweka kwenye signature yangu.. !
Wow, just goes to prove how low we have stooped, so low that we are eager to admit we have no pride left as a nation and so shamelessly brand our lack of stand a strategic ambiguity.In short, i think the strategic ambiguity works well for Tanzania in the Libyan crisis, wacha wajisortout kwanza, wakishajulikana mshindi nani na wakatengeza serikali, tutawaunga mkono tu. At the moment kuna lots of factors playin in kiasi kwamba huwezi jua ukiamua kusupport blindly
hao rebels utakua unamtumikia nani bila wewe kujua.
My 2 cents
Kweli kabisa, Mwanakatwe. Hawa waasi hawana utambulisho unaoekleweka. Kuna kila dalili kuwa siyo watu wengi katika Libya wanawaunga mkono. Vinginevyo Gaddafi asingekuwepo tena. Hivi kila kikundi kikijitokeza na kuasi serikali yake basi Tanzania inalo jukumu la kukiunga mkono? ANC, Frelimo, MPLA, n.k. those were different cases. Different causes, different era. Gaddafi anaweza kuwa amekaa madarakani kwa muda mrefu, hafuati demokrasia ya kimagharibi, bla bla bla, lakini kosa lake kubwa ni kwamba anakalia shehena kubwa ya mafuta ambayo haruhusu makampuni ya nchi za magharibi ziyamiliki moja kwa moja. Tanzania haina haja wala ulazima wa kuwatambua wahuni wa Benghazi. Bila NATO wale wangekuwa wameishaangamizwa. Hivi hayo mabomu ya NATO yana macho hayaui raia bali mizinga ya Gaddafi ndiyo inaua raia tu? Silaha za waasi je? Give me a break.Mi nafikiri wewe ndo wa kulaumiwa sio Tanzania, wewe mwenyewe umesema wale ni" waasi wa libya" na huo ndio ukweli, sasa ni vipi tz na heshima zake zote hizi ilizonazo iwatambue waasi? hilo haliwezekani ndugu yangu. Wale ni waasi wa libya, na nchi zote zilizowatambua ni nchi ambazo zimefuata karoti kujipendekeza kwa marekani na nchi za magharibi, hamna lolote zaidi ya hapo. Hatuwezi kuwatambua waasi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kukaribisha uasi nchini kwetu, ile ni njia haramu na ni vibaraka tu hawana lolote wale.
Hivi ule msikiti uliojengwa na Mwalimu Nyerere kule Musoma, pesa ilitoka kwa nani?.Mwanakijiji, Halafu nani atatujengea misikiti na kutuletea tende?.....au hukumsikia Mufti wetu alipolalama Libya kudundwa?