Kwanini Tanzania haijavunja Uhusiano na Gadaffi?

Suala la Libya ni gumu kwa serikali kuagree na upande wowote. Nani mwenye haki in Libya? wapinzani? Gaddafi? NATO? USA? Actions zinazochukuliwa na NATO na US ndiyo serikali ilitakiwa ipinge.
 
Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.

Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).

Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.

Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?

Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?

well kwanini Tanzania haijavunja uhusiano na nchi hizi?

640px-Flag_of_the_People's_Republic_of_China.svg.png

USA-flag.jpg

Saudi Arabia.png

uk-lgflag.gif

vatican_city-flag.png
 
Mkuu MMK,
Haya mambo kwa nje nje yanaweza kuonekana ni rahisi, lkn kwa undani ni magumu. Waangalie USA sasa hivi wanavyohangaika kuwa na msimamo wa aina moja kuhusiana na yale yanayotokea kwenye nchi za kiarabu. Kwenye nchi moja wanasema hivi, nchi nyingine wanasema vile; hawana consistent approach ya ku-handle situation. Kinachogomba hapa conflict kati ya "values" na "interests"
Wakati wa Mwalimu tulikuwa na values (Amali ?) tulizokuwa tunaziamini na kuzisimamia kwa vitendo. Tulikuwa tayari ku-sacrifice interests zetu pale zinapogongana na values zetu (Ref. tulipokataa misaada toka kwa mataifa yaliyotaka kutuchagulia marafiki).
Sasa hivi hatuna values tena, tunaenda tu bora liende. That means tunaongozwa na interests peke yake. Kwa hiyo kule ambako interests zinalalia, basi ndiko na sisi tunaelekea.
Kwa Libya, intersts bado ziko kwa Gadaffi.
 
Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.

Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).

Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.

Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?

Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?
Wanajamii kwani hamujui Tanzania ni nchi ambayo haina mfungamano na nchi yoyote. Kitu chetu cha maana ni amani na utu wa watu. Sasa sioni Marekani wamepeleka usuluhisho gani huko wao ndo kichwa kikubwa cha mwendawazimu. Raisi wao hasikilizi viongozi wa nchi yake na akaenda tuu kuanzisha vita huko. Kuhusu mzee Gaddafi nayeye anautata, kumpigia kifua utaambiwa kama unasaidia magaidi. Nchi nyingi sikuizi zinafuata mkumbo wa waamerika na waingereza nazani tanzania bado hatufuati mkumbo na hatujawahi kufuata mkumbo kwenye mambo ya ukombozi navyojua mimi. ndomaana msimamo wetu ni atufungamani na upande wowote. Tutamtetea mnyonge siku zote apate utu. Hatujali dini, kabila, wala rangi, kutoka huko seachels, afrika ya kusini, zimbabwe, mozambique na angola kote tumemsaidia mnyonge kumpa utu wake. Hatu ruki waamerica wakisema turuke. Kama wewe wafikiria waamerika wakisema turuke turuke fikiria tena utu wako.
 
Kwa matazamo wangu labda ningejiuliza ' Kwanini Tanzania haijatoa msimamo kuhusu Libya' kuvunja au kuunga mkono ingetegemea msimamo wa nchi. Haitoshi kuwa na kauli ya jumla 'Membe- tunaomba pande mbili zisikilizane'. Tanzania ya zama hizo ilikuwa bold na kwa influence iliyokuwa nayo ndiyo iliyoshawishi muafaka wa mambo mengi barani Afrika.

Mwaka 1965 tulivunja uhusiano na uingereza na 'kuadhibiwa' kimisaada baada ya Ian Smith kupewa uhuru na kutambulika licha ya sera zake za kibaguzi. Hapa tulikuwa ni wachanga kuliko leo, yaani miaka 4 tu baada ya uhuru.

Mwaka 1973? tulivunja uhusuiano na Israel kwa suala la Palestina, na ikumbukwe miradi kadhaa ilikuwa chini yao.

1973? Tanzania iliwatambua waasi wa jimbo la Biafra kule Nigeria chini ya Ojuku. Tulikuwa katika diplomatic row na Nigeria.

Tluliunga mkono suala la POLISARIO kwa sababu za haki za kibinadamu kama ilivyokuwa kwa SWAPO, ANC,PAC, FRELIMO n.k. Hivi vilikuwa vyama vya kupigania uhuru na ukombozi.

Tuliunga mkono PAC na ANC kwa pamoja kwasababu ya kutetea haki za kibinadamu dhidi ya ubaguzi na wapo wakiendeleza taifa lao kwa njia ya sanduku la kura, kinyume na hapo RENAMO hawakukubalina na sanduku la kura na wao kuingia mitini baada ya lengo lililokusudiwa kutimia tena kwa gharama za maisha ya watu, lakini waliporudi kuwa chama cha kisiasa sidhani kama watabaguliwa wakaingia madarakani kwa kura.

Katika mkutano wa commonwealth nchini Zambia Nyerere akiwa mwenyekiti wa frontline states alimwambia malikia wazi msimamo wa nchi za Afrika hasa kusini kuhusu siasa za ubaguzi kule Afrika kusini na ni baada ya mkuatano huo ndipo nchi nyingi za magharibi zikaanza kupunguza kasi kuunga mkono ubaguzi hadi kutokomeza ubaguzi.

Mwaka 2009 tulipeleka wanajeshi Comoro kumuondoa Mohamed Bakar, na pia tulishawahi kupeleleka vikosi kumuokoa Albert Rene kule Sychelles.

Kwangu mimi sababu za kuunga au kutounga mkono zinaweza kutofautiana kutokana na mitazamo ya watu, kinachonisikitisha ni kuona sisi kama taifa sasa hatujui tunasimamia wapi, tumebaki kujibanza nyuma ya AU au UN. Hili ndilo linanitia wasi wasi kuwa huenda nguvu zetu kama taifa huru zimeanza kupotea kufuatia umasikini na omba omba, na hii ina set bad precedent kwasababu ukishaanza kuwa mnyonge na kutokuwa na kauli kama Botswana na nchi changa zaidi yetu inafikirisha sana, there is something wrong somewhere !
 
Nguruvi kinachonitisha mimi zaidi siyo tu ule ukimya ni hicho ulichokisema - hatujui tunasiimamia nini. Mtu mmoja amesema kuwa diplomasia yetu ya nje ni ya uchumi - hili lilikuwa tangu wakati wa Mkapa na Kikwete ameliendeleza. Yaani, hatujali tena suala la haki, utu, uhuru n.k Kuna neno baya limenijia kulitumia naogopa lakini linaendana na wale mabinti wanaozunguka strips ya Las Vegas wakijipamba vizuri na kujitangaza kuwa ni maescorts. Sera zao ni za kiuchumi na haijalishi sana uchumi huo unatoka kwa nani na kwa nini. Tanzania imekuwa kama hao kwamba tuko tayari kulala na yeyote na hatuwezi kumkemea hata kama anafanya mambo ambayo hatuwezi kuyaandika hapa. Hii ndio Tanzania chini ya CCM hii.

Inashangaza kwenye kikao cha Bunge hadi hivi sasa hakuna hata mbunge mmoja (wa CCM au upinzani) ambaye amejaribu kupush serikali yetu kuchukua msimamo ambao unaendana na historia yetu (kama ulivyoidodosa kidogo hapo) na amali zetu kama taifa. Kwanini wabunge hawafikirii mambo hayo? Au wanafikiria Tanzania ni kama kakisiwa fulani tu.
 
Nguruvi kinachonitisha mimi zaidi siyo tu ule ukimya ni hicho ulichokisema - hatujui tunasiimamia nini. Mtu mmoja amesema kuwa diplomasia yetu ya nje ni ya uchumi - hili lilikuwa tangu wakati wa Mkapa na Kikwete ameliendeleza. Yaani, hatujali tena suala la haki, utu, uhuru n.k

Hata diplomasia ya uchumi inatafsiriwa vibaya na baadhi yetu. Diplomasi inasimamia kila kitu kuanzia siasa, uchumi na tamaduni. Iliposemwa diplomasia yetu inaelekezwa katika uchumi ilimaanisha tuondoke katika utaratibu wa zamani ambao watu kama mabalozi walisubiri dhifa za kitaifa kutuwakilisha na sasa wajikite katika shughuli zitakazo kuza uchumi. Haikumaanisha tuache misimamo ya kitaifa.

Dunia ya leo huwezi kutenga uchumi na siasa kwani vinaingiliana sana. Nchini kama za magharibi ambazo diplomasia yao hasa ni uchumi, maamuzi mengi yanafanywa katika mazingira ya kisiasa. Hao IMF wanaosimamia sera za uchumi, moja ya mambo wanayoangalia ni sera za kisiasa zinazojumuisha uhuru, haki za binadamu, utu n.k

Enzi hizo mwalimu akiwa na akina Indira, na wenzake waliziambia nchi za magharibi hakuna uwezekano wa magharibi kushirikiana na nchi masikini, akahoji Tanzania inaweza kufungua tawi la bank New york? Wakashauri uundwe ushirikiano wa south-south naye akawa mwenyekiti mwenza. Juzi wakiwa south Africa viongozi wamekubaliana kuwa na ushirikiano wa cape-Cairo, legacy ya influence ya Tanzania.Hiyo ndiyo diplomasi ya uchumi.

Ni kwa misimamo yetu kuhusu masula ya kimataifa na kijamii tuliweza kujulikana tunasimamia wapi. Mambo kama nuclear disarmament, ukombozi, haki za binadamu n.k.Kama tulikuwa na ofisi za PLO upanga, FRELIMO Iringa, PAC na ANC Mazimbu na dakawa, tukaandamana kumpinga hayati Henry Kissinger na siasa zake za marekani , leo msimamo wetu ni nini kuhusu Libya?
 
Leo tunashindwa hata kuonesha displeasure kwa jinsi Ahmedinajad anawatendea wananchi wake au Assad anavyowapopoa wananchi wake lakini wapo watu wanalalamika ati Nyerere aliwaweka watu detention... !!!
 
Kwanza watanzania wa leo sio wale wa kwenda kupata kibali ikulu kwa kuweza kumiliki TV au Video ni siasa zilizopitwa na wakati, hatuwezi kutumia siasa Pafmeca za enzi za makaburu , siasa zile karne yake imepita na Tanzania imeonesha msimamo imara wka kutoyumbiswa na Hilary Clinton juu ya shinikizo lake kuwa Tuwatambue waa si wa Libya vipi watu ushawaita waasi leo uwatambue ?
Hatuwezi kutolewa kafara Watanzania kwa maslahi ya nchi fulani za magharibi ikiwa kweli nchi za magharibi wana uso wasiingeingiza ALGERIA NA PALESTINE KWENYE MGAWANYIKO usio na lazima Waislamu wa Algeria waliiangusha serikali yao kwa sanduku la kura ila western conspiracy kuwa waislamu wasiokuwa na mueleo wa western wasiachiwe kutawala ALgeria tumeona ALgeria ilivyoingia kwenye civil war baada ya wafaransa kulilazimisha jeshi la ALgeria kuchukua madaraka kwa nguvu na kina Abas Madani walioshinda uchaguzi kutupwa magerezeni, Haya Niambie huyo Nyerere angekau Rais wa Tanzania leo wakati Hamas imeshinda uchaguzi kule Palestine angeitambua serikal i ya HAMAS ingawa Rafiki yake Jimy carter alithibitisha kuwa HAMAS Wameshinda haya tupe msiamo wako juu ya siasa ya Palestine ni PLO au HAMAS ndio wanaotakiwa kuongoza nchi?
Watanzania hatuwezi kuwa kama kichwa cha mwendawazimu tukaendeshwa kwa intrest za nchi nyngine ni uwongo na unafik wa Western countries kutaka rasilimali za Libya na jinsi aliyo zi challnge nchi za mgharibi huu ndio ukweli Wazungu walipomuekea vikwazo mugabe , ni Ghadafi ndie aliemsaidia Mugabe na kwenye Policy za Mkapa alisema hatuwezi kumpinga Mugabe ingawa chama kinachompinga Mugabe kinatandikiwa zulia jekundu Dar kweney ikulu yetu jee siasa za nje za mkapa na Kikwete ni tofauti?
Hao kina MWanakijiji watueleze hao wapinzani wa Serikal i ya Libya wamepata wapi uhalalali wa kuitawala LIBYA lini wlaipigiwa KURA sikuambii Wamisri waliomuondoa Mubarak bado wanaipinga serikali ya Kijeshi ya Egypt kuwa haiko halali ni extra revolution imefanyika au mapinduzi yamekua highjacked na CIA na MOSSAD kuhakikikisha bado wana icontrol EGYPT .
Watanzania kuheshimika duniani hatuwezi kuheshimika kwani hatuna utamaduni wak uj iheshimu sisi wenyewe itakuaje tuheshimiwe na wengine ?
Tanzania sisi wenyewe tuna matatizo kwa nini tujiingize kwenye matatizo mengine bado serkali LIBYA haijabadilika huu ndio ukweli hata USA hawajawatambua wapinzani wa Gadafi itakuaje sisis vichuguu?
Nina uhakika licha ya Nyerere angekua hai basi licha ya kutokua na mapenzi na Ghadafi basi angeishangaza dunia kwani angehakikisha African Union ingekua na msimamo mmoja na angepinga ubeberu wa kupigwa mabomu nchi ya Libya kwa kisingizio cha regime change under UN na south Africa iisngepiga kura ku support resolution ile ni curse ya bara la Afrika kuivunja vunja Libya.
 
Unajua kutaka kila kiongozi afanye kila kitu kama alivyofanya Nyerere Miaka 40 iliyopita ni "insult" kwa akili za watu, Nyerere hajwahi kuwa mtu pekee anayejua solutions za matatizo yetu, wapo wengi lakini walikuwa kimya kwa kuogopa repercussions za kumuingage yule mzee katika fierce debates. Wewe Mwanakijiji unafahamu wazi kwamba kinachoendelea libya kuna ulterior motives za kuiba mafuta ya libya, halafu unakuja kuishauri serikali yetu iwe kibaraka wa wezi are you serious?. Hebu nikuulize Unataka serikali yetu iwatambue waasi, hebu niambie ni walibya wangapi wanawaunga mkono waasi?, ni asilimia ngapi ya walibya wanawunga mkono waasi?, ni kipi kinachowapa waasi legitimacy ya kuwa representatives wa libya?.atleast serikali ya sasa ya libya inayoongozwa na waziri mkuu imechaguliwa na watu kupitia councils zao, sasa wewe niambie ni system gani imewapa legitimacy waasi?. Mkjj fungua macho wewe, uone forces za neocolonialism zinavyofanya kazi, usiwe blinded na akina hillary clinton wanaokija africa na arrogance kuwaamrisha viongozi wetu "what to do with Africa". najua uko marekani na unaipenda sana, lakini hiki unachoadvocate ni hatari kwa uhuru wa Afrika!. Nyerere alimsapoti Savimbi at one time, Nyerere alifanya biashara na makuburu at some other time, Nyerere alikuwa independent minded, alifanya kile alichoamini ni sahihi, sasa waache viongozi wetu wafanye wanachoona ni sahihi at this time!. The other thing ni kwamba Nyerere alikuwa na jeuri ya kufanya vile kwa sababu ya cold war, pande mbili zenye nguvu za ussr na usa, kila mmoja akijaribu kuwin marafiki, kipindi hicho ungeweza kujialign na mmoja ukajihisi safe kiasi, sasa leo hii yupo mmarekani, utathubutu kumuwekea usiku katika maslahi yako atakuacha? Aisee siwezi kuamini nguvu za neocolonialism ni kali namna hii, zinatwist na kutongoza akili za watu wetu tunaoamini ni best. amka ndugu jikomboe kutoka katika utumwa mambo leo,maisha ya mtu, heshima na utu, vinasimama mbele kabla ya nadharia za kidemokrasi , capitalism, socialism na blah blah nyingine!
 
Sasa kwa nini Tanzania inashindwa kujitokeza wazi wazi na kusema inamuunga mkono Gadafi ?
 
Nguruvi kinachonitisha mimi zaidi siyo tu ule ukimya ni hicho ulichokisema - hatujui tunasiimamia nini. Mtu mmoja amesema kuwa diplomasia yetu ya nje ni ya uchumi - hili lilikuwa tangu wakati wa Mkapa na Kikwete ameliendeleza. Yaani, hatujali tena suala la haki, utu, uhuru n.k Kuna neno baya limenijia kulitumia naogopa lakini linaendana na wale mabinti wanaozunguka strips ya Las Vegas wakijipamba vizuri na kujitangaza kuwa ni maescorts. Sera zao ni za kiuchumi na haijalishi sana uchumi huo unatoka kwa nani na kwa nini. Tanzania imekuwa kama hao kwamba tuko tayari kulala na yeyote na hatuwezi kumkemea hata kama anafanya mambo ambayo hatuwezi kuyaandika hapa. Hii ndio Tanzania chini ya CCM hii.

Inashangaza kwenye kikao cha Bunge hadi hivi sasa hakuna hata mbunge mmoja (wa CCM au upinzani) ambaye amejaribu kupush serikali yetu kuchukua msimamo ambao unaendana na historia yetu (kama ulivyoidodosa kidogo hapo) na amali zetu kama taifa. Kwanini wabunge hawafikirii mambo hayo? Au wanafikiria Tanzania ni kama kakisiwa fulani tu.

Mkuu, wakati mwingine sio kila jambo duniani ni lazima ulitolee msimamo. Sometimes, conveniently silence or ambiguity is the best recourse.
Wewe unasema tuilaani serikali ya Gaddafi, lakini hapohapo umesahau kwamba hukohuko NATO ujerumani haikusupport military operations pale
awali, Russia na China ziliabstain wakiitafsiri kama kuingilia mambo ya ndani ya Libya.

Pili kuna suala la large oil reserves zilizopo libya, hili nalo muhimu kulitazama ili kujua motives behind this so called "humanitarian intervention", miezi michache iliyopita tuliona atrocities za ajabu zikitokea Ivory Coast, tena mtu akifanya outright disobidience of the law baada ya kushindwa uchaguzi, lakini we never heard all these "humanitarian interventions" wala nini sababu IvoryCoast sanasana watapata cocoa tu na sio oil.

Tatu ANC na SouthAfrica, ambao ndani ya UN security council, walikua deceived na fake intelligence kwamba Gaddhafi alikua on the outskirts za bengazi na kwamba massacre ya watu 700,000 ilikua imminent, wakavote in support ya "kuprotect civillians" the resolution ikawa hastily drafted
na kupelekwa council with lots of grey, ambiguous language, matokeo yake juzi hapa ANC wametoa tamko kulaani ile resolution kutumika kutaka
kufanya regime change in Libya na wanaandaa tamko la kulipeleka UN security council kucomplain.

Nne hii uprising ya Libya ilianzia Bengazi, sehemu ambayo bado wana uchungu wa mfalme wao aliyetolewa na Gadhafi madarakani, na ndio maana
hata waasi ukiwatazama wana bendera zao tofauti na ile ya Libya tunayoifahamu. In short kuna beef la chinichini kati ya utawala wa gadhafi na watu wa Bengazi fo decades now.

In short, i think the strategic ambiguity works well for Tanzania in the Libyan crisis, wacha wajisortout kwanza, wakishajulikana mshindi nani na wakatengeza serikali, tutawaunga mkono tu. At the moment kuna lots of factors playin in kiasi kwamba huwezi jua ukiamua kusupport blindly
hao rebels utakua unamtumikia nani bila wewe kujua.

My 2 cents
 
Nimelipenda hili jibu kwa kweli; naomba niliweka kwenye signature yangu.. !
Hamna taabu.
In short, i think the strategic ambiguity works well for Tanzania in the Libyan crisis, wacha wajisortout kwanza, wakishajulikana mshindi nani na wakatengeza serikali, tutawaunga mkono tu. At the moment kuna lots of factors playin in kiasi kwamba huwezi jua ukiamua kusupport blindly
hao rebels utakua unamtumikia nani bila wewe kujua.
My 2 cents
Wow, just goes to prove how low we have stooped, so low that we are eager to admit we have no pride left as a nation and so shamelessly brand our lack of stand a strategic ambiguity.

Tusubiri tuone ushindi unaelekea wapi ndio tuwaunge mkono, ili iweje ? Wasitunyime msaada ? Serikali yetu hii inayoshindwa kuchukua hata uamuzi dhidi ya inaowaita mafisadi na wezi ?

Si ajabu na wananchi sasa wanasubiri nani atashinda kati ya Kikwete na Lowassa ili wamuunge mkono ! Lakini tofauti na Libya ni ukweli kuwa vita ndani ya Libya inapiganwa kweli wakati hii ya kwetu ndani ya CCM ni usanii mtupu.
 
Mi nafikiri wewe ndo wa kulaumiwa sio Tanzania, wewe mwenyewe umesema wale ni" waasi wa libya" na huo ndio ukweli, sasa ni vipi tz na heshima zake zote hizi ilizonazo iwatambue waasi? hilo haliwezekani ndugu yangu. Wale ni waasi wa libya, na nchi zote zilizowatambua ni nchi ambazo zimefuata karoti kujipendekeza kwa marekani na nchi za magharibi, hamna lolote zaidi ya hapo. Hatuwezi kuwatambua waasi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kukaribisha uasi nchini kwetu, ile ni njia haramu na ni vibaraka tu hawana lolote wale.
Kweli kabisa, Mwanakatwe. Hawa waasi hawana utambulisho unaoekleweka. Kuna kila dalili kuwa siyo watu wengi katika Libya wanawaunga mkono. Vinginevyo Gaddafi asingekuwepo tena. Hivi kila kikundi kikijitokeza na kuasi serikali yake basi Tanzania inalo jukumu la kukiunga mkono? ANC, Frelimo, MPLA, n.k. those were different cases. Different causes, different era. Gaddafi anaweza kuwa amekaa madarakani kwa muda mrefu, hafuati demokrasia ya kimagharibi, bla bla bla, lakini kosa lake kubwa ni kwamba anakalia shehena kubwa ya mafuta ambayo haruhusu makampuni ya nchi za magharibi ziyamiliki moja kwa moja. Tanzania haina haja wala ulazima wa kuwatambua wahuni wa Benghazi. Bila NATO wale wangekuwa wameishaangamizwa. Hivi hayo mabomu ya NATO yana macho hayaui raia bali mizinga ya Gaddafi ndiyo inaua raia tu? Silaha za waasi je? Give me a break.
 
Hakika umenena... Yapaswa kuwalaumu hao Angola na Senegal na hao Botswana maana hebu jiulize Africa ina nchi ngapi? Waliowatambua Waasi ni wangapi? Kwanini kitu halali kinatambuliwa na wanafiki wachache? Carrot zipatikanazo Libya(oil). Ndio shida ya western countries kupitia mgongo wa UN maana Un ni US na US ni un,hao waafrika wenzio maskini wa akili na kipato ndio maana wanawafuata wajanja matajiri na wenye upeo(NATO), WAASI MAANA YAKE UNAIJUA? unafahamu asili Yao? Unafahamu mipango na mikakati iliandaliwaje na wapi hapo awali? Sera Yao unajua ni ipi ? Wanaekiongozi si ndiyo? Maana yake wanatetarajia awe kiongozi, nani kasema kiongozi anajipa? Libya nzima haimpendi Gaddafi? Hujui labda na inawezekana umefunikwa ndani ya mfumo wa mawasiliano ya kimagharibi na vyombo vya habari vya kwao vyenye nia ya kueneza propaganda zao.. UNAFAHAMU MAMBO KUMI YANAYOWAFANYA NATO WAMPINDUE GADDAFI KWA KIVULI CHA WAASI? Angekuwa mbaya wananchi wa Libya wasingekuwa wanapata huduma za afya bora sambamba na Ufaransa na kuzizidi nchi zote za middle east.....
 
Mwanakijiji,
Halafu nani atatujengea misikiti na kutuletea tende?.....au hukumsikia Mufti wetu alipolalama Libya kudundwa?
 
Kweli kosa la Gaddafi ni kutofuata demokrasia na mfumo wa kisiasa wa kimagharibi na kuzuia uizi wa mafuta ya Libya... Wengine woote wezi wa kimya kimya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom