Mkuu hoja yako na wote walioiunga mkono ya kutokuupigia kura haina mashiko hata kidogo maana inaonyesha dhahiri umefikiria hatua moja mbele, naamini ungetulia kidogo na kufikiri miaka hata mitano mbele basi ungekuwa wakwanza kuupigia na kushawishi wengine waupigie kura pia....................kwani unadhani CCM watatawala milele?
Timiza wajibu wako kama mzalendo wa nchi hii maana kesho na keshokutwa wajibu wako utawasidia CUF au CDM au TLP au yeyote atakaye shika dola kuja kufaidi na matunda ya uzalendo wako

Pga kura MAFSADI Wanufaike
Maajabu ya dunia? Hivi watu wa Kilimanjaro wanauona mlima Kilimanjaro kuwa ni maajabu! Ni maajabu kwa wao wazungu wanaoshangaa theluji kuonekana katika mlima uliopo TZ!
Kuna safari ndefu kwa wabongo kuelewa mambo, haya ya wazungu na theluji ya mlima kili yanauhusiano na kupiga kura? Hamjui tunapozungumzia utalii tunazungumzia biashara ya ki-ulimwengu?, kwa taarifa yako Tanzania inapata kura kwa kupigiwa na watalii na siyo wabongo. Asilimia 5% tu ya wabongo/wa Tz ndio hutembelea vivutio vya Tanzania na mliochangia mada hii 000000000.1% yawezekana ndio mmefika angalau Hifadhi moja ya Taifa au Ngorongoro tena mlipokuwa mwanafunzi mkilipiwa na wazazi wenu, du!
Mkuu muheshimiwa ngaranumbe amekujibu vema kabisa hapa chiniMkuu tutimize wajibu Upi? Mkuu Sekta ya Utalii haijawahi kuwanufaisha Watanzania na Si dhana kama itakaa iwanufaishe, Chukulia Mfano wa Kule Serengeti, Kuna yule Mzungu wa SINGITA alipewa Kipande cha Iliyo kuwa Ikorongo Game resertve kwa MIAKA 99 mkuu unategemea nini hapo? na Mkijaribu kuvunja inakula kwenu ndo inakuwa yale ya RICHMOND kupelekana mahakama za Kimataifa za BIASHARA,
Kule LOLIONDO waarabu ni kama wako kwao, wanaua wanyama wanavyo taka, wanatorosha wanyama wanavyo penda yaani wao ndo wana amua waue wangapi na kwa stail gani,
MIMI SITAKAA NIPIGE KURA KWA SBABU SIONI FAIDA YAKE
Uliyeleta uzi huu hukujiandaa vyema, elewa hata usipopiga kura yako moja kakuna pigo. Suala hapa ni umaarufu wa vivutio na siyo wivu kwa wawekezaji, hakuna uhusiano na hoja yako. Hata kama eneo halikunufaishi halijiondoi kwenye ushindani, ndio maana tunarudi nyuma eti wakenya wanatangazia vivutio vyetu. Kama wewe hutambui vivutio vyako usilalamike eti Kenya wanadai mlima kilimanjaro uko kwao. Je serikali ya Tanzania ikugawie kiasi gani uli upige kura yako moja( kakura kamoja). Jipange, hapa ni voting. ebo!
Kuna safari ndefu kwa wabongo kuelewa mambo, haya ya wazungu na theluji ya mlima kili yanauhusiano na kupiga kura? Hamjui tunapozungumzia utalii tunazungumzia biashara ya ki-ulimwengu?, kwa taarifa yako Tanzania inapata kura kwa kupigiwa na watalii na siyo wabongo. Asilimia 5% tu ya wabongo/wa Tz ndio hutembelea vivutio vya Tanzania na mliochangia mada hii 000000000.1% yawezekana ndio mmefika angalau Hifadhi moja ya Taifa au Ngorongoro tena mlipokuwa mwanafunzi mkilipiwa na wazazi wenu, du!
Mkuu muheshimiwa ngaranumbe amekujibu vema kabisa hapa chini
Mkuu Chasha unachanganya vitu viwili tofauti kabisa. Swala la kuupigia mlima Kilimanjaro na swala la ufisadi wa sekta ya utalii,
madai yote unayosema kuhusu ufisadi ni ya kweli kabisa lakini sasa unatakiwa kuja mambo haya
Dunia inautaratibu wake wa kutambua mambo fulani fulani ambayo yanaleta tija, leo hii mamilioni ya watu wanakwenda Misri kuangalia mapiramidi, wanakwenda india kuangalia sijui nini, wanakwenda mto amazon kuangali, wanakwenda mlima everest kuangalia nk nk, hivyo vivutio vilipitia michakato hii hadi leo vinanufaisha wananchi wa maeneo husika hata kama wakati vinapigiwa kura vilikuwa chini ya utawala gani
Kinachokutatiza wewe ni ubovu wa usimamizi wa rasilimali hizi lakini tambua ukipiga kura yako leo na mlima ukashinda basi kimataifa utakuwa umeupa chati ambayo itasaidia zaidi watalii kuja kutaka kuona maajabu hayo na mapato yake yataisaidia serikali ya CDM huko mbeleni itakapo kuja kusimamia mapato ipasavyo, kumbuka kura haipigwi kila mwaka...only once
Ni nafasi yako sasa kuufanya mlima Kilimanjaro kuwa ajabu la dunia kama mzalendo wa kweli maana kuufanya hivyo ni kuja kuirahisishia itakayokuja kuwa serikali ya CDM kupata mapato zaidi ya utalii pindi itakapochukua nchi hii miaka kadhaa mbeleni.
Na usipopiga basi utabaki mlima wa kawaida ambao mapato yake yatakuwa kiduchu na kuja kuikosesha serikali ya CDM Mapato hapo mbeleni
Na ndio maana nikakwambia umefikiria hatua chache sana mkuu
Mkuu Kwanza si dhan kama Maajabu yote Duniani yalipigiwa Kura, Kwani Mto kama Amazon hata Bila Kupigiwa Kura si Inajulikana tu ulivyo? Kilimanjaro inajulikana ndo Mlima pekee wenye theluju na ulio Mrefu Balaani Africa,
Chukulia Mfano Wa ZANZIBAR, Zanzibar ilisha Ingizwa kwenye Urithi wa Dunia na Inatambuliwa Na UNESCCO, ila hata huko Zenji wanafaidika na Utalii wa Zanzibar ni WAZUNGU, ndo hao wanamiliki Mahoteli ya Kitalii ufukweni zanzibar na si Wazanzibar,
MKUU ISHU SI MAPATO, ISHU NI JE WATANZANIA WANGAPI WANA ENDESHA BIASHARA ZA KITALII? ISHU SI WATANZANIA WANGAPI WAMEAJIRIWA HUKO?
Mkuu si dhani kama Unajua Mapato ya Hoteli kama za Serena Zilizoko Ngorongoro, Manyara na Serengeti, ni Makubwa kuliko Pesa inazo Ingiza Hifadhi kama Ya Serngeti kwa Mwaka,
Kinacho sikitisha ni kwamba, Watanzania Hawajawezeshwa kuwa Waendeshaji wakuu wa shughuli za Kitalii, na matokeo yake wamechiwa Wazungu, Na hata watalii wakimiminika kama NZIGE watakao faidika ni WAZUNGU