CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,789
- 8,914
Wakuu mimi sitapiga kura kwa ajili ya Kutafuta Kivutio cha Tanzania Kitakacho Ingia Kwenye Maaajabu saba ya Bara La Africa kwa sababu zifuatazo,
1. Hifadhi za Taifa na Vivutio vingine havijawahi kunufaisha Watanzania
2. Watakao Nufaika na Hizo Kura ni Viongozi wa Ngazi za Juu pamoja na Wazungu, Ndo maana wazungu wako mbele sana kwenye kuhamasisha,
3. Hii kampeni ni neema kwa Wazungu na si Watanzania, sisi tutabakia kwenda kuomba vibalua tu kwao
4. Hoteli zote zilizo Jengwa kwenye Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro zinamilikiwa wa wageni kwa asilimia 100, hakuna mzawa mmoja mwenye hoteli huko hata Camp tu,
5. Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Zinginezo wanawathamini sana Watalii wa Kizungu na si Watanzania, watalii wa kitanzania huwa hawapewi umuhimu wowote ule katika hizo hifadhi, na Kuna Kipindi Hifadhi ya Ngorongori iliwahi kujenga Vyoo kwa ajili ya Wazungu na vingine kwa ajili ya Watu weusi/wabongo,
Na hadi leo hii Abilia wabongo wanaosafiri kwa Mabasi kwenda Musoma huwa wakifika Geti la Ngorongo hawaruhusiwi kutumia vyoo vya wageni bali kuna vya kwao viko Geti No 1 ukiwa unatokea Karatu kuingia Hifadhini
- Wakuu Sekta ya Utalii hapa Tanzania Inaongozwa na Wazungu Kutoka Ulaya, Marekani, South Africa na Wahindi, na watanzania ni wachache sana kwenye hii secta na wengi ni wafanya kazi tu na si wamiliki wa Makampuni ya utalii,
-Mlima Kilimanjaro- Huu Mlima wanao nufaika nao ni Makampuni ya Kitalii ya Wazungu yenye Makao makuu yao Mjini Arusha na Moshi, na asilimia zaidi ya 98 ya Makampuni ya Kitalii kanda ya Kasikazini yanamilikiwa na wazungu na ni asilimia kama 2 tu ndo inayo milikiwa na Wabongo na hata hivyo kampuni za wabongo ni Ndogo sana Kiuwezo ikilinganisha na Za wazungu
Makampuni mengi ya Kitalii yana Offisi huko kwao Ulaya na Marekani na Booking zote na Payment hufanyika huko huko Ulaya na Marekani huku wageni huja kupanda Mlima tu na mara nyingi na pesa za kununulia Vinyago na kuwapa Tips Madreva wanao waendesha, sasa je TRA inawezaje kukagua mapato ya hawa watu wakati acaunt ziko Ulaya na Marekani? na Malipo yanafanyika hukohuko Ulaya?
JE HAPO ANAYE NUFAIKA NI NANI?
2. HIFADHI YA SERENGETI
Hii nayo ni Hifadhi ya Taifa kwa Jina tu ila kimatendo wanao iongoza ni Wazungu kutoka Ulaya wa Frankfurt Zoological society, hawa ndo wana usemi wa mwisho kuhusu hizi hifadhi na si Serengeti pekee bali hata Ngorongoro, wakiongea hakuna wakupinga kitu na Maranyingi wamekuwa wanakuja na Policy za kuwakandamizaWatanzania na kuwaona wanyama ndo wana haki pekee na si watanzania
3. Ngorongoro- hii nayo ni jina tu kwamba ni Hifadhi ya Taifa ila kimatendo hii hifadhi ni kama Limited Company,
Kwa kifupi wanaonufaika na Hifadhi na Vivutio vingine ni Wazungu na Watanzania Wachache wanao Torosha Wanyama kwenda Nje ya Nchi, Wananchi wengine tumebakia Mashabiki wa kuhamasishwa kupiga kura tu,
Ni iliaumu sana Serikali kwa kuto kuwezesha Watanzania wazawa Kumiliki Makampuni na Badala yake Makampuni yanamilikiwa na Wazungu, na wazawa wamebakia kuwa Vibarua