Kwanini "Service charge" ya TANESCO ni tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka!

Naomba kisahihisha kwa wanao tumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi gharama ya umeme ni Tsh 100, na hawa ni wateja wa Tariff4 (T4). Unit zikizodi 75 wakati yupo T4 zile unit zilizozidi mteja analipia Tsh 350.

Na mteja wa T4 hana service charge na hawa ni low usage customer.

Ni kweli ni unyonyaji sana lakin siku hzi tanesco wamepunguza gharama kwa watu wanaotumia chini ya unit 75 per month unatolewa service charge ewura na rea na unit moja unanunua 150 per month nenden mchekiwe kwenye system issue ni nyumba za kupanga matumiz huwa makubwa sana kuliko mwenye nyumba yake
a
 
Ha
Mkuu hapa Arusha tumejaza fom siku nyingi kubadili hiyo tariff lakini hakuna kitu nimruliza naambiwa watu ni wengi wameomba kubadilisha ila wamegoma ili wapate hela

Hakuna mtu anaegoma/ shirika haligomi naomba uni PM namba ya simu tuwasiliane, tatizo lililopo unakuta mteja anasema anatumia chini ya unit 75 kwa mwezi ukifuatilia unakuta matumizi yake ya mwezi ni zaidi ya hizo unit.

Kumbuka ukitumia zaidi ya unit 75 utanunua umeme kwa gharama ya Tsh 350
 
Service charge ni wizi tu , mbona kwenye huduma binafsi hakuna hii kitu? Tungeambiwa basi tukipanda mabasi tulipie gharama za matairi, mafuta ama malipo kwa dereva na gesti tulipe chumba kisha kitanda na gharama za usafi. Kuna wajanja walishataka kuleta huu mchezo kwenye line za simu zilipiwe kila mwezi sh 1000 mbona hili jambo lilipingwa.
 
Wabunge na wadau wa maendeleo wetu hamlioni hili? Wananchi wanalalamika mbona mpo kimya? Huu ni wizi wa mchana service charge ni jipu,branch managers wa tanesco ni majipu yanahitaji kutumbuliwa ASAP,unawaandikia barua wakubadilishie kwenda low usage tariff zaidi ya miezi 6 hawajibu wakati statistics za usage ya meter yangu inaonyesha natumia umeme less than 75 per month.

✅Wabunge na Wadau wa maendeleo tusaidieni,fanyeni Kama mbunge wa kinondoni alivyowasaidia wananchi wake wa Kino wasibomolewe ma nyie pelekeni hoja binafsi bungeni kufuta huu wizi maana Hiyo 5500 na EWura na rea wanakula wajanja kina Singh na matapeli wenzake walioingia mkataba kiujanja na iptl mwaka 1995.

Cc: John Mnyika , Halima Mdee , Julius Mtatiro ,Balile , Kubenea , Pascal Mayalla , Manyerere Jackton , Henry Kilewo , Zitto

Mkuu tatizo halitatuliwi namna hiyo, naomba uni PM mita namba yako, na namba yako ya simu ili tuweze kuwasiliana.

Unapo unganishiwa umeme unatakiwa kukaa miezi 6 ndio uombe kubadili Tariff kwani hapo tunaweza kuangalia matumizi ya mteja kwa miezi sita.
 
Service charge ni wizi tu , mbona kwenye huduma binafsi hakuna hii kitu? Tungeambiwa basi tukipanda mabasi tulipie gharama za matairi, mafuta ama malipo kwa dereva na gesti tulipe chumba kisha kitanda na gharama za usafi. Kuna wajanja walishataka kuleta huu mchezo kwenye line za simu zilipiwe kila mwezi sh 1000 mbona hili jambo lilipingwa.

Hili ni kwamba service charge ni ajili ya kulipia gharama zote za dharula na zisizo za dharula kwa mfano unapopata tatizo lolote hutozwi gharama yeyote ile ila pesa hiyo ndiyo kazi yake, mita yako ikipata tatizo hutozwi chochote bali unabadilishiwa bure. Service charge inawahusu watu Wa tariff T1 hadi T3.

Hapo hakunawizi wowote
 
Halafu tulitegemea hao Ewura watutetee lakini wapi.Wanakusanya mihela kibao,halafu hawana wanachofanya kutetea walaji.
 
Service haipaswi kuwepo kabisa, for what? Hii ni kitu hatukupaswa kuwa tunajadili humu na kukipotezea muda kwasababu hakikupaswa kuwepo kabisa. Sasa hivi tulipaswa kuwa tunajadili mambo mengine kama tu tungekuwa na viongozi makini na wazalendo. Kimsingi service charge hiyo ijumlishie na muda huu tunaoutumia kuijadili. Hii ni aibu kubwa sana kutumia mamlaka na madaraka kuwaibia wananchi, kwasababu tu ya unyonge wao, hakuna wanachoweza kukufanya. Naichukia service charge na nimeiongelea mara kadhaa sehemu tofauti tofauti. DR JPJM, TUNATAKA UTUONDOLEE AIBU HII.
 
Kwanza naomba usipotezwe na maneno ''service charge'' ufikirie ni gharama ya Tanesco kuja nyumbani kwako kufanya service. Hizi fedha zinatozwa kwa sababu ya gharama za ku-mantain zile line za umeme kutoka kwenye source ya umeme mpaka pale nyumbani kwako. Kwa kifupi ni gharama za ku-transmit umeme kutoka from the source to the end point. Ni kama unavyoagiza pizza ukiwa nyumbani... inabidi ulipe gharama ya pizza na gharama ya kuletewa. Na hii service charge ipo sehemu nyingi duniani. Mara yangu ya kwanza kuishi nchi moja Europe nilichukua likizo ya miezi mitatu. Niliporudi nilikuta bill ya umeme inanisubiri (tulikuwa tunalipa bill kila baada ya miezi mitatu). Ilikuwa ni bill ya kipindi kile ambacho sikuwepo. Nikaenda kuulizia vipi nichajiwe umeme ambao sijatumia? Jibu nililopata ni ''hizi ni gharama za service! Yaani utumie umeme au usitumia, lakini kama umeingia contract ya kununua umeme wao ni laizima kuna basic cost ambayo utalipa plus gharama ya umeme. Labda uniambia kuwa hizo gharama za service ni kubwa sana Tanzania nitakubali...
Mkuu umechanganya aina ya huduma.Huko Ulaya hata mimi nilikaa kwa muda mrefu, ukiwa unatumia huduma ya kulipia kwa muda maalum (Contract) hizi tozo huwa zipo na haijalishi umetumia umeme au laa. Lakini kwa huduma ya malipo ya kabla (Prepaid services) haupati tozo ya aina yeyote ile. UNALIPIA UNACHOTUMIA TU!!!. Hivyo basi haya makato ya "Service charge" TANESCO walitakiwa wayapeleke kwa watumiaji wa umeme wenye mita za zamani (wanaolipa kwa mwezi) na sio watumiaji wanaotumia LUKU.
Nina mashaka na "Europe" uliyokaa wewe!!
 
Hili ni kwamba service charge ni ajili ya kulipia gharama zote za dharula na zisizo za dharula kwa mfano unapopata tatizo lolote hutozwi gharama yeyote ile ila pesa hiyo ndiyo kazi yake, mita yako ikipata tatizo hutozwi chochote bali unabadilishiwa bure. Service charge inawahusu watu Wa tariff T1 hadi T3.

Hapo hakunawizi wowote
kwa nini mnalazimisha hizo gharama ziwe pre paid? Mfano mimi, tangu nianze kujitegemea sijawahi pata tatizo wala kuwaita Tanesco. Kwa miaka yote hiyo nimelipa Service charges. Huu ni wizi boss. Ni wizi kabisa mchana kweupe. Kwa nini nisilipe ninapohitaji na sio kunilazimisha kulipa kila mwezi? Mfano kwa wapangaji mwenye kulipa gharama zs matatizo ya umeme ni mwenye nyumba lakini ninyi mnamkata mpangaji. Hivi kwa nini mnalazimisha hiyo Service charge iwe pre paid?
 
Wakuu,shida ya Tanesco ni matumizi yao ya anasa ,niliwahi pata tenda moja ndogo pale tenesco head office,ofisi zote ziko na friji na zaidi ofisi za mameneja ni flat tvs na dstv decoders yaani Si zile ofisi za umma tulizozizoea ,Kwa lifestyle ya pale lazima tuumizwe Kwa kulanguliwa umeme.
 
Mkuu hapa Arusha tumejaza fom siku nyingi kubadili hiyo tariff lakini hakuna kitu nimruliza naambiwa watu ni wengi wameomba kubadilisha ila wamegoma ili wapate hela

Kuomba kubadilishiwa tariff nayo imekuwa deal kwa kipindi hiki. Walibahatisha walioomba mwanzoni. Ukiomba kwa kipindi hiki unaambiwa kuwa matumizi yako ni makubwa wakati unakuwa umeishajitathimini mwenyewe katika matumizi yako ya miezi 3.

Ukiwapa pesa unabadilishiwa tariff haraka tu. Hii inafanyika hapa Morogoro. Yote wizi mtupu.!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu sio kweli unachokiongea, naomba unisaidie mita namba pamoja na namba ya simu.

Ntaweza kuangalia matumizi yako kwa muda wa miezi mitatu nyuma iili kujua matumizi yako, kuna wateja wengi ambao huwa wanalalamika lakini ukiangalia matumizi yake kwenye system unakuta anatumia zaidi ya hizo unit 75 kwa mwezi.

Pia iwapo matumizi yako yakizidi unit 75 kwa mwezi utanunua umeme kwa 350 kwa unit.

Wateja wengine wamekuwa wasumbufu leo anaomba kubadilishwa kesho anaomba atolewe tena.
 
kwa nini mnalazimisha hizo gharama ziwe pre paid? Mfano mimi, tangu nianze kujitegemea sijawahi pata tatizo wala kuwaita Tanesco. Kwa miaka yote hiyo nimelipa Service charges. Huu ni wizi boss. Ni wizi kabisa mchana kweupe. Kwa nini nisilipe ninapohitaji na sio kunilazimisha kulipa kila mwezi? Mfano kwa wapangaji mwenye kulipa gharama zs matatizo ya umeme ni mwenye nyumba lakini ninyi mnamkata mpangaji. Hivi kwa nini mnalazimisha hiyo Service charge iwe pre paid?

Kama hujapata tatizo kunawatu wengine wanapata, na pesa hizo ndio hutumika kutoa huduma.

Pia huwezi kujua leo hujapata lakini kesho ukapata tatizo.
 
Regulator kama EWURA hawezi tetea walaji au kuwabana Tanesco sababu mkate wake unatokana na watumiaji Wa huduma ambozo ewura wanazisimamia.
 
Service haipaswi kuwepo kabisa, for what? Hii ni kitu hatukupaswa kuwa tunajadili humu na kukipotezea muda kwasababu hakikupaswa kuwepo kabisa. Sasa hivi tulipaswa kuwa tunajadili mambo mengine kama tu tungekuwa na viongozi makini na wazalendo. Kimsingi service charge hiyo ijumlishie na muda huu tunaoutumia kuijadili. Hii ni aibu kubwa sana kutumia mamlaka na madaraka kuwaibia wananchi, kwasababu tu ya unyonge wao, hakuna wanachoweza kukufanya. Naichukia service charge na nimeiongelea mara kadhaa sehemu tofauti tofauti. DR JPJM, TUNATAKA UTUONDOLEE AIBU HII.

Hili ni kwamba service charge ni ajili ya kulipia gharama zote za dharula na zisizo za dharula kwa mfano unapopata tatizo lolote hutozwi gharama yeyote ile ila pesa hiyo ndiyo kazi yake, mita yako ikipata tatizo hutozwi chochote bali unabadilishiwa bure. Service charge inawahusu watu Wa tariff T1 hadi T3.
 
Kama hujapata tatizo kunawatu wengine wanapata, na pesa hizo ndio hutumika kutoa huduma.

Pia huwezi kujua leo hujapata lakini kesho ukapata tatizo.
Kwa nini nimlipie mtu mwingine aliyepata tatizo? Kwa nn msifanye anayepata tatizo alipe yeye mwenyewe? Na kwa nn mnalazimisha nilipe kila mwezi hata kama sijapata tatizo? Mkinilipisha ninapohitaji hiyo service yenu ni sawa kabisa ila mnaponilazimisha kulipia huduma ambayo sijaitumia huoni kama ni wizi? Okay sawa nimelipia mwaka mzima sijapata tatizo hizo hela mwapeleka wapi? Hamna kingine mnachojua zaidi ya kutoa huduma mbovu kukata umeme bila taarifa na hakuna anayeona ni tatizo au hiyo tabia ya kukata kata umeme ndo service charge yenyewe? Naombeni huu vizi muusitishe kidogo ikiwezekana mbadili na jina mjiite TADASCO-Tanzania Dark Supply Company tutawaelewa vizuri fikirieni njia mbandala Tanzania na resources zake ni aibu kununua umeme kutoka Uganda.
 
Back
Top Bottom