Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

sijakiona kigezo secific cha lowassa kua rais nchi hii na ndo maana hata afya yake inakataa
 
Tunapokuwa vyuoni tunaambiwa jiepushe na vitabu vilivyozidi umri wa miaka 10. Sasa na nyerere mawazo yake hayawezi kuwa sawa hadi leo.
nadhani kwenye hivyo vitabu biblia na Quran lazima vimo kwani vina umri zaidi ya miaka 10......vmeandikwa na watu ujue!
 
hivi huyu mzee lowasa akikosa urais ....na alivyo mgonjwa vile na mabilioni aliyomwaga ...sijui hali yake itakuwaje .....na vurugu la humo ndani ccm sitaki hata kusikia wakimtosa huyu jamaa inaonekana watu wamechota hela zake sana
 
twenden tusahau ya nyerere we respect him he is not our god, can make mistakes like anyother human being. so we don cream for nyerere ideas and stand kama tunaona mtu ni mzuri lazima tumchague. sishangai ukiwa bumbuu..!! wtu hatakuzungumzia lakin ukiwa potential lazima upate changamoto kama lowasa. silipwi kama mnaokukuruka just my stand.
 
one say of lowasa will change rumours, we need more audio visual information not your imaginative narration(we needs video/clips).
 
Mwaka 1995 katika kinyanganyirocha urais tz yalijitokeza majina 17 ya wanaccm waliotaka kupitishwa na chamahicho. Mmoja kati ya wagombea hao alikuwa ni ndg edward ngoyai lowassa aka laighwanan wakati huo wakati huo akiwakijana wa miaka 42. Mwalimu alijua fika kwamba lowassa ni fisadi mkubwa na kamailivyokuwa kwa mwalimu daima hakumungunya maneno na mbele ya kamati kuuakatamka kuwa lowassa na malecela wakipitishwa yeye anarudisha kadi yake ya ccmno.

1. Majina hayo yakakatwa fasta!!Mwaka 2005 malecela kwa kujuanyerere kaishafariki hivyo njia kwake ni nyeupe akatia timu tena mbele yakamati kuu bila kujua kuwa minutes za kamati kuu za 1995 bado zipo!! Matokeoyake mzee mzima akaangukia pua mbele ya kamati kuu!!Rais J.m. Kikwete alipuuza usiawa baba wa taifa na kumteua lowassa kuwa waziri mkuu wa tz.

Matokeo yake yakutotii usia wa baba wa taifa, lowassa akaweka rekodi ya kuwa waziri mkuualiyekaa kipindi kifupi kuliko wote.lowassa sasa eti anataka kuwarais wa tz!!! Kamati kuu minutes za 1995 bado zipo na kama kwa kamati kuu kutumiarushwa lo-rushwa kumpitisha lowassa basi laana ya nyerere itawatafuna wajumbewoote wa kamati kuu na nchi nzima italaanika!!



MSOME KATIBU WA MWALIMU NYERERE
MZEE SAMWELI KASORI

AKISIMULIA JUU YA MAHUSIANO YA MWL NYERERE NA LOWASSA....Mfuatilie

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma’. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.
Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!
Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”
Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”

Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.

Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!

Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.


Hili bandiko limeshiba!!!! Anayebisha aje aseme! Huo ndiyo ukweli kama anamasikio na asikie!
 
Ukweli uko wazi kuwa Nyerere alimkataa Lowasa kwasabu ya dini, kitabu cha siri cha Nyerere kinasema: Ni heri Mbuzi awaingoze wana CCM kuliko Mkristo kuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM. Jiulize ni raisi yupi wa TZ mkristo? ndo utajuu kuwa Nyerere alikuwa nani . Back Tanganyika.

I wish to know more
 
Huyu Lowassa huyu.......ana tesa mioyo ya watu wengi sana......

Tunapokuwa vyuoni tunaambiwa jiepushe na vitabu vilivyozidi umri wa miaka 10. Sasa na nyerere mawazo yake hayawezi kuwa sawa hadi leo.

Mbona EL anawakosesha sana usingizi? Hivi ni nani msafi ndani ya ccm wa kumnyoshea mwenzake kidole?

Lowasa ndio rais ajaye, hakuna cha nyerere wala nani. Nyere kisha kufa na usia wake hauna maana yeyote. Hii nchi itakaa sawa kama Lowasa atakua Rais.
Kutokana na ombi lako nilimtuma Kasori akuambie usiwe mjinga kama Lowasa...JK..
'Kutokana na comment zako naituma JF ikuambie usiwe mjinga kama .......'
 
Unajua sikuwahi kuwaza kwamba Lowassa anaweza kuwa raisi...

But mnavyomtajataja naona jina lake linazidi kupanda ngazi kwa list niliyo nayo kichwani...

Kila baada ya thread inayofuata ni Lowassa... daah
 
Hakuna kitu ambacho nakisubiri kwa hamu kama ccm kumsimamisha Lowasa uraisi 2015. Ukawa watakuwa na urahisi mno kwenye kampeni zao.
 
Wana CCM ! Kwa nini wagombea urais wa makundi yote na wafuasi wao wanaungana kumpiga vita vya kila aina Mhe.E. Lowasa ?
 
Alafu unafiki mwingine ni mbaya sana.Hivi Nyerere ni Mungu?Inamaana hakuwahi kukosea.Kwa hiyo kama nyerere alimchukia mtu basi wote tumchukie mtu huyo?Acheni kushikiwa akili nyie

uchawi ni mbaya kuliko vitu vingine,nyerere alilijua hilo lakini akaona ni sahihi,lowasa mcha Mungu kumbukeni nabii hakubaliki ni hila kisa yeye tajiri,sasa kawachia nini familia yake,mbona hakuweza kuwngua uwaziri mkuu aliopewa poor thinking ya wala viroba
 
Lowassa ni chaguo la mungu mtampinga ila hamtashinda, Ameanza Diallo na wengine mnaendelea siku zote mti wenye matunda ndo hupopolewa, Go go Edward
 
"Siku moja akitokea kiongozi wa Taifa letu, akatuambia huko nje kuna hela nyingi kuliko hapa nyumbani, mwambieni wewe ni mpumbavu" Mwl J.K. Nyerere

"Unapoenda kuomba siyo kwamba wewe unapenda tu kuomba, huko nje kuna mataifa yenye hela nyingi tu, unachotakiwa ni kujieleza, wakikuelewa watakupa" Jakaya Kikwete

"Kama kuna mtu ambaye anaamini nchi hii inaweza kuendelea kwa kusaidiwa, anajidanganya, narudia tena, katika nchi hii kama kuna kiongozi anaamini nchi hii inaweza kuendelea kwa kupewa misaada, anajidanganya" Benjamin Mkapa
 
Back
Top Bottom