Kwanini mawaziri wapya wa JK wanaingilia Bodi za wakurugenzi?

Ebu imagine mtu kama Msekwa yuko kwenye sijui bodi gani sijui ila nijuacho iyo bodi inadeal na utalii!
HUyu mtu toka miaka ya 1960 yuko serikalini ana kipi kipya mpaka anaendelea kuwemo.
Ukifuatilia sana bodi ni kwa ajili ya kulipana fadhira na vijiwe vy washikaji wa mkuu wa nchi

msekwa ana pensheni kibao lakini hatosheki
 
Hii ndio kazi ya Zitto Kabwe, tunamtegemea kuwakaanga hawa jamaa vizuri kadiri inavyowezekana.
 
1) sikatai kabisa atcl ilifanya madudu mengi sana katika nyanja zifuatazo:-

a) uteuzi wa wakurugenzi waandamizi bila ya kufuata taratibu.

B) ukodishaji wa ndege kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa hasara za mabilioni.

Hapa na pale anakuja waziri mwakyembe - huyu ni mpya kabisa kutoka dukani - badala ya kuiwajibisha bodi inayoongozwa na mustafa nyang'anyi yeye anawawajibisha watendaji waandamizi kazi ambayo siyo yake ni ya bodi ya wakurugenzi.

Mimi nilifikiri waziri shupavu atakachofanya ni kuiondoa bodi ya wakurugenzi kwa kuhalalisha madudu lakini yeye anairuka bodi iliyoko ndani ya uwezo wake na kuingilia kwenye majukumu ambayo yako nje ya uwezo wake na kuyafanya! Huu kweli ndiyo utawala bora?

2) sikatai kwenye shirika la tbs upo ushahidi wa kutosha wa ya kuwa tbs kufanya madudu makubwa ambayo yameligharimu taifa zaidi ya mabilioni 30.

Sasa waziri mpya kabisa naye kanunuliwa kwa bei mbaya kutoka dukani anakuja kuiagiza bodi ya tbs kumsimamisha kazi mtendaji mkuu kwa minajili ya kupisha uchunguzi, kazi ambayo bodi hiyo walipaswa waifanye na hawakuifanya.

Kwa lugha nyingine bodi tajwa imeshindwa kulisimamia shirika tajwa na ndiyo ilipaswa kufanya kazi na imechelea kwa sababu wazijuazo wao. Huu kweli ni utawala bora wa kuacha kuwajibisha chombo kilichoko ndani ya uwezo wa waziri na kuingilia bodi kwenye majukumu yake?

Sababu kubwa ya kuziweka bodi za wakurugenzi ni kupunguza na kufifilisha wanasiasa kuendesha taasisi za umma kwa minajili ya kukidhi mahitaji yao ya muda mfupi ya kisiasa.

Pamoja na nia nzuri ya kufuta ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ndani ya taasisi za umma lakini mawaziri hawa wapya wa jk wanapovunja taratibu kwa visingizio kuwa lengo ni kurekebisha makosa siyo sahihi hata kidogo. Huwezi kuvunja sheria na kutumia visingizo vya kuboresha wakati wewe mwenyewe ni mkosaji tu............

Nionavyo mimi ni kuwa hawa mawaziri wapya wa jk wanawaogopa wenyeviti wa bodi kwa sababu hawakuwateua wao bali wameteuliwa na raisi. Wanaogopa kuhatarisha posho yao n ahivyo wanzilinda bodi za wakurugenzi lakini wanaelewa pia ili kuulinda mlo wao lazima wachukue hatua na hivyo kusababisha huu muingiliano wa majukumu ambao unakatzwa na sheria.

Hivyo badala ya kuwaondoa watajwa hao basi mawaziri wanawaingilia kwa kufanya yale ambayo wao mawaziri wanataka yafanyike kwa sababu zao za kisiasa na hivyo kufifilisha maana nzima ya kuwa na hizi bodi za wakurugenzi ambazo zinatugharimu mapesa mengi sana katika kuzikarabati.




ndicho anachotaka rais wetu.....hataki kufanya maamuzi magumu.....,kwahiyo inawabidi mawaziri waangilie powers za rais za kuwafukuza kazi wateule wake....,wanaogopa kupendekeza ...wamsubiri rais achukue hatua yasije yakawakuta ya waziri wa zamani chami............ambaye kitendo chake cha kusubiri protocal ifanye kazi ....yaani apate bord resolution ...ya kupendekeza mkurugenzi wa tbs aondolewe toka bodi ya wakurugenzi ndio yeye aandike ministerial paper kwa rais kupendekeza uteuzi utenguliwe ilimgharimu.....

So kilichobaki sasa ni mawaziri kufukuza fukuza tu .....hakuna kusubiri bodi wala nini .....,lakini ifahamike kuwa mwenye uwezo wa kumfukuza kazi mteule tena hata bila ya kulazimika kutaja sababu ni rais pekee.....waliobakia wote wanatakiwa wafuate utaratibu.....wa kumshauri rais achukue hatua[sasa tatizo ni pale rais anapochelewa kuchukua hatua au hata kuchelewa kusoma madokezo
]
 
Inasemekana wakurugenzi ndo waliosababisha mawaziri wenzao kuwajibishwa!
Wapo makini kweli!

Naam wmeyaona yaliyowapata wenzao kutokana na uzembe wa BoD, sasa hawataki kabisa kucheza nazo mbali.
 
Hii ndio kazi ya Zitto Kabwe, tunamtegemea kuwakaanga hawa jamaa vizuri kadiri inavyowezekana.

Kasheshe Zitto hajahoji juu ya mwingiliano wa Waziri na Bodi yake............
 
Last edited by a moderator:
ndicho anachotaka rais wetu.....hataki kufanya maamuzi magumu.....,kwahiyo inawabidi mawaziri waangilie powers za rais za kuwafukuza kazi wateule wake....,wanaogopa kupendekeza ...wamsubiri rais achukue hatua yasije yakawakuta ya waziri wa zamani chami............ambaye kitendo chake cha kusubiri protocal ifanye kazi ....yaani apate bord resolution ...ya kupendekeza mkurugenzi wa tbs aondolewe toka bodi ya wakurugenzi ndio yeye aandike ministerial paper kwa rais kupendekeza uteuzi utenguliwe ilimgharimu.....

So kilichobaki sasa ni mawaziri kufukuza fukuza tu .....hakuna kusubiri bodi wala nini .....,lakini ifahamike kuwa mwenye uwezo wa kumfukuza kazi mteule tena hata bila ya kulazimika kutaja sababu ni rais pekee.....waliobakia wote wanatakiwa wafuate utaratibu.....wa kumshauri rais achukue hatua[sasa tatizo ni pale rais anapochelewa kuchukua hatua au hata kuchelewa kusoma madokezo
]
[MENTION]
Phillemon Mikael[/MENTION] sijasema mawziri wanamwingilia raisi kwenye majukumu yake bali wanawaingilia Bodi ambazo zinawajibika kwao..............badala ya kuziwajibisha Bodi wanaziogopa na hivyo kuzifundisha namna ya kufanyakazi kukidhi mahitaji yao binafsi......................ya kisiasa
 
Naam wmeyaona yaliyowapata wenzao kutokana na uzembe wa BoD, sasa hawataki kabisa kucheza nazo mbali.

BAK kama wako sahihi basi Bodi zifutwe na Waziri asimamie taasisi zilizoko chini yake moja kwa moja............kuna uhaja gani kuzifadhili hizi Bodi kumbe ni waziri ana mkono wake na wao wako picha tu?
 
Last edited by a moderator:
1) Sikatai kabisa ATCL ilifanya madudu mengi sana katika nyanja zifuatazo:-

a) uteuzi wa wakurugenzi waandamizi bila ya kufuata taratibu.

b) Ukodishaji wa ndege kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa hasara za mabilioni.

Hapa na pale anakuja Waziri Mwakyembe - huyu ni mpya kabisa kutoka dukani - badala ya kuiwajibisha Bodi inayoongozwa na Mustafa Nyang'anyi yeye anawawajibisha watendaji waandamizi kazi ambayo siyo yake ni ya Bodi ya wakurugenzi.

Mimi nilifikiri waziri shupavu atakachofanya ni kuiondoa Bodi ya wakurugenzi kwa kuhalalisha madudu lakini yeye anairuka Bodi iliyoko ndani ya uwezo wake na kuingilia kwenye majukumu ambayo yako nje ya uwezo wake na kuyafanya! Huu kweli ndiyo utawala bora?

2) Sikatai kwenye shirika la TBS upo ushahidi wa kutosha wa ya kuwa TBS kufanya madudu makubwa ambayo yameligharimu taifa zaidi ya mabilioni 30.

Sasa Waziri mpya kabisa naye kanunuliwa kwa bei mbaya kutoka dukani anakuja kuiagiza Bodi ya TBS kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu kwa minajili ya kupisha uchunguzi, kazi ambayo Bodi hiyo walipaswa waifanye na hawakuifanya.

Kwa lugha nyingine Bodi tajwa imeshindwa kulisimamia shirika tajwa na ndiyo ilipaswa kufanya kazi na imechelea kwa sababu wazijuazo wao. Huu kweli ni utawala bora wa kuacha kuwajibisha chombo kilichoko ndani ya uwezo wa waziri na kuingilia Bodi kwenye majukumu yake?

Sababu kubwa ya kuziweka Bodi za wakurugenzi ni kupunguza na kufifilisha wanasiasa kuendesha taasisi za umma kwa minajili ya kukidhi mahitaji yao ya muda mfupi ya kisiasa.

Pamoja na nia nzuri ya kufuta ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ndani ya taasisi za umma lakini mawaziri hawa wapya wa JK wanapovunja taratibu kwa visingizio kuwa lengo ni kurekebisha makosa siyo sahihi hata kidogo. Huwezi kuvunja sheria na kutumia visingizo vya kuboresha wakati wewe mwenyewe ni mkosaji tu............

Nionavyo mimi ni kuwa hawa mawaziri wapya wa JK wanawaogopa wenyeviti wa Bodi kwa sababu hawakuwateua wao bali wameteuliwa na Raisi. wanaogopa kuhatarisha posho yao n ahivyo wanzilinda Bodi za wakurugenzi lakini wanaelewa pia ili kuulinda mlo wao lazima wachukue hatua na hivyo kusababisha huu muingiliano wa majukumu ambao unakatzwa na sheria.

Hivyo badala ya kuwaondoa watajwa hao basi mawaziri wanawaingilia kwa kufanya yale ambayo wao mawaziri wanataka yafanyike kwa sababu zao za kisiasa na hivyo kufifilisha maana nzima ya kuwa na hizi Bodi za wakurugenzi ambazo zinatugharimu mapesa mengi sana katika kuzikarabati.



Nadhani kuna kasoro nyingi sana za kiutendaji kwenye mufumo wa utawala wetu, ifike mahala wanasiasa wasipewe nafasi ya kuingilia wataalamu wetu na badala yake wafanye kazi wanazotakiwa kufanya.

Sijui mamlaka ya uteuzi wa watendaji wa mashirika ya umma lakini kama waziri anaweza kuwasimamisha wakuu wa idara wa shirika la umma nadhani kuna tatizo kwenye mfumo wa namna hii kwani ningetegemea majukumu ya uteuzi/kufukuza ya waziri au rais yakomee kwenye bodi, basi! Bodi iachwe iwawajibishe au kuwateua wataalamu kwenye shirika husika
 
WKM hivi mwenyekiti wa Bodi unamsimamisha au unamwondoa kwani analindwa na sheria ipi ya ajira?

Mkuu,Wenyeviti hawalindwi na sheria yoyote zaidi ya mamlaka iliyomteua na unajua JK alivyokuwa slow kuchukua hatua wakati muafaka..nadhani kwa ATCL ilibidi Mwakyembe atumie nguvu mpaka zinapoishia kwa ajili ya kulinda mustakabali wa Taifa huko angani..ila kwa TBS bodi iliyopo sasa hivi haina hata miezi miwili ikizingatiwa kwamba hili timbwili ni la mwaka wa fedha ulioisha..!

Nadhani kuna haja ya kubadili utaratibu wa kuwajibishana uwe wazi kiasi kwamba mtu anajua akifanya fyongo ajue consequence zake ni zipi na sio kama ilivyo sasa.. watu wanarushiana mipira kama tulivyoona katika ishu ya Jairo! Niliskia wakati fulani kutaanzishwa bodi kwa ajili ya kuangalia ufanisi wa haya mashirika ya umma kwa pamoja na kupendekeza njia mbadala iwapo kuna tatizo ili lishughulikiwe mapema sijui iliishia wapi..! Japo inaweza kuongeza gharama nadhani ingekuwa inawasaidia watoa maamuzi nini cha kufanya kwa wakati muafaka!
 
Hii nchi sijui tutajigundua lini? hakuna lililojema, wakati kina Chami wanasulubiwa kwa kutokuwashulikia TBS, watu walilalamika, leo kigoda amechukua jitihada inakuwa amevunja sheria, hapo ndipo tunapo potezea mwelekeo na kazi inabaki kulalamika tu. Nashawishuka kuamini kuwa tatizo letu watanzania siyo viongozi, bali sisi wenyewe na uongozi, maana hata wale tuliotarajia ni wazuri kuwa viongozi bado hakuna kinachofanyika wakiingia wanaaza kusikiliza majungu na kuanza kujihami kwa kuweka makundi ambayo matokeo yake ni uhasama na kuanza kuwindana, ikitokea mmoja amekosea inakula kwake, then anakuja mwingine anaaza mipango mipya maana iliyokuwepo kwake siyo kipaumbele, naye akae mwaka aondoke aje mwingine. Binafsi nadhani hili ni tatizo kubwa, kubadilishwa kwa viongozi kila siku ndiyo mwanzo wa kukwamisha mipnago yote ya maendeleo kwa kuwa hakuna hata tathmini inayofanyika kuona nini kimefanyika bali tunaangalia eneo moja tu amekula ngapi
 
Nadhani kuna sababu kwa nini EKELEGE alikuwa anaogopwa sana ,mie nadhani huyu mzee ana kauchawi fulani. ushahidi upo wazi kabisa na watu walijitolea tayari kuwa mashahidi tena kwa gharama zao lakini jamaa ndio kwanza alipanda ndege kwenda japan. Nadhani pale ndio Kigoda akaona huu upuuzi sasa akakata zote, ekelege chali!
 
Nadhani kuna sababu kwa nini EKELEGE alikuwa anaogopwa sana ,mie nadhani huyu mzee ana kauchawi fulani. ushahidi upo wazi kabisa na watu walijitolea tayari kuwa mashahidi tena kwa gharama zao lakini jamaa ndio kwanza alipanda ndege kwenda japan. Nadhani pale ndio Kigoda akaona huu upuuzi sasa akakata zote, ekelege chali!

chilisosi kumbe wewe ni muumini wa ushirikina..............mimi siamini hata chembe nijuacho mwanadamu anataliwa na chapaa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom