Kwanini mawaziri wapya wa JK wanaingilia Bodi za wakurugenzi?

Waziri - KCU amemsimamisha kazi DG wa Bodi ya Pamba wakati ambao msimu unatakiwa kufunguliwa na bei ya pamba kutangazwa. System ime-paralyse hadi waziri mwenyewe anaonekana hajui cha kufanya. Bodi ilitakiwa kuwajibika kwa kushindwa kumwajibisha DG. Hii serikali sasa ndo inazidi kuwa kichekesho. Wasipostuka sijui km watafka 2015.

[MENTION]WKM[/MENTION] hivi mwenyekiti wa Bodi unamsimamisha au unamwondoa kwani analindwa na sheria ipi ya ajira?
 
Hapo umenena lakini kumbuka Wenyeviti/Wakurugenzi wanateuliwa na Raisi baada ya kushauliana na Waziri wa wizara husika, tatizo linakuja pale uteuzi unakuwa niwa kisiasa kisiasa badala ya kiutendaji na ndiyo maana inakuwa vigumu kwa waziri anayeteuliwa au kuhamishiwa kwenye wizara na kuikuta bodi hiyo ya wakurugenzi ambayo mara nyingi huteuliwa kisiasa kisiasa. Waziri kisheria anakuwa amepewa madaraka ya kuiwajibisha lakini "kisiasa", anakuwa hana hayo madaraka. Hapa ndo tunarudi kwenye tatizo la Raisi kuwa na madaraka makubwa.

masahihisho kidogo tu...........kuna baadhi ya Bodi mawaziri husika huteua wenyeviti wa bodi na wajumbe wake na kuna baadhi ni Raisi..................lakini hakuna Bodi ambayo Raisi huteua wajumbe wa Bodi hiyo ni kazi ya waziri husika..............
 
Nchi yetu inamatatizo makubwa sana kwenye governance kiasa kwamba watu hawaheshimu mipaka ya kazi zao tena. kwa ATCL haina bodi kwani ilishamaliza muda wake na sasa ni zaidi ya mwaka shirika linaendeshwa kimagumashi.
TBS kulindana kwingi kulianzia waziri hadi bodi kwani wajumbe si kawaweka waziri.

kinachotakiwa kifanyike kama sekta binafsi kwamba waziri angeteua wajumbe wa bodi kisha miongoni mwao wachague wenyewe mwenyekiti kisha wakabidhiwe shirika na wao ndio wafanye interview ya Mkurugenzi wa shirika(Kama hamna) ambaye atawajibika kwao. sio huu mtindo bodi kaweka waziri mkurugenzi kaweka waziri/raisi nani atawajibika kwa nani? wakurugenzi wanaviburi kwa bodi kama nini maana haijamuweka hapo.

Mnama kwa kiwango fulani ninaafiki na hoja zako. kkwa maoni yangu badala ya waziri kuteua wajumbe tuangalie washika dau wa kila sekta watusaidie kujichagua kam awadau khalafu majina wampelekee waziri utaratibu uliopo unamlazimisha waziri achague watu kwa kukidhi mahitaji ya kisiasa tu na wala siyo kukidhi mahitaji ya taasisi husika na matokeo yake bodi hushindwa kuzidhibiti menejimenti ambazo hugeuka na kuzitawala Bodi ..............ninaafiki wajumbe wa Bodi wapewe meno ya kuchaguana nafasi ya uenyekiti lakini wajumbe watokane na wadau wa sekta husika kwa kuchaguana kutumia taratibu za wazi na zenye kuheshimu misingi ya demokrasia.........
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwanini taratibu sizibadilishwe ili wenyeviti/ wakurugenzi wa bodi mbali mbali wawe wanateuliwa na mawaziri wa wizara husika ili pindi waziri ama mtendaji anapo vurunda waziri aonekane wazi wazi kufanya kazi..japokua kutakua na kukingiana kifua lakini hii itawamwaga sana watendaji wa mashirika ya umma kwa kutolewa kafara na bodi za wakurugenzi..mazashit!-

tatizo lipo palepale kwa sababu bado wanasiasa watamshinikiza kuteua mtu wao kwa sababu wanazozijua wao tu.................nionavyo bodi ziundwe na wadau wa sekta husika na kati yao wateue mwenyekiti na hapo nguvu ya wanasiasa kutuyumbisha kupitia uteuzi wa bodi utakuwa umefikia ukomo wake..................
 
ulaji................................ wameshapewa hint kwamba ulaji wao unaanzia kwenye bodi za wakurugenzi
 
Jamani eeeeeh Kazi itangazwe, wenye vigezo na uwezo waombe, interview ifanyike,naa aliyefaulu apewe kazi period ! huu umagumashi wa kuteuana ndio longolongo zinaanzia hapo na ubesti,undungunization dinilization na kabilarization na mengineyo yapoleta mushkeli.....
 
Sikubaliani na wewe kuhusu hili. Kuna mifano mingi tu ambayo inaonyesha kuwa wakati mwingine ni vizuri kuvunja sheria kwa manufaa ya umma katika mazingira yanayohitaji utekelezaji wa haraka ili kujipanga upya badala ya kusubiri taratibu za kisheria ambazo zinachukua muda mrefu kuzikamilisha. Kumbuka sheria zetu mara nyingi ni mbovu na zinahitaji marekebisho( sisemi kama ndiyo excuse) lakini hiyo ni sheria ya hekima na busara katika mazingira kama hayo.

Huu mtazamo wako kuwa ni halali kuvunja sheria kwa manufaa ya umma ni wa hatari sana kwa manufaa ya umma. Hivi ni nani anatafsiri sahihi ya maslahi ya umma? Je kumwachia waziri mamlaka ya kutafsiri maslahi ya umma kisha kuchukua hatua zinazokwenda kinyume na sheria ni mwelekeo sahihi kwa utawala bora wa nchi? Vipi kama tafsiri yake itakuwa imelenga kumnufaisha yeye na watu wachache wanaomzunguka kuna "checks and balances" zipi?

Kumbuka hata kwenye kashfa ya Richmond baadhi ya wakubwa walitumia hoja hiyohiyo ya kuvunja sheria kwa manufaa ya umma kumbe umma kwa tafsiri yao ni matumbo yao wenyewe na ya marafiki zao.

Kwa mtazamo wangu wanachofanya hawa mawaziri ni MICRO MANAGEMENT ya taasisi zilizo chini ya wizara zao kitu ambacho siyo sahihi. Kama kwa mtazamo wao Bodi za Wakurugenzi hazifanyi kazi basi wawajibishwe wajumbe wa bodi na wenyeviti kwa madudu yanayofanyika kwenye taasisi wanazozisimamia. Kama bodi hazijateuliwa ni vyema tukajulishwa ni nini hasa kinachochelewesha uteuzi wa wajumbe na wenyeviti wa bodi hasa kwenye hii wizara ya uchukuzi? Vinginevyo ni bora ikajulikana wazi ikiwa hizi bodi hazihitajiki basi ili zifutwe kabisa na hizi taasisi zirudishwe wizarani.

NB: Najua mawaziri hawawezi kuwawajibisha wajumbe na wenyeviti wa bodi za taasisi za umma kwa sababu zimeshageuzwa kuwa vijiwe vya viongozi wazee waliokwishastaafu kazi na marafiki wa karibu wa mawaziri wanaowateua.
 
Bro umeonyesha mawazo mazuri yenye nia njema na mlengo wa kimaendeleo. Nimependa hayo. Lakini kuna jambo moja dogo nalo ni kuwa MWENYEKITI WA BOARD huteuliwa na Rais na hivyo Waziri hawezi kumuondoa mwenyekiti. Jambo la msingi ni kuwa Waziri ameanza na wengine wafuate kwa kutekeleza wajibu wao. TUMPONGEZE WAZIRI KWA UJASIRI.
 
1) Sikatai kabisa ATCL ilifanya madudu mengi sana katika nyanja zifuatazo:-

a) uteuzi wa wakurugenzi waandamizi bila ya kufuata taratibu.

b) Ukodishaji wa ndege kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa hasara za mabilioni.

Hapa na pale anakuja Waziri Mwakyembe - huyu ni mpya kabisa kutoka dukani - badala ya kuiwajibisha Bodi inayoongozwa na Mustafa Nyang'anyi yeye anawawajibisha watendaji waandamizi kazi ambayo siyo yake ni ya Bodi ya wakurugenzi.

Mimi nilifikiri waziri shupavu atakachofanya ni kuiondoa Bodi ya wakurugenzi kwa kuhalalisha madudu lakini yeye anairuka Bodi iliyoko ndani ya uwezo wake na kuingilia kwenye majukumu ambayo yako nje ya uwezo wake na kuyafanya! Huu kweli ndiyo utawala bora?

2) Sikatai kwenye shirika la TBS upo ushahidi wa kutosha wa ya kuwa TBS kufanya madudu makubwa ambayo yameligharimu taifa zaidi ya mabilioni 30.

Sasa Waziri mpya kabisa naye kanunuliwa kwa bei mbaya kutoka dukani anakuja kuiagiza Bodi ya TBS kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu kwa minajili ya kupisha uchunguzi, kazi ambayo Bodi hiyo walipaswa waifanye na hawakuifanya.

Kwa lugha nyingine Bodi tajwa imeshindwa kulisimamia shirika tajwa na ndiyo ilipaswa kufanya kazi na imechelea kwa sababu wazijuazo wao. Huu kweli ni utawala bora wa kuacha kuwajibisha chombo kilichoko ndani ya uwezo wa waziri na kuingilia Bodi kwenye majukumu yake?

Sababu kubwa ya kuziweka Bodi za wakurugenzi ni kupunguza na kufifilisha wanasiasa kuendesha taasisi za umma kwa minajili ya kukidhi mahitaji yao ya muda mfupi ya kisiasa.

Pamoja na nia nzuri ya kufuta ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ndani ya taasisi za umma lakini mawaziri hawa wapya wa JK wanapovunja taratibu kwa visingizio kuwa lengo ni kurekebisha makosa siyo sahihi hata kidogo. Huwezi kuvunja sheria na kutumia visingizo vya kuboresha wakati wewe mwenyewe ni mkosaji tu............

Nionavyo mimi ni kuwa hawa mawaziri wapya wa JK wanawaogopa wenyeviti wa Bodi kwa sababu hawakuwateua wao bali wameteuliwa na Raisi. wanaogopa kuhatarisha posho yao n ahivyo wanzilinda Bodi za wakurugenzi lakini wanaelewa pia ili kuulinda mlo wao lazima wachukue hatua na hivyo kusababisha huu muingiliano wa majukumu ambao unakatzwa na sheria.

Hivyo badala ya kuwaondoa watajwa hao basi mawaziri wanawaingilia kwa kufanya yale ambayo wao mawaziri wanataka yafanyike kwa sababu zao za kisiasa na hivyo kufifilisha maana nzima ya kuwa na hizi Bodi za wakurugenzi ambazo zinatugharimu mapesa mengi sana katika kuzikarabati.

ndo walikoambiwa madudu mengi yanafanyika yanayoweza kuwaharibia kazi zao bila wao wenyewe kuharibu.. ndo maana wanabadili na kuweka watu 'wao'. akija mwingine nae atabadilisha vile vile...
 
Jamani eeeeeh Kazi itangazwe, wenye vigezo na uwezo waombe, interview ifanyike,naa aliyefaulu apewe kazi period ! huu umagumashi wa kuteuana ndio longolongo zinaanzia hapo na ubesti,undungunization dinilization na kabilarization na mengineyo yapoleta mushkeli.....

Mnama ukoi sahihi tunahitaji kwenye katiba mpya kuweka vigezo vya namna utumishi wa umma utakavyokuwa ukiendesha shughuli zake kwa taratibu za uwazi na shirikishi ili kuondoa upendele o unaotokana na kujuana...........
 
Last edited by a moderator:
Jamani eeeeeh Kazi itangazwe, wenye vigezo na uwezo waombe, interview ifanyike,naa aliyefaulu apewe kazi period ! huu umagumashi wa kuteuana ndio longolongo zinaanzia hapo na ubesti,undungunization dinilization na kabilarization na mengineyo yapoleta mushkeli.....

serikali imekuwa kama shamba la bibi, vile..lol
 
Bro umeonyesha mawazo mazuri yenye nia njema na mlengo wa kimaendeleo. Nimependa hayo. Lakini kuna jambo moja dogo nalo ni kuwa MWENYEKITI WA BOARD huteuliwa na Rais na hivyo Waziri hawezi kumuondoa mwenyekiti. Jambo la msingi ni kuwa Waziri ameanza na wengine wafuate kwa kutekeleza wajibu wao. TUMPONGEZE WAZIRI KWA UJASIRI.

MZALENDO MKUU 2 mimi nachelea kumpongeza waziri kwa kutotumia bodi yake ifanye kazi hata kama muda umeisha alipaswa aiongezee muda hadi nyingineyo itakapoteuliwa........................asitumie loopholes kufanya atakavyo...........
 
Last edited by a moderator:
Hayo ndo madhara ya kumrundikia raisi madaraka!
Imagine bodi zote zilizopo yeye kateua ivi atakuwa na umakini gani kama sio kuvurunda tuu ktk uteuzi ofcourse excluding zama za Nyerere
 
Huu mtazamo wako kuwa ni halali kuvunja sheria kwa manufaa ya umma ni wa hatari sana kwa manufaa ya umma. Hivi ni nani anatafsiri sahihi ya maslahi ya umma? Je kumwachia waziri mamlaka ya kutafsiri maslahi ya umma kisha kuchukua hatua zinazokwenda kinyume na sheria ni mwelekeo sahihi kwa utawala bora wa nchi? Vipi kama tafsiri yake itakuwa imelenga kumnufaisha yeye na watu wachache wanaomzunguka kuna "checks and balances" zipi?

Kumbuka hata kwenye kashfa ya Richmond baadhi ya wakubwa walitumia hoja hiyohiyo ya kuvunja sheria kwa manufaa ya umma kumbe umma kwa tafsiri yao ni matumbo yao wenyewe na ya marafiki zao.

Kwa mtazamo wangu wanachofanya hawa mawaziri ni MICRO MANAGEMENT ya taasisi zilizo chini ya wizara zao kitu ambacho siyo sahihi. Kama kwa mtazamo wao Bodi za Wakurugenzi hazifanyi kazi basi wawajibishwe wajumbe wa bodi na wenyeviti kwa madudu yanayofanyika kwenye taasisi wanazozisimamia. Kama bodi hazijateuliwa ni vyema tukajulishwa ni nini hasa kinachochelewesha uteuzi wa wajumbe na wenyeviti wa bodi hasa kwenye hii wizara ya uchukuzi? Vinginevyo ni bora ikajulikana wazi ikiwa hizi bodi hazihitajiki basi ili zifutwe kabisa na hizi taasisi zirudishwe wizarani.

NB: Najua mawaziri hawawezi kuwawajibisha wajumbe na wenyeviti wa bodi za taasisi za umma kwa sababu zimeshageuzwa kuwa vijiwe vya viongozi wazee waliokwishastaafu kazi na marafiki wa karibu wa mawaziri wanaowateua.

Tata uko sahihi hakuna aliyejuu ya sheria.........................waziri anayekaidi sheria analenga kuleta vurugu na upendeleo sehemu ya kazi kwa manufaa yake binafsi tu...........hakuna utaifa kwa yeyote anayejichukulia sheria mkononi.........
 
Last edited by a moderator:
Hayo ndo madhara ya kumrundikia raisi madaraka!
Imagine bodi zote zilizopo yeye kateua ivi atakuwa na umakini gani kama sio kuvurunda tuu ktk uteuzi ofcourse excluding zama za Nyerere

Njowepo uko kwenye mstari hapo.............katiba mpya kama itakuwepo basi haya majeraha inabidi iyatibu..........
 
Last edited by a moderator:
ulaji......................... ....... wameshapewa hint kwamba ulaji wao unaanzia kwenye bodi za wakurugenzi

TIMING Bodi za wakurugenzi zimekuwa ni nafasi nyingine ya wanasiasa kujaza wapambe zao na hata mahawala hujazwa huko wakapate mshiko wa kulea familia zao...........
 
Last edited by a moderator:
Ebu imagine mtu kama Msekwa yuko kwenye sijui bodi gani sijui ila nijuacho iyo bodi inadeal na utalii!
HUyu mtu toka miaka ya 1960 yuko serikalini ana kipi kipya mpaka anaendelea kuwemo.
Ukifuatilia sana bodi ni kwa ajili ya kulipana fadhira na vijiwe vy washikaji wa mkuu wa nchi
 
ulaji......................... ....... wameshapewa hint kwamba ulaji wao unaanzia kwenye bodi za wakurugenzi

tunakazi kubwa katika kuirekebisha nchi hii.....................tujikite katika kuangalia kwa makini mfumo mzima wa uendeshaji nchi badala ya kuwa watumwa wa vyama vya siasa...............
 
Back
Top Bottom