Kwanini makanisa hayaoekani kutoa misaada kwa waliokumbwa na mafuriko?

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.
 
Tayari makanisa yameisha ipunguzia serikali mzigo kwa kusaidia huduma za jamii kwa kiasi kisisichomithilika. Ni jukumu la serikali na taasisi zingine kusaidia pia.
 
Hii imetulia Kamanda!
Aseme lingine kama analo.
 
Pia nafikiri wanachoshwa na results za uongozi Mbaya wa serikali! Wanawaacha Wa-clear their own mess!
 
imeandikwa. . 'nawe utoapo sadaka mkono wako wa kushoto usijue litendalo mkono wako wa kuume'
 
Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.

Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..
 
Tayari makanisa yameisha ipunguzia serikali mzigo kwa kusaidia huduma za jamii kwa kiasi kisisichomithilika. Ni jukumu la serikali na taasisi zingine kusaidia pia.
Nakubaliana na wewe kuwa makanisa yanatoa huduma nyingi za jamii. Kuna mashule, hospitali n.k vinamilikiwa na makanisa. Lakini bado naona vitu hivyo ni 'vitegauchumi' na ukijaribu kuangalia mfano shule zinazomilikiwa na kanisa ni very expensive! Sasa hapo msaada uko wapi?
 
imeandikwa. . 'nawe utoapo sadaka mkono wako wa kushoto usijue litendalo mkono wako wa kuume'

They are not "event driven person" but they got strategies and they know when to do what!!!!! Kutoa kajimsaada kisha kukimbilia kwene media ni ulimbukeni!!!!!

Haya ndio majibu sahihi. Na ninyi mnaojitia kuuliza ndio mnaofanya watu wakisaidia watoto yatima wanataka na waandishi wawapige picha. Huo ni ulimbukeni.

Kuna kampuni kubwa ya simu ilikataa kuacha misaada kwenye kituo cha Jangwani (jengo la Yanga) kwa kuwa waandishi wa habari/wapiga picha hawakuwepo. Imagine inatia hasira kiasi gani? :angry:
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

Wewe ni muumini uchwara. I'm sorry to say that. Tunafundishwa mkono wa kushoto ukitoa, hata wa kulia usijue umetoa nini.

And just for the sake of knowlegde. Something to ponder: If you don't see it, it doesn't mean its not happening!
 
Uongo at its highest point! Hujawahi kusikia msaada wowote wa Katoliki? Then quit kutoa sadaka. I guess hata elimu na afya uliyonayo kama si wewe basi mmoja wa ndugu zako ni courtesy ya kanisa
 
hivi huu utaratibu wa kuwasaidia watu wanaojitakia majanga umeanza lini!??
Mimi hata hata angekuwa ndugu yangu amepata mafuriko pale jangwani, nisingemsaidia....coz, ningekuwa nimeshamwambia asiishi pale, na kama ameendelea kutaka ku-enjoy kodi ya sh 4,000 kwa mwezi basi, apige mbizi sasa.
 
Yeah, nilikua nafanya kazi moa fulani kipindi fulani, tukawa tunaenda kutoa msaada kwa watoto yatima na wazee, eti ikatoka hoja kwamba ni lazima media iwepo ili jamii ijue kwamba tunatoa msaaada, kwa hasira siku ya tukio nkiansingizia kuumwa. I always find it nonsense mtu kutoa msaada kisha kujitangaza kwene media. Ni Ujinga na udhalilishaji wa hali ya juu, kwa mfano, mfanyabiashara fulani tapeli tapeli hapa mjini kipindi fulani alienda kutoa msaada wa vifaa fulani kwa polis na akaita media na vijeba vyote vya polisi walipokuwepo pale, hivi huyu mtu ambaye ametoa zawadi kibao tena mbele ya bosi wenu na bosi nae kammwagia masifa kibao, keshokutwa wewe polisi ukiambiwa nenda kamkamate utaweza kweli???
Haya ndio majibu sahihi. Na ninyi mnaojitia kuuliza ndio mnaofanya watu wakisaidia watoto yatima wanataka na waandishi wawapige picha. Huo ni ulimbukeni.

Kuna kampuni kubwa ya simu ilikataa kuacha misaada kwenye kituo cha Jangwani (jengo la Yanga) kwa kuwa waandishi wa habari/wapiga picha hawakuwepo. Imagine inatia hasira kiasi gani? :angry:
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada...
Inaelekea ukiwa kanisani huwa unachunguza nani anaenda kutoa sadaka na nani haendi kutoa, tena unaangalia nani anatoa shilingi ngapi !!! Hebu tuwekee majina ya taasisi zilizotoa, maybe na wewe umo tukupongeze!
 
Nakubaliana na wewe kuwa makanisa yanatoa huduma nyingi za jamii. Kuna mashule, hospitali n.k vinamilikiwa na makanisa. Lakini bado naona vitu hivyo ni 'vitegauchumi' na ukijaribu kuangalia mfano shule zinazomilikiwa na kanisa ni very expensive! Sasa hapo msaada uko wapi?

Huna lolote! Ungekuwa RC kama unavyojisingizia, ungejua ngazi mbalimbali za misaada kuanzia unapoishi hadi kwenye ngazi ya taifa.

Wewe siyo RC wala siyo mkristo na bahati mbaya sana huna hata akili ya kufanya utafiti kidogo ukajua kanisa linavyofanya kazi ndipo utunge hiki ulichotunga.

Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.

Kanisa limeona serikali yote iko hapo na imetoa mpaka na jeshi kusaidia hao ambao ndio huwa wanaonekana kuwa ndio Watanzania halisi. Nenda huko vijijini kulikosahauliwa ndio utaona kazi ya kanisa wanajua kuwa hao kweli ndio wanahitaji msaada na hawana wa kuwasaidia. Bahati mbaya hakuna makamera na waandishi wa kutoa hizo taarifa na wala haziitajiki. ''WANAWAFUNDISHA KUVUA SAMAKI NA HAWAGAWI SAMAKI''
 
Wewe ni muumini uchwara. I'm sorry to say that. Tunafundishwa mkono wa kushoto ukitoa, hata wa kulia usijue umetoa nini.

And just for the sake of knowlegde. Something to ponder: If you don't see it, it doesn't mean its not happening!

Wewe unaamini kwamba mkono wa kulia unaweza kutoa halafu wa kushoto usijue? Mi sisemi waite media wala nini, kwanza huku nilipo hakuna media. Ishu ni kwamba hawatoi misaada! Wangekuwa wanatoa hata kimyakimya jamii ingejua.
 
Kanisa limeona serikali yote iko hapo na imetoa mpaka na jeshi kusaidia hao ambao ndio huwa wanaonekana kuwa ndio Watanzania halisi. Nenda huko vijijini kulikosahauliwa ndio utaona kazi ya kanisa wanajua kuwa hao kweli ndio wanahitaji msaada na hawana wa kuwasaidia. Bahati mbaya hakuna makamera na waandishi wa kutoa hizo taarifa na wala haziitajiki. ''WANAWAFUNDISHA KUVUA SAMAKI NA HAWAGAWI SAMAKI''

Mimi nipo huku vijijini. Sijaona.
 
Back
Top Bottom