Kwanini makanisa hayaoekani kutoa misaada kwa waliokumbwa na mafuriko?

Huna lolote! Ungekuwa RC kama unavyojisingizia, ungejua ngazi mbalimbali za misaada kuanzia unapoishi hadi kwenye ngazi ya taifa.

Wewe siyo RC wala siyo mkristo na bahati mbaya sana huna hata akili ya kufanya utafiti kidogo ukajua kanisa linavyofanya kazi ndipo utunge hiki ulichotunga.

Wewe ambaye ni mkristo, mwenye 'akili' na ambae umefanya utafiti, hebu tuambie kanisa limetoa wapi msaada? Na ujue kutofautisha msaada na huduma. Mimi nimesema, kwenye jamii ninayoishi SIJAONA WALA KUSIKIA kanisa limetoa msaada.
 
imeandikwa. . 'nawe utoapo sadaka mkono wako wa kushoto usijue litendalo mkono wako wa kuume'

Nafıkırı huu msemo unatakıwa kutumıka kama anayetoa msaada nı mtu mmoja (kama wewe bınafsı) lakını kama nı Taasısı kama Kanısa nı vızurı watu wengı wajue. Itasaıdıa hata watu wanaotoa sadaka waone kwamba sadaka zao zınatumıka kuwahudumıa pıa watu wengıne wenye mahıtajı mbalımbalı.
 
Wewe ni muumini uchwara. I'm sorry to say that. Tunafundishwa mkono wa kushoto ukitoa, hata wa kulia usijue umetoa nini.

And just for the sake of knowlegde. Something to ponder: If you don't see it, it doesn't mean its not happening!

What happened to 'seeing is believing'? If no one has ever seen maybe its not happening. Hence this thread!
 
Nafıkırı huu msemo unatakıwa kutumıka kama anayetoa msaada nı mtu mmoja (kama wewe bınafsı) lakını kama nı Taasısı kama Kanısa nı vızurı watu wengı wajue. Itasaıdıa hata watu wanaotoa sadaka waone kwamba sadaka zao zınatumıka kuwahudumıa pıa watu wengıne wenye mahıtajı mbalımbalı.
Ekuzakutire!
 
Mkuu umesahau kuwa katika kanisa wana methali yao kuwa unapotoa msaada basi mkono wako wa kushoto usipate taarifa kabisa ni kiasi gani umesaidia. Hujaona wakisaidia kwasababu unasubiri media wakuonyeshe kwenye tv mchungaji,askofu, padre, shehe, imam nk kuwa wametoa msaada kwenye kambi flani. dini si siasa ama kampuni nyengine kuwa zitakuwa maarufu zikionyeshwa kwenye tv basi zitapata wateja wengi ama umaarufu. Au subiri wale madhehebu mengine ya wokovu ndo wanapenda umaarufu kama huo
 
Kabla sijahitimisha kwa kusema sitegemei ushahidi wa kuona toka kwa kipofu, naomba nikuulize swali:

Wewe umeona nini huko ulipo?

Acha kujichanganya, umeshasema hutegemei ushahidi wa kuona toka kwa kipofu, halafu unaniuliza nimeona nini? Wewe 'mwenye macho' umeona nini?
 
Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.

Wewe umetoa nini?

Catholic Relief Services; www.catholicrelief.org
Christian Children’s Fund: www.ChristianChildrensFund.org
Christian Reformed World Relief Committee: www.crwrc.org
CWS: Church World Service; the service agency for the National Council of Churches (USA); www.churchworldservice.org
International Aid: www.internationalaid.org, www.gospelcom.net/ia
International Catholic Migration Commission: www.icmc.net
Latter-Day Saint Charities: 800-240-1201
Lutheran World Relief: www.lwr.org
MCI: Mercy Corps International: www.mercycorps.org
Salvation Army World Service Office: www.salvationarmyusa.org
ADRA: Adventist Development and Relief Agency International: www.adra.org
CARITAS International (tafuta mwenyewe website yao)

Haya ni baadhi ya Mashirika ya Kikristo ya misaada ya kibinadamu na sheria. Nimeweka na website zao ili upate kuona namna yanavyooperate kila kona ya dunia bila kujali anayehudumiwa ni Myahudi au Msomali, Muislamu au Mkristo, Muafrika au Muasia.

Ulichotaka kuleta hapa ni concern ya 'fulani hajali' kwa hiyo yeye siyo bora. Sasa jiulize wewe mwenyewe kama individual; Umesaidia nini? (usinijibu mimi, jijibu wewe na Mungu wako kwa imani ya dini yako)

Labda cha muhimu kufanya hapa ni kubadili swali lako na contents za topic yako. Andika hivi: Kwa nini makanisa hayajitangazi yanapotoa misaada?
 
Au subiri wale madhehebu mengine ya wokovu ndo wanapenda umaarufu kama huo
From 'wahanga's point of view, nadhani ni heri hao wanaotoa msaada na kutangaza, kuliko wanaokaa kimya na msaada hawatoi.
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

Kwani ni lazima kanisa litoe msaada? Au kwa vile fulani mfano PPF katoa basi na wao watoe msaada?
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

Kuwa kwako Mkristo sio manufaa kwa kanisa, bali ni kwa manufaa yako. Ikiwa unalilaumu kanisa kwa kutotoa mchango, umeshajilaumu mwenyewe kwa kutotoa?

Unapotoa sadaka unajua maana yake au unaleta siasa kanisani?

Mimi nakushauri, kama unaendaga kanisani kwa ajili ya roho yako, basi jishibishe imani na usaidie kwa kadiri unavyoweza kama wanavyofanya wakristo wengine wenye imani. Unaweza kwenda CARITAS au Red Cross na kupeleka mchango wako kwa moyo na imani. Kama unasubiri siku ya Kanisa kutafuta ujiko kwa binadamu utasubiri sana.
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

acha kuandika usichokijua.mimi ni muumini wa rc na parokia ninayosali ya chuo kikuu inatoa msaada mara nyingi majanga yakitokea kama mabomu yalivyolipuka gongolamboto,mbagala nk.mara zingine tunachangia pia kwaajili ya misaada kwa wafungwa na yatima!na kuanzia mafuriko yatokee wanakusanya michango kwaajili ya waathirika then wanaipeleka jimboni ipelekwe kwa wahusika.wewe unayedai kanisa katoliki halitoi misaada una yako!sio lazima uone kwenye media ndo ujue
 
Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.

Kule Mafia hakuna shule wala hospitali ya maana. Hivi karibuni Kanisa litajengwa huko na huduma za jamii zitafika tu huko am sure. Sasa nikukumbushe jambo: moja kati ya majanga makubwa ya Tanzania ni ukosefu wa elimu. Kama kanisa litajenga chuo kidogo cha ufundi kule Mafia (Vocational School) utaona jinsi maisha yatakavyobadilika kule ikiwa watu wataamua kuweka kando imani zisizo na msingi na kuingia shuleni. Kwa sasa huduma za afya zenye uhakika kwa wakazi wa Mafia zinapatikana kwa kuvuka bahari kuja bara mpk MCHUKU MISSION iliyopo Ikwiriri.

Hii ndio namna ya misaada endelevu. Kutoa kilo mbili za unga ni jukumu la waumini na sio taasisi. Wewe kwa dini yako na imani yako, nenda pale jangwani na nguo zote ambazo unaona zinaweza kuwasaidia waliokumbwa na maafa na sio kusubiri kanisa lifanye hivyo. Ulitaka Padre atoe nguo zake kuwapa wahanga mbele ya kamera ndio uone msaada wa kanisa?
 
Tangu janga la mafuriko kwa wakazi wa mabondeni litokee watu mbalimbali, taasisi za serikali na kampuni binafsi zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa waathirika hao. Katika kutazama kwangu uko sijaona/sijabahatika kuona makanisa yakitoa msaada. Nataka kufahamu kwanini makanisa ni magumu katika kutoa misaada.

Roman Catholic ndo wanakusanya kwa pamoja ili wawasilishe
 
acha kuandika usichokijua.mimi ni muumini wa rc na parokia ninayosali ya chuo kikuu inatoa msaada mara nyingi majanga yakitokea kama mabomu yalivyolipuka gongolamboto,mbagala nk.mara zingine tunachangia pia kwaajili ya misaada kwa wafungwa na yatima!na kuanzia mafuriko yatokee wanakusanya michango kwaajili ya waathirika then wanaipeleka jimboni ipelekwe kwa wahusika.wewe unayedai kanisa katoliki halitoi misaada una yako!sio lazima uone kwenye media ndo ujue

Mtu asiyeenda kanisani au ambaye misa ikiisha tu anawahi pombe zake hawezi kujua activities kama hizo. Kwanza nina shaka kama huyu ni Mkatoliki kweli. Manake kanisa huwa lina utaratibu wa kuwatumia watoto kupeleka misaada kwa watoto yatima ili kuwajenga watoto kuwatambua wenzao wenye shida. Labda angetueleza anasali wapi
 
Wewe unaamini kwamba mkono wa kulia unaweza kutoa halafu wa kushoto usijue? Mi sisemi waite media wala nini, kwanza huku nilipo hakuna media. Ishu ni kwamba hawatoi misaada! Wangekuwa wanatoa hata kimyakimya jamii ingejua.

Una umri gani ndugu? Mdogo wangu ambae anasoma komunio ya kwanza anaweza kulifumbua hilo fumbo. Nasikitika umeshindwa! Asiyejua maana haambiwi maana. Siku njema
 
Mtu asiyeenda kanisani au ambaye misa ikiisha tu anawahi pombe zake hawezi kujua activities kama hizo. Kwanza nina shaka kama huyu ni Mkatoliki kweli. Manake kanisa huwa lina utaratibu wa kuwatumia watoto kupeleka misaada kwa watoto yatima ili kuwajenga watoto kuwatambua wenzao wenye shida. Labda angetueleza anasali wapi

afadhali ndugu yangu unisaidie,coz watu wengine wanakurupuka kuandika wasichokijua.sikatai labda kuna makanisa ya kikristo mengi na sio yote yanayotoa misaada!ila hapo kwa Rc amewakosea sana kwa kusema hivyo.
 
By the way, you should be looking at the bigger picture. The church has done and keeps doing a lot as far as community services are concerned.

Now, as an RC, as you claim, what have you done to help when you felt it hasn't?
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

wewe ni muongo...wewe si RC. hapa ni JF...so jipange vizuri next time.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom