Kwanini makanisa hayaoekani kutoa misaada kwa waliokumbwa na mafuriko?

acha kuandika usichokijua.mimi ni muumini wa rc na parokia ninayosali ya chuo kikuu inatoa msaada mara nyingi majanga yakitokea kama mabomu yalivyolipuka gongolamboto,mbagala nk.mara zingine tunachangia pia kwaajili ya misaada kwa wafungwa na yatima!na kuanzia mafuriko yatokee wanakusanya michango kwaajili ya waathirika then wanaipeleka jimboni ipelekwe kwa wahusika.wewe unayedai kanisa katoliki halitoi misaada una yako!sio lazima uone kwenye media ndo ujue

Huyo muanzisha mada atakuwa ni Kalapina huyo,maana ndio anaeongoza kwa huo upupu kwa sasa.
 
Acha kujichanganya, umeshasema hutegemei ushahidi wa kuona toka kwa kipofu, halafu unaniuliza nimeona nini? Wewe 'mwenye macho' umeona nini?

Nimekupa nafasi ya kujithibitisha kuwa una uwezo wa kuona, tumia hiyo na si kuibua madai mapya.
 
Mkuu umesahau kuwa katika kanisa wana methali yao kuwa unapotoa msaada basi mkono wako wa kushoto usipate taarifa kabisa ni kiasi gani umesaidia. Hujaona wakisaidia kwasababu unasubiri media wakuonyeshe kwenye tv mchungaji,askofu, padre, shehe, imam nk kuwa wametoa msaada kwenye kambi flani. dini si siasa ama kampuni nyengine kuwa zitakuwa maarufu zikionyeshwa kwenye tv basi zitapata wateja wengi ama umaarufu. Au subiri wale madhehebu mengine ya wokovu ndo wanapenda umaarufu kama huo

Taasısı za kıdını za kııslam hasa wahındı uwa wanaonekana wakıtoa mısaada kwenye Medıa kwenye matukıo kama haya. Inasaıdıa kutıa faraja kwa wahanga na wasıo wahanga kuona sadaka zao hazııshıı tu kwenye mıshahara ya vıongozı wa dını balı hata kwa wahıtajı. Pıa ınawapa moyo watoajı sadaka kuendelea kutoa zaıdı ılı kuwezesha kanısa kutekeleza majukumu kama hayo.
 
Nakuunga mkono 100% kwa observation yako. Mimi ni muumini wa RC, lakini sijawahi kuona hata siku moja kanisa langu likitoa msaada kwa jamii inayotuzunguka pamoja na waumini kutoa sadaka tatu hadi nne kwa siku. Hata tunapokuwa na michango, sijawahi kusikia mchango huu ni kwaajili ya kusaidia watoto yatima/wasiojiweza n.k zaidi ni kujenga nyumba za masista, maaskofu, n.k. Sijauona ushiriki wa makanisa kwenye majanga. Labda nyie wana jf..

labda kama wewe ni muumini wa pasaka na christmass ndo maana huoni wafanyayo wenzio. sisi RC tunasaidiana kuanzia kwenye jumuia zetu ndogondogo mpaka kanisani. Acha uongo
 
Wewe unaamini kwamba mkono wa kulia unaweza kutoa halafu wa kushoto usijue? Mi sisemi waite media wala nini, kwanza huku nilipo hakuna media. Ishu ni kwamba hawatoi misaada! Wangekuwa wanatoa hata kimyakimya jamii ingejua.

kwa maneno haya inadhihirisha wewe sio mkristu na zaidi sio mkatoliki. ungekua mkristu mkatoliki ungeyaelewa yana maana gani.
 
Nafıkırı huu msemo unatakıwa kutumıka kama anayetoa msaada nı mtu mmoja (kama wewe bınafsı) lakını kama nı Taasısı kama Kanısa nı vızurı watu wengı wajue. Itasaıdıa hata watu wanaotoa sadaka waone kwamba sadaka zao zınatumıka kuwahudumıa pıa watu wengıne wenye mahıtajı mbalımbalı.

kanisa halifanyi kazi ya kujitangaza., vodacom watatangaza wametoa msaada ili watu wajue wapate umaarufu wanachi wanunue na kutumia line/mtandao wa vodacom.

kanisa linapotoa msaada linawaona wahusika, bila kuita media/kulipa posho waandishi/ kuwapa kitu kidogo wahusika wa media ili habari irushe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! la hawafanyi hivyo, wanawaona viongozi/waratibu na kutoa misaada yao.

tena kumbuka misaada hiyo ni sadaka, kwa maana waumini wametoa kile mtu alichonacho kwa ajili ya kusaidia wahanga au jamii husika iliyopata tatizo, hata akienda askofu kupeleka nyuma yake ni michango ya waumini utasemaje hiyo si sadaka? hata wakitoa kwenye fungu lililopo kanisani source ya hilo fungu ni nini? sio sadaka mbalimbali za waumini?

maandiko yametukataza unaposaidia mtu au kutoa sadaka mpaka watu wajue/waone, hiyo ni siri kati yako na Mungu wako. vivyo hivyo kanisa halijitangazi. ukitaka kujua wamepeleka kiasi gani waone waratibu wa majanga husika utaambiwa.
 
Back
Top Bottom