Kwanini Mabele Marando yuko CHADEMA?

Mkuu umemaliza,mapadre wengi Tiss na nina hakika sana na hili

Mkuu Kassim Awadh wengi ni mashushushu tena wengine ni CIA na wengine walikuwa KGB. Hasa mapadre wa kikatoliki. Inaaminika kwamba wakoloni walikuwa wakiwatumia mapadre kipata siri wa wananchi. Kilichokuwa kinafanywa ni kutangaza dini na kuwabatiza. Wakishabatizwa wanaambiwa ukifanya kosa unatakiwa uje utubu kwa padre. Basi ukiua unaenda kutubu kwa padre na kimwambia kila kitu ukidhani unaongea na Mungu kumbe jamaa ni kachero wa serikali anatoa taarifa unayiwa nguvuni!
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli asiyekujua hakuthamini. Marando ni mpiganaji wa kupigiwa mfano Miaka ya sabini se Mwanafunzi wa stashahada ya Udhamili chuo kikuu cha DSM alifanya mahojiano radio TZ kuhusu harakati za vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika na hapo Alisema Tanzania inahitaji kurejesha mfumo wa vyama vingi. Tamko Hilo lilimfanya sites ikulu na kupewa kazi maalumu jambo ambalo lilikatisha masomo yake. Alikwenda Cuba ambalo alifundishwa ujasusi wa jinsi ya kuwakabili makaburu na vibaraka wao. Anasema yeye mwenyewe aliipenda kazi hiyo japonica alijua lengo lilikuwa kumdhibiti. Baada ya vita ya Uganda ambapo alikuwa advance part (millitary intelligence) alitakiwa kutoa maelezo kwann si mwanachama wa CCM, badala ya kutoa maelezo aliwapa notice ya saa 24 ya kuacha kazi. 1984 ndiye aliyemtetea James Mapalala aliyetiwa kizuizini kwa kumwandikia Rais akitaka mfumo wa vyama vingi. 1989 aliratibu uanzishwaji wa kamati ya kuratibu maoni ya wanananchi juu ya uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi nchini. Kumnyamazisha Rais Mwinyi alimteua kuwa kwenye Tume ya Jaji Nyalali, alikataa huo uteuzi na kusema hayuko tayari kutumia raslimali za Watanzania kwenda kuwauliza warudishiwe haki waliokuwa wamenyang'anywa au wasirudishiwe? 1991 aliratibu kongamano la kitaifa la siku mbili Diamond jubilee ambapo azomio la kuanzishwa vyama vingi baada ya mwaka mmoja liliazimiwa na vyombo viwili vya kuratibu harakati hizo vikaundwa: Tanzania Bara (National commitee for constitutional reforms kifupi NCCR ambayo ndiyo iliyokuja kuwa chama cha nccr - mageuzi) kwa Zanzibar iliundwa KAMAHURU ambayo ndiyo CUF ya l eo. 1994 alijaribu kuunganisha NCCR MAG. EUZI na CHADEMA kuunda chama kimoja chenye nguvu kiitwe UDETA jitihada hii ilikwamishwa na vibaraka wa CCM kina Prince Bagenda. 1995 alimkabidhi Ndg Mrema uenyekiti wa Chama kwa azomio la kamati kuu. Mrema alikigeuza chama kutaka taasisi kuwa jukwaa na duka lake jambo ambalo halikuwa lento la kuanzishwa kwake ndipo aliporatibu harakati za kumwondoa Mrema na kufanikiwa. Alichafuliwa sana. James Mbatia kwa kusaidiwa na Usalama wa Taifa alifanikiwa kumzuia Marando kukiongoza tena chama na kukirudisha katika male go. Ya awali. Alikaa kimya na kurudi katika sheria. 2003 Anthony Komu alihama NCCR na kujiunga Chadema, aliendesha harakati za kuwashawishi Watu makini waliokuwa wameamua kubaki kimya ndani ya nccr Kama Marando, Baregu, Chacha Wangwe, Selasini, nk. Mh. Alitoa wito kuwa kama tumeshindwa kuunganisha nguvu za vyama basi tuunganishe watu.Hue ndio msIngi wa Marando kuwa CHADEMA?
Hii ndiyo sababu ya Marando kuwa p
 
Kwanini viongozi wa CHADEMA walipiga kelele na kusema yeye ni kibaraka wa CCM wakati alipochaguliwa kuwa mbunge wa Africa mashariki?
 
Mimi ni mwananchi wa Tanzania ninataka kujua sababu za Marando kupokelewa CHADEMA. Hivi tuseme viongozi wa CHADEMA hawako makini? maana huyu mtu alikuwa NCCR na akasadikika kuwa ni shushu wa CCM, na wengi wa viongozi wa CHADEMA walisema hilo.

Mimi ninataka kuelewa kwann Marando yuko CHADEMA na amepewa nyazifa za juu?

Acha kutoa povu jingi kiasi hiki kwan unachafua screen yako´.Ebooo.....!
 
Mkuu yohane umenikumbusha habari za UDETA. Lakini kumbuka katika siasa ukiwa chama pinzani unaweza kupewa kila jina lakini ukijiunga na wao basi unatakaswa. Marando kweli ni mpiganaji kama ulivyosema lakini siku zote watu wamekuwa wakimshutumu kwa kuiua NCCR. Hako kadoa kanamsumbua kweli na ndio maana naona huko CDM ana play low profile.
 
Last edited by a moderator:
mkuu wewe ni noma,nafikiri hilo ndilo jibu sahihi la kwanini kamanda mabere mrando yupo CHADEMA!respect sana!
 
Kwanini viongozi wa CHADEMA walipiga kelele na kusema yeye ni kibaraka wa CCM wakati alipochaguliwa kuwa mbunge wa Africa mashariki?

Sidhani kama walimjua vizuri lakini pia kumbuka aliyeongoza kelele hizo ni Kabourou ambaye ilidhihirika baadaye kuwa alikuwa kibaraka wa CCM.
 
Sasa kunauhakika upi basi kuwa Marando si kibaraka wa CCM maana hata akina Slaa na akina Zitto walipiga kelele hizo, na mpaka sasa hawajasema chochote kuhusu Marando kwa niaba ya kumsafisha na kukiri kuwa walikuwa hawamuelewi mbele ya watu kama walivyokuwa wakidai hadharani. au wewe unasemaje?
 
Back
Top Bottom