KakindoMaster
JF-Expert Member
- Dec 5, 2006
- 1,356
- 88
Tafuta vizuri utapata jibu, ukitaka kusolve soln usiende na mambo mengi nenda na moja baada ya jingine
Tusiwe wepese wa kujumuisha mambo.Hakuna ushahidi kwamba JK alikataa kumrudisha Marehemu Balali.Alichokifanya JK kwa nafasi yake ni kutengua uteuzi wa marehemu kutokana na udhaifu aliounyesha katika kuidhinisha fedha za EPA.Hilo ndilo lililokuwa jukumu lake la msingi baada ya taarifa ya wakaguzi kukabidhiwa kwake.Sasa kwa kuwa mengine ilikuwa ni lazima yafuate mkondo wa kisheria kwa kuzingatia kuwa nchi inaendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria,ilibidi auunde tume kuchunguza makampuni yaliyotajwa na repoti ya wakaguzi kuhusika kuchukua fedha za EPA.Sasa kamati ilishaanza kazi,JK hakuwa na haja tena ya kuingilia majukumu ya kamati.Alichokuwa anasubiri ni kamati kukabidhi repoti kwake.Ni upotoshaki mkubwa kwamba Marekani ilishamuona Balali kama shahidi mkuu.Marekani ni taifa linalozingatia haki na sheria kwa kila raia.Sio rahisi kuropoka vitu wasivyokuwa na uhakika navyo mpaka mamlaka zinazohusika kisheria zithibitihse.Alishosema Balozi ni kwamba "kama wakimuhitaji" hii ni sentensi muhimu kuilielewa,sio kukurupuka tu.Ilikuwa ni maoni ya jumla,sio kwamba kwa kusema hivyo balozi alikuwa anatoa msimamo wa nchi kwamba Balali ni shahidi muhimu.Na majuzi tumesikia taarifa ya Ikulu kwamba kama serikali ingemhitaji isingekuwa shida kumpata.Harafu tusisahau kwamba marehemu Balali alikuwa ni mgonjwa wakati huo.Alikuwa ni mgonjwa kweli kweli.Alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa masaa 24 mpaka anafariki dunia.Sasa mtu anapohoji kwa nini JK hakumrudisha mgonjwa nyumbani kutoka kwenye uangalizi wa madaktari,nadhani mtu huyu ana matatizo ya akili kama sio kusukumwa na hisia za jazba sizokuwa na msingi wowote.Tukumbuke JK ni kiongozi wa nchi,sio rais kilabu cha mpira.Hawezi kukurupuka kufanya maamuzi kwa kila anachokisikia kwa lengo la kuwafurahisha baadhi ya watu.Hiyo sio misingi ya utawala wa sheria.
Tom, yawezekana kabisa kuwa na wewe ni mmoja wa wale waliofaidika na pesa za EPA. Huwezi kuingia leoleo JF na kuona wenzio wanarukia wasichokijua! Ina maana wewe hukusikia Mustaffa Mkulo akidai hakumuona, siku hiyo hiyo Rweyemamu anadai ni mtu huru akitakiwa atapatikana! Ina maana wewe huoni walau japo kwa fikra za kawaida kuwa kuna mchezo rafu wa kifo chake ambacho kilitangazwa kwa ukali bila kuhitaji maelezo kikiwa kimechelewa kutangazwa na pia mazingira ya mazishi?
Hebu muweni wazalendo jamani! Balali alikuwa shahidi wa kwanza katika EPA. Mbona kina Mwanyika hawakuwahi kumuhitaji huku tukiambiwa ni mtu huru??
hebu fikiria kwa ubongo wa mbele rafiki.
Halafu maajabu mengine ni kuwa..Mustafa Mkulo na Rweyemamu walisema kuwa serikali haimtafuti Ballali at the same time Mkullo naye akasema eti alimtafuta alipokwenda Washington DC..Sasa alikua akimtafuta kwa niaba yake binafsi ama kwa niaba ya serikali?
Na kama ni kwa niaba ya serikali kwanini then alisema hawamtafuti?
Na vile vile kama ni kwa niaba yake binafsi..Then nia yake ilikuwa ni ipi?
nyinyi hapa naona mtajiumiza vichwa ! hakikisheni familia zenu zinajaa matumbo kwanza na mna akiba, then ndio muanze mambo ya kufuatilia kwa ukaribu mambo ya taifa. Kuna jamaa mmoja namfahamu ameshakata tamaa hadi hivi sasa, na bahati mbaya hana akiba, yaani ameshakata tamaa kabisaaaaaaaaaaaaa jinsi mambo yalivyo sivyo !
Mimi ni mmoja wa hao waliokata kata tamaa mpaka tamaa ikatamauka! Maana mlo watoto hawana, na mambo yalivyo ndivyo siyo! Waweza nisaidia nije nipate walau mlo wa leo! Maana ndo maana tukiona EPA na balali kafa, tunakata tamaaa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hivi bunge haliwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, ili tukaondokana na huu mzigo? 2010 naona ni mbali sana kumuundoa huyu jamaa.
mhm, asije akavunja tu bunge (if possible), na kuwavua wabunge viti maalum. akidai je alichaguliwa na wananchi na sio bunge itakuwaje ? na kama bunge litasema linaweza kumuondoa madarakani then i get the mind kwamba hata yeye anaweza kuwavua ubunge wabunge wote ! (if possible)
Hivi bunge haliwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, ili tukaondokana na huu mzigo? 2010 naona ni mbali sana kumuundoa huyu jamaa.
Nakupa ushauri tumia kamuda kidogo kuipitia Katiba ya Nchi na iko hapa kwa lugha zote 2 then uje na hoja mkuu.Ndiyo maana ninapinga pia wabunge wa kuteuliwa na Rais na wabinge wa viti maalumu kwamba wafutwe ni mzigo kwa Taifa .
Bunge haliwezi kupiga "kura ya kutokuwa na imani na Rais" linaweza kufanya hivyo kumuhusu Waziri Mkuu.
Jamani, Rais hawezi kuvunja bunge kwa kujisikia tu. Hawezi kuamka asubuhi moja na kusema "Bunge sucks" halafu akalivunja.
.