Waziri Mchengerwa aagiza wanaodaiwa kuhusika na tukio la moto Mnadani Kariakoo wafikishwe Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaodaiwa kuhusika na uchomaji wa moto kwenye baadhi ya majengo yaliyopo Kariakoo.

Agizo hilo amelitoa Novemba 15, 2023 alipofanya ziara kwenye soko la Kimataifa la Kariakoo Jijini Dar es salaam ambalo linaendelea kujengwa, ambapo Mchengerwa amesema kuwa vitendo hivyo ni makosa makubwa ambayo mtuhumiwa akitiwa hatiani anaweza kupata adhabu kali.

"Kosa la uchomaji wa majengo ni kosa kubwa sana, na linaweza kupelekea kifungo cha hadi miaka 30"amesema Waziri Mchengerwa

Hivyo amesema wahusika hawatakiwi kufumbiwa macho, ambapo ameagiza watuhumiwa kufikishwa mahakamani haraka.

"Kwahiyo maelekezo yangu Wale wote waliohusika wote wakamatwe kwa sababu wanafahamika waliopelekea moto huu kuzuka na kusababisha hasara na kusambabisha maumivu makubwa kwa watanzania ambao walikuwa wanafanya shughuli zao eneo hilo"amesema Waziri Mchengerwa.
Mchengerwa.jpg


Aidha amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuunda kamati ya uchunguzi ambayo ilitoa ripoti, hata hivyo amesema kuwa pia yeye alituma watu kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo la moto, ambapo amesema atampatia ripoti yake ili aweze kujumuisha na ripoti ya Kamati iliyoundwa na Chalamila ili wahusika wachukuliwe hatua.

"Niseme kwamba Mkuu wa Mkoa wakati huo wewe unafanya uchunguzi namimi nilituma watu wangu kufanya uchunguzi, kwahiyo hiyo ripoti niliyonayo nitakuletea uiunganishe na ripoti uliyonayo wewe"amesema Waziri Mchengerwa

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa mara baada ya agizo hilo amesema kuwa utekelezaji wake utaanza mara moja kwa wahusika kuchukuliwa hatua kulingana na maagizo ya Waziri Mchengerwa.

Hata hivyo Chalamila amesema kuwa wanakusudia kufunga mifumo ya picha ya kisasa (CCTV Camera) katika soko hilo ili kusaidia kuwabaini waharifu. Ambapo soko hilo imedaiwa kuwa ujenzi wake umefikia asilimia 85 likitarajiwa kukamilika miezi mitatu mbeleni.

Itakumbukuwa Oktoba 1, 2023 eneo la Mnadani Kariakoo uliibuka moto ambao uliteketeza baadhi ya majengo na bidhaa mbalimbali ambazo zilikuwa eneo hilo, katika maduka na vibanda vya biashara.

Kufuatia moto huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila aliunda Kamati kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.

Akitoa taarifa ya uchunguzi huo Chalamila alisema Kamati ilibaini moto huo haukutokana na ajali, bali ni hujuma za Wafanyabiashara wenyewe ambapo aliweka wazi kuwa moto huo ulianzia katika eneo la Mnadani (Kariakoo Auction Mart) na haukusababishwa na Jenereta kama ilivyodaiwa awali.
 
Back
Top Bottom