Kwanini Kikwete alikataa kumleta Ballali?

Na ni nini hasa Kikwete alichowapa Wamarekani kuwafanya wanyamaze?

Hiyo mikataba yote na makubaliamo ipitiwe!

MAAANA MAPOKEZI ALIYOPEWA BUSH YALIONYESHA WALAKINI MKUBWA SANA!

BENDERA ZILIPANDISHWA KILA MAHALI NA KWA WAMAREKANI HIYO NI ISHARA YA KUTOKA KWA KIKWETE KUSEMA SASA TUNAWAACHIA NCHI HII NA NI KAMA SIGN YA KUSSURENDER ILI ASIULIZWE KUHUSU UHARAMIA HUU DHIDI YA WANANCHI!

Hiyo inaweza ikawa ni ishara kutoka kwa Kikwete kuwa ndio tuna makosa na sasa tutawapa chochote mnachotaka ili msiwasikilize wapinzani!?

Ni wazi kabisa yale mapokezi ya Bush yalijawa na unafiki ili asiulize...Kwasababu hata mkataba wenyewe waliousaini ambao sisi wananchi tunaujua ni wa pesa za kupambana na rushwa na kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa wahusika wote kuwekwa ndani na kuchukuliwa hatua stahili za kisheria.
 
Na mimi ndiyo mawazo yangu hayo ya Balali kuhongwa zaidi asionekane, akafanyiwa plastic surgery, wakatengeneza kinyago cha wax wakaweka kwenye coffin. Du ama kweli lakini yote yana mwisho Mungu mkono wake ni mrefu.Subiri tu mtaona, nani alijua wakina saddam, Mobutu wataishia walikoishia??????????
 
Issue ya jinsi bendera zilipopandishwa imekaa hivi...

Kiutaratibu bendera huwa zinatakiwa kuwa mbili za tofauti side to side ili kuonyesha mshikamano!

Tatizo ni kuwa Bush alipokuja ilikuwa ni bendera za Marekani pekee!

Na kwa wamarekani..Bendera yao pekee husimamishwa kwenye nchi nyingine kama nchi hiyo imeangukia kwenye utawala wa marekani mara baada ya vita nk!

Ishara ya bendera ilikuwa ni kama kuwapigia magoti wamarekani na kuwaambia chochote mnachotaka wazee!
Noma ndio hapo ilipopozwa!

Sasa sisi hatutaki iwe hivyo pekee...TUNATAKA HAKI IAMBATANE NA URAFIKI WA KWELI BAINA YA WANANCHI WA NCHI HIZI MBILI!

THE ACT OF SURRENDER DOES NOT CONSTITUTE TO COOPERATION OR MAKING SURE THAT JUSTICE WILL PREVAIL!
 
Kauli kwamba Ballali alikuwa huru na kuwa haitajiki hazikuanza leo...

Mzee Mwanakijiji
user_offline.gif

JF Senior & Premium Member
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 9,411
Rep Power: 43
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 3,818
Thanked 4,228 Times in 1,847 Posts
Credits: 325,532

icon1.gif
Re: Kikwete Akataa Balali Asiletwe!
ingawa sijapenda kichwa cha habari lakini mantiki ndani yake ni dhahiri. Je, serikali ya Rais Kikwete inataka Balali arudi nyumbani. Arudi kufanya nini?

a. Hadi hivi sasa Balali ni mtu huru hajatuhumiwa kosa lolote lile.

b. Kuvuliwa visa yake ya Marekani hakuhusiani hata kidogo na kitendo chochote cha kihalifu.

c. Serikali ya TAnzania aidha inao ushahidi wa vitendo vya kihalifu vya Balali au hauna. Kama haina basi hakuna sababu ya kumtaka Balali arudi.

d. Kama serikali inaamini Balali ameshiriki kwa namna yoyote ile na ubadhirifu (kwenye tamko lake haisemi hivyo), basi wangekwisha kufikisha kesi mahakamani, mbona ya Rada wameifikisha mahakamani wakati Vithlani hayupo?

HIvyo, hadi hivi sasa serikali ya JK haijaonesha nia ya kutaka Balali arudi kwani hawajamtuhumu kitu chochote.
__________________
Hoja Hujibiwa kwa Hoja!
Magoli yanafungwa, lakini yapo yanayokubalika na mengine yanabishiwa!
TODAY NEWS TODAY
 
Viongozi wetu wamefanya uhaini kwa wananchi!

Mushi,

That is the key statement on everything about leadership in Tanzania. Labda tufafanue kidogo tafsiri ya Uhaini na isichukuliwe literarily kwa ni Uhani kupindua.

KInachofuata;
Tuwachukulie hatua za namna gani? Tuna na tutumie nguvu gani kuwa wajibisha kwa makosa na uhaini wao?
 
Litakuwa jambo la maana sasa kama tukiondoa matengano na kuanza mjadala honest wa kizalendo bila kuonyesha bias.
Nashukuru kwa kuelewana licha ya kwamba ni mara chache sana ndio tumekuwa tukifanya hivyo!
Cha msingi hapa ni HONESTY...Mimi maslahi yangu ni haki kwa mtanzania.
 
Ya Balali tuyaache maana tumeshaibiwa. Tubanane na hawa mafisadi waliobaki. Tuwafunge na kuwafirisi na iwe mfano kwa mafisadi wengine.
 
Litakuwa jambo la maana sasa kama tukiondoa matengano na kuanza mjadala honest wa kizalendo bila kuonyesha bias.
Nashukuru kwa kuelewana licha ya kwamba ni mara chache sana ndio tumekuwa tukifanya hivyo!
Cha msingi hapa ni HONESTY...Mimi maslahi yangu ni haki kwa mtanzania.

Narudia swali kwako, umebaini Uhani ulio/unao fanywa na viongozi wa Tanzania. Je tutasahihishaje? kwa njia zipi?

This is where we are lacking direction and energy; how to solve a problem.

We are masters of investigating, researching, blaming, criticisng and probing, but when it come to solutions, methods and how to execute solutions we are extremely inferior and we end up going back in circles probing the same thing from a different angle and perspective!
 
Nataka kujua kuwa ni nani aliyemwambia Ballali amwambie Meghji aandike barua ya kuidhinisha malipo kutoka kwenye akaunti ya EPA!
Kama ni kweli Kikwete ndio alimwambia Balali hilo nalo liwekwe wazi...Kama ni someone else kutoka ikulu pia atajwe...Na kama ni Ballali alitunga uongo ili Meghji aandike hiyo approval letter pia tuambiwe!
Mbona maswali ni mepesi sana?
 
Okay, let say the answer is Mkapa or Kikwete for that sake(remember pesa za Kagoda ziliidhinishwa kabla ya Kikwete kuwa Raisi, alichouliza Meghji ni kutokana na ripoti ya wakaguzi wa mahesabu), then what will you do?
 
Serikali ijiuzulu ili kupisha uchunguzi wa haki na kweli!
Waikabidhi nchi kwa jeshi letu kwa muda wakati tukifanya mchakato wa maridhiano,makubaliano na ukweli ili sasa tuanze tena kujenga Taifa lenye nguvu na demokrasia ya kweli.
Ama wafanye uungwana wawaeleze wananchi ukweli na waombe msamaha kama wanadamu!
Wasipofanya hivyo historia itawageuka na watakuja kuiona Tanzania chungu one day kama hawatumii akili zao!
 
Tumeshajua kuwa ni kwanini mama Meghji aliandika barua kwa kuambiwa na Ballali?

Na baadae kuandika barua mpya ya pili kuipinga ile ya kwanza?

Nani alimwambia Meghji kuwa maelezo ya Ballali yalikuwa si ya kweli?

Alijuaje kuwa maelekezo ya Ballali si ya kweli na wakati aliamini kuwa ni ya kweli mwanzoni?

Kwanini Ballali hakuulizwa kuwa hiyo kauli kuwa pesa ni za "usalama wa Taifa" na ni "Kikwete amesema zitolewe" aliitoa wapi?

Kama alimsingizia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani...Then ni kwanini yeye hakuwa suspect ama witness?

Kwanini JK alikuwa hamtaki BALLALI nchini ili ahojiwe kama si yeye aliyemwambia ampe order Mama Meghji ya kuwa KIKWETE KASEMA PESA ZITOKE NA KUWA NI ZA USALAMA WA TAIFA?

Kwanini ilimchukua Mama muda wote huo kujua kuwa amri nzito aliyoitoa haikuwa ya kweli? Je ni mchezo wanaoujua KIKWETE NA MAMA MEGHJI?

Je ni kwanini Mama na yeye hakufanya uamuzi wenye logic kama hana yake?

Ilikuwa vipi akapokea amri kutoka kwa Ballali na si Bosi wake ambaye ni either Rais mwenyewe ama Waziri Mkuu? Je mama kama alikiuka maadili ya kazi ameshahojiwa ili kuupata ukweli?
 
Mushi ,

Nataka nitumie nafasi hii kukupongeza kwa michango yako unayoleta humu . Ingawa sikubalini na kila kitu unachosema nafurahia jinsi unavyojenga hoja zako zaidi jinsi unavyofikiri tofauti kabisa na watu wengi humu mimi nikiwa mmoja wapo.
 
Tumeshajua kuwa ni kwanini mama Meghji aliandika barua kwa kuambiwa na Ballali?

kwa sababu Ballalli alikuwa Gavana wa Benki Kuu na alikuwepo wakati fedha zinaidhinishwa. Meghji ameingia amekuta dili tayari. Kumbuka Kikwete amechaguliwa mwishoni mwa 2005.

Nani alimwambia Meghji kuwa maelezo ya Ballali yalikuwa si ya kweli?

Ungekuwa unatumia muda kutafuta majibu badala ya kuuliza tu usingekesha kuuliza. Majibu yalishatolewa ni nani alimuambia kuwa majibu ya Ballali si kweli. I won't tell you ili utafute mwenyewe. Sikiliza mahojiano yangu na mama Meghji utapata jibu la swali hilo.

Alijuaje kuwa maelekezo ya Ballali si ya kweli na wakati aliamini kuwa ni ya kweli mwanzoni?

Kwa sababu yalipangana na ya yule aliyemuambia na hao wote wawili Ballali na huyo aliyemwambia walikuwepo wakati fedha zinaidhinishwa.

Kwanini Ballali hakuulizwa kuwa hiyo kauli kuwa pesa ni za "usalama wa Taifa" na ni "Kikwete amesema zitolewe" aliitoa wapi?

Moja Ballali hakusema fedha ni "za usalama wa Taifa" na pili hakusema "Kikwete amesema zitolewe". Ukichukua muda kufuatilia alichosema au alichoandika Meghji kufuta barua yake utashangaa what actually she said. Tatizo you won't take time to find answers isipokuwa kuuliza tu wakati majibu yalishatolewa.
Kama alimsingizia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani...Then ni kwanini yeye hakuwa suspect ama witness?

Hakumsingizia Rais wa Jamhuri ya Muungano mahali popote isipokuwa katika maombezi yako. Tafuta majibu usibakie kuuliza tu ili wengine wakutafutie majibu. Take time to search for answers ukishindwa kabisa ndio unauliza. Vinginevyo naona dalili ya kauvivu kaaina fulani ka kutafuta majibu.

Kwanini JK alikuwa hamtaki BALLALI nchini ili ahojiwe kama si yeye aliyemwambia ampe order Mama Meghji ya kuwa KIKWETE KASEMA PESA ZITOKE NA KUWA NI ZA USALAMA WA TAIFA?

Mpigie simu msemaji wa Rais utafute majibu ya hilo swali la kwanza. Usibakie kuuliza tu, mpigie simu Waziri wa Habari, hata Waziri Mkuu. Do something to get the answers!

Kwanini ilimchukua Mama muda wote huo kujua kuwa amri nzito aliyoitoa haikuwa ya kweli? Je ni mchezo wanaoujua KIKWETE NA MAMA MEGHJI?
Je ni kwanini Mama na yeye hakufanya uamuzi wenye logic kama hana yake?
Ilikuwa vipi akapokea amri kutoka kwa Ballali na si Bosi wake ambaye ni either Rais mwenyewe ama Waziri Mkuu? Je mama kama alikiuka maadili ya kazi ameshahojiwa ili kuupata ukweli?

Hivi unajuaje kama Ballali hajahojiwa kabla ya kufa? Nikikuambia kuwa alihojiwa na hakuna mtu anayejua isipokuwa kalee ka "nzi" kanakopepea angani utaamini? Baadhi ya maswali subiri usikie Tume ya Rais ndipo tuanze kutoa maswali ya ziada. Vinginevyo take the initiative to ask the right questions to the right people.
 
kwa sababu Ballalli alikuwa Gavana wa Benki Kuu na alikuwepo wakati fedha zinaidhinishwa. Meghji ameingia amekuta dili tayari. Kumbuka Kikwete amechaguliwa mwishoni mwa 2005.

Ungekuwa unatumia muda kutafuta majibu badala ya kuuliza tu usingekesha kuuliza. Majibu yalishatolewa ni nani alimuambia kuwa majibu ya Ballali si kweli. I won't tell you ili utafute mwenyewe. Sikiliza mahojiano yangu na mama Meghji utapata jibu la swali hilo.

Kwa sababu yalipangana na ya yule aliyemuambia na hao wote wawili Ballali na huyo aliyemwambia walikuwepo wakati fedha zinaidhinishwa.

Moja Ballali hakusema fedha ni "za usalama wa Taifa" na pili hakusema "Kikwete amesema zitolewe". Ukichukua muda kufuatilia alichosema au alichoandika Meghji kufuta barua yake utashangaa what actually she said. Tatizo you won't take time to find answers isipokuwa kuuliza tu wakati majibu yalishatolewa.

Hakumsingizia Rais wa Jamhuri ya Muungano mahali popote isipokuwa katika maombezi yako. Tafuta majibu usibakie kuuliza tu ili wengine wakutafutie majibu. Take time to search for answers ukishindwa kabisa ndio unauliza. Vinginevyo naona dalili ya kauvivu kaaina fulani ka kutafuta majibu.

Mpigie simu msemaji wa Rais utafute majibu ya hilo swali la kwanza. Usibakie kuuliza tu, mpigie simu Waziri wa Habari, hata Waziri Mkuu. Do something to get the answers!

Hivi unajuaje kama Ballali hajahojiwa kabla ya kufa? Nikikuambia kuwa alihojiwa na hakuna mtu anayejua isipokuwa kalee ka "nzi" kanakopepea angani utaamini? Baadhi ya maswali subiri usikie Tume ya Rais ndipo tuanze kutoa maswali ya ziada. Vinginevyo take the initiative to ask the right questions to the right people.

Mwanakijiji,

Mbona huna huruma unabana korodani za watu kwa kutumia pliers?
 
Mwanakijiji,

Mbona huna huruma unabana korodani za watu kwa kutumia pliers?

wacha nimtolee uvivu.. naona ana lengo la kuhamisha maovu yote ya Benki Kuu kwa mtu mmoja huku haulizi maswali kuhusu Mgonja, na timu nzima ya wezi walioiteka nchi yetu. Kwake yeye anafikiri kuwa Ballali ndilo jibu la maswali yake. Nimejaribu kumsaidia aulize maswali sahihi naona yeye na "Ballali" tu.. badala ya kuangala the syndicate of corruption and a network of thuggery that has blossomed in our country.

Tishio kubwa katika Tanzania hakuwa Ballali, once this young lad get that.. he'll understand tunapambana dhidi ya falme, na mamlaka, tawala za nguvu za giza na maadui wa uhuru wetu. Angejiingiza kwenye mapambano badala ya kukaa pembeni kuuliza maswali tu!!!

Naamini ana sababu ya kwanini hataki tuwajadili wezi wa mali yetu na tumng'ang'anie mtu aliyekufa kama tuna wazimu!
 
Kufa kwa balali sioni kama ni tatizo, ile ofisi haikuwa ya balali peke yake kuna watu wengi walifanya kazi ya kuamisha pesa wakati wanajua kuwa hazikuwa halali, kwahiyo bado kuna watu wa kuwajibishwa na kurudisha PESA yetu iwapo serikali yetu itakuwa makini, wengi bado wako ofisini wanafanya kazi kama kawaida.
 
Maisha Kweli Ni Safari Ya Hatari
Maisha Ni Safari Yenye Siri
Maisha Tahadhari Na Kiburi
Maisha Usubiri Kila Shari

Maisha Ni Shubiri Si Sukari

Nimejifunza Hayo Katika Jambo Hili, Nnaomba Kushare Na Wenzangu
Machache Mazuri Mengi Shari
 
Kwa wale wasioamini...Haya wanasheria wanawaeleza...

Serikali inaficha ukweli – Wanasheria

na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wanasheria wameshangazwa na usiri wa serikali kuhusu kuugua hadi kufa kwa aliyekuwa Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima Jumapili mwishoni mwa wiki, wanasheria hao walisema lazima serikali inaficha jambo kuhusu Dk. Ballali.
Mmoja wa wanasheria hao, Mabere Marando, alitoa lawama kuhusu ukimya wa serikali, katika kuugua hadi kufariki dunia kwa Dk. Ballali, na kuongeza kwamba kutawafaidisha watuhumiwa wa wizi wa fedha katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), uliofanyika BoT.
"Nimesikitishwa sana na kifo cha Dk. Ballali, alikuwa Mtanzania mwenzetu. Lakini kinachosikitisha zaidi ni ukweli kwamba kifo chake kitaathiri sana uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA.
"Ukimya wa serikali kuhusu kuugua hadi kufa kwa Dk. Ballali, unashangaza, ni wazi kuwa kuna jambo inaficha, kwa sababu haiwezekani isijue mahali alipo gavana wake wakati ilikuwa ikimlipia sehemu ya gharama za matibabu kama tulivyoelezwa na gavana wa sasa," alisema Marando.
Alieleza zaidi kuwa kitendo cha tume iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuchunguza tuhuma hizo kutomuhoji Dk. Ballali hadi mauti yalipomkuta, nacho kinashangaza, kwa sababu alipaswa kuhojiwa kwanza, kwani alikuwa shahidi muhimu katika kesi hiyo.
Mwanasheria mwingine wa serikali aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alizungumzia suala hilo na kusema ni jambo la ajabu kwa timu inayochunguza kashfa ya EPA kutomuhoji Dk. Ballali hadi anakufa.
"Huyu alikuwa ‘key' katika uchunguzi huu, timu ya rais ilipaswa kumuhoji mapema kabisa, inashangaza kusikia mpaka anakufa hakuwahi kuhojiwa na serikali inasema haimtafuti.
"…Huu uchunguzi unaofanywa ni lazima utiliwe shaka na mjuzi yeyote wa mambo ya kisheria. Uchunguzi unaofanywa ni kama mchezo fulani hivi! "Na hapa wa kushakiwa kwanza ni serikali, haijulikani inaficha nini kuhusu huyu ndugu yetu, kwa sababu tangu alipougua mpaka anakufa, habari zake zimekuwa siri kubwa," alisema na kuongeza kwamba, ni ajabu kwa serikali kutokujua alipo mtuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya shilingi. Alisema, hata taarifa zilizotolewa kuwa amefutiwa hati ya kuishi Marekani ziliongeza mashaka, kwa sababu alitakiwa kuondoka nchini humo baada ya kutotambuliwa, lakini hadi anakufa alikuwa huko. Aidha, aliwataka Watanzania kuihoji serikali kwa nini ilifanya siri matatizo ya kuugua hadi kufa kwa Dk. Ballali, na kuongeza kwamba Marekani inatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi wa kifo chake ili wananchi wajue, kwa kuwa ni haki yao kufanya hivyo.
 
wacha nimtolee uvivu.. naona ana lengo la kuhamisha maovu yote ya Benki Kuu kwa mtu mmoja huku haulizi maswali kuhusu Mgonja, na timu nzima ya wezi walioiteka nchi yetu. Kwake yeye anafikiri kuwa Ballali ndilo jibu la maswali yake. Nimejaribu kumsaidia aulize maswali sahihi naona yeye na "Ballali" tu.. badala ya kuangala the syndicate of corruption and a network of thuggery that has blossomed in our country.

Tishio kubwa katika Tanzania hakuwa Ballali, once this young lad get that.. he'll understand tunapambana dhidi ya falme, na mamlaka, tawala za nguvu za giza na maadui wa uhuru wetu. Angejiingiza kwenye mapambano badala ya kukaa pembeni kuuliza maswali tu!!!

Naamini ana sababu ya kwanini hataki tuwajadili wezi wa mali yetu na tumng'ang'anie mtu aliyekufa kama tuna wazimu!

Mzee Mwanakijiji naona huo muhindi hapo juu unaangalia kama umekomaa na watu wanasubiri yakomae ili tuanze kuyachoma..!

Si siri kuna wakati ulikuwa ukipiga mlusi...ulituambia mwenyewe baada ya kauli zenu za kuficha ficha kuhusu kifo cha Ballali mpaka watu wameshaanza kutokwa na imani!

Wakati ukipiga mluzi na wenzio wakipiga soga kumbe wewe ulikuwa umeshachoma muhindi wako wewe mwenyewe huku sisi tukisubiri kama ni mahindi yaliyokomaa na kufaa kuliwa!

Hizo habari zako za siri sasa hamna mtu ana haja nazo...Hako kanzi kweli ni kale kale?

Maana kwa ufahamu wangu kanzi kanaishi kwa siku saba kisha kanakufa hivyo lazima utrain vinzi vingine kila mara baada ya siku saba?

Sasa habari hiyo hapo juu ya Wanasheria wa bongo inatofauti gani na mjadala wangu na mabishano yetu toka Ballali akiwa hai hapa Marekani january mwaka huu?!

Akiwa mtaani hapa marekani ulikuwa ukimsapoti Kikwete na kudai Ballali ni mtu huru ambaye haitajiki?

Kuiponda pointi yangu kuwa Ballali is a key suspect!

MKJJ unataka kuumbuka mara ngapi?

Omba msamaha ndugu yangu na urudi upande wa wazalendo!

Usilete siasa na zoga kwenye issue nyeti zinazohitaji black and white kinda thinking!
 
Back
Top Bottom