Kwanini Dr. Slaa anawasifia polisi?

Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.

source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa

kauli za Dr. Slaa siyo za kujadili kijuu juu kwa sababu zimejaa 'falsafa'.

napita tu.
 
nadhani Chadema imepata uungwaji mkono mkubwa toka jeshi la polisi mara baada ya kutetea vilivyo maslahi ya polisi katika kikao cha bunge kilichopita ndio maana kila unapopita kwenye kambi za polisi unawasikia wanasema wanatii amri ya viongozi wao lakini wao mkombozi wao wa kweli ni Chadema.

Lakini kwa upande wa pili wa kitendo hiki cha polisi kuanza kuunga mkono harakati za ukombozi kinawashitua sana watawala na ndio maana wanatafuta kwanini hasa kunakuwa na tabia hii ndani ya taasisi yao na pengine kunapelekea mkanganyiko baina ya viongozi wa serikali wanaowatuma na polisi wenyewe.

polisi wamechoka kuendelea kupata mshahara mdogo huku gharama za maisha zimepanda. hii itapelekea sitofahamu ndani ya jeshi hili na kuna mgawanyiko mkubwa kati ya makamanda wanaotaka mabadiliko na wale waliozoea kufanya mambo ya kale na unyanyasaji.

kwa ujumla serikali iliyo madarakani imechoka na watendaji wake hawawezi tena kuwa team moja , uchumi wa nchi umedondoka na kunakoelekea ni serikali kushindwa kulipa mishahara kwa watumishi wake.
 
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.
source:twitter akaunti ya Dr slaa
twitter@drwilbroadslaa

I suspect huwa wanampa information fulani hivi ahead of time (behind the scene) ambazo mimi na wewe hatujui. Hatuwezi kujua baada ya kuwakamata huwa wanamueleza nini kuhusu the "enemy next move/plan". This is just the theory though.
 
Dr. anawalainisha ili next tym akifanya mgomo au akichochea vurugu, wasipige.. Dr..... plse tafuta approach nyingine, hiyo ya kukwaruzana na polisi na magwanda haina tija. Naona ni bora ukatuhamaisha vijana tukaingia street, kumpinga kikwete. Wewe tutafutie sababu yoyote ile tutiunga mkono, mpaka kikwete tumtifue kama Gaddafi, na Ridhwan tummalize hadharani.. Plse dr. slaa, do something
 
Mhhh maneno haya angesema Zitto (muislam), basi ungesikia ooh CCM huyo, pandikizi, msaliti, na sifa zote mbaya...lakini kasema PADRI mstaafu Slaa (mkristo), basi sifa zote nzuri anapewa, sijaona post iliyo against na kiongozi wao wakiroho na kisiasa!

Bravo, ukitaka kujuwa rangi ya CDM njoo JF, ni typical udini mtupu! Wanachuki na uislam na waislam, sipati picha hata kwa bahati mbaya mkatawala nchi hii...hivi waislama watasalimika kweli?

Kweli nimechoka na CCM lakini na CHEDEMA hapana, sitojaribu! Haihitaji kurunzi kujuwa ni chama chenye wafuasi na itikadi ya dini gani!

Wamesema waungwana "Zimwi likujualo, halikwili likakwisha" Bora nibaki na zimwi hili linijualo (CCM) kuliko hilo lisilonijuwa! Ntaendelea kusubiri mpaka kitakapo kuja chama mbadala wa CCM!
 
Ukiwa mdini,kurunzi lako litakuonyesha udini.
 
kuna watu wameponda sana ishu ya cdm kuweka kambi pale nmc wakisema kuwa ni kitendo cha kitoto. Hawaijui siasa. Siasa inapimwa kwa vitu vingi. Wanaofanya siasa ndio wanaojua. Sasa cdm wangefaham vipi kuwa polisi wamepunguza kupiga? Hii inaitwa longitudinal research. Wanaisoma dola hatua kwa hatua na sasa wamegundua kuwa dola iko pamoja nao. Kinachosubiriwa ni muda tu waweze kusaidia upinzani in full
 
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.

source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa

Sasa kati ya wewe na Slaa nani aaminiwe, maana yeye ndiye aliyekuwa arusha na amejionea matendo ya polisi wakati alipokamatwa.
 
kuna watu wameponda sana ishu ya cdm kuweka kambi pale nmc wakisema kuwa ni kitendo cha kitoto. Hawaijui siasa. Siasa inapimwa kwa vitu vingi. Wanaofanya siasa ndio wanaojua. Sasa cdm wangefaham vipi kuwa polisi wamepunguza kupiga? Hii inaitwa longitudinal research. Wanaisoma dola hatua kwa hatua na sasa wamegundua kuwa dola iko pamoja nao. Kinachosubiriwa ni muda tu waweze kusaidia upinzani in full

Acha justification zako za kitoto katika mambo serious. Huwezi kukusanyika NMC kuilazimisha mahakama kumuachia huru mtuhumiwa aliyekataa dhamana yeye mwenyewe. Hata kama Lema alikubali kutoka nje kwa dhamana, mahakama zina mamlaka zake na mamlaka hizo haziwezi kuvurugwa na mikusanyiko na mikesha ya NMC. Na wala mkusanyiko huo haukuwa na lengo hilo la longitudinal research unayoizungumzia wewe.
 
Shida ipo kwa huyo chagonja, nadani hapo alipo fikia (Cheo) ni cha kupewa kama zawadi, na ndo maana yeye anabwabwaja tu. akili yake ni kama ya Mahita. Watu wasio na elimu na kupewa majukumu makubwa ni shida kweli
 
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.

source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa

Dr. yuko sahihi kwa specific event ya NMC, tambua hao jamaa hutumia nguvu only if kama kuna resistance or security threats, bt kama kuna diplomacy approaches hawako kihivyo. By the way wanasoma sana Rules of engagement na Human Rights.

Gd day.
 
Hauna taarifa ktk uchaguzi uliopita CDM iliongoza ktk vituo vyote vilivyokuwa kwenye kambi za polisi?
nakuunga mkono hata wanajeshi walikuwa wanavalia kiraia wanahudhuria mikutano ya cdm.Polisi nao maisha ni magumu maana pesa hiyohiyo ya mshahara wanatunza familia zao na kusaport wazazi wao tunaoishi nao mitaani kwenye maisha magumu.
 
Pia nami nilishangaa kidogo hasa askari alikuwa na Dr. slaa alionesha upendo sana na alikuwa tayari kumshika mkono ili ashuke vizuri kwenye karandinga. wanapofanya vizuri tuwapongeze, hata wafuasi wa chadema kimara hawajapigwa
 
Mhhh maneno haya angesema Zitto (muislam), basi ungesikia ooh CCM huyo, pandikizi, msaliti, na sifa zote mbaya...lakini kasema PADRI mstaafu Slaa (mkristo), basi sifa zote nzuri anapewa, sijaona post iliyo against na kiongozi wao wakiroho na kisiasa!

Bravo, ukitaka kujuwa rangi ya CDM njoo JF, ni typical udini mtupu! Wanachuki na uislam na waislam, sipati picha hata kwa bahati mbaya mkatawala nchi hii...hivi waislama watasalimika kweli?

Kweli nimechoka na CCM lakini na CHEDEMA hapana, sitojaribu! Haihitaji kurunzi kujuwa ni chama chenye wafuasi na itikadi ya dini gani!

Wamesema waungwana "Zimwi likujualo, halikwili likakwisha" Bora nibaki na zimwi hili linijualo (CCM) kuliko hilo lisilonijuwa! Ntaendelea kusubiri mpaka kitakapo kuja chama mbadala wa CCM!
Na vipi angesema prof Safari au Mh Halima mdee??? Kwanza mkuu Zito angesemaje wakati hayuko Arusha bali ni mgonjwa na yuko India??? Wewe unayejua itikadi za wengine una itikadi gani?! Katika post zote hapa ni nani ameonyesha udini kama siyo wewe?! Hizi dini zenu angalau zingewasaidia kuacha unafiki na chuki, tungeziona za maana... Hivi mtu kama Shibuda au Chenge ni waislamu?! Yaani imefika mahali watu kama wewe mnataka kabla mtu hajakosolewa mkosoaji aangalie jina, kama siyo wa dini yake asimkosoe kwa sababu tu mtasema anamkosoa kwa sababu si wa dini yake...!!!
 
Waheshimiwa nimetambua mambo mengi aliyotumia dr.slaa kutoa kauli yake , nadhani yupo sahihi kwa kauli yake kwani nimejaribu ata kuwauliza polisi na wanajeshi wa nchi wetu wanaonyesha kuchoka na jinsi serikali inavyowatumia vibaya na kuwalipa mafao madogo. watumishi wengi wanafikiria zaidi ya maisha na kazi zao za wakati huu.yaani watapostahafu watafanya nini na je jamii wanaitendea haki?
 
Hapo nami naona mnasema ukweli, hii inaonesha ni jinsi gani Dr slaa ni chaguo la wengi na anachokisema lazima kila mtu akikubali, angesema Rahisi Jakaya kila mtu angemkemea na kusema ashindwe na alegee takribani viungo vyote.
 
Back
Top Bottom