Kwanini Dr. Slaa anawasifia polisi?

king11

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
327
79
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. Mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.


source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa
 
Kuna mabadiliko kidogo katika jeshi la polisi lakini bado wanahitaji kufanya mambo mengi ili wapate heshima katika jamii ya watanzania.

Pia ni sababu ya kamanda Siro mkuu wa operation maalum jamaa huyu alitoka Mwanza kabla ya kuchukua nafasi ya Tossi ni kamanda bora kuliko wote katika jeshi la polisi na mwenye kutenda haki pia.

Mambo yake ayaendeshi kisiasa nadhani kama siku akiwa IGP basi jeshi la polisi litapata heshima kwa jamii yote ya kitanzania
 
Police waachane na taarifa za ki-intelijensia wanatupiga changa la macho wanavyotumia hiyo kauri
 
Mbona akiwakosoa hushangai ila akiwasifia unabweka? kwani mtazamo wangu na wako lazima uwe sawa? polisi wa sasa na wale wa enzi ya mwinyi/mkapa unadhani wako sawa? kasema wanabadilika na kujitahidi kuwa wasafi hajasema ni wasafi 100%
 
Hawa Polisi wadogo nao ni watanzania jamani, unafikiri wanfurahia kupiga watu? Lakini tatizo ni nidhamu ya kijeshi ndiyo inayowaponza. Ukiambiwa piga unatakiwa kupiga kwanza kabla ya kuuliza kwa nini.

Wenye shida na matatizo ni akina Mwema, Chagonja, Sillo, na huyu jamaa wa kanda maalum ya Dar. Hawa wanajitahidi kumpendeza mkuu wa kaya. Lakini wajue iko siku hawa wanaowatuma kupiga raia watageuza hizo bunduki kwao, na hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Dr. Slaa amesema siku nyingi Polisi wanalazimishwa kufanya wanayofanya na wakubwa zao, vinginevyo ukweli ni kwamba Polisi hawawezi kusema hadharani lakini wanaunga mkono harakati zetu za kudai uhuru kutoka kwa hawa wakoloni weusi.

Yeye Dr. Slaa anaweza kulinganisha kilichotokea juzi, kilichotokea jana na kinachotokea leo, anaweza kujua kama wamepunguza mabavu ama la.

Anachosema hapa ni kwamba anaona kuna jinsi wamepunguza mabavu, ni dhahiri wanaelewa hali halisi na sasa wanahofia hali kuchafuka kama wakitumia mabavu badala ya kutumia akili.
 
Dr. Slaa yuko sahihi kwa sababu polisi wangeweza kuua alfajiri ile pale NMC lakini waliwakamata na kuwapeleka panapohusika.
 
Kuna mabadiliko kidogo katika jeshi la polisi lakini bado wanahitaji kufanya mambo mengi ili wapate heshima katika jamii ya watanzania.

pia ni sababu ya kamanda Siro mkuu wa operation maalum jamaa huyu alitoka mwanza kabla ya kuchukua nafasi ya Tossi ni kamanda bora kuliko wote katika jeshi la polisi na mwenye kutenda haki pia, mambo yake ayaendeshi kisiasa nadhani kama siku akiwa IGP basi jeshi la polisi litapata heshima kwa jamii yote ya kitanzania

Huo UIGP anajiteua yeye? Anayemteua ni Rais wa Nchi ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama kilichopo madarakani. Hawa Polisi sio kila kitu wanafanya kwa kupenda bali ni mashinikizo kutoka juu. Hapa kuna umuhimu wa kuliangalia wakati wa Uundaji wa katiba
 
Nimeshangazwa na kitendo cha Dr.slaa kulisifia jeshi la polisi kuwa limeanza kuelewa maana ya majukumu yake kwa kutenda haki na kutowapiga wanachadema waliokamatwa kwenye sakata la viwanja vya Arusha. mimi binafsi naona jeshi ili bado linaendesha ukatili kwa wanchama wa vyama vya upinzani kinyume na usemi wa katibu mkuu wa Chadema.


source:twitter akaunti ya Dr slaa

twitter@drwilbroadslaa

Dr Slaa anaonegelea specifically kwa issue ya Arusha (mkesha) - "hakuna aliyepigwa" kama nimekuelewa vizuri!
 
Alichokifanya Dr ni on-going-evaluation ameangalia kilichotokea jana na kulinganisha na yaliyotokea nyuma kwahiyo yupo sahihi.
 
Who is presidential material....hell No..too old to lead us....he is doing great by being activist.......labda mbowe Au LEMA
 
Yes, kadiri siku zinavyosonga mbele polisi nao, na watu wengine waliopo katika utumishi wa umma, wanaanza kujiona kuwa ni sehemu ya mapambano ya kuleta mabadiliko. Dk Slaa amekuwa akiwaelimisha polisi kila siku kuwa wao nao ni sehemu ya watanzania waliopigika, na wameanza kuielewa hii zana. Na hapa tunaongelea askari wa kawaida ambao ndio wengi na sio hao vibosile ambao ni sehemu ya mfumo tunaoupinga.
 
Kwa mtu ambae una ndugu yako polisi unaweza kuelewa nini anachomaanisha Dr. Slaa

Polisi ni wafuata order na unapokuwa nao sehemu tofauti na "order" utawagundua ni binadamu sawia na wenye kuumia pale wanapolazimika kutekeleza order

Kwa taarifa nilizonazo kwa watu Arusha, wako Polisi wengine ambao waliwasaidia vijana wengi tu wa CHADEMA "kutokea" kwenye njia na pande ambazo hawawezi kukutana na polisi ambao wako chini ya "makamanda watoa order"
 
kwa kuwa kasema dr. slaa post karibu zote zina sapoti wangesema wengine humo tungesikis wametumwa na magamba na majina kibao wangepewa
 
Back
Top Bottom