MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,233
- 22,317
Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba kueleza sababu chache za muhimu kwanini CHADEMA bado wanastahili kuadhibiwa kwenye sanduku la kura na wazalendo wote. Kwanza kabisa niseme kuwa sina chuki yoyote na hiki chama kinachojifia. Mimi kama mkristo ninaamini kila kitu kina mwisho wake isipokuwa Mungu tu. Siwezi kuzuia mwisho wa CHADEMA. Tatizo ni huu mwisho umekuwa wa ghafla. Huwa tunasema "nimevipiga vita vilivyo vizuri, na mwendo nimeumaliza" lakini kwa CHADEMA vita walivipiga ila mwendo ukakatishwa mwaka 2015 kwa tamaa za watu wachache walioamua kumuuzia chama mtu waliyemwita fisadi.
Pamoja na kwamba ni chama kilichopo kwenye mwisho wa uhai wake bado kinastahili kuendelea kupokea adhabu kali kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ndani ya Tanzania. Sababu zifuatazo zizingatiwe;
1. KUTOTII KATIBA YAO WENYEWE: Hii sababu inaweza kuwa inatosha kabisa kusema CHADEMA hakistahili kushinda uchaguzi wowote. Kabla ya utawala wa Sultani Mbowe hiki chama kilikuwa kinafuata katiba yake na kuheshimu sana vipindi vya uongozi. Ila kwa sababu anazozijua Mbowe akaamua kubadili katiba na kujiruhusu kugombea uenyekiti kwa nyakati zote. Watu wote waliojitokeza kutaka uenyekiti waliishia pabaya. Kama ndani ya chama hali ni hii vipi wakipewa nchi?
2. UKANDA, UDINI NA UKABILA: Hii ni kansa ambayo imeshindikana kutibiwa. Imeshaitafuna CHADEMA vya kutosha. Tunaona walioko mstari wa mbele kwenye hatari zote ni watu wa kanda zingine na makabila mengine kama Mdude na Lissu. Ila wamiliki wa chama toka kaskazini huwakuti kwenye hekaheka zozote. Kuhusu udini sina haja ya kuelezea sana kwa sababu CHADEMA wenyewe waliamua kujitokeza hadharani kuonyesha rangi zao kwa kupitia mkutano wa kisiasa uliohutubiwa na viongozi wa dini. Mkutano wa Temeke ni doa baya lisilofutika kwenye siasa za CHADEMA.
3. UBADHIRIFU NA UFISADI WA FEDHA ZA CHAMA: Hapa viongozi na makada wa chama hiki huwa wakali sana wanapoulizwa kuhusu matumizi ya fedha za chama. Kimsingi fedha za hiki chama zinatafunwa na wajanja wachache. Kumekuwa na matumizi ya hovyo yanayoacha maswali mengi. Hadi leo michango ya Join The Chain haijulikani ilitumikaje. Viongozi wote wanakwepa kuongelea. Bilioni 1.5 wametumia kununua pagale huko Mikocheni. Yaani thamani ya pesa haionekani unapotazama lile pagale na 1.5b. Hawa wakipewa hazina ya nchi si itakuwa balaa?
4. KUTOKUWA NA SERA WALA AGENDA: Hili tatizo halikuwepo kabisa kabla ya 2015 lakini baada ya hapo chama kimebaki na makada watupu vichwani wanaowaza kutukana tu. Wanatukana hadi Rais wa jamhuri Hata kwenye huu uzi wanaweza kujitokeza. Baada ya cream nzima ya CHADEMA kuondoka na kuunga mkono juhudi za serikali ya CCM ikawa pigo kubwa kwa Mbowe na chama chake. Kimsingi viongozi na wanachama waliopo kwa sasa hawana hoja zaidi ya matusi.
5. KUTOKUWA NA MSIMAMO: Hili tatizo linarekebishika kwa kupata wanachama wapya watakaopata nafasi ya kuongoza. Hiki chama kimekosa msimamo na kuamua kudandia kila hoja itakayojitokeza mbele yake. Kuna wakati chama kizima kilijitokeza kupinga mwanamuziki Diamond Platinumz asipigiwe kura kwenye tuzo. Ilikuwa ni aibu.
6. HAKINA HESHIMA KWA WANAWAKE: Hapa hakuna cha kuongea sana kwasababu kila kitu kipo wazi. CHADEMA kuwaita wabunge wake wa viti maalum Covid19 ni jambo watakalojutia daima. Kina mama waliokipigania chama kwa jasho na damu walizawadiwa jina la Covid19. Hii ni laana. Bahati nzuri hata wanawake wa CHADEMA kupitia BAWACHA walishatambua janja janja ya kina Mbowe na kuamua kumwalika Mama Samia kuwa mgeni rasmi kwenye siku yao. Hii inamaanisha kuwa 2025 wanawake wote kura kwa Samia.
Nimalize kwa kuwasihi wazalendo wote wa nchi hii kufanya kama tulivyokubaliana. Ni kukiadhibu chama cha Mbowe kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ule.