Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi.

Naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zinazotoka kila siku ya Jumatatu kwenye gazeti la Raia Mwema, hili likiwa ni bandiko mwendelezo wa Licha ya CCM kuwa chanzo cha umasikini, ujinga, rushwa na ufisadi, kwanini CCM bado huwa inashinda chaguzi mbalimbali?

Declaration of interest
Kabla sijaendelea, naomba kwanza ku declare interest kuwa japo mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, mimi ni kada Mzalendo mwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa ndipo cha kinafuata.

Leo naanzia nilipoishia wiki iliyopita, nikiendeleza Makala zangu elimishi Kwa Maslahi ya Taifa, nikizungumzia mambo mbalimbali ya taifa letu. Leo nikiendelea kueleza kwa nini, licha ya kuwa CCM ndio chanzo cha umasikini wa taifa hili, lakini bado ni CCM imeendelea kushinda ushindi wa jumla katika chaguzi mbalimbali hata baada ya Tanzania kuanzisha mfumo wa vyama vingi zaidi ya miaka 25 iliyopita.

Tumefanya chaguzi kuu 5 za vyama vingi, 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na zote CCM imekuwa ikiibuka mshindi, jee kushinda huku kwa CCM, ni kwa sababu CCM inapendwa na inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeleo haya yaliyopo. Pia CCM inashinda kwa kukosekana kwa upinzani imara na madhubuti. Pia CCM inashinda kwa sababu ya mazoea tuu ya Watanzania, kutokana na elimu duni ya mpiga kura, na umasikini, uliotopea, hivyo wapiga kura wengi wa Tanzania kujikuta hawana uwezo wa kufanya informed decision?.

Tanzania tulipoingia mfumo wa vyama vingi, tuliuparamia tuu, bila kujiandaa kimawazo, kimifumo na kisheria, kuwa nchi ya vyama vingi, hivyo tumeingia kuwa nchi ya vyama vingi, kwa kubadili tuu katiba, bila kubadili mifumo, sheria na mitazamo, matokeo yake, tumeanzisha vyama vingi ndani ya set up ya mfumo wa chama kimoja, huku CCM kikiendelea kuwa chama dola CCM, na vyama vingine vikaanzishwa kushindana na chama dola.

1. Hoja ya kwanza, ni kutoka kwa wana CCM wenyewe kuwa CCM inashinda kwa sababu CCM ndicho chama pekee kilichotapakaa nchi nzima hadi vijijini, na kinapendwa na Watanzania, na kimekubalika kwa kuwaletea Watanzania maendeleo, nitaeleza kidogo kupendwa huku kwa CCM ni kupendwa gani, na hayo maendeleo CCM iliyoyaleta ni maendeleo gani.

2. Lakini sababu halisi ya CCM kuendelea kushinda chaguzi mbali mbali kwa mtizamo wangu kada mimi, sio kwa sababu tuu CCM inapendwa sana na inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeleo kiduchu haya, bali CCM inashinda na kuendelea kushinda kwa sababu, Tanzania bado tuko kwenye setup ya mfumo wa Chama kimoja, na CCM bado ni chama dola, chama bado ndio kimeshika hatamu za uongozi wa nchi hii, hivyo bila kubadili setup ya mfumo wa chama kimoja na kwenda kwenye setup ya mfumo wa vyama vingi, iliwemo kukiondoa chama dola kwenye mindset ya Watanzania, CCM itaendelea kushinda na kutawala nchi hii kwa miaka mingi ijayo, iliwemo kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa 2020 and in fact, CCM itatawala milele!.

3. CCM ni chama tajiri, ambapo kimeanzishwa kwa ku loot mali za Watanzania. Tulipoanzisha vyama vingi ilibidi CCM kivunjwe kwanza, na zile mali za CCM, zilizotokana na michango ya lazima ya Watanzania wote, yakiwemo majengo ya serikali, viwanja vya umma ambavyo CCM ilivimiliki wakati wa mfumo wa Chama kimoja, vilipaswa virudishwe serikalini na kuwa mali ya umma, CCM ianze moja kwa mali zake halali tuu, kama vyama vingine, lakini kitendo cha CCM kusajiliwa hivyo hivyo kilivyo na ukwasi mkubwa wa loot ya Watanzania, hakuna Chama cha kushindana na CCM na kuingia ikulu!.

4. Mind set ya vyombo vyote vya kiutendaji na kiutawala, iko ki CCM CCM tuu, kuanzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, vyombo vya dola, na watendaji wa vyombo vingine vyote vya kiutendaji, akiwemo Msajili wa vyama vya Siasa, wote wako ki CCM, CCM!. Mimi sisemi kuwa NEC sio tume huru, NEC ni Tume Huru ila sio inclusive. Japo uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za tume huru, lakini kwa vile NEC kuanzia Mwenyekiti wake, Mkurugenzi, makamishna, na wakurugenzi wote wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi, wanateuliwa na Mwenyekiti wa chama kimoja wapo, kuna uwezekano akateua makada watupu wa CCM, hivyo zoezi la uchaguzi kuendeshwa kwa ukada ukada zaidi kuliko utendaji ndio maana kuna watu wa chama kimoja wanapewa barua za utambulisho, watu wa chama kingine wananyimwa!. Kama mtu kama Jaji Mkuu wa Tanzania, anakwenda kugombea urais CCM, au CDF mstaafu!, hii maana yake hawa ni makada!. Kinachotakiwa kufanyika ni kubadili set up ya NEC iwe inclusive na kubadili sheria ya uchunguzi kipengele cha wasimamizi wa uchaguzi wasiwe makada, watafutwe watu waadilifu ambao ni neutral kabisa kuongoza NEC, na Ofisi ya Msajili wa vyama, na makamisha kufanyike ushirikishwa wa wadau katika composition yao, nafasi za usimamizi wa uchaguzi zitangazwe wenye sifa waombe na sio makada wateuliwa na mmoja wa wagombea ili neutrality sio tuu ionekane bali kuonekana ikitendeka. Pia tubadili sheria zetu za uchaguzi ziwe za haki.

5. CCM imejikita Vijijini, Wapinzani Wamejikita mijini, vijijini ndiko kwenye kura za uamuzi, yaani decisive votes, kutokana na ukongwe wa CCM ambacho kilikuwa chama dola kilichoenea nchi nzima kwa mujibu wa sheria, kuanzia wajumbe wa nyumba kumi, mashina, matawi nchi wamesambaa nchi nzima, kutokana na utajiri wa CCM, CCM ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuwa na ofisi nchi mzima, tena sio ofisi moja, bali ni ofisi nne kwenye baadhi ya maeneo, ofisi ya CCM, ofisi ya UVCC, ofisi ya UWT, na ofisi ya Jumuiya ya Wazazi, ambako kote huko kuna maofisa wanaolipwa mishahara, wakati ofisi za vyama vya upinzani ni watu wanajitolea nyumba zao na wanavitumikia vyama hivyo kwa mapenzi yao tuu bila kulipwa chochote!, hivyo chochote ambacho CCM inakipanga kinawafikia wananchi wa chini, na wakati wa kampeni, kama CCM inawafikia Watanzania, ni wengi zaidi vijijini na ndiko kwenye kura za ushindi, kwa sababu CCM imewafikia, lakini akitokea mpinzani kusema ukweli, ukweli huu huishia mijini tuu, msihadaiwe na wingi wa watu kwenye mikutano ya kampeni za mijini, hizo sio kura, kura za kweli ziko vijijini hivyo kwa mazingira haya, huwezi kushindana na CCM, ukaishinda.

6. Ukosefu wa elimu ya uraia kwa Watanzania, tangu tumeanzisha mfumo wa vyama vingi, hakujawahi kutoa elimu yoyote ya uraia, kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa uwepo wa vyama vingi, hivyo waliowengi wamedanganywa kuwa vyama vya upinzani vinakuja kuharibu umoja wetu kuleta fujo na kuhatarisha amani yetu na utulivu, sasa ukiwasikia viongozi wa upinzani wanavyoongea kwa jazba, na vyama vyenyewe ni vya kiharakati, vingine na sare za kijeshi jeshi, Watanzania wapenda amani, wanaogopa kuviamini. Ingetolewa elimu rasmi ya uraia na kuwafikia Watanzania wote, na Tanzania ikawa na vyama serious vya upinzani wa kweli, na Watanzania wakaelimishwa siku nyingi CCM ingeisha pumzishwa kwa amani!, hakuna mtu yoyote anayependa kula mboga moja siku zote!, Watanzania wangependa sana kubadili mboga, tatizo ni hakuna hata hiyo mboga ya kubadilisha!.

7. Umasikini uliotopea, ambao pia pia unakwenda sambamba na ujinga. Mtu masikini wa kipato, chakula cha shida, mlo mmoja kwa siku, anaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, akili yake pia inadumaa. Mtu kama huyu shida yake ni mlo, na mavazi, sasa akiletewa ile Tshirt na kofia, na pilau ya siku moja, inatosha kabisa kukichagua chama kilichokulisha na kukuvisha, anakuwa hana uwezo kusikiliza sera na kufanya informed decisions, angalieni maeneo yenye umasikini uliotopea na elimu duni ndio strong holds za CCM. Mikoa yenye ehueni kiuchumi kama Arusha, Kilimanjaro, Bukoba, Iringa, Mbeya. Tanga na maeneo ya mijini, watu walioelimika, kidogo wanaweza kuchagua upinzani, lakini mikoa yenye umasikini wa kutupa kama Dodoma, etc, usitegemee upinzani unaweza kushinda!, shida ya masikini ni njaa tuu, CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kugawa rushwa, ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na fedha za Kagoda upo!. Hivyo CCM kuutumia umasikini wa Watanzania na Ujinga wa Watanzania kama mtaji wake wa Ushindi.

8. CCM inaendelea kushinda kwa sababu, uwanja wetu wa mashindano ya siasa ni uwanja tenge ambao umelalia upande wa CCM, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili, halafu mgombea mmoja ameshika kwenye mpini, na mwingine kwenye makali. Vyombo vyote vinaipendelea CCM, kuanzia mfumo uliopo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, vyombo vya dola, huku mgombea mmoja mwenye ving'ora na kila kitu, JWTZ, Polisi, ukwasi mkubwa, ameishika dola na kuitoa igombewe na wengine wasio na kitu kabisa!.

9. CCM inaendelea kushinda kwa sababu Tanzania bado hatuna upinzani Imara, huu upinzani uliopo sasa ni upinzani uchwala, upinzani lege lege, hivyo kamwe hauwezi kushinda kushika dola hivi hivi ulivyo. Mimi nakubaliana kabisa na hoja ya Baba wa Taifa kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM!, huu upinzani dhaifu uliopo sasa, na utitiri wa vyama, vyama vya kiharakati, hauwezi kuwapeka wapinzani ikulu. Kujiengua kwa Lowassa kutoka CCM ile 2015, na kujiunga upinzani, ndiko kulikoupatia upinzani mafanikio makubwa kabisa katika upinzani nchini Tanzania, tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, ingekuwa sio hali ya afya ya Lowassa, wafuasi wake na wale wote wenye Imani na Lowassa wangemfuata!, CCM ingepigwa chini!. Kama kwa hali ile tuu alivyo, ameweza kuvuna kura milioni 6, ambazo ni nyingi kuliko zilizomrudisha Kikwete ile 2010, tena kwa taarifa tuu, kwa upande wa Zanzibar, Lowassa ndio aliyepata kura nyingi kuliko Magufuli, kwa mujibu wa matokeo ya NEC, hivyo Zanzibar CCM ilipigwa chini!, hivyo kama Lowassa angekuwa fiti kabisa kiafya na hana mazongezonge ya ufisadi, amini usiamini, CCM ingepigwa chini ile 2015.

10. Wapinzani hawana sera, wala hawajui wanatakiwa kufanya nini, upinzani wa kweli, unapaswa kuonyesha sera mbadala na CCM, mfano sera ya elimu ya CCM ni elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, upinzani wao wakasema sera yao ni elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu. Hapa wangekuwa ni wapinzani makini, sera hii tuu ingetosha kuipiga chini CCM!. Au sera ya Afya bure. Wapinzani hawakupaswa kuishia kusema maneno matupu tuu ya elimu bure hadi chuo kikuu, walipaswa kuja na roadmap ya how?. Wangewaeleza Watanzania watabana wapi matumizi ili kupata kupata fedha za kugharimia elimu bure, kwa kuainisha ufisadi wa serikali ya CCM, mfano kusema utaunda baraza dogo tuu la mawaziri lenye wizara 10, hizi zitaokoa kiasi hiki ambacho kitapelekwa kwenye elimu. Au kujumlisha jumla ya fedha zote zilizofujwa na CCM kwenye ufisadi wa EPA, Deep Green, Meremeta, Escrow, etc na kuonyesha jinsi ambavyo zingetumika kugharimia afya na elimu bure, ili kuwapa Watanzania chaguo mbadala!.

Hitimisho
Ujio wa Dr. John Pombe Joseph Magufuli kama rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM, hii sasa ndio funga kazi!. Kwanza huyu jamaa ni mchapakazi kweli kweli hivyo ataimarisha CCM na kuufifisha upinzani, hivyo uchaguzi wa 2020, upinzani hautafurukuta, tunairejelesha Tanzania chini ya mfumo usio rasmi wa chama kimoja cha siasa, japo jina la Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa, litaendelea, na vyama vya upinzani vitaendelea kuwepo, vitakuwa vipo kama havipo, na CCM ikiimarika kabisa Kiuchumi 2020-2025, kuna uwezekano ruzuku kwa vyama vya siasa ikafutwa, hivyo chama kubakia CCM pekee!.

Nawatakia Furahi Dei Njema

Wasalaam

Paskali
 
Pascal Mayalla baada ya miaka 30 wale wa vijijini (lumpen proletariat) ambao hawana class consciousness watakuwa wameisha na hivyo kuwa na kizazi chenye kujitambua being class conscious, then mabadiliko yatakuja. Pamoja na kuwa kwa sasa CCM haishindi na ndiyo maana kuna matumizi makubwa ya corporal organs of the state,,,, instruments of oppression!
 
Pascal CCM inashinda kuna kitu kinaitwa Poverty au Umaskini, Mikoa mingine wanashinda kwa kugawa kofia na madela tu baada ya hapo wananchi wanasahau

Wananchi wanatakiwa siku moja wajibu mapigo kwa watawala, Na Hali inavyoenda watajibu mapigo

Mtwara ni mji mdogo walipojibu mapigo, Serikali ilihamisha kambi zote na wanajeshi wa Ruvuma huko kwenda kuzuia, wakaleta mpaka Polisi wa Zanzibar na kamji kadogo, Leo story za gesi kuwa uchumi watawala wamezizima

Yapasa mikoa Kama 10 kwa wakati mmoja ijibu mapigo kwa maandamamo na mapambano kama Polisi wataua maelfu miili ya watu itajaa barabarani itafika sehemu watawala wataacha

Mtwara walijibu mapigo, Polisi wote mtaani walihama na wananchi walikubaliana adui yao namba moja ni polisi hivyo hakuna aliyeruhusu kupangisha polisi

Serikali ilitumia wenyeviti kuomba msamaha leo mambo yametulia ingawa Uchumi wa gesi waliodanganya umekufa kifo cha mende
 
Kwa sababu wale ambao walionekana kuwa mbadala waliwasaliti wananchi dakika za mwisho kwa vipande thelasini vya mwenyekiti.

Kumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa 2014. Chama chetu kilikuwa kinashinda kwa speed nzuri tu! na kulikuwa na kila dalili ya matumaini kuwa safari yetu haiko mbali kufika Kanani.

Lakini tamaa za kupata kula na kura bandia za wenye hasira ndani ya CCM za mgombea wao kukatwa jina tukadhani tumepata kumbe ndo tulipopatwa.

Wakaja watu hawana mapenzi yeyote na chama chetu wao mapenzi yao "mtu" wao apate URAIS tu.

Baada ya uchaguzi kuisha na kuona Ngosha kachukua nchi, wengi kama sio wote wamesharejea kwao na kura zao. Sasa wametubu na wanaeneza injili yao.

Sie tulichachafua injili yetu hata tukiihubiri waumini wanatuona mashetani tu.
Siku hizi CHADEMA masalia tuliobaki chunguza hoja zetu humu ndani asilimia kubwa ni matusi tu na kumlaumu Ngosha utadhani waliotangulia walikuwa wanatupenda saaaana!
Tumesahau wengine tulikuwa tukiwaita DHAIFU.
 
Ccm must go...
Haijawahi kushinda uchaguzi.
Kila mtu anaelewa hilo, muulizie @Nnape, Evarist Chahali, Poise, Lowasa.

Ni busara tu zinatumika ili nchi yetu isizame kwenye vita.

Mfano, Nyerere alisema hawezi kumpa nchi Fulani yulee,

Mkapa, Akasema, hakuna kutangaza mpinzani kuleee, kila mtu anakumbuka kilichotokea.

Kikwete akasema, waache watasambaratishwe / hawatafika popote hao.
Mfano: 2010 JK hakushinda , kumbuka JK 2005 alipata 80+% mwaka 2010 akapata below 60% unadhania zilikujaje !? Ni baada ya kupigwa hasa ikabidi kitu kiwekwe Kichwa chini kwa miguu juu .

Hata hii 2015, Lowasa alishinda ila busara alizonazo Lowasa siyo za dunia hii.
Hakika, Lowasa, angekuwa ni tamaa mbele ya kuingia nadarakani jumba jeupe leo tungekuwa zaidi ya genocide ya Rwanda japo yetu ingekuwa ya kisiasa.
Mtu asibishe kuhusu 2015 bali wekeni yale matokeo yaliyotangazwa na jaji sijui nani (sitaki kumtaja jina, kila mtu anamfahamu) kisha angalieni zile figures mtaona vituko kwa uchaguzi wa 2015.

Zanzibar penyewe tuliona sarakasi za tume ya uchaguzi uo huo mwaka 2015 ni maajabu ya Nane ya Dunia, ila busara ya Seif na baadhi ya wazee nahisi ilitumika kuacha tu ile hali isijesababisha matatizo makubwa.

Juzi pale tuliona waliojiandikisha uchaguzi fulani wa marudio nafasi ya mbunge (siyo siha na Kinondoni, Bali uchaguzi wa kabla ya hizo areas mbili tuliona huo muujiza wa wapiga kura kuwa automatically multiplied )
Yaani waliojiandikisha ni Elfu 25+ ila waliojitokeza kupiga kura ni 46+.

Hiyo hoja , ilipoletwa mezani ikabidi waseme kuwa aliyekuwa hana ID ya mpiga kura alitumia driving license kupiga kura ndiyo sababu ya idadi ya mshindi wa CCM kuwa na idadi kubwa.
Jiulize, je hilo jimbo kila mkazi ana driving license!? Inabidi tu ucheke na uendelee na maisha.

Kwa hiyo, tambua kuwa Tanzania tunaangalia kuwa nchi yetu itaendelea kuwepo ila vyama na hawa wanasiasa uchwara mbuzi wote watapita na kuacha Tanzania ikiishi hivyo watu wanaachilia tu ili tuishi kwa amani.

Pascal Mayalla , nikuulize swali:- unadhani ni kwa nini awamu hii ina hasira, visasi, chuki kwa baadhi ya watu hadi mikoa!?
Ukijibu hilo swali aidha hapa jukwaani au moyoni mwako basi utaelewa ninachokiandika.

Nnape, namnukuu, Hata kwa bao la mkono CCM itashinda akiwa kanda ya ziwa kwenye kampeni kampeni.

Tena, siku akitolewa Pistol ,, Alisema amepigana porini kufa na kupona miezi 28 ili CCM irudi madarakani (hakumaanisha kuwa alikuwa analala Serengeti au mikumi porini,,, akili kubwa tu ndiyo zinaelewa alichokisema).

Any way, everyone knows the rule of the game, but they are not respected at all.
 
Binadamu unawaita takataka ( lumpens)! Miongoni mwao wapo ndugu, jamaa, walezi na wazazi wako.
Lumpen wapiga kura. Nyie wasomi mnashindwaje kuwashawishi hao lumpens?
Unashindwaje kumshawishi mzazi wako asiichague Ccm?

Exactly, wapo wazazi, ndugu zangu, they are not conscious of themselves! Nakubaliana na wewe. Ni takataka interms of class consciousness! Kwa hilo nakubali. Nadhani wewe ni kijana wa juzi hukusoma political economy of capitalism and socialism and thats why you lack class consciousness!

Lumpen huwa hajielewi, lumpen kipande cha sabuni kinamtosha, lumpeni fulana inamtosha, lumpen hafikiri kuwa kula uchafu kuna hatari, lumpen huwa hafikiri kesho itakuwaje. Lumpen haweiz kuchanganua mambo, lumpen anaamini bado Nyerere yuko hai!

Note: sina chama, naangalia welfare ya society na human rights, basi. CCM ikizingatia hayo, haina shida kwangu, CDM, ACT wakizingatia hayo haina shida kwangu
 
Hapo kwa maoni yangu ni mchanganyiko wa vitu vingi hasa # 5 na # 6 lakini kuna hizi hesabu rahisi.CCM kimetokana na TANU ambayo ilianzishwa mwaka 1954 (2017-1954=63),vyama vingi vimeanzishwa 1992 (2017-1992=25),upo hapo?Nakubaliana na mchango wa mdau mmoja kwamba wanaoweza kuitoa CCM madarakani (kwa kura) ni kizazi hiki kilichozaliwa kuanzia 1990s na siyo mimi wala wewe!
 
Watu wanakufa unaandika siasa, Nonsense

Week Haijaisha Mauaji Makubwa Matatu,Kiongozi Chadema Kinondoni,Mwanafunzi NIT sasa Diwani Chadema Morogoro,Vyote hivi vina mlengo wa Kisiasa! Its Time kama Tumeshidwa Kuzuia haya Tuachane na Siasa Tulinde Roho za watu au Tutafute Suluhisho lingine!
 
Paskili CCM inashinda kwa Sababu CCM iko madarakani, hakuna tofauti kati ya CCM na governments organs. CCM ndio serikali, CCM ndio jeshi, police, usalama wa taifa n.k. Tatizo tulikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kubadili katiba. Katiba tunayotumia sasa hivi ni ya mfumo wa chama kimoja. Na tukiendelea na hii katiba CCM itaendelea kukaa madarakani hadi 2100, na JPM ikimpendeza anaweza kutawala maisha.
 
Pasco ni sehemu ya watanzania wajinga wanaoishindisha Ccm.

Pasco ni sehemu ya mafisadi na watetezi wa mafisadi waliotaka kuingia kwenye mfumo wa utawala lakini ikashindikana au niseme ikazuiliwa na watanzania waliobobea kwenye ujinga.

Pasco anaishi kwa vibahasha kama ilivyo wanahabari wengi nchini.
 
CCM inashinda kwa sababu hivi:

1. Umasikini kuto kujitambua kwa watu wengi vijijini kwa kupewa vitu vidogo, nilishawahi sikia wana wa sema wa pinzani kuwa wanaenda mikono mitupu

2. Watu wengi wanapiga kura kwa mazoea, hapa na maanisha tunaenda kupiga kura hatujui sababu za msingi kwanini tuna mchagua mtu flani na chama chake.

3. Tunapiga kura kwa ukanda na kujuana, mfano mwaka 2015 mikoa ya kanda ya ziwa hususani Mwanza ambayo huko nyuma ilikuwa na wapinzani wote walipigwa chini kisa mgombea urais katoka huko. Vile vile arusha na Kilimanjaro walipiga kura kwa kumuangalia mgombea urais alikuwa wa kwao.

4. CCM wanatumia vyombo vya dola na udanganyifu mwingi kwenye chaguzi
 
Back
Top Bottom