Kwanini Africa ukifikisha 35, 45, 55, tunasema ni mzee?

ward41

JF-Expert Member
Apr 3, 2022
397
1,394
Obama alianza uraisi akiwa 48 yrs na tulimuuita kijana.

Elon Musk ana 53, tajiri mkubwa namba moja duniani, tunamuuita kijana
Mark Zuckerberg ana 39, tajiri mkubwa tunamuita kijana

Kwanini Africa ukifikisha 35, 45, 55, tunasema ni mzee?

Nataka, kutoa somo moja Leo. Chanzo kingine cha Africa kuwa maskini ni kudharau watu wenye mkubwa.

Ni kawaida, mwanadamu anapifikisha 50 yrs, huwa anakuwa.

Kwenye ukomavu na utimamu wa akili. Chini ya hapo ni kubahatisha.

Viongozi wengi kwenye mashirika, makampuni, nchi huwa kwenye huo umri kuanzia 50-70 yrs.

Huwezi kupata maendeleo kwa kujaza uongozi kwenye kampuni, shirika, nchi watu wenye umri chini ya hamsini. Huo ni utani. Hutapata maendeleo.

Nchi zilizoendelea wanalijua hilo ndiyo maana labour tegemezi ni hiyo miaka.

Chini ya hapo mtu anakuwa Hana experience ya Mambo mengi hence makampuni mengi hayakuwi au kufilisika kabisa

Binadamu mwenye miaka kuanzia 50-70, anakuwa na uwezo mkubwa sana wa ki akili

Hata chunguza, wagunduzi wengi zamani walifanya ugunduzi wakiwa ni hiyo miaka.

Ni wachache walifanya maajabu chini ya hiyo miaka. Tukijaza watoto kwenye maendeleo ya jamii yetu ni hatari mno. Hatuwezi
Kusonga, mbele kama jamii

Old is Gold
 
Sio Africa pekee, hata ulaya, marekani na kwingineko iko hivyo.

Nafasi ya mtu katika jamii ndio husababisha awekwe kwenye kundi flani.

Kuna aina flani ya nafasi zinataka watu wenye umri mdogo. Hivyo ukifikisha tu miaka 30 unaitwa mzee kwa sababu huko ni kwa watu wenye umri mdogo. Mfano kwenye mpira, ukifikisha 30 wewe tayari ni mzee. Christiano ronaldo, messi na wengine wanaitwa wazee kwa sababu ya nature ya mpira.

Pili, kwenye mafanikio ya kiuchumi, hapa mara nyingi watu hupata ukwasi wa maana wakiwa wazee, mostly above 55 years walau ndio unaanza. Ndio maana Elon musk, Mo dewji waanaitwa vijana sababu wamepata fedha mapema zaidi kabla ya umri uliozoeleka wa watu wengi kupata mafanikio ya kiuchumi. Search orodha ya mabilionea duniani halafu angalia umri wao, majority wako 70+. Kumbuka msemo wa life starts at 40, miaka arobaini ndio unaanza kujitafuta sasa then unakuwa na interval ya miaka 15 hapo mbele ya kustabilize. Ukiwa bilionea chini ya hapo wewe utaitwa kijana tu.

Pia, kwenye siasa. Normally umri wa kushika nyadhifa za juu zaidi za kiuongozi kisiasa zinakuwa miaka 50+. Ndio maana Obama kuwa rais akiwa na 48 alionekana kijana. Vipi kama angetaka kucheza mpira kwa umri huo, je bado angeitwa kijana? Mwana FA amekuwa naibu waziri akiwa na 40+. Huyu anaitwa waziri kijana kwa sababu umri wake kisiasa bado ni mdogo. Lakini vipi kama mwanaFA akirudi kwenye bongo flava, utakuwa na guts za kumwita kijana bado?
 
Njaa baba,
Mtu ana miaka 35 na mimi over 60 lakini nilimpa shikamoo 😄
Kavurugika mpaka mwili
Kachoka kama alikuwa anakimbia miaka yake yote
Dhiki na umasikini mbaya sana aisee
Mimi huku wananisalimia MAMBO kidding
Sio kweli mkuu huyo ni mnywa mataputapu wala sio njaa kwa mujibu wa doctor janabi kula sana ndo kunazeesha ndo maana anashauri walau mara Moja kwa siku
 
48 kwa Rais ni kijana; 30 au hata 27 kwa mcheza mpira unaweza kuonekana mzee......

Its all in perspective.... By 32 Alexander the Great alifariki lakini at that time alisha-conquer Sehemu lukuki...; kwahio kwa alichofanya sio kwamba alikuwa ni kijana tu bali mtoto...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom