Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Wazazi na walezi wengi hujisahau kuwapa watoto maji ya kunywa....ukiona mtoto analialia jaribu yafuatayo
-mgeuzegeuze huku ukimminyaminya kila sehemu inawezekana kuna mahali kaumia au amaumwa
-mpe maji
-pengine joto limezidi inabidi umpunguzie nguo au umuweke kwenye hewa
-njaa
-uchovu
-usingizi
Homa nk
Si mara zote mtoto akiwa na mabadiliko yoyote ukimbilie hospitali, ni vema kujiridhisha kwanza kama kuna uhitaji wa kwenda hospital
 
Mimba inapotungwa mpaka kuzaliwa ni miezi tisa tumboni, haitimii mwaka, kwahiyo mtoto anapozaliwa itabidi mwaka wa kwanza apitie vipindi na majira ya mwaka mzima kwa mara ya kwanza hapa lazima kuna kuwa na mabadiliko kila wakati na hii ndio initial stage ya makuzi ni kipindi muhimu mno cha wazazi wote wawili kuwa wamoja na mtoto kupata maziwa ya mama to the fullest. ...kwa njia hii mtoto ataokoka na matatizo mengi ....vema wazazi wakaachana na mambo ya S26 lactogen lishe nk
 
Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.

Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.

Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2

Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.

Mimi nashukuru Mungu ka-baby kangu kwa miaka yake mitatu yote kanifaidi kwa 100%. Yani hakuna cha dada wa kazi wala mwalimu. Raha sana kwakweli maana kila nnachotaka ajifunze namfundisha mwenyewe na nisichotaka namkataza.

Nadhani nae ka-enjoy sana kuwa na mimi muda mwingi maana he is a very happy kid.

Sema huwa nakuwa dissapointed sana kuona watu wengine hawana hata muda kidogo na watoto wao.Unakuta mtoto na mzazi wake ni strangers, dada wa kazi ndo anaemjua na kumuelewa mtoto na mtoto kamzoea kuliko mama na baba yake.
 
Asante Dr.
Please fafanua kidogo kwa watoto wanaolialia usiku .kuamka amka na kulia....
Unampaje hiyo kitunguu saumu?
 
Hili jambo nimekuwa najaribu kusema lakini wazazi wetu yani wakwe na mama zetu huchangia sana kuumiza watoto ktk eneo hili kwa kisingizio mtoto anahitaji joto mtoto huwa hasikii joto wanashindwa kuelewa dar ni tofauti pengine na mkoani ulipozaliwa wewe au bibi huyo alipokuzia watoto wake wengine unaenda clinic daktari anakushangaa jinsi ulivyomjaza mtoto nguo nyingi kabaki macho tu.wazazi tuwe makini hawa ni wakubwa zetu ila panapobidi kuwaelewesha tufanye hivyo vinginevyo ni sisi ndio tunakuja kupata shida na watoto wetu badae.

Watu huwa wanadhani watoto miili yao ni kama sponge. Wakati in reality, kama wewe sio mgonjwa basi joto unalolisikia wewe ndo analosikia mtoto.

We ukiwa sehemu ambayo ukivaa nguo nyingi unajisikia un-confortable basi na mtoto nae anajisisikia hivyo hivyo.
 
Kwa wale wenye watoto wanaosoma
-ni lazima na ni muhimu kumpa namba zenu wazazi au kuziandika kwenye begi lake ni muhimu na zimesaidia wengi

-kumuonya tabia ya kuombaomba na kuwa makini na watu asiowajua. ..watoto wengi wanaopotea hupotea kwa staili hizi

Hawa watoto wanaosoma ni vema kuzifuatilia nyendo zao kwa karibu tabia zao marafiki walionao na vitu walivyo navyo kwenye mikoba na vyumbani mwao
 
Mada zako mshana jr nyingi ni nzuri na zenye mafunzo mazuri ila nadhani humu wengi ni vijana ambao hawajaanza kulea na mara nyingi mada kama hizi wachangiaji wanakuwa si wengi sana lakini weka mada ihusianayo na ngono uone!
 
Kama mtoto akipaliwa unapaswa kufanya nini?

Wengi wetu hukimbilia kumpa maji au kumpiga piga mgongoni bila kujua hasa nguvu anayotumia hii ni hatari kwa afya ya mishipa na mifupa ya mtoto.

Mtoto akipaliwa mpulize taratibu kwenye paji la uso na hata puani
 
Mshana ungefafanua vizuri kuhusu Asali, nijuavyo ni hatari sana kumpa mtoto mdogo Asali mbichi. At least akishazidi miaka mi5.

Kuhusu Pneumonia inasababishwa zaidi na baridi. Ukimwona mtoto anatetemeka sanaaa wakati wa baridi usitumie dawa yoyote zaidi ya chai ya rangi yenye tangawizi kidogo then mfunike alale. Akiamka yupo shwariii.

Shukran mshana jr kwa ubunifu wa mada hii.
Chai ya tangawizi mtoto mdogo atakubali kunywa kweli?


Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Umri gani mzuri?
 
Kwa wale wenye watoto wanaosoma
-ni lazima na ni muhimu kumpa namba zenu wazazi au kuziandika kwenye begi lake ni muhimu na zimesaidia wengi
-kumuonya tabia ya kuombaomba na kuwa makini na watu asiowajua. ..watoto wengi wanaopotea hupotea kwa staili hizi
Hawa watoto wanaosoma ni vema kuzifuatilia nyendo zao kwa karibu tabia zao marafiki walionao na vitu walivyo navyo kwenye mikoba na vyumbani mwao

Sio tu kuwaonya kuomba omba, ni muhimu pia wazazi wajitahidi kuwapa watoto wao vitu vidogo vidogo ambavyo wengi hushawishiwa navyo. Ukisikiliza kesi nyingi za watoto waliolawitiwa utagundua kwamba wengi hupatikana kwa kudanganywa na vitu vidogo vidogo (mf. Soda, pipi, biskuti, chips, karanga, kucheza game kwenye simu nk.), na wakishadanganywa mara moja, mara mbili inageuka mazoea kwasababu ya tamaa.

Ila mtoto anapojua kwamba mzazi wake anaweza kumnunulia vitu kama hivyo pale anapokuwa vizuri mfukoni sio rahisi apapatikie vitu hivyo kutoka kwa mtu asiyemfahamu. Kuna watoto wazuri mpaka raha, hata apewe hela au pipi na mtu asiyemjua au hata jirani hapokei ng'o. Na kama mzazi wake yupo karibu unakuta anamuangalia kwa muongozo, akiambiwa pokea anajua its owwkey, asipoambiwa chochote anajiongeza mwenyewe na kugoma kupokea.

Besides, vingi ya hivi vitu sio hata gharama. Ni vitu vya sh 50, 100, kwenda mpaka 1000. Mtoto akipata mara moja moja anazoea na kujifunza kutotamani anapoona mtu mwingine akila au akinywa.
 
Teh sijui kwanini uji ndio ratiba zetu wamama sijui nani alifundisha hii, huwa unawapa nini badala ya uji?
Nadhani ni kama ulivyosema hapo juu, NI CHAKULA RAHISI kwa gharama na maandalizi pia. Ukiacha wale ambao hujitahidi na unga wa lishe+butter+maziwa, ukiwa na unga wa mahindi tu na chumvi tayari mtoto anaacha kulia njaa.

Mi huwa nawapikia chakula kabisa kama wali, viazi, ndizi, ugali na mboga kama nnazokula mie (samaki, nyama, za majani n.k). Wa kwanza nilimsagia sana mchanganyiko wa chakula ila last born kala bila kusagiwa, sema tu mwanzo nilikuwa navifanya vilaini. Alafu ilikuwa rahisi maana last-born alianza kula kwa kuonja tu kidogo kidogo maana bado alikuwa ananyonya muda wote mpaka alivyofikisha miezi 10 ndo akaanza kula kwa kushiba chakula.
 
Nadhani ni kama ulivyosema hapo juu, NI CHAKULA RAHISI kwa gharama na maandalizi pia. Ukiacha wale ambao hujitahidi na unga wa lishe+butter+maziwa, ukiwa na unga wa mahindi tu na chumvi tayari mtoto anaacha kulia njaa.

Mi huwa nawapikia chakula kabisa kama wali, viazi, ndizi, ugali na mboga kama nnazokula mie (samaki, nyama, za majani n.k). Wa kwanza nilimsagia sana mchanganyiko wa chakula ila last born kala bila kusagiwa, sema tu mwanzo nilikuwa navifanya vilaini. Alafu ilikuwa rahisi maana last-born alianza kula kwa kuonja tu kidogo kidogo maana bado alikuwa ananyonya muda wote mpaka alivyofikisha miezi 10 ndo akaanza kula kwa kushiba chakula.
Ooh kumbe hata asubuhi anaweza kuanza na msosi heavy mi huwa nadhani vema kuanza na vitu laini kama vile maziwa na yai, au supu au uji kumbe hata ndizi samaki anakula tu, ahsante kwa experience mupya
 
Back
Top Bottom