Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Haya haya,mtoto wangu hapendi kula wala kunywa uji ama maziwa,anakunywa juice tu na kunyonya.Nipeni mbinu.
Umri miezi saba
Mshana Jr
 
Habari waungwana. Hivi mnadeal vipi na mtoto ambae ana jeuri? Ni mtoto wa kiume miaka 4 ukimkataza kitu anakirudia tena huku anakutazama usoni like kuona reaction yako. Ukimtandika anaenda kufanya kitu kingine ambacho anajua pia huwa unamkataza kufanya na anafanya kwa vurugu kweli kweli, Mwanzoni mama yake alikuwa ni harsh yaani hadekezi mtoto lakini dogo akawa na jeuri, mama akajaribu kuwa mpole na kumwambia vitu kwa upole na kutomtandika sana hata akikosea bado dogo ndo kama alizidisha kuwa jeuri. Hivi sasa mama yake yuko harsh nae lakini mwendo ni uleule dogo hasikii.
Mnadeal vipi jamani na hii tabia?
 
Back
Top Bottom