Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kaka samsun...
Me nazikubali sana zile ambazo wanavaa MAPAZIA..!
Zile za wavaa suti na tai sizielewagi kabisa..!
Hapo zilizo nyingi ni za "mashambani" na hizo chache ni 50/50,yaani karibia nusu ya picha ni "mashambani" na nusu ya picha ni "mjini" Inaanza shambani inamalizia mjini.
 
Nimemaliza kuangalia tamthilia ya terms of endearment (conditions of love) ni tamthilia ya mwaka 2004 inayozungumzia migogoro na changamoto zinazotokezea ndani ya ndoa na pia matatizo yanayotokezea pindi mwanamke anapoamua kuishi kinyumba na mwanamme asiyemuaminifu bila ya kufunga ndoa na bila wazazi kutambua(huku kwetu Zenji tunaita kusomana tabia). Nimeiweka kwenye rekodi kuwa ni miongoni mwa tamthilia iliyonifanya nilie kama mtoto mdogo nilipokuwa naiangalia.

Kang Han Geol ni mzee aliyekuwa na watoto wa tatu wa kike,kang geunpah,kang eunpah na kang jin pah.Kang geun pah ndie mtoto wa kwanza kuzaliwa aliolewa na mwanamme ambae alikuwa ni wakili Jin jung han,mwanzoni mwa maisha yao waliishi kwa raha na upendo wa hali ya juu na walibahatika kupata mtoto wa kiume walimwita jina la sukbin,ila baadae maisha yao ya ndoa yalibadilika baada ya jin jung han kuwa na michepuko na mfanyakazi mwenziwe jambo hilo lilimuumiza sana kang geun pah mpaka siku moja akamfumania mumewe akiwa na mchepuko wake hotelini ila kwa ujasiri akaamua kuvumilia bila ya kuiambia familia yake wakati huo mume wake alikuwa hajamalizia kujenga nyumba yao kwa hivyo walikuwa wakiishi apartment ya mzee kang han geol, geun pah aliamini mume wake anaweza kurudisha upendo wake wa zamani kwake yeye na familia yake kwa ujumla ila hali ilizidi kuwa mbaya na kufika mahali mume wake alikuwa anarudi usiku wa manane akiwa amelewa.mambo yalizidi kuwa mabaya ndani ya ndoa yao baada ya geun pah naye kushindwa kuvumilia vitendo vya mumewe na yeye kujikuta akiingia kwenye dimbwi la michepuko na kuwa na uhusiano wa karibuni na mwanamme mwengine hadi siku moja mume wake akamfumania na mwanamme balaa likaanzia hapo wakaamua kuachana ila mwishoni walirudiana na mapenzi yao yakaimarika tena.

Kang eun pah ndie alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa ambaye naye maisha yake ya kimapenzi yalikuwa mabaya,ni mwanamke aliyependana sana na yun taek na wote walisoma pamoja na walikuwa na ndoto ya kuwa walimu ila mahusiano yao hawakuweza kuzaa matunda kwani eun pah alijikuta akiwa na mahusiano na mwanamme ambaye aliitwa jung san ki aliishi nae miaka miwili pasina kufunga nae ndoa na hakuwa mwanamme muwajibikaji jambo lililomfanya kang eun pah kujituma yeye zaidi.baada ya kusomana tabia kwa muda mrefu eun pah alipata ujauzito jambo lililosababisha familia yake kuchukizwa na mwishoni familia ikataka jung san ki amuoe eun pah ili wafiche aibu ya binti wao kuzaa nje ya ndoa lakini siku ya ndoa jamaa aliingia mitini (alikimbia kwenye sherehe ya harusi) baadae eun pah alilazimishwa na familia atoe ile mimba yake kwa sababu mtoto angelikosa matunzo ya baba.

Maisha yaliendelea hadi siku moja eun pah akakutana na mwanamme mwengine ambaye alikuwa ni jang soo ambaye mwanzo alikuwa marekani kwa masomo alikuwa anatokea kwenye familia ya kitajiri,jang soo alivutiwa mno na eun pah ila mwanzo eun pah hakumpenda jang soo ila kadri maisha yalivyosogea mapenzi yao yalikuwa ya furaha na amani ila kikwazo ikawa ni wazee wa jangsoo hawakuvutiwa na eun pah kwa kuwa ni masikini na pia alikuwa ameajiriwa kwenye kitengo cha kulelea watoto kinachomilikiwa na mama yake jang soo ila jang soo alikataa maamuzi ya mama yake na kuamua kutangaza ndoa,kosa kubwa alilofanya eun pah ni kutokumueleza ukweli jang soo kuhusu maisha yake ya zamani kwani maisha yalikuja kuwa mabaya kwake baada ya jang soo kujuwa maisha ya zamani ya mke wake ambaye ni eun pah na kupelekea mgogoro wa ndoa kumkumba eun pah na familia yake. Jang soo alikuwa ni mwanamme aliyeonyesha mapenzi ya dhati kwake na hata kufikia kumsamehe mke wake kwa kushindwa kumwambia ukweli ila tatizo likawa kwa familia ya jangsoo wao hawakutaka kumwona eun pah akiwa na mtoto wao.

Pia nimevutiwa na original sound track (ost) zilizotumika ni nzuri sana.

Cast member

Chae siraa (geum pah)
View attachment 407936

Han ga in (eun pah)
View attachment 407937

Ji sung (yun taek)
View attachment 407939

Lee jung won (jung han)
View attachment 407940

Han jin hee (geum pah and eun pah father)
images

Song il kook (jang soo) ameanza kuonekana kwenye episode ya 25
images

Lee bo hae (jin duk)
View attachment 407943

Nimeshuhudia love chemistry nyingi sana ambazo zimenivutia ila baada ya kuangalia drama hii nimevutiwa sana na love chemistry ya

Song il kook na han ga in

Ji sung na han ga in

hii ndio tamthilia iliyoanza kumpa umaarufu song il kook na alishinda tunzo ya best couples pamoja na han ga in baadae song il kook akapewa ofa ya kucheza tamthilia ya emperor of the sea na kwa mara ya kwanza akachaguliwa kucheza kama muigizaji mkuu kwenye tamthilia ya jumong

hiyo series action zipo au ni love story tu?????????
 
Zipo nyingi sana hujaziona.
Iljimae.
East of Eden.
The return of iljimae.
Shine or go crazy.
Swallow of the sun.
Triangle.
Giant.
Road no 1.
Real Monster.
Healer.
Mr black.
Sasa Iljimae na The return of Iljimae tena?
 
Best asante kwa kushare na sisi, kwa maelezo tu uliyoyatoa machozi yamenilengalenga sasa nikiiangalia sijui itakuwaje! Nimeitamani sana kwa kweli nitaitafuta ASAP na hao cast members nawakubali saana tu hasa hasa Ji sung,Lee jung won,Song ii Kook, na huyu mzee Han jin hee. Ndio nimeanza scandal naona haijaniangusha ila bado sijakutana na OST ya maana.
 
Back
Top Bottom