Kwa wanaume, epuka aina hizi za wanawake

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Naanza kwa kusema apataye mke anapata kitu chema naye anajipatia kibali machoni pa bwana. Hii inamaanisha ukipata mke mwema hata sala zako kukubalika kirahisi sana. Haya yangu kupanda vyeo na kufanikiwa sio shida

Tazama bwana amefanya neno jipya, mwanamke atamlinda mme wake. Kumbe kupata mke ni sawa na kupata ulinzi kamili.

Heri walio wawili maana mmoja akianguka mwingine atamwinua mwenzake, kumbe kupata mke ni kupata uhakika wa msaada ukiwa na shida.
Lakini pia kuepuka mwanamke malaya na kamwe usiangukie kwenye shauri yake au njia yake

Sasa nirudi kwenye mada baada ya kuelezea faida za kupata mke kiunaga ubaga.
Kwa vijana kama mimi pamoja na maombi jua shetani yupo karibu na wewe wakati wote ili akutege uanguke.

Epuka aina hizi za wanawake. Huwa hawaleti nyumba bali makelele na fujo

1. Mwanamke anayeabudu elimu. Hawa mara nyingi huwa ni wasomi na wana maisha ya kati na ya juu. wengi huwa wanaona ndoa ni mume namba mbili na elimu ni mume namba moja. Huwa hawana utii kabisa na hata ukimsema kidogo atakimbilia basi kila mtu ashike yake. Huwa hawaishi kunyanyasa waume zao. Hata akiwa na hela itafanya mambo yake binafsi na mambo ya familia na watoto ni kipaumbele namba mbili. Ukimjua kabla hujao jipe muda zaidi ili umbadilishe kabla hujala kiapo kitakatifu

2. Mwanamke anayejifanya matawi ya juu. Hawa mara nyingi huwa ni washamba au wa mjini mjini tu. Mwanamke aliyetokea familia bora hajionyeshi kuwa yeye ni bora. Hujua utu na anachotafuta kwa mwanaume ni mapenzi ya dhati. Usidanganyike na gari,mikufu ya dhahabu na nguo,hivyo anaweza kuwa navyo kwa gharama ya mwili wake. Watoto waliolelewa kimaisha ya kati na juu hawana ushamba wa kujionyesha au kumtisha mwanaume. Mara nyingi atashuka kwenye level yako kama anakupenda.
3. Ogopa mwanamke anayekuomba pesa iwe kwa shida yake mwenyewe au kwa matatizo ya kifamilia. Kumbuka wewe huwezi kumaliza matatizo ya familia yao na pia ni makosa kumpa pesa wakati hujamuoa. Wapo wazazi wake wake wenye jukumu hilo. Pia kama anajishughulisha na shughuli halali hana haja ya kukuomba wewe hata kama ni kumuongezea mtaji. Kama ana lengo la kuishi na wewe asubiri muoaene ili mfanye pamoja. Wengi wanaoomba pesa ni wadada wa mjini tu. Mashamba yao ni wanaume na waume za watu. Angalia usiwe pando katika shamba lao
4. Muepuke huyu usiyejua familia yake na hata ndugu zake na hata msikitini au kanisani hamna. Umemkuta geto. Kama una lengo naye jitahidi kufahamu ndugu zake hata kwa siri. Lakini pia kama anafanya kazi basi jitahidi ujue hata ofisini kwake angalau tip ya mahusiano yake na wenzake ofisini. Epuka wale wa kuficha utambulisho wao. Mara nyingi huwa historia zao sio nzuri na pia hawajajisamehe na hawajaziacha. Kama ukikosea na umeamua kuliona Kama kosa huwezi kuishi kwa kuogopa kusema ukweli
5. Aliyelelewa na mzazi mmoja au bila wazazi kabisa. Huyu mpe jicho la pili na muone Kama anapenda kujifunza na kuingiza Mambo mapya. Waliolelewa na mzazi mmoja hasa wa kike huwa wanaubabe fulani na kuthamini mahusiano huwa Ni tabu Sana.

5. Muota ndoto wa mchana. Hawa pia huwa Wana mipango miiiingi na utakuta mala Yuko kwenye biashara la MLM, network marketing na mara huku kila kipya kikija anayaka awemo. Lakini uliza faida ataishia kusema napata pesa nyingi lakini maisha na kipato tofauti. Day dreamers wa kuogopwa pia. Hawa ndio wale unaoa alafu unashangaa kachukua mkopo kwa kuweka colleteral ya nyumba bila wewe kujua huko mtaani. Sahihi kufoji rahisi Sana. Kama unamuona hivi ebu mfundishe na mpe muda wa kubadilika.
6. Habari zake toka asubuhi Hadi jioni Ni Mambo ya utajiri na biashara na mipango miiiingi. Huyu Kama ndio mnaanza mahusiano maana yake Ni kwamba anataka kuthibitisha kitu. ukweli wake ni kitu ambacho kihalisia Hana. Mafanikio sio mipango tu Bali na utekelezaji. Matapeli huwa Ni wazuri Sana kuongea ila huangukia pua kwenye kutenda. Maisha Ni zaidi ya mipango na Mali na ndoa Ni maisha halisi
7. Pia muepuke mpokeaji na sio mtoaji au mwanamke bahari. Wapo watu wao Ni wachoyo Kama bahari.mito midogo yote wananyonya ielekee kwao na hawashibi. Waogope Sana watu bahari. Hata uwape vipi hawashibi maana wao ndio pekee wenye haki ya kupokea sio kutoa. Na hata ujitolee vipi kuwafurahishi furaha yao huishi njaa onapoaza kiwauma. Wengi wamejaa mjini hapa. Usiwekeze kwa kwa hao watu. Kama una mtu ili akupe lazima ulipe tofauti na anauejiuza Ni Nini?
8. Mwanamke mkoloni. Yaani Hawa huwa rigid Sana. Huwa wanakuwa na tabia Kama za kiume. Huyuni mbishi, sio mnyenyekevu na mara nyingine Ni mbabe.
Ni vigumu Sana kundi kujifunza vitu vipya. Hawa hujifunza kwa kukosea na kuteseka na makosa yao. Tena Hawa huwa Ni Mrs right wakati wote. Huwa ndio wanaokuwa wanaelezea mapungufu ya mwenzake kwa watu na rafiki.
Standard ya biblia kwa mke Ni obedience na submission kwa mume wake.

Asanteni kwa leo
 
Naanza kwa kusema aoataye mke anapata kitu chema naye anajipatia kibali machoni pa bwana. Hii inamaanisha ukipata mke mwema hata sara zako kukubalika kirahisi sana. Haya kupanda vyeo na kufanikiwa sio shida

Jokate anaingia kwenye namba ngapi hapo?
 
Hizo sifa zote hata sisi wanaume tunazo.

Hakuna binadamu aliyemkamilifu.

Oa kutokana na viwango vyako.
 
Umejitahidi kuwachambua vizuri sana. Nadhani kwa wanaotaka kuoa huu uwe kama muongozo ingawa najua ni vigumu mwanamke kuwa mkamilifu. Mkamilifu ni Mungu tu
 
Mwanamme atakaefatisha huu uzi indeed atapotea. Doesn't make sense at all.

1. So mwanamke asiwe msomi?:confused:

2. Asiwe matawi hata kama kazaliwa kuzuri na haiwezi kufichika??

3. Asiombe hela? What nonsense is this?

4. Ukishawajua familia yake na ofisini then what?

5. Here we go again, watoto wa single parents watengwe.

No point reading till the end.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom