Kwa wanaotaka mkopo wa kusoma chuo tuuuu!!! - je hii ni dawa?

salosalo

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
596
278
jaman katika pitapita yangu ya hapa na pale nimekutana na kitu ambacho ama kwa hakika ni msaada mkubwa kwa tatizo la mikopo ya kusomea elimu ya juu hapa nchini. Kinacho niuma zaidi ni kwamba hii taasisi inaonyesha ilianzishwa siku nyingi sana ila watu wengi hawaijui na hivyo kushindwa kunufaika nayo ama sivyo mimi ndo nimechelewa kuijua.Ni hii NGO iitwayo "HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF)". hawa ni watu wanotoa mikopo kwa wanafunzi wa chuo na wengineo kwa mujibu wa maelezo yao.

Unaweza kufuatilia hapa Home
HLSSF ni NGO ambayo ilisajiriwa tarehe 30/10/2008 chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.Ilipata usajiri namba 00NGO/00002621.

SWALI: Je, HLSSF inatoa huduma gani kwa ujumla?

JIBU: HLSSF inatoa huduma zifuatazo kwa kifupi;


  1. Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo.
  2. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili.
  3. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao.
  4. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kisomi zaidi.Hii itafanikiwa kwa kuanzishwa kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo mbalimbali nchini ambapo wanafunzi wanachama wa HLSSF watakutanishwa pamoja na kuweza kuandaa michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa mitaji na HLSSF ili kikundi husika cha wanafunzi waweze kuanzisha na kuendesha rasmi biashara yao.
  5. Kufanya utafiti juu ya matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya elimu nchini;pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera husika.
  6. Kuendesha workshops,events na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na uboreshaji wa mitaji,risk management,changamoto za soko huria n.k
  7. Kutoa ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya kusoma pamoja na kozi muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.
  8. Kutoa msaada wa kufanya maombi ya vyuo kwa njia ya mtandao(TCU ONLINE APPLICATIONS) pamoja na kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).

SWALI: Ada za uanachama ziko vipi? Je, zinalipwa mara ngapi?

JIBU: Ada za uanachama ni kama ifuatavyo:

  1. Ada ya uanachama wa mwanafunzi wa sekondari na mwanafunzi wa chuo ni Tsh.10,000.
  2. Ada ya uanachama wa mzazi/mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi ni Tsh.50,000.
  3. Ada ya uanachama wa taasisi isiyo ya serikali,kampuni au chuo kikuu ni Tsh.100,000.

ADA hizi zinalipwa mara moja tu;pale ambapo mwanachama anajiunga na HLSSF.



Maswali yangu:
  • Je hii NGO ni ya kweli na je kuna yeyote aliyepata kunufaika nayo kwa mkopo wa kusoma?
  • Vip wanataka vigezo gani ili wapate kukusaidia mkopo( nahisi kuna vigezo hawajaweka wazi)?

Tafadhali nisidieni michango yenu kabla sijaliwa ka elfu kumi kangu maana wanahitaji ili ku-register
 
Wanaojua watufahamishe, watu tukapate elimu za juu.

Kweli kabisa mkuu, mimi baada ya kupata hii habari sikutaka kuingia kichwa kichwa maana siku hizi ujasiliamali umekua sana TZ. watu hawachelewi kukuliza.

Wadau leteni mawazo pls
 
Je, kama mtu alikuwa anapata mkopo toka Heslb anaweza akaomba huko HLSSF na akapata?, maana mimi bodi wanazingua kutoa mkopo kwa mwaka huu wa masomo.
 
Ahahahahah! Hawa hlssf ni full usanii. Hao waliotajwa kufaulu kupata mkopo mpaka leo mkopo haujaingia na ni full mizinguo.
 
Ahahahahah! Hawa hlssf ni full usanii. Hao waliotajwa kufaulu kupata mkopo mpaka leo mkopo haujaingia na ni full mizinguo.

kuna mtu namfahamu yuko udom,aliniambia kuwa aliwapigia kujua ni lini watatoa mikopo wakamwambia asiwasumbue na kwamba aache kiherehere cha kuwafuatilia.
 
Hii ni bongo na kila mtu anakula kwa kutumia akili yake hasa ukishakuwa karibu na kile chama cha majambazi wa mchana kweupee!!?
 
matapeli wa kutupwa.......wamefanikiwa kutengeneza pesa nyingi mno kutokana na pesa zetu za forms.......search humu ndani kuna threas imeandikwa kuweni makini na HLSSF
 
Du! kweli serikali yetu imelala, hata haya ya namna hii wanashindwa kuyaona. Niliwahi kuambiwa serikali kaina macho sasa nimeamini.
 
Sasa naomba kufahamu kama hizo shughuli zingine walizodai wanaziendesha mavyuoni zinafanyika kweli? na kama zinafanyika tafadhali taja chuo kilichonufaika au kutembelewa na hawa jamaa
 
Jamani,msije mkaingia mkenge,hawa jamaa sio wa kuwaamini,ni matapeli tu.
 
Back
Top Bottom