Nina rafiki yangu mmoja ambaye anaishi wilaya ya kinondoni (eneo na mtaa sitataja kwani ni kisa cha kweli) yeye na mke wake walikuwa wamejaliwa kupata mtoto mmoja. Rafiki yangu huyo siku moja usiku wa manane alishtushwa na makelele yaliyokuwa yanatoka kwenye chumba chao kingine ambacho pia hukitumia kama jiko. Baada ya kushtuka usingizini na kuwasha taa hakumuona mke wake bali mtoto akiwa peke yake kwani chumba wanacholala ameniambia kina vitanda viwili hivyo mtoto na mama yake hulala pamoja, kutokana na kelele zilizokuwa zimepamba moto, alikuwa na uhakika kuwa mke wake itakuwa ametoka kwenda kuhushudia tukio hilo. Hakuamini macho yake baada ya kukuta mke wake amefumaniwa akiwa na mume wa mpangaji mwenzake, mke wake alikuwa na khanga moja tu na vitu Fulani vyeupe vikiwa vinachuruzika miguuni.
Kilichoelezwa pale ni kuwa kijana huyo aliyefumaniwa na mke wa rafiki yangu alitiliwa mashaka na mke wake baada ya kujifanya amekwenda msalani bila kusikika akifungua mlango wa nje, hivyo baada ya kufuatilia alisikia mguno kutoka chumba cha jikoni ambapo baada ya kuingia alimkuta mumewe akiivunja amri ya sita na mke wa rafiki yangu. Baada ya rafiki yangu huyo kushudia kilichotokea hatua alizochukuwa ni kurudi chumbani na kuanza kumbembeleza mtoto ambaye alikuwa analia, baada ya muda mke wake alirudi chumbani naye akapanda kitandani na kwa maelezo ya rafiki yangu huyo hakumsemesha kitu mapaka asubuhi alipomuaga mkewe kuwa anakwenda kazini.
Rafiki yangu aliporudi kutoka kazini alikuta mkewe huyo ameacha ujumbe kuwa amehamia magomeni kwani hawezi kuishi tena pale, katika kuhama huko alikuwa ameacha visturi viwili pamoja na kitanda kimoja na vyombo vichache. Kwa kifupi ni kuwa rafiki yangu huyo hakumfuatilia na huo ndiyo ulikuwa mwisho wao. Kwa yule mpangaji aliyefumaniwa yeye na mkewe walizozana vikali na mkewe aliamua kuondoka na kumuacha naye muwewe.
Kijana yule aliyemfanyia kitu mbaya mke wa rafiki yangu karibu miezi miwili alikuwa akikwepa kukutana na yule rafiki yangu kwani awali walikuwa ni watu wanaoheshimiana sana. Hatua alizochukua rafiki yangu siku moja ya jumapili ni kumuita yule mpangaji na kumwambia kuwa haina haja ya kujificha kwani lililotokea limetokea hivyo waandelee kuishi kwa amani hii inamaanisha kuwa alimsamehe kwa aina hiyo.
Je umejifunza chochote juu ya kisa hiki?