Kwa waliopanga Uswazi fumanizi hili linaweza kukufundisha kitu!!

na vitu Fulani vyeupe vikiwa vinachuruzika miguuni.
nanukuu hiyo red,vitu vyeupe,ina maana mama alikuwa analiwa pekupeku,bandugu bapenzi,tutasalimika kweli? hata kama kuna babu kwa mtindo huu................

Huduma hizi za fasta mkuu ni sawa na watu waendao msibani hawabebi vyandarua!!!!!
 
Bora hiyo kuliko kuvunja nyombo vya kila mtu!!!Hata mimi ningeondoka kimya kimya!!

Ya nini malumbano bwana!
lakini mimi najiuliza hivi kuna binadam wana akili timam kweli? yaani wewe unajiamini vipi kumhama mwenza wako kwenye shuka na kwenda jikoni au uwani kusulubiana na njemba nyengine?
 
Hata akiwa nayoa tayari ameshaonyesha busara zake kwa kutogombania kuku asiyetaka kukaa kwake....kama kuku ndiye aliyeenda kwa jirani kwanini yeye agombane na jirani????v
jamaa anatufundisha sisi tulio owa tuwe na subira kama ukiamua kutoa hukum utajuta. Tuwe maamuzi ya busara kwa faida ya wote.
 
Huduma hizi za fasta mkuu ni sawa na watu waendao msibani hawabebi vyandarua!!!!!

Kwa huyo mke kaondoka na mtoto.....
Kuna ule wimbo wa J. Zuma na wenzake....Umshini Wam
 
Sad stor. Nahisi ingekuwa mim nisingeweza vumilia kama jamaa. Ila ndo ivo ya nin malumbano...
 
lakini mimi najiuliza hivi kuna binadam wana akili timam kweli? yaani wewe unajiamini vipi kumhama mwenza wako kwenye shuka na kwenda jikoni au uwani kusulubiana na njemba nyengine?
Huo unaitwa ufisadi wa kibazazi!
 
uswahilini kuna mambo ya ajabu sana. huwezi amini kipindi hicho miaka ya 2000 nilipanga Magomeni mapipa pale, kuna jamaa mmoja yeye ni bonge la mtu, kamke kake ni kadogo kama karanga...kuna rafiki yangu alikuwa anamvizia anapoenda kuoga, mwenye mume akiwa ndani anasubiri mkewe akaoge (kwasababu hawaogi wote), mke mzuri ajabu, sura nzuriiii, ni mchaga wa machame mweupe huwezi amini...lakini akifika bafuni anashika ndoo...yaani anainama kama vile unafua nguo kwenye ndoo ya lita kumi alafu jamaa anapiga ya chapchap kwa nyume kama chuma mboga fulani hivi...na bwanake yuko ndani hajui...

majuzi nimekutana na yule mama, anasali kanisa la ufufuo na uzima ameshaathirika na Bwanake amekonda kwisha mbaya...mwanamke kamletea na ngoma....uswahilini kuna mambo ya ajabu ajabu...

mtu akiamua kukusaliti ni tab kumzuia ila atalipizwa hapa hapa dunia
 
mkuu rudi tu, ila hiki ni kisa cha kweli. huyu jamaa niliyemuelezea hapa ana visa vya mapenzi ambavyo ni watu wachache wanaweza kuhimili. mpaka sasa namshangaa sana.

Mkuu hiki kisa kinafaa kutengenezea hela subiri nianze kuandika script ya kuuza bongo...
 
Mkuu hiki kisa kinafaa kutengenezea hela subiri nianze kuandika script ya kuuza bongo...
mkuu anavisa vingi vinavyohusu mapenzi ambavyo nikiviweka humu hakuna atakayeamini. Ingekuwa ni mchezo wa kuigiza nafikiri angepata tuzo.
 
Huyo kaka mwenye mke ana busara sana!!!

walikuwa wameshachokana hao. mama analala na mtoto. mama anamwacha baba amelala anaenda kwenye mambo zake. baba anafumania hakuna reaction. mama anaondoka , baba hana habari nae. angekuwa na busara angemsamehe waendelee na maisha.
 
mi najiuliza kwa nini wanawake?
manake katika mkasa huu utaona mwanamke aliyefumaniwa
kahama chumba kamuachia mumewe na upande wa pili
unakuta mwanamke aliyefumania nae kama chumba kamuachia
mumewe!
au ndio masuala ya mfumo dume?
 
Nina rafiki yangu mmoja ambaye anaishi wilaya ya kinondoni (eneo na mtaa sitataja kwani ni kisa cha kweli) yeye na mke wake walikuwa wamejaliwa kupata mtoto mmoja. Rafiki yangu huyo siku moja usiku wa manane alishtushwa na makelele yaliyokuwa yanatoka kwenye chumba chao kingine ambacho pia hukitumia kama jiko. Baada ya kushtuka usingizini na kuwasha taa hakumuona mke wake bali mtoto akiwa peke yake kwani chumba wanacholala ameniambia kina vitanda viwili hivyo mtoto na mama yake hulala pamoja, kutokana na kelele zilizokuwa zimepamba moto, alikuwa na uhakika kuwa mke wake itakuwa ametoka kwenda kuhushudia tukio hilo. Hakuamini macho yake baada ya kukuta mke wake amefumaniwa akiwa na mume wa mpangaji mwenzake, mke wake alikuwa na khanga moja tu na vitu Fulani vyeupe vikiwa vinachuruzika miguuni.

Kilichoelezwa pale ni kuwa kijana huyo aliyefumaniwa na mke wa rafiki yangu alitiliwa mashaka na mke wake baada ya kujifanya amekwenda msalani bila kusikika akifungua mlango wa nje, hivyo baada ya kufuatilia alisikia mguno kutoka chumba cha jikoni ambapo baada ya kuingia alimkuta mumewe akiivunja amri ya sita na mke wa rafiki yangu. Baada ya rafiki yangu huyo kushudia kilichotokea hatua alizochukuwa ni kurudi chumbani na kuanza kumbembeleza mtoto ambaye alikuwa analia, baada ya muda mke wake alirudi chumbani naye akapanda kitandani na kwa maelezo ya rafiki yangu huyo hakumsemesha kitu mapaka asubuhi alipomuaga mkewe kuwa anakwenda kazini.

Rafiki yangu aliporudi kutoka kazini alikuta mkewe huyo ameacha ujumbe kuwa amehamia magomeni kwani hawezi kuishi tena pale, katika kuhama huko alikuwa ameacha visturi viwili pamoja na kitanda kimoja na vyombo vichache. Kwa kifupi ni kuwa rafiki yangu huyo hakumfuatilia na huo ndiyo ulikuwa mwisho wao. Kwa yule mpangaji aliyefumaniwa yeye na mkewe walizozana vikali na mkewe aliamua kuondoka na kumuacha naye muwewe.

Kijana yule aliyemfanyia kitu mbaya mke wa rafiki yangu karibu miezi miwili alikuwa akikwepa kukutana na yule rafiki yangu kwani awali walikuwa ni watu wanaoheshimiana sana. Hatua alizochukua rafiki yangu siku moja ya jumapili ni kumuita yule mpangaji na kumwambia kuwa haina haja ya kujificha kwani lililotokea limetokea hivyo waandelee kuishi kwa amani hii inamaanisha kuwa alimsamehe kwa aina hiyo.

Je umejifunza chochote juu ya kisa hiki?

Kwa huyo rafiki yako ashukuru Mungu kwani mke amekimbia tu,kuna klisa kilitokea sehemu fulani mkoani Shinyanga ila sitaitaja,mke alifumaniwa kisha jamaa(mume) akamchukua kwa upole akarudi naye nyumbani mke akajua zangu zimeisha lakini jamaa akamuambia wakaoge na wakaoga pamoja na bwana wala hakumgusa,ilipofika saa ya kulala wakalaa ila mume hakuulizia tendo na mwanamke akawa na woga akijua nikimsemesha mume wangu labda nitampandisha hasira.Zikapita wiki mbili bila tendo lakini mengine yote yalikuwa kama kawaida.Siku moja wakati jamaa amerudi kazini jioni hakumuona mkewe kama ilivyokuwa kawaida akaingia chumbani na kumkuta mkewe ameshakunywa sumu na kumuachia ujumbe kuwa hawezi kuishi kwa aibu kiasi kile na wala hawezi kushitaki kunyimwa unyumba na mumewe kwani yeye ndiye alikuwa mkosefu.Basi jamaa alilia sana kwenye msiba na alikuwa akisema kuwa zilibaki siku mbili tu ifike siku ya wapendanao na alikuwa amemuandalia surprise mke wake ili waanzishe upya penzi lao lililokuwa limeingiliwa.
 
Nilishawahi kusimuliwa mkasa kama huu nikiwa na miaka 14.
 
nimecheka sina mbavu,tripoli kwa gadafi,si mchezo.
jamaa ana moyo wa kiume wa ustahimilivu
kuna binadamu aina flani hasira zao zinapanda gradually kwa kufikiria mambo for a period of time na nazani na huyu ni mmoja wapo, na mara nyingi hawa wakifika break even point basi balaa lao bora ukaishi tripoli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom