"Kwa wale waliokosa mkopo tu"

Daud omar

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
2,458
977
Habari zenu wandugu

--Husika na kichwa cha habari hapo juu, kama tulivyoazimia kesho kwenda kudai haki zetu za msingi, Yafuatayo tunapaswa kuizingatia na kukubaliana ili kuweza kufanyikisha:-
1.Hapana kutumia fujo na vurugu kwani haya ni maandamano ya wasomi, kwahiyo amani inapaswa kuwa mbele
2.Epusha sana kutumia maneno ya kashfa, kwa mtu yoyote yule au kiongozi yoyote wa kitaifa, kwani kuna vitu vizuri wanatufanyia na tunapaswa kuwashukuru
3.Tunatakiwa kujua maandamano yanaanzia wapi na kuishia wapi, na hili ni jambo la msingi, kwani kuna wengine wanasema tunaazia Bodi ya mikopo mpaka wizarani na wengine wanasema tunaenda moja kwa moja mpaka wizarani,
Hapa tukubaliane tu.
4.Taarifa hii inakuhusu hata wewe pia uliyepata mkopo, kwani waliokosa walikuwa wanasifa na vigezo vya kupata mkopo kama wewe
5.Kwa mliopo Dar es salaam na mikoa ya jirani kufika kwako ni muhimu, kwa walio mbali tupo pamoja tutwajulisha kinachoendelea
6.Ukipata taarifa mjulishe na mwenzio
7.Nakaribisha mchango na mawazo yako..
 
nimesikia hakuna get litakalofunguliwa pia FFU wameaza mazoezi . Tujipange wandugu kutetea haki zetu kwa utulivu zaid. Hata tukiandamana yawe maandamano ya amani. Mana watu wakifika pale hua na mukari sana nimeyashuhudia hayo kwani tangu j3 nilikua hapo bodi. Haki ya mtu haizurumiwi bali uchelewa
 
FFU hilo ni jukumu lao, na sisi jukumu letu ni kuhakikish hatuvunji sheria, chonde chonde jamani, hiyo ni serikali na tunapaswa kuiheshimu
 
Back
Top Bottom