Kwa nini wanawake mko hivi?

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Ishu ni zilezile kila siku ila zinakuwa na staili tofauti. Hebu tusome kisa hiki halafu tuendelee kujadili mada,

;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;​
Kuna kaka mmoja ameoa na ana mke na mtoto wa mwaka mmoja na nusu hivi. Kaka huyo amebahatika kupata kazi nzuri na ana kipato kikubwa tu kinachoweza kukidhi mahitaji ya familia hiyo.

Sasa siku moja kulitokea matatizo fulani kazini kwa kaka huyo na ikabidi apewe barua ya kusimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea huko kazini. Kwa kipindi hicho cha kusimamishwa kazi kama unavyojua mwanaume lazima uhangaike. Katika kuhangaika kaka huyo akabahatika kupata sehemu ya kujishikiza kwa muda wakati suala lake likiendelea kushughulikiwa. Kwa bahati nzuri au mbaya kazi aliyopata kwa muda inafanyika hadi usiku.

Siku moja akiwa kazini masaa ya usiku kulikuwa hakuna kazi na wafanyakazi wakaambiwa watafute usafiri warudi nyumbani. Baadaye akatafuta usafiri anaoujua yeye na akafanikiwa kufika nyumbani.

Sasa ishu yenyewe inaanzia hapa.

Huyo kaka akafika hapo nyumbani alipopanga na akaanza kumgongea mke wake mlango ili amfungulie. Mke akawa hafungui mlango, mara baadaye wakaanza kujibizana kwa muda mrefu na mke wake. Baadaye akaja mpangaji mwenzake kumsaidia huyo kaka. Hatimaye akafungua mlango. Alipofungua tu mlango kumbe kulikuwa na lijamaa linajiexpress na mke humo ndani, halafu lijamaa likaamua kuondoka.

Baada ya hapo huyo kaka akaamua kumuacha mke wake hapo hapo na kwenda kulala nje ya nyumba. Sijui alilala gesti. Akamwambia mke wake utabaki na huyo huyo (lijamaa). Huyo kaka hakurudi tena hapo nyumbani. Bila shaka alibaki kazini maana kazi yenyewe ni ya mchana na usiku.

Lakini baada ya takribani wiki moja hivi baada ya tukio. Huyo kaka aliyesimamishwa kazi akarudishwa kazini. Mke naye aliposikia kuwa mme wake aliyekuwa amesimamishwa kazi amerudishwa kazini, eti akaenda kwa mume wake kumwomba msamaha kwa yaliyotokea nyumbani.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::​
Sasa kilichoendelea hapo mimi sijui. Hebu sisi tuendelee kujadili hii mada. Kwanini wewe mwanamke unamthamini mmeo wakati ana kazi au kipato kizuri, halafu ikitokea bahati mbaya kama hiyo unaona mmeo hana thamani. Ina maana upendo wako uko kwenye pesa tu????????????????
Kwa nini wanawake mko hivi?????????????

Tuendelee kuchangia mada
 
Matatizo yote haya yanatokana na kuoa.

mwanamke yoyote hajakamilika kabisa hajui kuna kupanda na kushuka.

wengi wako hivyo ila mwisho wa yote inakuwa aibu kwao na kwa jamii.

kuoa kaka kunahitaji moyo ......KUISHI NA MWANAMKE NI SOOO,YANI akili zao wanazijua wenyewe.
 
siyo wanawake wote wako after money...ila ndiyo hivyo samaki mmoja akiodha wote wameodha.....ila tahadhari tuu wakaka msije mkakata tamaa ya kuoa thinking kila mwanamke ni golddigger or so...if that the case nendeni makasani au book store/Library.....huko mtapata wanawake wa maana......full top
 
siyo wanawake wote wako after money...ila ndiyo hivyo samaki mmoja akiodha wote wameodha.....ila tahadhari tuu wakaka msije mkakata tamaa ya kuoa thinking kila mwanamke ni golddigger or so...if that the case nendeni makasani au book store/library.....huko mtapata wanawake wa maana......full top

siku hizi mashangingi ya mjini siku hizi nayo yanakimbilia makanisani kujifanya yameokoka ,,,,,so sio solution,usanii mtupu.
 
siku hizi mashangingi ya mjini siku hizi nayo yanakimbilia makanisani kujifanya yameokoka ,,,,,so sio solution,usanii mtupu.

Dont judge the book by its cover....hata kuna wanaume wale mafisi pia wanakwenda kanisani kutafuta wanawake......wameshaharibu watoto wa watu sasa madai yao wanataka kutuliya.....mtoto wa kanisa utamjua tuu anavaa skkirt hadi chini kama za kijewish....hutamkuta anavaa ki-top kuonysha tumbo lake na lazima aambatanishe na lhanga kwa juu....
 
dont judge the book by its cover....hata kuna wanaume wale mafisi pia wanakwenda kanisani kutafuta wanawake......wameshaharibu watoto wa watu sasa madai yao wanataka kutuliya.....mtoto wa kanisa utamjua tuu anavaa skkirt hadi chini kama za kijewish....hutamkuta anavaa ki-top kuonysha tumbo lake na lazima aambatanishe na lhanga kwa juu....

for me i will prefer the genuine and open types,like the buddest........ha ha ha,,,
 
kuoa kaka kunahitaji moyo ......KUISHI NA MWANAMKE NI SOOO,YANI akili zao wanazijua wenyewe.

I sense bitterness and heartbreak in your words...Am I way off? Right on the money? Or somewhere in between?
 
mwanamke yoyote hajakamilika kabisa hajui kuna kupanda na kushuka.

wengi wako hivyo ila mwisho wa yote inakuwa aibu kwao na kwa jamii.

kuoa kaka kunahitaji moyo ......KUISHI NA MWANAMKE NI SOOO,YANI akili zao wanazijua wenyewe.

1.Kuoa/kuolewa ni hiari.Hakuna aliyewekewa kisu shingoni aingie humo.
2. Kipato cha mwanaume kina nafasi na maana yake lakini siyo kila mwanamke anapapatika sana na kazi ya mume.Wapo wengi wenye kazi zao na vipato vyao tena vya kutosha.
3.Kila mwanamke ni individual huwezi kuwajumlisha wote na kuwawekea tabia moja.Kadhalia wanaume nao ni tofauti , siyo lazima tabia za wanaume wachache zichukulike kuwa ndi tabia za wanaume.
4 Ukimpata mwenza mzuri awe mwanamme au mwanamke shukuru Mungu.
 
sawa sawa kabisa apo Vera
 
Back
Top Bottom