Kwa nini wanaume wanachakachua sana ndoa?

royna

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
479
335
Jamani kwa nia njema tu, niko nafanya kama kautafiti kujua kwa nini wanaume wanapenda kutoka nje ya ndoa!Na je mtazamo wa jamii kama mume na mke wakitoka nje ya ndoa unafanana au ni tofauti? please colleagues naomba mchango wa mawazo yenu!
 
wewe umeoa kama bado usiulize hili swali kama tayari toka na wewe nje utapata jibu kwanini wanatoka nje ya ndoa..
 
Ni kama vile watalii, leo wako London kesho wako Washington kila mjii una raha zake :violin:
 
Jamani kwa nia njema tu, niko nafanya kama kautafiti kujua kwa nini wanaume wanapenda kutoka nje ya ndoa!Na je mtazamo wa jamii kama mume na mke wakitoka nje ya ndoa unafanana au ni tofauti? please colleagues naomba mchango wa mawazo yenu!

Ujinga, ushamba na uwezo mdogo wa kutawala tamaa zao! Wanavitii sana viungo vyao vya uzazi kwa maana nyingine wanaongozwa navyo!
 
Wakamatwe ugoni mwanaume na mwanamke, mwanamke ataambiwa malaya. mwanaume ataambiwa mkali. mfumo wa jamii unampendelea zaidi mwanaume. ipo haja ya jamii kuelimishwa kuwa, kosa halichagui jinsia. wanaume wanapaswa kukwepa vishawishi vinavyoweza kuwatumbukiza ktk dhambi ya uzinzi km ulevi, makundi potofu na zaidi wafanye mazoezi ya mwili ili mwili u relaxe na kupunguza kuwaka kwa tamaa za mwili.
 
Ni mwanaume tu ndo anatoka? hata wanawake kibao wanatoka nje. Hii imechangiwa na kuvunjika kwa maadili ktk jamii na kupungukiwa na khofu ya MUNGU.
 
mwono wangu ni kuwa mjadala unaohusu cheating humu jf huwa umejaa unafiki,hatuwi wakweli na kukiri kuwa there is a lot of cheating katika married couples na members wa jf are no angels!

Ni kweli Bishanga...halafu hao wanaume wanaocheat, wanacheat na nani? Si wanawake kama wanawake wengine?
 
Saa nyingine kazini kele, nikirudi nyumbani makelele yanaendelea, nikipata ninapothaminiwa najituliza bila ku feel guilty.
 
hii research yko utatulipa cc respondents au unataka kuhangaisha tu watu wazima
 
Back
Top Bottom