Elections 2010 kwa nini nafurahi kikwete kuanguka jukwaani?

Mkuu hakuna haja ya kusema video ipo au laa wewe nakuomba uyaandike hapa aliyosema Kinana kisha wanabodi watapima wenyewe..najua tu utasema waandishi wa KiTanzania ndio wenye makosa lakini hawezi kuwa Kinana.

Nilichosoma mimi kinasema hivi:-
Kinana alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wanachama, wapenzi na mashabiki wa CCM kwamba hali ya afya ya Kikwete ilikuwa njema na ataendelea na ziara yake ya kampeni leo hii mkoani Mwanza na kwingineko nchini.
Mbali ya hilo, Kinana alisema uamuzi wa Kikwete kufunga ulikuwa ni kinyume cha ushauri aliopewa na madaktari wake ambao walishauri asifunge.
Alisema tayari chama hicho na madaktari wake wameshachukua hatua zote za tahadhari ili kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa urais anaendelea na kampeni zake za urais pasipo kukwama.

Usiamini kila unachosoma,

Angalia dakika ya 1:39 mpaka 1:49

"Wanachama, wapenzi, washabiki, wakereketwa na wananchi kwa ujumla" Muandishi wa wapi asiye hata na tape recorder huyu ? Au anataka kutoa mambo yaliyo untruthfully partisan ?

 
Last edited by a moderator:
Wewe unafurahia mtu kuanguka kwa ugonjwa, mtu anakupinga unasema hiyo ni theory?

Wewe unataka aachie madaraka kwa sababu ya kuanguka? Asipoanguka tena ? Wewe una strategy gani zaidi ya kutegemea kudra za mtu kuanguka mwenyewe? Is this the best upinzani can do? Kusubiri mtu aanguke ? Unajuaje kama akianguka tena na tena ataachia wenye uwezo watawale? Akiwaachia wazembe wengine utasemaje? Utaombea nao waanguke ?

Huna uhakika kwamba atakayekuja ni mzuri lakini bado unaona ni one step ahead? Unajuaje kama si one step back ?

Hivi kama hupendi siasa za Kikwete huwezi kumpinga Kikwete kisiasa na kuonyesha udhaifu wa hoja zake bila kumtakia aanguke kimwili?

Hivi kumuangusha Kikwete kisiasa wapinzani hawana njia nyingine zaidi ya kuombea aanguke kimwili ?

Mimi nataka kuona upinzani unaokuja kwa fikra mpya, unaoleta matumaini, unaotupeleka kwenye uongozi unaojiheshimu na na wenye nidhamu kwa dhamana ya uongozi wa wananchi.

Nafurahi kuona viongozi wa upinzani wameweka ubinadamu mbele ya siasa. Alipoumia Slaa Kikwete alimtumia pole, Kikwete kaanguka Slaa amemtumia pole. Angalau kuna ubinadamu.

Hawa fanatics wanaokuja hapa kutaka kumla nyama binadamu mwenzao hawana support ya official positions za upinzani ninazozijua. There is a reasopn for this, the reason being these positions do not make sense humanely or even politically - they backfire terribly, Tanzanians do not like a ruthlessly inhumane politics-, ndiyo maana hata kama - I am not saying they actually do this, note hata kama- upinzani unataka kumuona Kikwete anaanguka na kufa jukwaani viongozi wao, kwa kujua responsibility ya ku project image ya ubinadamu, hawawezi kusema hivyo kamwe .

But I guess some people will never get that through their heads.
Kiranga;
Una-argue na mtu ambaye hamko kwenye uelewa unaoshahibiana, na ninadhani hata elimu yenu itakuwa tofauti sana, nadhani mithili ya mtoto wa darasa la pili na profesa wa chuo kikuu. Hii ndiyo tofauti yenu na dniyo maana hamuwezi kuelewana,... utapoteza mda wako!
 
Kiranga;
Una-argue na mtu ambaye hamko kwenye uelewa unaoshahibiana, na ninadhani hata elimu yenu itakuwa tofauti sana, nadhani mithili ya mtoto wa darasa la pili na profesa wa chuo kikuu. Hii ndiyo tofauti yenu na dniyo maana hamuwezi kuelewana,... utapoteza mda wako!
Kuna uwezekano mkubwa wewe ukawa ni Professor Juma Kapuya au yule ant Muddy almaaruf pale Kariakoo. Usiniulize ni kwanini!
 
ni kawaida binadamu kutofurahia maanguko au mateso ya mtu mwingine waziwazi. lakini kwa nini hili la kikwete nachelea kumsikitikia?

ninazo sababu zangu nyingi lakini baadhi tu ni hizi

1. kiwete ni msanii alitukuka, yeye na wasanii wenzake wameeendelea kuwasanii watanzania kwa muda wa miaka mitano, wakati wananchi wanakufa njaa, hawana matibabu yeye anatumbua mapesa na mali asili zanchi hii na wateule wachache. kwa kuwa kuna wananchi wanaoanguka kwa njaa, kwa nini nijali kuhusu msanii kama kikwete kuanguka jukwaani, tena wakati anawaghilibu wananchi kwa kuwasomee litania ndefu ya mafanikio anayoyajua yeye na msanii mwenzake rostam aziz?

2. bado ule wizi wa epa na kagoda unanisumbua akilini. wakati kikwete na wenzake walichota mabilioni wakahonga mpaka akawa rais, badala ya kuwakamamta wale walioiba wanajulikana waziwazi, rosta, lowasa, nimrod mkono, kingunge, yeye na vibaraka wenzake wakawasweka ndani wasiohusika kama wale wafanyakakzi wa BOT. sasa wananishi maisha ya dhiki hawana mbele wala nyuma. kwa nini sasa nisifurahi kidogo anguko lake ambalo ni adhabu toka kwa MUNGU?

3. jakaya kikwete anataka kujenga usulatni wa ajabu hapa nchini, sasa yeye na wanawe ndo waamuzi wakubwa kabisa katika maisha na mustakabali wa nchi yangu, kama alivyokuwa sadam na wanawe wawili ndivyo alivyo kikwete, mkewe, na wanawe , kwa nini nisifurahie anguko la mtu kama huyu?

4.JK, WATU WANAKUDANGANYA, UMEZUNGUKWA NA WEZI, MAFISADI, PALE JUKWAANI JANGWANI UNAPOANGUKA KILA WAKATI WA KAMPENI KUNA ZINDIKO KUBWA, SEPTEMBER 5TH, 1990, MTU WA HAKI, NA MTUMISHI WA MUNGU BABA MTAKATIFU YOHANE PAULO WA PILI, ALIHUTUBIA TAIFA, AKALIKABIDHI TAIFA HILI KWA MUNGU, ILI WAONGO, WAZANDIKI, WAHUNI, WASANII, WALA RUSHWA, WAFISADI, WAKARIBIAPO PALE WAPATE KUANGUKA!

UTAANGUKA DAIMA
Adui mwombee njaa atanyosha mikono hata kama alikuwa shujaa.
 
Anatakiwa aanguke uraisi, sipendi aanguke majukwaani. Mungu ampe afya njema...
 
umekosa utu; sababu zilizofanya aanguke siyo hizo 4 ulizoelezea, ni afya yake kama binadamu na hata mpinzani wake kisiasa WS amempa pole.
 
Mimi ni CCM , ingawa natofautiana na JK na CCM katika mambo kadhaa ya kimsingi lakini hili la kushangilia kuanguka Mkuu wa Nchi hadharani ni ukosefu wa ustaarabu.
Siasa si uadui, na sote ni watanzania na nafikiri ni ukosefu wa hekima kwa hali ya juu kushangilia ugonjwa wa mtu yeyote yule.
Waswahili walisema Mungu si Athumani, kile uchekeavyo kimpatapo yule uneyemfikiria adui yako , Mungu in all fairness anaweza kukupatia kama si wewe basi jamaa wa karibu sana na wewe.
Kwa hili nampa pole JK na Mola amrudishie afya yake.
 
Watu wengi na hasa viongozi wa CCM na serikali wanaliona tatizo la kuanguka kwa rais (Amiri Jeshi Mkuu) kama kitu cha kawaida tu. Mawazo yao yote yako kwenye kampeni ili waweze kuchuma pesa. Hii ni hatari kubwa kwa kiongozi wa nchi kuanguka mara kwa mara ninashauri uchunguzi wa afya yake ufanyike na kupata matibabu yanayostahili ili kumuweka katika hali nzuri ya afya yake na hali hii isitokee tena. Pia madaktari wake wawajibishwe kutokana na uzembe wa kutokuweza kutambua vizuri afya ya rais hadi anaanguka kwa mara nyingine tena!!!
 
Back
Top Bottom