Elections 2010 Kwa Mh Mengi na ITV (IPP MEDIA)

Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,555
9,330
Napenda kutoa shukrani zangu kwa Bw Mengi na timu nzima ya ITV, kwa kuweka historia ya mapambano/ demokrasia Tanzania kwa kuweza kutoa coverage ya 3hrs kwa CHAMA CHA UPINZANI, hata kama ni kulipia lakini kupata huo muda ni kama ndoto, lakini kwa hapo mwanzo ilikuwa ni vigumu, na kwa taarifa zisizo rasmi ilisemekana watu wa ITV walikataa kufanya Biashara na Chadema (niko tayari kurekebishwa)

Mengi wewe ni Mpiganaji wa kweli lakini bado sijajua kwa nini unakuwa Mguu ndani/nje na nachelea kusema haya yote yamefanyika ni kwa sababu ya ile njama ya mwanao iliyotaka kutokea pale JKN airport na ki ukweli hukupata support ya maana kutoka serikalini, na kwa kuanzia ulianza na Guardian na ile kashfa ya msg za kumchafua Dr Slaa

pamoja na hayo yote, mimi binafsi ninaona ni mipango ya Mungu tu, hata kama umelipwa kwa mdahalo wa leo lakini thamani ya hizo fedha haziwezi kabisa kulingana na idadi ya watu waliopokea huu ujumbe, nilikaa na kujiuliza hivi tangu siku ya mwanzo ungeamua kufanya hii kitu nadhani watanzania wote wangekuwa wako tayari kumkaribisha Mh Slaa Ikulu kwa ushindi wa kishindo na wala kampeni zisingekuwa ndefu, za gharama na za kuchosha,

ushauri wangu ni kuwa kwa hizo siku zilizobakia mnaweza kurudia huu mdahalo kwa hata siku mbili tu, say kesho Jpili na siku moja ya katikati ya wiki ili hata kwa wale waliokatiwa umeme na kwa wale ambao Mh Dr Slaa atashindwa kuwafikia basi nao wajue Slaa anataka kufanya MAbadiliko ya aina gani na kwa jinsi gani ataonyesha maisha bora kwa kila mTanzania kwa vitendo
 
Nimependa kila kitu ulichoandika na nakuunga mkono kwamba huo mdahalo urudiwe kila siku hadi October 30.
 
tusisahau kumpongeza kikwete pia kwa kuonyesha udhaifu mkubwa uliofanya hata wananchi kumchoka na kuangalia njia mbadala za kufika the promised land
 
Hata kama itabidi kulipia, mimi nashauri CHADEMA kama chama wajaribu kufuatilia gharama, nadhani wengi tutakuwa tayari hata kuchangia kutangazwa kwa marudio kwa kidogo tulichonacho, cha muhimu muda utangazwe ili watu wengi waweze kuangalia na tujulishwe tunachnagia vipi.
 
Nakubaliana nawe kabisa kuhusu suala la kurudia huu mdahalo ili ambao hawakuuona wapate nafasi.
 
Hata kama itabidi kulipia, mimi nashauri CHADEMA kama chama wajaribu kufuatilia gharama, nadhani wengi tutakuwa tayari hata kuchangia kutangazwa kwa marudio kwa kidogo tulichonacho, cha muhimu muda utangazwe ili watu wengi waweze kuangalia na tujulishwe tunachnagia vipi.

Utadhani uliingia kichwani mwangu :peace:
 
MUNGU ambariki sana huyu Mzee wa watu, sina cha kuongeza.
 
Yap nampa big up Mengi,Lakini aache kuhubiri kuwa uchaguzi una udini kwenye graduation alioalikwa atoe nasaha,anaanza kufanya kazi ya Kiravu na wengine.Haya mambo ya udini yanakuzwa na wanasiasa na watu kama yeye na yazidi kurudiwarudiwa ili hatimaye baada ya uchaguzi muanze kusema udini ulitawala na hatimae kuchochea vurugu.
 
Naishauri CHADEMA waipeleke tape ya mahojiano kama ilivyo halafu wakalipie AIR time pale TBC1 wasisahau Channel Ten maana wao kila siku wanaonesha ya ccm.
Hebu wafanze hivyo na wakigomea kurusha hata kama ni kwa kulipia basi waje kuwashtaki kwetu sisi wananchi
 
Nakubali kuwa huu mdahalo Chadema wanaweza kuuchukua na kurudia katika radio na vyombo vingine ambavyo vitakuwa tayari kurusha

ITV kwa upande wao Mungu atawalipa tu kwa kukubali kurusha live mdahlo huu mhimu

Mheshimiwa Mengi kweli wewe ni mpiganaji, na tupo nyuma yako na hivyo ndivyo Mungu amekuleta ulete ukweli katika nchi hii iliyopoteza njia kama vile haina dereva mwenye leseni.
Big Up usiogope maana utendalo ni haki kabisa aipendayo Mungu wetu. wamiliki wengine pia waige mfano wako japo wanaweza wasikufikie maana umetangulia
 
Naona kuna haja ya kuivunja vunja huo mdahalo ili angalau kila siku tupate dondoo kuelekea 31 oct.
Naona ela ndo itakuwa kikwazo
 
nimesikia Dr. atakuwepo kesho Dar na atahutubia maeneo ya hapa. Nadhani CHADEMA wangetumia muda huo kupitisha mchango kwa wahudhuriaji special kwa ajiri ya kulipia ghalama za kurudia kurusha mdahalo huo. Najua si mali ya CHADEMA bali ya waandaaji na ITV ambao kimsingi nadhani kwa Hekima za Mzee Mengi na hasa baada ya kujeruhiwa basi utaweza kurushwa tena ili kwa wale ambao hawajapata fursa ya kumsikiliza Dr. wa ukweli waweze kupata fursa hiyo muhimu katika ujenzi wa TANZANIA YENYE NEEMA
 
Back
Top Bottom