Kwa mgao huu wa umeme bora hata January Makamba

leoleo-tu

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
1,272
3,515
Yaani kwa kipindi cha miaka 4 sijawahi experience shida ya umeme iliyopo sasa. Sijawahi kumuamini bwana January lakini hata wakati akiwa waziri umeme ulikuwa haukati hivi.

Sasa hivi ni week sasa ikifika saa moja au mbili wanapita na umeme walianza wanarudisha saa 12 naona jana wamerejesha saa 2 leo sijui watarejesha saa ngapi. Yaani sisi tunaotegemea biashara zinazohitaji umeme tumekwisha kabisa.

Hii nchi ni rahisi sana kuwa kiongozi hata huhitaji kuumiza kichwa kutatua changamoto maana chawa watakutetea kwani yeye ndiye anayeleta mvua.
 
Kituko cha mtaani kwangu hapa umeme upo tunalingishiwa tu unawasha taa chaajabu feni hauwashi yaani nnapromiss na shemeji yako mpya nikasema nichukue mashine nijinyoe nywele zakule dah yaaaani mashine inatoa nguvu kwambaliiiiii hainyoi kabisa leo nnaumbuka
 
Tafuta ulipo jikwaa SIO ulipoangukia! Name droping haisaidii chochote kutatua tatizo, sera za chama tawala zinasemaje kuhusu suala hili la umeme? Je zinatekelezeka? Au ni politics tu kwa wapumbavu??
 
Maskini Biteko yawezekana kaachiwa msala ili achafuliwe na aondolewe kwenye system
Kama ni jumba ndio alishaangushiwa...na huo unaibu PM ni kumfunga kamba mguuni. Bi Tozo ameshauriwa na wakata kiuno wake Biteko ndio nyota ya Lake Zone akae nayo kwa tahadhari.
 
Sipendi kunyoosha nguo usiku zinapoa napenda ninyooshe nivae, sasa imekuwa ni utaratibu wao, kila asubuhi wanakata, ofisini pia kila jion saa 12 wanakata dah.

Sijui leo navaa nini? Jana nilibeba pasi nikanyooshea ofisin, nimechoka.

Miaka ya nyuma sikuwahi kuona umeme unakatika kati kati ya jiji, sasa hivi tumezoea, wanakata umeme hata asubuhi, mchana au jioni tunahangaika kwenye wenye jenerator zao nako unakuta foleni. Nyie hii shida ni kubwa.
 
Yaani kwa kipindi cha miaka 4 sijawahi experience shida ya umeme iliyopo sasa. Sijawahi kumuamini bwana January lakini hata wakati akiwa waziri umeme ulikuwa haukati hivi.

Sasa hivi ni week sasa ikifika saa moja au mbili wanapita na umeme walianza wanarudisha saa 12 naona jana wamerejesha saa 2 leo sijui watarejesha saa ngapi. Yaani sisi tunaotegemea biashara zinazohitaji umeme tumekwisha kabisa.

Hii nchi ni rahisi sana kuwa kiongozi hata huhitaji kuumiza kichwa kutatua changamoto maana chawa watakutetea kwani yeye ndiye anayeleta mvua.
Dotto Bieko kabebeshwa Zigo la misumari, mmetuona NYANI
 
Tatizo ni huyo huyo January, ye kaachia madaraka mgao ukiwa ushaanza

Si waliingia kwa mbwembwe kumchafua Magufuli kuwa mashine hakuwa anazifanyia service, haya ngoja tuone wao watatufikisha wapi.
 
Back
Top Bottom